ITV, Mengi to be dealt with soon

ITV, Mengi to be dealt with soon

Kuna kitu alisema Enigma.. I need to that again... I probably missed something. Is this it?
 
Kumbe ni kosa kukiuka ratiba ya vipindi ??!!! Sasa kama kuna breaking news inakuwaje?

ha ha ha, kile kipindi maalumu cha Rostam kumjibu Mengi TBC1 kilikuwa ndani ya ratiba? by the way TV ya Taifa vipindi maalumu hupewa Rais na mnaomkaribia, sasa RA! na hakuna hata kupewa kemeo la mdomo. Kweli Rostam ana nguvu...
 
ha ha ha, kile kipindi maalumu cha Rostam kumjibu Mengi TBC1 kilikuwa ndani ya ratiba? by the way TV ya Taifa vipindi maalumu hupewa Rais na mnaomkaribia, sasa RA! na hakuna hata kupewa kemeo la mdomo. Kweli Rostam ana nguvu...

Nziku, tupo pamoja mkuu. Nilikuwa tu ninashangaa kwamba kati ya makosa ambayo ITV inatakiwa kujitetea ni kuvuruga utaratibu wa vipindi. Hizi sheria zimepitwa na wakati sana.
 
Nziku, tupo pamoja mkuu. Nilikuwa tu ninashangaa kwamba kati ya makosa ambayo ITV inatakiwa kujitetea ni kuvuruga utaratibu wa vipindi. Hizi sheria zimepitwa na wakati sana.

But the thing is why only ITV??
Mbona Fisadi papa RA alivo enda TBC haijakemewa? yaani sielewi watu wazima wenye akili zao wanapo weza kufanya blanda kama hizi kwa ajili ya kumlinda fisadi mmoja tu!

Labda niungane na Mwanakijiji kuuliza hivi RA hizi nguvu alizo nazo mbona ni za ajabu sana? anazitoa wapi? hivi ni kawaida kweli? ama kuna sayansi za ajabu zinaendelea juu yake kumfanya awe na utiisho juu ya binadamu wenzake? I dont get it!..
 
Tanzania inaogopesha sasa Mzawa anaponyanyaswa na Serikali yake kwa vile tu amewataja wezi wa mali ya umma ambao kwa bahati mbaya au nzuri wote ni MaG.A.BACHOLI-Wakuja.

Ni lini nchi yetu itarudi kule uzalendo-uzawa (indigenous) unanathaminiwa kama nchi nyingine za Africa?
 
Last edited:
Hapa na mimi ndiko nimekoma kabisa::

Mengi program yake ilikuwa aired na ITV na TCRA wameandika hii compliance order blah blah sababu ya ITV kurusha hiyo program ya Mengi

Rostam Aziz program yake ilikuwa aired na TBC, Je TCRA WAMEWAANDIKIA TBC COMPLIANCE ORDER KAMA HII YA ITV???

Kama sio, sasa tofauti ya ilichofanya ITV na TBC ni kipi??

Hivi Serukamba ni mjumbe wa bodi ya TCRA?? Je aliwekwa na Lowassa through Chenge wakati huo chenge alipokuwa waziri mwenye mamlaka ya TCRA???
 
Biography (fupi) ya Prof. Nkoma hii hapa, huenda naye ni fisadi au anatumiwa....


Mwenye taarifa aniambie kama huyu Nkoma alishakubalika kwamba ni M-Tanzania.

Prof. Nkoma haionyeshwi alizaliwa wapi lakini tangu alipoletwa nchini kutoka huko Botswana, ilieleweka yeye ni raia wa Malawi. Kusoma hapa na kuajiliwa hapa ilikuwa ni makosa ya ujamaa wa enzi hizo. Ano ndugu pia walioko nchini bila uraia wetu na wanaishi maeneo ya Kunduchi.

Pamoja na suala hilo kuzimwa na ikulu, je alishakuwa M-Tz? Isije ikawa tunasumbuliwa na raia wa nchi jirani.
 
Watanzania vita hii si ya Mengi pekee yake, hii ni vita ya watanzania didi ya mafia waliojificha kwenye nembo ya mtandao.Mhusika mkuu ni Mh.Kikwete hana jinsi anavyo weza kukwepa lawama hizi za kuiuza nchi.

Hawa wahindi miaka yote hawakujiingiza kwenye siasa maana ikulu ya wakati huo haikuwa pango la wanyanga'anyi,tangu wanyang'anyi waingie ikulu imekuwa kimbilio lao.Wahindi hawa si wa kuaminika mnamkumbuka bwana Amir Jamal mhindi aliyekabidhiwa hazina mnakumbuka alipo kufa alizikwa wapi? familia yake hadi sasa iko Canada je hakuwa na raia mbili au tatu,mhindi gani aliye na uchungu na nchi hii ya Tanzania nilibahatika wakati fulani kutembelea Machester Uingereza wahindi wote walio hamisha wazungu kwa kununua nyumba zao ni kutoka Tanzania maana wale wa Uganda Amin ali wa "time".Wakikujua wewe ni mtanzania wanakwambia wanatoka Uganda ukienda kesho yake ukajitambulisha wewe ni mganda mhindi huyohuyo wa jana anakwambia ni mtanzania,sasa leo hii tumekufa maana wameingia Ikulu wanatawala nchi kwa sababu ya kuwa na viongozi wadhaifu na waroho wa mali.

