🧠 Intuition vs Reasoning: Ipi Inapaswa Kuongoza?

Ok.
Kwenye "hamna maarifa kwenye mafanikio hapo nimekukataa".
Hakuna ndio, unayeweza kukataa hili sio wewe tu ila hata tukisema tupige kura humu ndani nusu na robo ya member wote wataikataa hii😂😂 ila ndio hivyo, maarifa yako yahawezi kuamua mafanikio yako, unaweza ukawa na maarifa tele kichwani ila ukafa maskini.
 
Intuition na reasoning zinapaswa kuongoza kwa kutegemeana kulingana na hali unayokabiliwa nayo.

Intuition (Hisia) iongoze kwenye dharura, hatari, na maamuzi ya kijamii au mahusiano ambapo maamuzi ya haraka yanahitajika.

Reasoning (Mantiki) iongoze kwenye maamuzi makubwa ya kifedha, biashara, au mambo mapya magumu yanayohitaji takwimu na utafiti.

Tumia intuition kupata wazo au mwelekeo wa kwanza, kisha tumia reasoning kuhakiki kama uamuzi huo unafaa.
 

Mkuu nimekukubali, upewe medali zako tuu🎖️🏅🎖️🏅.

Just to ask??? Huwa unatumia haya majani(w**d) joking

You are good at reasoning, seems like you got so much time to observe everything that goes around you & you're surrounding. This is the highest level of intelligence someone have. I real like it and love it.

Back to the topic.

Cha kwanza ni INTUITION maana mambo yote huanza ndani ya mtu. ( Mtu ajionavyo nafsini mwake ndivyo alivyo). Kwa hiyo kwa vyovyote vile mtu anavyoonekana nje bhasi na ndani ndivyo alivyo.
Ikiwa mtu alivyo ndani ni tofauti na nje bhasi REASONING yake haipo vizuri.

Binafsi naweza kusema kwamba INTUITION ndio hunipa sababu ya kuREASON.
 
Mimi ndio manaa nauliza hivi vitu haviwezi kufanya kazi kwa pamoja?
 
Naunga mkono hoja
 
Shukran sana mkuu
Vipi hivi viwili haviwezi kufanya kazi kwa pamoja?
 
Shukran sana mkuu umeeleza vyema sana 👏👏
 
Shukran sana brother 🙏🙏
 
Shukran sana mkuu
Vipi hivi viwili haviwezi kufanya kazi kwa pamoja?
Vinaweza na vinapaswa kufanya kazi kwa pamoja kila wakati. Havipingani, bali vinakamilishana.

Wataalamu wa akili wanaita ushirikiano huu "Akili Jumuishi" (Integrated Mind), na hufanya kazi hivi:

Intuition inaleta wazo (The Spark)

Akili yako ya ndani inakupa mwelekeo au hisia ya haraka kuhusu jambo fulani bila kutumia nguvu.

Reasoning inachambua wazo (The Filter)

Akili yako ya mantiki inaingia kati kukagua kama hisia hiyo ina ukweli, ushahidi, au mantiki.

Mfano halisi:

Unapotaka kumuajiri mtu, intuition inakuambia "Mtu huyu anaonekana mwaminifu na mchapakazi", huku reasoning ikikusaidia kukagua vyeti na kumbukumbu zake za nyuma ili kuthibitisha hisia hiyo.
 
Ooh vizuri sana
Unajua unachokifanya brother
 
Lazima tujue kwamba Intuition sio hisia kuna tofauti kubwa. Kusikiliza Intuition pia sio kila mtu anaweza, kama unaweza kuisikiliza na kuitenganisha na hisia zako hii huwa haidanganyi.
Watu wengi tunapenda reasoning sababu unaweza kuwajibika kwa matokeo yake (yani nafanya hiki kwa sababu hii na natarajia matokeo haya).
Intuition yenyewe haina sababu, haiachi kukwambia jambo, ukiiipuza siku likitokea la tofauti ndo unakumbuka aah lakini kuna kitu kiliniambia nisifanye hii. Na inaua reasons zako zote zilizofanya ufanye hilo jambo.
At the end "Fuata moyo wako, usisahau akili yako"
 
Shukran sana mkuu 🙏🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…