ITV, Mengi to be dealt with soon

Muulizeni Spika SAMUEL SITTA kwa nini alikataa ile kamati ya ADAM MALIMA vs MENGI haikuwa public

from there ndipo utaona picha kamili jinsi Mengi anavyotumia vyombo vyake vya habari...hilo la kumshut down halipo ila mwenyewe akiamua kufanya hivyo well and good as long as ana bide by sheria zinazomruhusu kurusha hayo matangazo


Kuhusu JF...hapo hakuna kitu unless unataka kutuambia Mengi keshainunua lakini kama hajauziwa then it wont be a bad idea kuuziwa akifika bei...ohhhh kuhusu JF kuwa shut down hilo halipo nyie endeleeni tuuu

in a nutshell nzi leo naona exclusive yako imekuwa haina kiambatanishi cha upupu kama sikuzote unless utauleta baadae as attachment

Kweli huyu Game Theory ni kama Mkuchika/Salva kwa Bongo na Alfred Mutua kwa Kenya, who are their respective Govts mouthpieces!
 
Wakubwa nakubali kabisa maoni yenu lakini tatizo ni sie kujipanga na kwendana na vile tuandikavyo' nafkiri hakuna mmoja wetu ambaye ni mfuasi wa hawa wanaotuhumiana' sie sote tunatazama uwepo wa utawala bora,haki na mgao sawa wa mali ya taifa au sivyo? Vita kubwa ni kati yetu tulokosa na wao wanolimbikiza' hakuna hata mmoja anotaka zaidi ila sote tufurahie nchi kama wananchi na si vingine au kwa ajili ya wachache, tuamke na tushike lile litufaalo
 
La ITV kufungiwa halimo, serikali haiwezi kuifungia, ila Mzee Mengi, ana ajenda yake na anaitumia ITV kama moja ya strategies za kuifikia ajenda hiyo. Kitu ninachojua, ITV haitafungiwa bali itakufa natural death baada ya ajenda ya mmiliki kutokamilika.
Ajenda hiyo haitokamilika kwa sababu anatumia mlango wa nyuma kutimiza malengo yake.
Wengi wanamuona Mzee Mengi kama mkombozi fulani kwa mtindo wake wa kuuma na kupulizia, amamuuma adui fisadi papa, huku anampulizia mlezi wa fisadi papa kwa kisingizio cha kutaka kumsaidia.
Tatizo atakalokumbani nalo mzee wetu huyu ni kuwa hawa anaojidai anataka kuweasaidia, ndio hao hao wanaomuona kuwa yeye ni adui na kwa hakika, watammaliza.
Vita dhidi ya ufisadi ni vita kubwa inayohitaji kupigwanwa from within. Mzee Mengi kwa kutumia media yake, anataka kuwashawishi watanzania tukae nyuma yake kuelekea kwenye ukombozi wa kweli dhidi ya ufisadi. Tatizo watu anaotaka kupigana nao, wana nguvu zaidi yake, hivyo he is fighting a loosing battle na ndipo atakapoangamia na ITV yake na familia nzima ya IPP.
Mimi naungana na ile filosofia isemayo 'If you can't beat them, join them', vita hii ndio mwanzo wa mwisho wa Mengi kwa sababu nchi iko mikononi mwa mafisadi Left, Right and Centre.

Mtazamo wako Pasco sio. Mapambano, hasa haya magumu ya kupambana na ufisadi na mafisadi yana strategies nyingi; Mfano Kule Bungeni wapo wawakilishi wanaopambana, wengine ndani ya CCM mf. Dk. Mwakyembe, Anne Kilango, Selelii, Shelukindo, Spika Sitta na wengineo. Wengine wapo nje ya CCM mf. Dk. Slaa na wengine. Mengi na yeye anatumia nafasi yake kupambana kwa upande mwingine. Tukubali kuwa Mengi amepata ujasiri wa hali ya juu sana kuwataja kwa majina hao aliowatuhumu kuwa ni Mafisadi Papa hapa nchini, huku akifahamu nguvu zao, hasa za huyo RA a.k.a Kingmaker.

Hebu tuache unafiki, na tuongelee reality, hivi nani asiyejua jinsi baadhi ya wafanyabiashara waliowahi "kutembelewa" na TRA baada ya kujionyesha waziwazi kuitupa mkono Serikali na kuelemea upinzani? Au mfano wa Thomas Mollel a.k.a Askofu wa Arusha na Mirerani ilivyotangazwa kuwa anafilisiwa mali zake ikiwemo hotel ya Pallsons baada ya kuamua kuwa mfadhili wa NCCR Mageuzi enzi za Mrema? Alipoelewa somo akarudi kwenye mstari, matatizo yake yakaisha.

You win by right strategies man, and use your brain, not just feelings/heart. For Mengi to say that he named and shamed the "corruption sharks" in order to help Kikwete is a strategy because Kikwete can't say "No no no, I am not fighting against corruption in Tz". JK has to use proxies, as you heard, those who criticized Mengi are the members of "mtandao". But note that they (especially Sophia Simba and Mkuchika) couldn't criticize Rostam's counter-accusations because they are "his" people. Shame on them!