Hawa wahindi hawawezi kutoa shs milioni 400. eti kusaidia vijana wa CCM bure mbona hawawapi mdawati watoto wanaosoma wakiwa wamekaa chini?.

Watu tulio wapa dhamana ya kulinda katiba wameshindwa leo hii inadhihilisha wazi ni jinsi gani hatuna uongozi dhabiti hivyo nidhahili vita hivi si vya Mengi ni vyetu na imefika mahala sasa pa kukomboa nchi kwani Tanzania haijawa huru ilikombolewa toka kwa wazungu na kuingizwa kwa mamuluki weusi ndo maana Tangu enzi na enzi hakuna mtanzania amewahi kuchagua Rais au kiongozi wa nchi mara zote kikundi kidogo cha watu kimekuwa kikiwaletea watanzania mtu wao na sisi tunampigia kura ya maoni "referendum" Je nani alimpendekeza Kikwete,Mkapa,au Mwinyi?
Si haohao tulio waamini kumbe ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo?

Leo hii wanamiliki kila mradi kuanzia madini mpaka stendi za mabasi.

Ni wakati wetu wa kufunguka macho maana mkuu wa nchi amekuwa Vasco Da Gama wa karne ya leo, hana uchungu na nchi alipewa naye atawapa wengine lakini hatima ya yote wananchi ndo mnaopata cha moto.

Tufunguke sasa tuchuje makapi.
 
Huu ni mwanzo wa mwisho wa "amani ya woga" ilikuwapo Tanzania. Wananchi wataamka na kulipinga hili jambo waziwazi na huu ndiyo mwanzo wa machafuko kuelekea kupatikana uhuru kamili wa wananchi.
 
Wapuuzi tu,wapuuzieni hawa kujaribu kuwaelewesha ama kuwatowa ktk uongonzi kwa ballot ni kupoteza kalolii zako tu,hii ni kama kujaribu kumwelewesha KUNGUNI ya kwamba asijaribu kukunyonya damu unapolala usiku maana akikunyonya damu usiku anakusumbuwa na akiendelea na tabia hiyo basi unaendelea kumweleza ipo siku utamtafutia theodani.



Hapa mimi nafikiri watanzania Tuseme kama Nyerere alivyosema ya kwamba SABABU,NIA na UWEZO wa kukupiga tunao Full stop.
 
Last edited:
But the thing is why only ITV??
Mbona Fisadi papa RA alivo enda TBC haijakemewa? yaani sielewi watu wazima wenye akili zao wanapo weza kufanya blanda kama hizi kwa ajili ya kumlinda fisadi mmoja tu!

Labda niungane na Mwanakijiji kuuliza hivi RA hizi nguvu alizo nazo mbona ni za ajabu sana? anazitoa wapi? hivi ni kawaida kweli? ama kuna sayansi za ajabu zinaendelea juu yake kumfanya awe na utiisho juu ya binadamu wenzake? I dont get it!..

Nakushangaa, TBC haiwezi kukemewa kwa kuwa RA aliitisha press conference katika public hotel,
walioenda wameenda waliobaki wamebaki na walioona inafaa kurushwa wakairusha na walioona
haifai kurushwa wakaiacha. Its an event not like Mengi did.
 
Nadhani kwa hali inavyojionesha sasa na kwa namna TCRA walivyojichomeka kwenye hii issue hata kama mtu alikuwa amelala usingizi atajua tu kwamba hapa kuna kitu! Na kwa hili wazalendo wa-Tanzania walio wengi watakwenda na Mengi. Na ole wao MAFISADI wanaoshirikiana na MAGABACHOLI, yaani sijui nisemeje lakini siku zao zimehesabiwa! Kama wanaweza soma alama za nyakati basi ni wakati wa kujiandaa kutuachia nchi yetu. Nasema HAIWEZEKANI kunyanyaswa ndani ya nchi yetu wenyewe, unless hatujawa huru!! Warudi kwao wakalime na kula pilipili!! Haiwezekani watu wachache watufanye wengine vikaragosi vyao, watunyonye, wachukue nyumba zetu, viongozi wetu na hata kufikia hatua ya kutunyima uhuru ndani ya nchi yetu wenyewe, HAIWEZEKANI!! Nadhani wakati umefika sasa, Wa-TANZANIA tuungane na tuseme tumechoka nao, huyo Mkulu anaweza ungana nao, hatutamshangaa, maana yeye mguu na njia, kama kawa kila kukicha, ndio zake! Maana tuliodhani wako upande wetu wametusaliti na hatuoni dalili zozote za kutusaidia.

