libya mmarekani alikwenda fasta fasta huko syria anaogopa kwa sababu ya mrusi
ni makosa kuilinganisha marekani na israeli, mmarekani ni wa kumlinganisha na mchina na mrusi labda na nato
Asilimia 65 ya NATO ni Mmarekani!
Imeandikwa kuwa, kila atakayeilaani Israel atalaaniwa, na kila atakayeibariki atabarikiwa. Endeleeni kupata laana na warabu wenu. Poleni sana.
Imeandikwa wapi hiyo? Marekani ilipe fadhila kwa kichw kimoja cha kisayansi kwa miaka yote? Do your homework brother... huyo Albeto eistein a; myahudi hivyo marekani inalipa fadhila mpaka kufa!
Mleta mada kasema mumpe ushahidi wa hizi nadharia, kwa sababu kuongea tu bila ushahidi haileti maana...utake ustake uchumi wa marekani wameshika wao! wanatoa mfuko wa kulia wanaweka kushoto!
..Na hao marefa ndiyo wanaoifanya inaonekana ina ubavu wa kushindana katika vita, ilhali hali si kama hiyo. Kwa hoja hiyo, unakubali kwamba Israel bila 'kuomba omba' kwa marefa (Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya) si lolote wala chochote. Iwapo Israel wameshindwa kutokomeza kikundi kidogo kisicho na serikali cha Hizbollah, kikiongozwa na Hassan Nasrallah, wataweza kweli kupigana na 'nchi' yenye uwezo wa kuleweka kivita?.... Kwa Asilimia kubwa ISRAEL ana Marefa wengi sanaaaaaa
I second the idea.....On the other side, Iran si wa kupuuzwa hata kidogo, na kuna karespect flani hivi wanapewa na haya mataifa, kwanza wanajuwa uwezo wao kupitia Hizbolah pamoja na Syria, Bashar amepewa msaada wa unmaned drones from Iran.Israel peke yake vs Iran itabidi wawe makini sana.
Pole sana. CNN na BBC inaonesha zimekuharibu sana.Hakunaga MBABE kama Israel.
Hakuna kosa. Ila kuna watu humu bila hata soni eti wanasemaga Israel ni zaidi ya Marekani katika kila kitu ikiwamo uchumi, nguvu za kijeshi, influence, na kadhalika, kitu ambacho si cha kweli hata kidogo.
HATA Mwingireza akienda US anajisifia katoka STATES bana.....
Kwa mtu asiyejua siasa za mashariki ya kati anaweza kushawishiwa na ulichoandika. Kumbe ni UTUMBO tu. Nani asiyejua kuwa Jeshi la Israel (IDF) ndiyo jeshi makini zaidi na committed kuliko jeshi la taifa lolote duniani including Marekani! Ukisoma historia ya IDF na mambo waliyofanya maeneo mbalimbali duniani utabaki kinywa wazi na kama una akili nzuri utajiuliza kama matendo hayo yalikuwa yanafanywa na binadamu au la. Ipo mifano mingi sana mojawapo ikiwa ni 90 minutes to Entebbe na kulipuliwa kwa ndege za kirusi zikiwa Egypt zikijiandaa kushambulia Israel. Endeleeni kujipa moyo kwamba Israel hakina kitu wakati mataifa yote ya kiarabu pamoja na hasira zao za kujitoa muhanga, wameshonwa mdomo na hawakohoi hata sekunde mbele ya wayahudi.
Taifa la israel linalozungumziwa kwenye biblia ni wale wacha mungu wote pasipokujali huyu ni muha, msukuma au muyahudi. Tatizo mtu akisoma biblia anachukulia jinsi ilivyo bila kutafakari. Sasa kama ni Taifa teule basi wale waha wakigoma ni Taifa laaniwa na hamna hata haja ya kusali kwa sabab wote wataenda moton kasoro waisrael ambao wataenda mbigun hata kama walikuwa mashoga
Wengine wanadhani hata waziri Mkuu wa Israel ni Musa, na waziri wa Fedha ni Yuda eskarioti.
Does this say anythings in relation to America and Israel ? Out of over Eigh hundred Nobel Prizes awarded to date 20% of the Nobel laureate are JEWS, although JEWS population comprise of only 0.2% of the world's population. kama Noble prize kwenye nyanja zote muhimu hawa jamaa wanazo wao,haina maelezo nyuma ya pazia kuonyesha kuwa wao ndiyo vinara wa technologia ya marekani ikiwa ni pamoja na uchumi wao ? wanaweza wakawa dhaifa kitechnologia ndani ya Israel lakini wana access na technolojia yao iliyoko Amerika...
Mkuu jaribu kutafuta mlokole yoyote kaa naye muulize maswali kuhusu Israel halafu umsikie, unaweza kuona hata huruma. Mpaka leo kuna watu wamejipa majina ya kiyahudi halafu wanajiita wakristo, kuna wengine wanasema Israel ni taifa teule na wanaona hata mataifa yao yamelaaniwa. Kibaya zaidi angalia hawa watu wanaoisifu Israel wanavyofanywa wakienda huko Israel kwenyewe, wengine wanatukanwa hadi utacheka. Unajua hili ndio tatizo la umaskini, Bible inapitkana bure kwa hiyo ndio source of education kwa walokole, bila kujali ni education ya mwaka gani. Wengine wanadhani hata waziri Mkuu wa Israel ni Musa, na waziri wa Fedha ni Yuda eskarioti.
Source(s) please....
jewish virtual library
Una hasira na walokole hadi basi,kuna wakati Musa amewahi kuwa waziri mkuu wa Israel au Yuda Eskariot kuwa waziri wa Fedha ? ungesema wanadhani bado mfalme Daudi/Suleiman au pontio pirato bado wanatawala ukgemaanisha kweli,njee ya hapo nawe kama unachemsha vile. Ukiwalaumu unawaonea bure,mambo ya imani at times watu wanakuwa kama mazombies mbele ya watu waaminio tofauti na wao.