Issue ya Mikopo ya Elimu ya Juu itamharibia sana rais Magufuli

Issue ya Mikopo ya Elimu ya Juu itamharibia sana rais Magufuli

Watanzania ni muhimu kuwa na msimamo. Tulipomchagua JPM hatukumchagua kwa sura yake wala Lowasa hatukuacha kumchagua kwa sura yake bali kwa yale ambayo wangeyasimamia.

Haya mambo ya elimu bure hayakuwemo kwenye ilani ya JPM japo aliyatamka jukwaani. Serikali hii inaongozwa na msimamo wa kutobembeleza mtu yeyote eti tu kwaajili ya kumfurahisha, ndiyo maana wale wa tetemeko wameambiwa wazi serikali haitamjengea mtu nyumba, kama umenusurika, jenga mwenyewe. Kama wewe au mwanao hakuchagua masomo ya kipaumbele, ajisomeshe au mzazi amsomeshe au la aache. Hayo mambo ya kusema watoto wa maskini ndiyo wanaosoma masomo ya arts, siyo sababu ya kuvuruga vipaumbele vya serikali hii ya kujenga uchumi wa viwanda na gas.

Kwa kawaida unapopiga kura kumchagua mgombea fulani au chama fulani, tayari umekwishachagua aina ya maisha unayoyataka. Na wale waliokuwa wamemchagua mwingine kwa sababu hawakuyataka maisha ya sasa, ni bahati mbaya wale walioyataka maisha haya ya sasa walikuwa wengi, mnalazimika kuwaunga mkono.

Ninawashangaa wale walioyachagua maisha ya sasa, halafu wakati wa utekelezaji wanaguna. Kwa nini wanakuwa vigeugeu? Sisi wengine tumekwishaukubali ukweli kimwili, kiroho na kifikra. Hata wakiundoa moja kwa moja, kusiwepo hata mkopo wa shilingi hata 1, hatutalalamika kwa sababu tunajua vipaumbele vya serikali hii, viwanda kwanza. Elimu baadaye, afya kesho, michezo keshokutwa. Mafanikio ya maisha ni kuwa flexible kufuatana na wakati na mazingira.
 
Safi sana Magu , endelea kuwanyoosha , tulipowaambia wasikuchague walituona wapiga deki baarabara , yaani nafurahia kwa kila baya linalotokea nchini either linilenge au lisinilenge ......Kaza buti Baba jsca wanasema tulizoea vya bureeeee
 
Taifa kusomesha watu wake sisitafsiriwe kama ujasiliamali. Hii ni huduma ndo tatizo linaanzia hapo. Kikichotakiwa ni sirikali kugharamia elimu iache longolongi


si ndio hapo mkuu,sijui kinachoshindikana ni nini wakati kuna nchi za scandinavia kama finland zinatoa huduma hii ya kuwapa elimu raia wake bure hadi chuo kikuu bila kudaiwa chochote,naamini tuna rasilimali za kutosha sana kugharamia zoezi ili,kama serikali inaona elimu ni ghali basi ijaribu ujinga
 
Hao wote wanaoingia chuo kikuu sasa hivi, mwaka jana walipiga kura kumchagua rais, na alishasema elimu bure mpaka kidato cha nne, fullstop. Na mpo mliompigia kura.

Kuendelea mbele lazima uzame mfukoni.
Anatimiza ahadi aliyotoa kikamilifu. Tena mnyamaze nisiwasikie mkilalamika. Ole wenu mkaandamane huko chuoni, hakuna kuleta askari mwenye kirungu, ni askari mwenye bunduki. Umeshindwa mwaka huu, subiri 2020, chuo kikuu hakihami.
 
"""Viwanda kwanza elimu baadaye""
Na mtanyooka tu
Mamvi alisema elimu bure mpaka chuo kikuu ila mkamuona Hana maana
 
Mm ninaona elimu bure itolewe hizo pesa ziende kuwalipia mikopo wanafunzi vyuo vikusasa!jamani watoto wa maskini wanateseka sana kwa hili Rais waonee huruma watoto hawa maskini, hata hili LA kuweka masharti ya kuwa na D mbili form six ndo ujiunge chuo kwa kweli limeumiza sana wanafunzi wetu ila tutafika tu , mungu ibariki Tanzania maana hakuna asiyepata maumivu hata wanaoshabikia kisiasa kama hawajaguswa basi atakuja kuguswa mdogo wako au mtoto wko ambae yupo form one au form three kwa sasa
 
Maajabu no kwamba vyuoni watoto wanatakiwa kuripoti ilihali mikopo ya helsb haijajulikana no Mani kapata kiasi gani. Hii HELSB ni jipu linalohitaji kutumbuliwa haraka. Hapa hawajafikia target benchmark ya kazi yao.
 
Kuna kijana mmoja masikini wa watu alisoma pcb jina la shule silikumbuki na kachaguliwa chuo kimojawapo cha maswala ya afya nje ya dar es salaam,kapata mkopo sawa lakini tatizo linakuja chuoni huko alikochaguliwa maana sehemu ya ada na fedha zote anazopaswa kujilipia ni kama milion hivi na kwa uwezo wa familia yake hyo pesa ni msamiati!!!Kijana wa watu kaenda chuo kuwaelewesha na kuwaomba wamsajili hyo pesa itakuwa analipa kidogokidogo kwa kujibana kutoka kwenye mkopo wake lakini chuo KIMEMKATALIA yaan daah inaumiza sana.
Kaamua kuhairisha mwaka kusudi mwakani aombe ualimu
 
Ukajiuze wapi, kama umepata kidogo Tumia vizuri, Mimi nilianza chuo kwa kukosa hostel, ikabidi nipange pale survey miaka minne bila hata kulipiwa na mzazi maana hakuwa na uwezo hata wa kunipa nauli kuja Dar, Na wakati huohuo natakiwa kulipa ada na direct cost, kimsingi maisha yalikuwa magumu sana ila yanahitaji uvumilivu sana , lazima ujikatae kwa kujinyima then utafika. Na hata nilipo hitimu chuo mwaka jana na ajira nazo zikapigwa stop . My take watoto wa maskini tunateseka ila tuwe wavumilivu tutafika ndoto zetu.
Hata hicho kidogo sina....nipo tu namsikiliza Goodluck Gozbert....ipo siku yangu tuuuuuuu....
 
Acheni kulalama kama watoto Wa kambo
Mkuu unapata wapi ujasiri wa kuwaita wanalalama kama watoto wadogo?. Je unaona busara kuufumbia macho ukweli?. Jitazame Mara mbilimblili huenda hili suala halijakugusa au kumkuta ndugu yako.Usingesema maneno hayo.
 
Ngoja nipitie yale matokeo ya utafiti ili nijuwe dalili za awali za mtu kuwa kichaa ni zipi,nakumbuka tuliahidiwa hili na maelfu ya vichaa walishangilia pale Tabora.Iko wapi ahadi ya mh?Tusilaumu sana,tumeambiwa katika kila watanzania 4,1 ni kichaa.
Asante Kwa hy video...duuh Yaan naishiwa pumz...kwel siasa ni si hasa
 
"Mimi nikiwa Rais mtalima kwa meno" ( By John Pombe Magufuli - akipiga stori na best yake Kitwanga)
 
Aliangalie kwa jicho la tatu,maana aliwaaminisha wanafunzi wote watapata mikopo kwa minaji kuwa wamepandisha grade za kudahiliwa vyuoni sasa walichofanya watapeelekea wanafunzi kutosoma
 
Back
Top Bottom