Iramba: DC Suleiman Mwenda aagiza walimu wanaodai fedha za uhamisho na madai mbalimbali kulipwa stahiki zao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,895
940

DC MWENDA AAGIZA WALIMU WANAODAI FEDHA ZA UHAMISHO NA MADAI MBALIMBALI KULIPWA STAHIKI ZAO.

Na Mwandishi wetu:

Mkuu wa wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda amewaagiza maafisa Elimu msingi na sekondari kuwalipa walimu wanaodai stahiki zao mbalimbali. DC Mwenda ameyasema hayo wakati akiongea na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wake ulioitishwa kwa lengo la kujitambulisha, kusikiliza na kutatua kero za wananchi na watumishi katika mkutano uliyofanyika Kijiji Cha Tyegelo, kata ya Kidaru.

DC Mwendai alizitaka idara za elimu Msingi na Sekondari ziweke kipaumbele katika kuboresha mazingira ya shule za ukanda wa kidaru kwani walimu wanaivumilia sana serikali na wanafanya kazi katika mazingira magumu. Pia wahakikishe wanawapa kipaumbele walimu wa Luono, Ndurumo na Mwamapuli kwani mazingira wanayofanyia kazi yana changamoto nyingi sana.

Kwa upande wake Afisa elimu Msingi ndugu. Frank Samike alimuhakikishia Mkuu wa wilaya kuwa idara ya elimu Msingi ina mkakati wa kumaliza vyumba vya madarasa shule ya msingi Mwamapuli na kipindi bajeti ikiruhusu watajenga nyumba za walimu ila aliwashauri wananchi kuanzisha boma alafu waje kulimalizia. Kuhusu madai ya walimu, Ndugu. Damian Machemba (Afisa elimu vifaa na takwimu) aliwaambia watumishi waliohudhuria mkutano huo kuwa Serikali imeleta fedha mwishoni mwa mwezi Julai na wajinaandaa kwa ajili ya kulipa madeni ya walimu wote wa idara ya elimu msingi na sekondari. "Ninaomba nikuhakikishie kama ulivyooagiza Mhe Mkuu wa wilaya tutaanza kulipa walimu wa kata hii kama ilivyoagizwa kwa kuwa wanaishi kwenye mazingira yenye changamoto nyingi sana" alisema Damian Machemba idara ya Elimu Sekondari

Mkuu wa wilaya amewaomba walimu kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi,wananchi.

Mkuu wa wilaya yupo kwenye ziara ya kujitambulisha, kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika kata ya Kidaru mara baada ya kuteuliwa na Rais Juni 22, 2021

IMG-20210804-WA0025.jpg
 
View attachment 1879867
Maisha haya, mume DC na mke DED

Screenshot_20210803-102711-1.jpg
 
Back
Top Bottom