I dont see any reason for crucifying reginald mengi.He is a patriot, a tanzanian businessman employed lots of Tanzanians, he pays taxes to the government and infact he is a senior citzen who can come out publicly to speak evils. It is quite unfortunate that poor corrurpt countreals tends to cooprate with foreigners than locals. This is a deadly syndrome of poor and corrupt government ..putting the locals for the last. Would you emaging an employee of ultimate security owned by somaiya earns only 60,000 monthly gross pay???.
Ive read all letters, ya TCRA na ITV Advocate!
dont know why theyre here! Unless kama sijazielewa, otherwise theres nothing burning here!!! Mnataka kutushawishi kwamba ITV (Mengi) inataka kuhujumiwa? If I can remember, Manji alipeleka malalamiko TCRA kwa kile alichoona (yeye Manji) kwamba Mengi anatumia nafasi yake kama mmiliki wa vyombo vya habari kutumia vyombo hivyo kuwadharirisha wenzake! Au kwa maana nyingine, anatumia vyombo vyake kwa maslahi yake binafsi.
Whether thiss true or not, ni kweli sheria za vyombo vya habari zinakataza kuweka mbele maslahi binafsi badala ya yale ya kitaifa!! Hii si mara ya kwanza kwa ITV kushutumiwa kwa jambo hili, kuna wakati ilisemwa kwamba hata muda anaopewa JK kama kiongozi wa nchi ni mdogo ukilinganisha na ule anaopata Mengi( am not sure abt this, and its none of my businesss)! Sasa kama TCRA walipelekewa hayo malalamiko na Manji, what could they do?!
Hawakutakiwa kuwaandikia ITV kwenda kuji-defend? Mbona kwenye hiyo order ya TCRA sijaona popote panapoonesha dalili za kutaka kuihujumu ITV? Au ni kwavile TCRA walipiga biti kwamba ITV wasipo-appear before Authority watakuwa punished? I dont think kama kuna something wrong hapo. TCRA ni mamlaka inayotambulika kisheria hivyo order yake lazima iheshimike whether mtuhumiwa(Say ITV) kafanya kosa au hapana!!!
Kwangu mimi hii nayo ni ilele ya kutaka kumuonesha RM kwamba ni mtu anayehujumiwa!! Kila anapohisi kunafanyika mambo negative dhidi yake, anatafuta defensive mechanism ya kutaka kujionesha anaonewa!! Nakumbuka last year, or year before kuna wapuuzi fulani waliongea kwamba eti RM ni mbaguzi wa kidini!! Katika kutaka kuonesha yeye si mbaguzi, few days later ( if not hours) ITV wakarusha kipindi cha karibu nusu saa (kama sio saa nzima) ikimuonesha RM akila msosi na watoto wa Madrasa kule Kibaha kama sikosei! Katika maongezi yake hiyo siku, nakumbuka RM akisema ..watoto, kuna watu wanasema eti mimi nawabagua nyinyi ! Nilicheka sana siku hiyo na kujiuliza how can such great man look for such cheap popularity!
Unataka kutushawishi yale ya TBC1 na RA ni ya kitaifa? Au kwa makusudi ume skip issue hii kuizungumzia kwenye details zako?
Mengi angeenda kulalamika kwenye tume ya mawasiliano nauhakika nao wangeandikiwa hivyo bye the way RA hakulalamika aliyelalamika kwenye tume hiyo ni ManjiBut the thing is why only ITV??
Mbona Fisadi papa RA alivo enda TBC haijakemewa? yaani sielewi watu wazima wenye akili zao wanapo weza kufanya blanda kama hizi kwa ajili ya kumlinda fisadi mmoja tu!
Labda niungane na Mwanakijiji kuuliza hivi RA hizi nguvu alizo nazo mbona ni za ajabu sana? anazitoa wapi? hivi ni kawaida kweli? ama kuna sayansi za ajabu zinaendelea juu yake kumfanya awe na utiisho juu ya binadamu wenzake? I dont get it!..
I dont see any reason for crucifying reginald mengi.He is a patriot, a tanzanian businessman employed lots of Tanzanians, he pays taxes to the government and infact he is a senior citzen who can come out publicly to speak evils. It is quite unfortunate that poor corrurpt countreals tends to cooprate with foreigners than locals. This is a deadly syndrome of poor and corrupt government ..putting the locals for the last. Would you emaging an employee of ultimate security owned by somaiya earns only 60,000 monthly gross pay???.
Mengi kajipalia makaa chachandu,
Hakujua kuwa alipomgusa Rosta Aziz alikuwa anaugusa mtandao mkubwa sana wa watuhumiwa vitendo vya ufisadi,ambao kama kweli Mengi ana ushahidi zidi ya Rosatam tu, basi ni sawa kuwa mlolongo huo wote anaohusiana nao unaweza kuwa hatarini na kupelekea balaa kwa serikali ya awamu ya nne kabla ya hata uchaguzi wa 2010, ndo maana idara za usalama zinajaribu kupata kile ambacho Mengi anakusudia kukisema mahakamani kabla hakijafika huko.
Nadhani kuna tatizo hapa!
Kila kitu kinachukuliwa kama ni siasa.
