Itakuwaje Lowassa akifukuzwa CCM, CHADEMA watampokea?

Itakuwaje Lowassa akifukuzwa CCM, CHADEMA watampokea?

hawawezi kumtimua very likely ataamua kutoka mwenyewe kama wasipopitisha jina lake
Njooni tena myarudie yale mlio yasema
Acha kupotosha umma, Lowasa sio waziri mkuu mstaafu, ni waziri aliyejihudhuru kwa matumizi mabaya ofisi ya umma, huyo ndiye mzee wa richmundi, kuhusu kwenda Chadema, unaota ndoto za alinacha, hiki ni chama cha watu makini.
 
Baada ya kuzisoma comments za wachangiaji hapa na kufananisha na michengo yao ya hivi sasa nilibakia kucheka tu....
 
CHADEMA kwa sasa hawapokei "viongozi" toka CCM, hivyo Lowassa hawezi kujaribu kuomba kujiunga CHADEMa.

Ila wanachama wa kawaida wa CCM wanaoguswa na elimu ya uraia pamoja na kuzinduliwa toka usingizi wa ujinga, maradhi, ufisadi na kulindana (hivyo kukosa uzalendo na haki zao za msingi) hao wataendelea kupokelewa kila iitwapo leo.
Uliona mbali sana
 
Acha kupotosha umma, Lowasa sio waziri mkuu mstaafu, ni waziri aliyejihudhuru kwa matumizi mabaya ofisi ya umma, huyo ndiye mzee wa richmundi, kuhusu kwenda Chadema, unaota ndoto za alinacha, hiki ni chama cha watu makini.
Rudia kaulii hii tena kaka tusikie
 
Nilishawahi kusikia kuwa jeuri ya EL ni kwamba anawatishia eti wakimtema, ataenda upinzani. Tusije tukawa mbulula tukampokea CCM wakapata credit. Huyu jamaa nadhani ndio katuletea matatizo ya umeme kwa maslahi yake binafsi. Umeme unapanda mara dufu tunahoji tukiwa bar afu tunatulia (tuingie barabara kidogo-tuonyeshe anger). Wenzetu Kenya walipandishiwa bei ya chakula, wakaingia barabarani na mabango, tumekuwa wabinafsi sana.
Lowassa leo anazunguka nchi nzima na gia yake kubwa ni ruswa kwa watanzania maskini na bodaboda. Na matatizo mengi tunayoyapata, kielimu(shule za kata), kiuchumu (ki-umeme) yalikuja akiwa PM, leo aje upinzani tumpokee. Tutakuwa waroho wa madaraka.
Ulipiga kura? Na uliyakumbuka haya? Au nawe ulipitiwa na mafuriko yasiyo na muelekeo
 
Akifukuzwa azunguke aeleze namna ilivyoshiriki kuhujumu nchi kwenye richmond na EPA, halafu baada ya hayo astaafu siasa tu akafuge mifugo yake Monduli..
Nahisi kuna watu mmeshabadili na majina
 
Kwa uroho wa madaraka alinao hasa nafasi ya urais ataanzisha chama chake haraka na kukisajili haraka hata kama ni wanachama wake ni masai wa zanzibar na atatoa rushwa kwa msajili atagembea urais na kama akishindwa ataenda mahakamani kudai atangazwe rais halali wa nchi
Uliona hebu rudia tena
 
Back
Top Bottom