Ugua pole Mzee. Mungu akusaidie upone haraka na kurejea katika afya yako
Huyu mzee ni mzee wetu wote...na zaidi ya hapo ni baba wa mmoja wa member mwenzetu na rafiki yetu ...sasa you can not hate him on both.....
Ugua pole mzee jsm....mungu akupe uponyaji ...na aijalie familia yake na madaktari kumuuguza vyema!![/b]
Ugua pole mzee Male tingatinga linakukokotoa magugu,
Mungu akupe tawfif,mchango wako bado unahitajika sana katika taifa hili.
Naona jamii forums wakati mwingine kuna kuna na tabia zisizojali maadili na utu. Masuala ya itikadi yasiingizwe kwenye nafsi ya mtu au familia ya mtu. Tunapingana na hoja hatupingani na mtu. Tunajadili hoja na kama mtu anaelewa abadilike na si kumpinga mtu huko ni kuishiwa hoja na kuwa mfinyu wa mawazo.
Mzee Malecela amekuwa mtumishi wa umma katika maisha yake, na wengi tunamkumbuka sana, na tunasikitika kwa yaliyompata, na Tunamwomba Mungu amrejeshee afya yake apate nguvu maridhawa. Na poleni kwa familia yake na wote wenye mapenzi mema.
Ugua pole Mzee. Mungu akusaidie upone haraka na kurejea katika afya yako
Ugua pole mzee Male tingatinga linakukokotoa magugu,
uGUA POLE MZEE WATU!
Ugua pole Mzee JSM
ugua pole mzee wetu
ugua pole
Ugua Pole Mzee John Samwel Malecela
Labda huo ndio u CDM, maana inaonekana jambo la maana hapa ni kutukana viongozi hata wakati ambao tulipaswa tuwe na ubinadamu.Naona jamii forums wakati mwingine kuna kuna na tabia zisizojali maadili na utu. Masuala ya itikadi yasiingizwe kwenye nafsi ya mtu au familia ya mtu. Tunapingana na hoja hatupingani na mtu. Tunajadili hoja na kama mtu anaelewa abadilike na si kumpinga mtu huko ni kuishiwa hoja na kuwa mfinyu wa mawazo.Mzee Malecela amekuwa mtumishi wa umma katika maisha yake, na wengi tunamkumbuka sana, na tunasikitika kwa yaliyompata, na Tunamwomba Mungu amrejeshee afya yake apate nguvu maridhawa. Na poleni kwa familia yake na wote wenye mapenzi mema.
Labda huo ndio u CDM, maana inaonekana jambo la maana hapa ni kutukana viongozi hata wakati ambao tulipaswa tuwe na ubinadamu.
Duh hii kali, afu yeye mwenyewe ndo muonjaji.teh teh teh du hakuna huruma kabisa vipi mkuu unafanyakazi kiwanda cha kutengeneza sumu nini?
ametusaidia nini kwa utumishi wake wa umma zaidi ya kutuharibia nchi yetu,
mimi sio mnafikie,,mwacheni afe aondoke zake tupunguze mizigo
Kakimbilia Uingereza kama Nyerere.Alisema kuwa Malecela alikwenda Uingereza kwa safari za kawaida ikiwa ni pamoja na kuangaliwa afya yake...
Malecela alitoa taarifa serikalini ambapo walimtumia fedha haraka na kumsafirisha mke wake (Anne Kilango) ili akamuuguze wakati amefanyiwa upasuaji.
Kakimbilia Uingereza kama Nyerere.
Malecela na Anna Kilango hawana dola 800 za tiketi ya Anna kwenda Uingereza mpaka waiminye Serikali bankrupt? Pole tujipe Watanzania tutakaofia majumbani jioni ya leo kwa kukosa anti-malaria pills, sio hivi vi vizee self-serving masquerading as socialist leaders.
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Malecela azungumzia afya yake
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Wednesday, 22 June 2011 21:40
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]digg
Boniface Meena
MWANASIASA mkongwe na kada maarufu wa CCM, John Malecela, amezungumzia afya yake kutokea nchini Uingereza, akieleza kuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Hospitali ya Wellington North nchini humo.
Hata hivyo, taarifa za kitaalamu zilizolifikia gazeti hili zinaonyesha kuwa Malecela alipata tatizo la kuvimba kwa mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini na kusababisha mtiririko wa damu kuyumba kwa kiasi.
Taarifa zilisema kutokana na hali hiyo, njia pekee ya kuondoa tatizo hilo ilikuwa kumfanyia upasuaji mkubwa wa moyo ambapo madaktari walilazimika pia kuchukua mishipa kutoka katika mguu wake na kuweka kwenye moyo wake.
Lakini jana, Malecela mwenyewe aliyezungumza na Mwananchi kutoka Uingereza alikolazwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo, alisema kuwa madaktari wamemshauri afanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita ili waangalie hali yake na baada ya hapo wataweza kumpa ruhusu ya kurudi nchini.
"Ninaendelea vizuri na madaktari wameniambia nifanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita kuiangalia hali ikoje ili waweze kunipa certificate (cheti) ya kuweza kurudi nyumbani,"alisema Malecela.
Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, amezungumzia hali ya mwenendo wa afya yake baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuwatangazia wabunge taarifa za kutokuwapo bungeni kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kutokana na mumewe kuwa mgonjwa na kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mama Kilango naye azungumzia
afya ya mumewe
Akizungumzia hali ya mumewe, Kilango alisema kuwa walikwenda nchini Uingereza Mei 11 mwaka huu wa ajili ya kumfanyia Malecela uchunguzi wa kawaida wa afya kama ilivyo kwa viongozi wa Serikali na alikuwa hana tatizo lolote.
Alisema kuwa yeye na mumewe wana kawaida ya kufanya mazoezi kila siku na kwamba walipokuwa katika mazoezi ya kawaida nchini Uingereza ambapo Malecela alianza kulalamika kuwa anapumua kwa shida, ndipo walikwenda hospitali ambapo alipimwa na daktari kumweleza kuwa ana matatizo ya moyo.
"Madaktari walimpima wakaona kuna mishipa inayotoa damu moyoni kwenda mwilini ambayo ilikuwa imevimba kutokana na Calcium kujikita kwenye mishipa na kuzuia mtiririko wa damu," alisema Kilango.
Kilango alisema upasuaji huo ulifanyika Mei 31 mwaka huu katika Hospitali ya Wellington North na daktari aitwaye Rakesh Uppal.
"Upasuaji umefanikiwa na yuko nyumbani sasa. Anatakiwa afanye mazoezi mara tatu kwa siku, dakika 20 asubuhi, dakika 20 mchana na dakika 20 jioni. Anafanya mazoezi akiwa na mlinzi wake pamoja na mimi hapa,"alisema Kilango.
Habari za kuumwa kwa mwanasiasa huyo ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini na CCM zilitangazwa juzi na Makinda wakati akiahirisha Kikao cha Bunge.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mungu wangu...... huyu mtu atatia umaskini watz"Ninaendelea vizuri na madaktari wameniambia nifanye mazoezi kwa muda wa wiki tatu hadi sita kuiangalia hali ikoje ili waweze kunipa certificate (cheti) ya kuweza kurudi nyumbani,"alisema Malecela
Mungu wangu...... huyu mtu atatia umaskini watz
umri aliofikisha unamtosha sana hata akifa hakuna hasara kwa taifa coz ni mzigo toka zamani
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Benard Membe amesema hali ya mwana siasa mkongwe nchini,John malecela inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo nchini uingereza.