Issue ya Mikopo ya Elimu ya Juu itamharibia sana rais Magufuli

Issue ya Mikopo ya Elimu ya Juu itamharibia sana rais Magufuli

Lowasa alipowaambia elimu bure mpk chuo kikuu mlimwona kenge ni mgonjwa anatetemeka.sasa tutaimba wote wimbo mmoja tu!..mtalimia meno.
Huyu mzee aliposema ELIMU ELIMU ELIMU watanganyika wengi hawakumuelewa kbs sasa athari za kutokumchagua zinatutafuna watanganyika Mungu akupe maisha marefu mzee Lowassa
Jaman umenikumbusha uchungu, mkali Sana, nife au nibaki jaman, uwiiiiiiiiieeee yeuwuiiiiiiioii, auwiiiiii bora nife
 
Juma kashindwa kuongoza, sema zigo la lawama wataangushiwa Bodi ya Mikopo, na hali ikiwa mbaya Mkurugenzi wa Bodi atatumbuliwa, Mtukufu ye hakosei!
 
Good kumbe umeamini kama hatukumchagua eeh?= tulimpiga chini na si kwamba aliibiwa kura. okay hapo nimekuelewa vizuri sana. la pili umesema yeye alisema elimu elimu elimu yaani wewe kwa mfano unaamini kipi kati matendo na maneno.? alipokuwepo madarakani hakufanya ila yupo upinzani anasema ELIMU ELIMU ELIMU eti unaamini. duh kumbe ndio maana kiongozi wenu ni form.................
Kwani hizi shule unazoona za kata alisimamia Mamaako??...Hilo ni swali usikereke maana unaudhi kujifanya kipofu na kiziwi kutoelewa Adha watu wengine wanayo/watakayopitia..
 
Ushauri kwake Mhusika Mkuu.

Yeye katoka Familia Masikini, anajua changamoto vizuri.

Ebu basi wangetangaza mapema sasa vyuo vimeshafunguliwa, halafu unatangaza mabadiliko sasa wanafunzi na wazazi wao watafanya nini harakaharaka hivi?. Au mnataka Watoto wa kike waendelee kujiuza au waoolewe bila kupenda zile ndoa Colleteral Marrige?. Taarifa zimekuja late sana na vyuo tayari vimeshafunguliwa. Ivi mkikaa Wasomi wenzetu mnawawaza Masikini wa Kitanzania kweli. Hili jambo mshaurini mkubwa alibadirishe haraka iwezekanavyo.
 
"Mimi nikiwa Rais mtalima kwa meno" ( By John Pombe Magufuli - akipiga stori na best yake Kitwanga)
Mkuu hivi haya maneno ni kweli alisema au watu wanatania??kama ni kweli aisee basi acha niishie hapa nitaitwa mchochezi.
 
Vyuo vya elimu ya juu vimefunguliwa huku wanafunzi wengi wakiwa njiapanda kuhusu mikopo yao ya ada pamoja na chakula na malazi. Suala la means testing kwa mwaka huu limekuwa tight sana kiasi kwamba kuna wanaojuta kuomba kudahiliwa na vyuo kwa sababu hata ule mkopo wa chakula na malazi hawapewi wengi wao na huwezi kusajiliwa chuoni bila kulipa angalau ada ya semester moja!

Serikali inasema inaweka kipaombele kwa baadhi ya kozi/fani,fine bt ni asilimia ndogo saaana ya wanafunzi wanaochukua fani hizo za kipaombele ukilinganishwa na wengine,haiwezekani wooote wasome Petroleum Engineering,architechture,medicine,anatomy, and the like!

Na wengi wa watoto wa maskini ndo hawa waliosomea shule za Kayumba ambako Physics na Biology ni msamiati mgumu sana so walilazimika kusoma masomo ya arts ili waweze kufaulu kwa sababu ya kukosa walimu wa sayansi na miundombinu ya maabara.

Nionavyo mm,pesa nyingi inatumika zaidi huku kwenye 'ELIMU BURE',hali ikiwa mbaya zaidi hawa wanafunzi wa elimu ya juu wanaweza kugoma na hii itamletea shida kubwa sana JPM. Naomba washauri wake mliopo humu #JF mumfikishie salamu hizi,watoto wengi wa maskini ndo waliosoma masomo ya arts na ndo wanaokosa mikopo.
Hapokei ushauri wa mtu na anaomba malaika azime hii mitandao yenu ili kuepuka maoni kama haya .
 
