Ni hivi: 1) Mfanyabiashara ni nani na anatabia gani? kabla hujaanza kuleta hoja zako ni vema unachokizungumza, kwa mfano mfanyabiashara hawezi kupewa sifa moja na mwananchi kwa kuwa yeye hulenga kutengeneza faida zaidi badala ya kutoa huduma, ndo maana Mwalimu Nyerere alisita mtu huyu kujihusisha na siasa au ufanyaji wa maamuzi bila kuangalia upande wake. Kwa bwana Mengi hakuna anayejua lengo lake la dhati katika mambo anayoyafanya. Sasa ni muhimu kumtengenesha yeye na wewe hasa linapokuja suala la maslahi ya kitaifa
naona kama una komplicate situation. yeye alisema mafisad ni hawa. yaani alisema wezi wetu ni hawa. na akataja na makashfa yawahusuyo. sasa kwanin tuanze kuangalia huyu mengi anashughulika na nini? haya chukulia ni mshindani wao katka biashara au anataka uraisi baada ya jmk. kwahiyo tusimsikilize au hana haki ya kusema ukweli?
yaani, wafanyabiashara wote tusiwasikilize wakiwashutumu wenzao kuwa wanalihujumu taifa. tuwadharau kabisa. tuseme kwenda huko kwanza wewe mwenyewe ni mfanyabiashara kama hao wezi. tuseme tunataka mfanyakazi wa kuajiriwa au mkulima ndo atupe habari za sisi kuibiwa na wafanyabiashara?
kwanini?
hapana. tumsikilize kila mtu. la muhimu iwe usahihi wa hizo habari. then vyombo vya dola vifuatilie. after all tunawalipa kwa hilo
afande kova kila mara anasema anaomba 'ulinzi shirikishi'. ambapo raia watatoa taarifa kwa polis na polis watafuatilia. alichofanya mengi ni kumuunga mkono kova
hata kama angekuwa anataka urais bado anastahili kusikilizwa. asikilizwe na vyombo vinavyohusika vifuatilie. akija kuanza kugombea urais tuje tumhukumu kwa matendo yake na michango yake kwa tz
4) Ndugu ya Mukandara nafahamu fika msimamo wako kwenye sakata hili, hata mimi pia ninao wa kwangu, hebu tujaribu kuweka pembeni hii na tuwe wa kweli kwa watanzania wenzetu. Ni ushahidi gani ambao Mengi aliutoa wakati anawataja watuhumiwa hawa zaidi ya maneno yenye kujenga chuki kati yetu na watanzania wengine. Kama kweli alikuwa na haja ya kumsaidia Rais, je unataka kuniambia njia ile ilikuwa sahihi? Mimi, wewe na Mengi nani mwenye uwezo wa kuonana na Rais na kukaa nae pamoja kunywa gahawa, ni kweli mengi anania ya dhati ya kumpa tafu Kikwete kwa staili ile? Yaani hata kutumia ushawishi wake ameshindwa kumkabidhi kikwete ushahidi kwa kuwa haviamini vyombo vyake vya dola? Mi siamini kama kweli alikuwa na lengo hilo, okay tuseme kweli alikuwa na lengo hilo sasa kama serikali imeshindwa kuwachukilia hatua yoyote pamoja na uwezo na nguvu za kijeshi na kisheria ilizonazo, kitu gani kimemshawishi yeye angeweza? Yapo maswali mengi ya kujiuliza kama mjadala huu ila nia yangu si kufufua msiba huu bali ni kuwekana swa katika mambo ya msingi na yasiyo ya ubishi.
kuna namna nyingi za kumsaidia mtu kufanya kazi yake ipasavyo.
nionavyo na nifikiriavyo mimi vyombo vya serikali vina ushahid na uwezo mzuri zaid ya mengi katka hili. kwa hiyo kwa mengi zaid ilikuwa - ebanaeee, mbona hufanyi kazi yako!
hata maskin kabisa hapendi kuibiwa au kudhulumiwa. hata asiyejua kuwa anaibiwa pia hapendi kuibiwa. kwangu alichofanya mengi ni kuungana na mamilion ya watz wengine kupiga kelele, kulalamika. na makelele haya yanaweza kuwa very effective. na huo ni mchango bora kabisa pia
Ukweli wa yote anaujua yeye mwenyewe mimi na wewe ni washabiki kama ilivyo Man na Barca...mwisho wa siku rekodi zetu ziko sawa.
si kweli kuwa mkandara na wewe au mimi na wengineo suala la mengi na rostam ni kama ushabiki kwa man na barca. si kweli kabisa. suppose man au barca inashinda, mkandara kama mshabiki wa timu inayoshinda kikawaida atapata nini? kwa upande mwingine chukulia mkandara ni mtz na anamuunga mkono au kumshabikia kama unavyoita bwn mengi. je mengi akishinda - na hapa kushinda ni kuwa mkweli na kuchukuliwa hatua kwa hao mafisad, je mkandara kama mtz hatanufaika kivyovyote?
au unataka kutufundisha hapa kuwa anachosema mengi si kwa manufaa ya taifa?
hilo somo mi siwezi kulielewa. labda unifafanulie zaid.
haiwezekani mtu anakuja anasema, ebanaeee, tunaibiwa, halafu wewe hapa useme hasemi hayo kwa faida yetu sote. sikatai inaweza kuwa inamnufaisha directly au indirectly, leo au kesho but still hainiumi kama sie, kama watz inatusaidia pia
mapesa ya serikali au kama yale ya epa ilikuwa yatusaidie sisi sote. yakiibwa tumeibiwa sote