Nilishawahi kusikia kuwa jeuri ya EL ni kwamba anawatishia eti wakimtema, ataenda upinzani. Tusije tukawa mbulula tukampokea CCM wakapata credit. Huyu jamaa nadhani ndio katuletea matatizo ya umeme kwa maslahi yake binafsi. Umeme unapanda mara dufu tunahoji tukiwa bar afu tunatulia (tuingie barabara kidogo-tuonyeshe anger). Wenzetu Kenya walipandishiwa bei ya chakula, wakaingia barabarani na mabango, tumekuwa wabinafsi sana.
Lowassa leo anazunguka nchi nzima na gia yake kubwa ni ruswa kwa watanzania maskini na bodaboda. Na matatizo mengi tunayoyapata, kielimu(shule za kata), kiuchumu (ki-umeme) yalikuja akiwa PM, leo aje upinzani tumpokee. Tutakuwa waroho wa madaraka.