This is a multi-pronged war:
Some fighters are within CCM,
Some fighters are with other Political parties,
Some fighters are not affiliated with any political party,
Some fighters are media practitioners and owners,
Etc, etc, etc.

Aluta Continua!
 
Kuna umuhimu wa vita kulipuka hapa nchini. Tuteketezane weee kamamtu milioni 5 hivi, vumbi likitulia itakua akili na heshima kwa taifa na watu milioni 35 watakaobaki. Sio hivi sasa kila mtu anamamlaka ya urais. Hajulikani rais nani, waziri nani, fisadi nani. Kila mtu ana call the shots. Usalama wa taifa kazi wanayoiweza ni kufatilia zeutamu, ndio wanachoona cha maana kwa taifa. Wakati wabaka uchumi wamewaweka mfukoni.

Nataka mawazo ya tufanye nini ili tumalizane, heshima kwa taifa irudi, ili waje kufaidi nchi ya maana wajukuu???... tusiogope damu, U.S na Japan wapo shwari sababu walimwaga sana damu zamani. Rwanda sasa hivi kuna nidhamu sababu hiyohiyo, hapa tunaremburiana tu... Bullshit!
 
Last edited:
Ku-shutdown ITV lazima kuwepo kwa kukiukwa kwa sheria, kwa mfano, Tanzania Broadcasting Act (ipo hii) au nyinginezo. Ugomvi kati ya mtu na mtu hautoshi kuifungia ITV. Habari nd'o hiyo. Siungi mkono upande wowote ule, naelezea mtazamo wa kisheria.

Show me a dead body, I will show you the murderer.

Do we have a dead body here?
 
Baada ya kucomment kwenye andiko la mwanzoni la Max nimeamua ku withdraw ile statement yangu ........... jamaa wa UWT wangeshirikiana na wadau wa JF kwa ukaribu kumbe kiulaiini wangempata mmiliki wa zeutamu!!! duuh kweli kuna madogo wamepinda ila sasa utawafanyaje kama ndio wameshakuwa madogo wanatoka kwenye familia za kiukweli!!!
 
Baada ya kucomment kwenye andiko la mwanzoni la Max nimeamua ku withdraw ile statement yangu ........... jamaa wa UWT wangeshirikiana na wadau wa JF kwa ukaribu kumbe kiulaiini wangempata mmiliki wa zeutamu!!! duuh kweli kuna madogo wamepinda ila sasa utawafanyaje kama ndio wameshakuwa madogo wanatoka kwenye familia za kiukweli!!!

fafanua mkuu..madogo gani wanamiliki ze utamu..
 
Kuna umuhimu wa vita kulipuka hapa nchini. Tuteketezane weee kamamtu milioni 5 hivi, vumbi likitulia itakua akili na heshima kwa taifa na watu milioni 35 watakaobaki. Sio hivi sasa kila mtu anamamlaka ya urais. Hajulikani rais nani, waziri nani, fisadi nani. Kila mtu ana call the shots. Usalama wa taifa kazi wanayoiweza ni kufatilia zeutamu, ndio wanachoona cha maana kwa taifa. Wakati wabaka uchumi wamewaweka mfukoni.

Nataka mawazo ya tufanye nini ili tumalizane, heshima kwa taifa irudi, ili waje kufaidi nchi ya maana wajukuu???... tusiogope damu, U.S na Japan wapo shwari sababu walimwaga sana damu zamani. Rwanda sasa hivi kuna nidhamu sababu hiyohiyo, hapa tunaremburiana tu... Bullshit!

Sober, una kifua cha kusimama vitani au ngwamba za manati?? au ndiyo yaleyale ya mgahawani?? Sio vita inaanza wewe unaangalia tu kwenye CNN. Si lazima kupitia route moja kuelekea nchi ya "maziwa na asali". All we need is a change of mindset na kufuta siasa kwenye kazi na utawala bora

...Ngoma yataka Matao Mjomba!!!!!
 
Hakuna atakayeifungia ITV. PERIOD

Na wala sijui mnajadiliana nini hasa humu.

Mibongo bwana!
 
Hakuna atakayeifungia ITV. PERIOD

Na wala sijui mnajadiliana nini hasa humu.

Mibongo bwana!

FP

Tunajadili "ITV to be shut down soon" ...au ulitaka tujadili nini?

Tufundishe sie "mibongo" cha kujadili basi!!!
 
Kumfunga Mengi asiongee, ni one thing, Kuifunga ITV ni issue nyingine. Maana japo inamilikiwa na Mengi, lakini inafanya kazi nyingi na nzuri tu kwa jamii. Inasaidiana na madaktari wa kike kuwafanyia tiba mama zetu ambao wamesahauliwa na serikali, wanasaidia kuchangisha sasa hivi kwa ajili ya vifaa maalumu vya watoto wenye ulemavu. Kama wana hasira na Mengi, watafute njia nyingine. Na wananchi tuache ujinga wa kuingiza ushabiki katika mambo ya msingi.
 
