Itakuwaje Lowassa akifukuzwa CCM, CHADEMA watampokea?

Itakuwaje Lowassa akifukuzwa CCM, CHADEMA watampokea?

Baada ya Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni super man, nimemkumbuka naomba nimdurusu kidogo, niliwaji kusema nini humu kumhusu mtu huyu.

P.
 
Acha kupotosha umma, Lowasa sio waziri mkuu mstaafu, ni waziri aliyejihudhuru kwa matumizi mabaya ofisi ya umma, huyo ndiye mzee wa richmundi, kuhusu kwenda Chadema, unaota ndoto za alinacha, hiki ni chama cha watu makini.
Wapi umakini?

Aaaasubutu
 
Nyuzi kama hizi, kuna watu wanatamani kufuta kauli 😀🙂😀😀😀😀
 
IDs nyingi za Uzi huu zimetelekezwa. Sio nyumbu sio lb7 wote wamezihepa IDs zao.
 
Duuu hizi nyuzi ni za kinabii. Na hapa ndipo tunapopaswa kuzingatia usemi Wa bakisha maneno
 
Naombeni mnitafutie comment ya Salary slip,erythrocyte kwenye huu uzi
 
"Chadema haiwezi kumpokea fisadi Lowasa"
hawa watu wako wapi?
 
Nilishakumbuka mkuu😀👍🏽 Lakini kiukweli baada ya mengi ambayo umewahi kuyasema yametokea, basi naona giza tororo huko mbele.
Mkuu JMushi, humu jf tuna tatizo la pre conceived negativity, mtu akiisha kuwa mbaya ni mbaya milele. Hata akibadilika watu hawaamini. Japo ni kweli kuna giza tororo tuendako, but there is light at the end of the tunnel.

Mimi nimemfanyia psychoanalysis, nikagundua jamaa ana tatizo la deep rooted neurosis, hivyo ni erratic, lakini kichaa huwa kinacharuka na kinatulia na kuna wakati kinapona. Take it from me,jamaa is changing for the better.
P.
 
Mkuu JMushi, humu jf tuna tatizo la pre conceived negativity, mtu akiisha kuwa mbaya ni mbaya milele. Hata akibadilika watu hawaamini. Japo ni kweli kuna giza tororo tuendako, but there is light at the end of the tunnel.

Mimi nimemfanyia psychoanalysis, nikagundua jamaa ana tatizo la deep rooted neurosis, hivyo ni erratic, lakini kichaa huwa kinacharuka na kinatulia na kuna wakati kinapona. Take it from me,jamaa is changing for the better.
P.
Haya mkuu. Lakini pia unakiri kuwa suala la Tanzania ya viwanda ni blah blah? Maana hapo kwa maoni yangu binafsi, ndipo penye “bottomline”

Kama vitendo vingeendana na maneno, yani tuone mikakati ya ukweli kwenye kutekeleza sera ya viwanda, nakuhakikishia tungesema ukweli tu bila kujali mtu yuko chama gani. Yote yanayoendelea ni kama tumeingia chaka mazima!

Sasa action speaks louder, tuone hatua zinazochukuliwa kuelekea kwenye viwanda. Serikali ina majukumu makubwa sana! Nilidhani wako serious hata aliposema “hakuna siasa”, “hapa kazi tu”, lakini hakuna kinachoonekana.

Ni mambo gani ambayo serikalini imeyafanya ili tuone iko serious? Achilia mbali taarifa za kuhonga wapinzani waunge juhudi mkono, juhudi zenyewe ni zipi? Maana nguvu nyingi na resources vinaelekezwa kwenye kujinaliza sisi wenyewe kwa kujikita kwenye yale yanayotutenganisha.

Kuna incentives zozote ambazo serikali imeweka ili kuencourage viwanda?

Mfano punguzo la umeme, ili kuwapa unafuu wenye kutaka kufungua viwanda, maana umeme ndiyo namba wani! Je kuna punguzo la kodi za kuagiza mashine au vifaa vya uzalishaji viwandani? Urahisishaji wa kupatikana kwa malighafi nk.

Kila siku ni porojo tu na pia watu wanaona kumwaga misifa ndo basi. Hao ni Matumbo yao tu wanayajali. Kamwe hakuna mzalendo anayezidiwa nguvu na tumbo. Kuliko hivyo ni heri asishiriki kwenye hizo siasa.
 
Haya mkuu. Lakini pia unakiri kuwa suala la Tanzania ya viwanda ni blah blah? Maana hapo kwa maoni yangu binafsi, ndipo penye “bottomline”.
Hii Tanzania ya viwanda, naomba nisiizungumze, yule professor wa Ben Saanane aliyemzunguza, baada ya kumuweka kwenye zile tume zake za madini, sasa ndio KM pale!, Mkemia anaende kusimamia industries , trade na investments, wee acha tuu!.

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!. - JamiiForums

Je, Maendeleo ya Kweli ni Maendeleo ya Watu au Vitu?- Wachumi Tusaidieni, Magufuli Analisaidia Taifa au Ataliangamiza?. - JamiiForums

Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa kiuchumi? - JamiiForums
P
 
Back
Top Bottom