kamili
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 1,219
- 855
ni uongo.wakati fulani nilibahatika kutazama program fulani ya cnn ambayo ilikuwa inaonyesha safari za rais bush kwenye eneo la mashariki ya kati. Walionyesha mojawapo ya safari za hatari ambazo bush amewahi kufanya akiwa na airforce one. Msimuliaji alieleza namna vyombo vya ulinzi vya jeshi la anga la marekani vilivyokuwa vinahangaika masaa 24 kuhakikisha kwamba ndege ya rais inakuwa salama wakati wote. Sasa kilichonishangaza ni kwamba eti fursa pekee ya kupumzika ambayo wanajeshi wa jeshi la anga la marekani walikuwa wanapata ni wakati ambapo ndege ya rais imekanyaga ardhi ya israel. Kwa maneno mengine, wamarekani wanauamini sana ulinzi wa israel.