Sober, una kifua cha kusimama vitani au ngwamba za manati?? au ndiyo yaleyale ya mgahawani?? Sio vita inaanza wewe unaangalia tu kwenye CNN. Si lazima kupitia route moja kuelekea nchi ya "maziwa na asali". All we need is a change of mindset na kufuta siasa kwenye kazi na utawala bora

...Ngoma yataka Matao Mjomba!!!!!

MTM you said it all.

Hakuna silaha cheap kama physical weapon many dont understand that. Ukitaka kujua gharama ya elimu jaribu ujinga then you can know what it means by the word 'mind set'. In general kama huna sound mind there is no where u can be a winner in any aspect of life. sasa watu wanaofikiri ki mabavu bavu huwa wanamatatizo ya kifikira they think their masculine character can solve problems. Mfano rahisi mtu ambaye hana knowldge ya chemistry akiosha chombo kilichogandamana na rangi atachukua a sharp object kuanza kukwangua ili kuondoa rangi. Now think of how long it will take that person to complete the task. How about the one who has a knowlegde of solvent he just pour into the object and the thing is dissolved within no time.

Nachojaribu kueleza nikuwa kama tukiwekeza kwenye change of mind set of our people at the time their attitude is changed hakuna fisadi atakae baki maana mafisadi wana win kwasababu wametuzidi ujuzi wa kuvuna bila kupanda sasa wewe ukiweza kuwa na raia wenye 'sound mind' kwamba u can not give ur right of birth in exchange of one day meal you are already a winner before you enter the fight. why then should you embark in a war which would loose 5mil people while you can still win without loosing one and yet arrive at the same destiny in a shortter time than if u r to use the former strategy? And I think this is what we do here in JF what else do we want?
 
Nadhani ni vigumu kufunga ITV, isipokuwa kama sheria iliyopo jikoni itapitishwa basi Mzee Mengi atapaswa kuchagua moja kati ya TVs, Radios au Magazeti. Sheria mpya inamtaka mmiliki kuwa na chombo kimoja tu cha habari. habari ndo hiyo, eti uhuru wa vyombo vya habari unakuwa!
 
Jamani kuna jamaa kanidokezea sasa hivi kuwa amenyetishiwa na ofisa mmoja (A very senior officer)anayefanya kazi ofisi ya muungwana, kwamba ni kweli kituo cha ITV kitafungiwa anytime from now. Hii ni baada ya vikao kadhaa kufanyika kujadili uvunjaji wa makusudi wa taratibu za uendeshaji wa kituo cha TV na kukiuka maadili ya utangazaji. Nimetonywa kwamba maamuzi hayo yana baraka zote za muungwana!!!
 
Jamani kuna jamaa kanidokezea sasa hivi kuwa amenyetishiwa na ofisa mmoja (A very senior officer)anayefanya kazi ofisi ya muungwana, kwamba ni kweli kituo cha ITV kitafungiwa anytime from now. Hii ni baada ya vikao kadhaa kufanyika kujadili uvunjaji wa makusudi wa taratibu za uendeshaji wa kituo cha TV na kukiuka maadili ya utangazaji. Nimetonywa kwamba maamuzi hayo yana baraka zote za muungwana!!!

yaah ka-inzi huwa hakosei kunyaka uchafu hilo tunalitambua, kinachoongelewa hapa ni kutodhaniwa kwa jambo, no body could easily accept this information. Endapo wataifungia ITV namshauri Mengi agombee U-Rais, he will be supported than JK, Mbowe, Lipumba or anybody else except Dr. Slaa.
 
Nijuavyo mimi kumekuwa na shinikizo kubwa sana kutoka kwa mafisadi la kutaka ITV ifungiwe haraka. Bila shaka wapiganaji wote mnajua kwamba iwapo ITV itafungiwa mafisadi watakuwa wamepata ushindi mkubwa kwani baada ya hapo wananchi wote watalazimika kuangalia TV zinazomilikiwa na mafisadi: TBC1 (Rostam na Manji), Channel 10 (imenunuliwa na Tanil Somaiya). Tv stations hizi zitatumika kupotosha taarifa zote zinazohusu ufisadi na kuwasafisha mafisadi papa. Kazi hiyo kwa sasa inafanywa na magazeti uchwara ya SAUTI HURU (la Subash Patel), TAIFA TANZANIA ( la Nazir Karamagi), TAZAMA (Lowassa, et al) na mengine ambayo majina yake siyakumbuki. Ikitokea hivyo ni hatari kubwa, hivyo inabidi tujadiliane namna na kuzuia nguvu hii mpya ya mafisadi.
 
Last edited:
sio siri kwa nini wanataka kufanya hivyo, hakuna maana ya kuwa na vyombo vya habari katika taifa ili.
 
Back
Top Bottom