TCRA ni chombo kinachojitegemea na ndani ya TCRA kuna CCC; hawa jamaa ukitukanwa kwenye mtandao au kwenye nyanja yoyote ya ICT, au service provider akilamba salio lako kwenye simu etc na mengi mengine unawapelekea... wakishapelekewa wana mwita aliyetuhumiwa kumsikiliza.
Sasa katika hili sijui kwamba wanatakiwa waendelea hata kama kuna hoja mahakama au lah!.
Lakini kule hamna siasa.
Let be serious, kwa sheria za nchi Mengi alichemsha kwa sympathy ya wananchi na kwa kuwa tumekata tamaa huenda hana kosa.
Turudi nyuma gavana wa Benk juzi tu amekataa wabunge wasiwe wajumbe wa bodi wa bank ambapo serikali ina shea... hii ilikuwa kilio cha watu wabunge wa upinzani na chama tawala lakini rais ameendelea kuwateua na mawaziri wameendea kuteua wabunge wenzao, Ndulu mteuliwa wa Rais amekataa... lakini hawezi fanywa lolote kwa kuwa BOT inajitegemea... anayefuata maelekezo ya serikali ambapo sio lazima ni udhaifu wake... na wala sio matatizo ya serikali.
Sasa mimi naona tukubali msumeno unakata pande zote.
kuna mtu anayeshindana na dola naye akashinda?
Kuna wakati ni ngumu kukaa ukiona mjadala unavurugwa kwa makusudi. Ngojeni niwapeni dondoo kidogo hasa kwa wale wanaokurupuka bila kujua namna shughuli za media zinavyofanya kazi na maadili yake.
Mengi si mtu wa kawaida, kitendo cha kumiliki vyombo vya habari na makampuni kadhaa imemtoa katika sifa ya mtanzania wa kawaida na kuwa mfanyabiashara. Hapa kimaadili ndipo linapokuja tamko la TCRA kwa ITV. Kiufupi bwana mengi amekosea kwasababu yeye ametumia vyombo vyake kutuhumu watu wengine regardless kuwa anaushahidi au laa....waandishi wa habari wanamaadili mengi lakini moja kuu ni lile la kutochagua upande na kusema ukweli kama ulivyo.
Sasa kwa nguvu alizo nazo mengi isingekuwa rahisi kwa wafanyakazi wake kumhoji uhalali au ukweli wa taarifa alizotoa na labda wangejitahidi kuwapa nafasi watuhumiwa kujitetea au kurespond tuhuma hizo. Hapa ndipo ilipoingilia kati TCRA kwani walijua fika hakuna wa kumbana mengi juu ya ukweli wa tuhuma hizo na pia mjue kuwa kuna watu katika jamii huuamini kila kinachosemwa kwenye TV ni UKWELI, hata humu JF wapo wanaoshabikia kitendo cha mengi kwa mapenzi yao binafsi pengine waliwahi kusaidiwa na mjamaa huyo au ni kweli wanaushahidi wa aliyosema mengi, FINE let them join hands with HIM...ila ukweli unabakia kuwa hawapaswi walazimishe wote kuamini mengi alikuwa sahihi.
Kwanini TBC haikupewa order kama ya mengi...ni hoja na swali muhimu la kujiuliza. Kama wapo wanaopenda majibu ya kweli bila kuleta ubishi wa Man na Barca, ni hivi, baada ya tuhuma RA alitambua umuhimu wa kusema upande wake na ni wazi waandishi wa mengi hawakuonyesha nia ya kufanya hivyo aliwajibika kutafuta kituo kisicho na upande wowote na chenye kuaminika na wananchi (wapo wenye mtizamo tofauti), na TBC pia waliamini kuwa hiyo ilikuwa habari muhimu kwa wananchi kufahamu upande wa pili wa watuhumiwa, kwa kituo chochote makini na chenye kufuata misingi ya uandishi bora na wenye weledi wasingeweza kukataa kurusha hewani taarifa hiyo. Na pia walikuwa na uwezo wa kuchambua hoja na kuueleza umma nini kilikuwa kikiwasilishwa na Mtuhumiwa.
Tuache kumshabikia Mengi wakati anavuruga utaratibu na kama kweli anataka kumsaidia rais angeanzia mahakamani na kwa kuwa alikuwa na ushahidi basi isingekuwa rahisi kwa mahakama kupindisha sheria na kama ingefanya hivyo basi ndipo angetumia rungu lake kuuelezea umma kilichokuwa kinaendelea.
Aende tu kujibu kwani anaogopa nini.
Unaposema inamtoa Mengi ktk sifa ya Mtanzania wa kawaida na kuwa mfanyabiashara una maana gani?.. yaani mfanyabiashara sii Mtanzania wa kawaida au kumiliki chombo cha habari ambacho unakitumia kutangaza habari hiyo huondoa Utanzania wa kawaida!..Mengi si mtu wa kawaida, kitendo cha kumiliki vyombo vya habari na makampuni kadhaa imemtoa katika sifa ya mtanzania wa kawaida na kuwa mfanyabiashara. Hapa kimaadili ndipo linapokuja tamko la TCRA kwa ITV. Kiufupi bwana mengi amekosea kwasababu yeye ametumia vyombo vyake kutuhumu watu wengine regardless kuwa anaushahidi au laa....waandishi wa habari wanamaadili mengi lakini moja kuu ni lile la kutochagua upande na kusema ukweli kama ulivyo