Mkuu Bube naungana na wewe, ukiangalia simple logic ni kuwa Air force one inalindwa popote inapotua, iwe Washington DC, Tel Aviv, Dar au Arusha. Kwa hiyo si suala la kujadili, si kweli kwamba Israel ni most safe place duniani. Rabin alipigwa risasi akiwa analindwa na kidon na Mossad, kuna magaidi wa kiyadi ambao hata serikali ya Israel inapambana nao, Israel pia kuna magereza ambayo wayahudi pia wanafungwa. Kismingi ni sehemu sawa kabisa na sehemu nyingine, jews are humas just like you and me. Kushambulia ndege zikiwa uwanjani kama walivyofanya Israel kwa Misri au Tamil Tigers walivyofanya pale Colombo ni jambo moja, na kutungua ndege ni jambo lingine. M-nazi alichosema ni ushabiki tu, ni point isiyo na maana.
Issue hapa kuna watu wanaoitwa walokole, ambao wanashindwa kutumia simple logic (wanatumia unazi) kuona kuwa Israel ni nchi ndogo ambayo haiwezi kuishi yenyewe na kujilinda bila msaada wa wakubwa, au bila kuheshimiana na wengine. Marekani pamoja na kuwa na jeshi bora zaidi duniani, kila siku inasema nguvu yake ipo kwenye values na ideals, kwa hiyo silaha au jeshi peke yake si kitu. Ndio maana Marekani inawapa wasaudi na wamisri mabilioni ya dola kila mwaka kuhakikisha kuwa wanailinda Israel. Sio kuwa Israel inawapa Marekani hela, au inawapa Saudia na Misri hela. Wanasoma kweye biblia wanadhani kile kilichoandikwa mule ndio reality kuhusu Israel.
Mkuu ukinaimbia nichague sides kati ya Israel na Iran, ntachagua Israel kwa sababu binafsi. Lakini ni kweli Israel inaweza ku deal na Iran? peke yake? ni kweli IDF ni best military in the world? au ni kweli Israel ni super power duniani? ni kweli unaamini kuwa Israel ni taifa teule? Kama Israel ni taifa teule then why the hell mataifa mengine are we doing on earth. Kama Mungu amewateua wao who are we here, wasindikizaji tu? au ni kama mbuzi na kuku? Ina maana hatuna maana kabisa, hata walokole ambao wamejiteua wenyewe pia nao hawana maana. Sidhani kama Mungu anaweza kuwa na maana hiyo. This is very simple logic, it does not need research or college degree.
Point anayo-make Nyani Ngabu ni very simple. Bila US Israel haiwezi kudeal na threat ya Iran, na US is a million times better than Israel, ni simple facts za ku google na kujua ukweli. Tatizo ni kwamba walokole are so myopic, wao source yao ya elimu ni biblia hata hawajui kuwa Biblia iliandikwa miaka 2000 iliyopita, kuna mambo mengi yamebadilika. Bible ilipoandikwa US as a country haikuwepo, na ukiangalia kwenye bible "ramani ya dunia" ya wakati ule na ramani ya dunia tuliyonayo leo unaweza kuona tofauti sana. Ndio kuna wachache wana elimu ya juu sana, lakini hao wachache hawawzi kuwabadilisha mamilioni waliopo. This is the fact which walokole do not want to admit.