Tanzania ni ya wa-Tanzania na si WAASIA!! Sijawahi na najua haitatokea hata siku moja mtu mweusi kuwa hata katibu tarafa - ASIA, Lakini sijui sie Tanzania tumerogwa?? Maana hao ndo tumewapa nchi watuongoze!! Nadhani sasa inatosha, ONDOKENI!! Msiseme nimekuwa mbaguzi ila matendo yao yanakera, na SIYAPENDI ni heri waondoke tu, wameiharibu sana nchi yetu kwa utapeli na ufisadi wao wakishirikian na ndugu zetu wenye njaa na uchu wa madaraka ambao akili zao ni kama maamuma, wanaojali matumbo yao na waliopoteza uzalendo!!
 
Faida ya kuwepa document hapa Online ni kwamba hata wakiziiba kule kwa kina afande nanii watu wa jamvini hapa wanakuwa na back up ambayo imesambaa dunia nzima. Ubarikiwe
 
this is a wrong move

I dont like it at all

iko namna ya kudeal na Mengi lakini siyo hivi....

Sasa GT,si unajua kuwa Rostam plus hao waliokosea namna ya ku-deal na Mengi wanafika hapa JF kupekua tunaongea nini?Kwanini basi usiwasaidie hizo MBINU ZA KU-DEAL NA MENGI (kama zipo,at all)?

Nadhani miongoni mwa makosa makubwa sana unayofanya ni kum-underestimate MENGI.....
 
Tanzania ni ya wa-Tanzania na si WAASIA!! Sijawahi na najua haitatokea hata siku moja mtu mweusi kuwa hata katibu tarafa - ASIA, Lakini sijui sie Tanzania tumerogwa?? Maana hao ndo tumewapa nchi watuongoze!! Nadhani sasa inatosha, ONDOKENI!! Msiseme nimekuwa mbaguzi ila matendo yao yanakera, na SIYAPENDI ni heri waondoke tu, wameiharibu sana nchi yetu kwa utapeli na ufisadi wao wakishirikian na ndugu zetu wenye njaa na uchu wa madaraka ambao akili zao ni kama maamuma, wanaojali matumbo yao na waliopoteza uzalendo!!
Mkuu, wacha ubaguzi 🙁
 
this is a wrong move

I dont like it at all

iko namna ya kudeal na Mengi lakini siyo hivi....

Hahahaha...wacha kunifurahisha hapa. Eti iko namna ya ku-deal na Mengi.
Unakuwa kama hujui maana ya uhuru bwana!!
Hapa ITV iende mahakamani na hopefully mahakama itabidilisha sheria kutokana na haki ya msingi ipatikanayo katika Katiba. Haki hii ni freedom of expression. Kwa nini ITV, as a broadcasting corporation, isiwe na uwezo wa kubadilisha ratiba yake ipendavyo yenyewe?! Ujinga huu!

Katiba inasema hivi:-

Haki ya Uhuru wa Mawazo
18.-
(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.


hahaha...hapa blue na nyekundu vitapambana!

Sheria ipi ifuatwe? Katiba au Broadcasting Service (Content) Regulation 2005?
 
SASA WATANZANIA BADO MNAIMANI NA HII TCRA AMBAYO INASIMAMIA TELECOMS PIA? KWENYE THREAD MBALIMBALI TUMELIA WEE KUHUSU USHINDANI WA KWELI..This is the same Manji early this yr kapewa na TCRA license, rostam (mbunge ccm) we all knw his story (voDACOM),,,lowassa (mbunge ccm) ndo hayo (alphatel,ABC TV) ....Kikwete sijui anataka watanzania tumkumbuke vp after 2015! Laaana hizi!

Kwa kweli inauma kuona government institutions makini kama TCRA ambayo inanguvu sana kwenye uchumi wa nchi zikiendeshwa kisiasa!nchi inaelekea pabaya.

2010 tuwe makini na kura zetu...tusione aibu kuuliza hela za tshirt na pilau zinatoka wapi? 2005 tulilala saaaaana.
 
Mimi nadhani hakuna haja ya kupiga kelele na kulalamika, ITV haiendeshwi juu ya sheria na taratibu za nchi. Kama ilikubali masharti ya kufanya shughuli zake ndani ya Tanzania, basi haina budi kufuata taratibu hizo. Na kama wataonekana wamekosea ni imani yangu kuwa hatua zifaazo za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Lakini hata hivyo ITV inayo haki ya kupinga adhabu yeyote katika vyombo au mamlaka husika ya kisheria.
Sikubaliani na hii tabia ya Mengi kuanika hizo barua kwa kutaka kuonewa huruma, atumie mawakili wake na awaache wafanye kazi zao kitaalam bila ya kuanza kuanika hizo correspondences za mawakili na hizo taasisi zingine. Kwa kifupi Mengi anaifanya kazi ya mawakili wake kuwa ya kisiasa zaidi na kuingiliwa na influences za public.
 
Back
Top Bottom