Mtapata mtakacho 2019,mtafurahi na kushangilia !! Kwa sasa sorry!
 
wabongo bana,hapa kazi tu tumetenga trilioni moja kwa ajili kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa,elimu ya msingi ni bure,elimu ya chuo mjisomeshe hakuna hilo fungu maskini nyie,jitu linalalamika halijapata mkopo halafu halifanyi kazi,fanya kaziii
 
ACHA KUDANGANYA WATU. Itamuangusha kivipi? Wanaopata mikopo hiyo miaka yote wamekuwa mashabiki wa upinzani au kutopiga kura kabisa. Kwahiyo msitutishe. Magufuli 2020 atapita kwa ushindi wa SUNAMI NA KISHINDO KIKUBWA AMBACHO HAKIJAWAHI TOKEA. Wananchi wengi hata wa upinzani wanamuunga mkono Magufuli. Kama mleta mada umekosa mkopo nenda kalime. Usipoteze muda mwingi kuleta vitisho vyepesi kama hivyo. Hata usipompigia kura sawa tu. Tuna stock ya kura nyingi 2020.
Akili ndogo inapoongoza akili kubwa. Wewe ni hasara hata kwa mama yako mzazi !!!!
 
Salary Slip Msambichaka Mkinga mimi nakubaliana na ninyi . Ujue kuna watu wanataka kumlaumu JPM bila sbb zenye mashiko. Tukumbuke ya kwmba mhe. Rais alishasema ya kwmba elimu bure mwisho ni form four tu. Sasa nashindwa kuelewa watu sasa hivi kwa nini wanamlamu mtukufu Rais?? Tukumbuke ya kwmba JPM aliahid ahadi nyingi sana wkt wa kampeni. Sasa tumpe muda na nafasi ili aanze kuzitekeleza hizo ahadi zake.
 
Tatizo hamkumuelewa vizuri mheshimiwa haiwezekani mtu ametumia gharama hadi akahitimu na kufaulu masomo ya sayansi vizuri halafu akose mkopo wakati nyinyi wa masomo ya Sanaa ambao wengi wenu ni pangu pakavu mtake nanyi kufaidi mema ya bodi ya mikopo...sasa ni zamu ya sayansi..sayansi...uhandisi..teknologia wengine tutasamehana kwanza...kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake,kama serikali tunasema tuna mambo muhimu ya ku deal nayo hili muwe wavumilivu..
Mikopo ilianzishwa kwa ajiri wasiojiweza sasa mambo ya sayansi ni ujinga tu maana akija mwanasheria atasena sheria iwe kipaumbele , nazani asiyejiweza apewe mkopo full stop
 
Mbara mbara tu, zaidi yakipiga ng'ombe na kukatana mapanga hakuna jingine wanaloweza
 
...unampigia mbuzi
violin.png
 
Naona kuna NG'OMBE wanasema eti shahada za fani za Arts zimetosha, pumbavu kabisa! Kwa hiyo kuelekea uchumi wa viwanda tunahitaji madaktari na wakemia pekee tu? Hatuhitaji wataalamu wa masoko, uchumi, sheria nk? Elimu ya juu sio option ni suala la LAZIMA kwa taifa lolote linalohitaji kupiga hatua.
Ndio na mini sielewi tuliowapa madaraka kama wanatumia vichwa kufikiri
 
Ukajiuze wapi, kama umepata kidogo Tumia vizuri, Mimi nilianza chuo kwa kukosa hostel, ikabidi nipange pale survey miaka minne bila hata kulipiwa na mzazi maana hakuwa na uwezo hata wa kunipa nauli kuja Dar, Na wakati huohuo natakiwa kulipa ada na direct cost, kimsingi maisha yalikuwa magumu sana ila yanahitaji uvumilivu sana , lazima ujikatae kwa kujinyima then utafika. Na hata nilipo hitimu chuo mwaka jana na ajira nazo zikapigwa stop . My take watoto wa maskini tunateseka ila tuwe wavumilivu tutafika ndoto zetu.
Zamani boom lilikuwa mnapewa sawa sasa nasikia nalo lina % mzee
 
A means test is a determination of whether an individual or family is eligible for government assistance, based upon whether the individual or family possesses the means to do without that help.
Hii "Means testing" sijaielewa kabisa naomba msaada wenu.
 
Back
Top Bottom