Kimsingi swali hili ni zaidi ya 1 lakini nitalijibu kwa namna hii:
Hata hivyo kuna upande wa pili wa shilling wa lawama za hapa na pale toka kwa washiriki wachache ambao ni wazoefu na wapo kwa kitambo hapa.
Nikiulizwa kuhusiana na 'wazoefu wa JF' binafsi naweza kuwataja walau 100 (ninaowakumbuka kichwani) ambao ni 'active' (wapo mpaka sasa) hapa JF na tumekuwa nao tangu 2006 hadi 2009; hawa ndio naweza kusema kuwa ni JF haswa; wao wanaweza kumjibu mtu na huyo anayejibiwa akahisi huenda hao ni moderators; hawa wameona mabadiliko kadhaa ndani ya JF, ya kufurahisha na ya kusikitisha; baadhi ni hawa:
Abdulhalim,
Mkandara,
Kibunango,
Mzee Mwanakijiji,
Sikonge,
Ibrah,
MgonjwaUkimwi,
Ogah,
Kiranga,
Zitto,
Alpha,
Lunyungu,
Halisi,
Shadow,
Mchambuzi,
JokaKuu,
Mpita Njia,
Gembe,
Kakalende,
SMU,
Bongolander,
Questt,
Ngambo Ngali,
Chamoto,
The Boss,
jmushi1,
Semilong,
Kang,
Nyambala,
KiuyaJibu,
PakaJimmy,
Zogwale,
Kinyau,
Saharavoice,
Amoeba,
Ndahani,
Mfamaji,
MAMMAMIA,
Mwazange,
Crashwise,
zomba,
Bujibuji,
Nyani Ngabu,
Mpenda Kwao,
BAK,
Binti Maringo,
Nyamgluu,
Steve Dii,
Desidii,
Mdondoaji,
Mvina,
Kivumah,
Power to the People,
Kisusi Mohammed,
Msanii,
Mafuchila,
FirstLady1,
Fixed Point,
Mbogela,
Balantanda,
Pretty,
TANMO,
Riwa,
Hofstede,
Nemesis,
Kaa la Moto,
Remmy,
MamaParoko,
Mama Joe,
simplemind,
AmaniGK,
Buchanan,
Bramo,
Gbollin,
MwanajamiiOne,
Masaki,
Bubu Msemaovyo,
Freetown,
Amina Thomas,
Choveki,
MwanaFalsafa1,
TIMING,
X-PASTER,
BelindaJacob,
Saikosisi,
MziziMkavu,
Injinia,
Original Pastor,
Preta,
Zion Daughter,
Chamoto,
NGULI,
vivian,
rmashauri,
Susuviri,
MwanaHaki,
Masanilo,
Yegomasika,
Belo,
Mahesabu,
Kaizer,
Gaijin,
King'asti,
MpigaKelele,
Mag3,
Nicholas,
Mlalahoi nk
Hawa, wanaweza kuielezea JF wanavyoifahamu; imepitia kipindi gani; imekumbana na 'challenges' gani na wao wanaona wapi pana kasoro na wameshiriki vipi katika kuhakikisha inaboreshwa.
Malalamiko hayawezi kuisha lakini vema tukatoa ufafanuzi kama ambavyo umeniuliza:
Unajibu vipi hizo lawama kwa kuzingatia mpangilio huu ufuatao:
A]. Sasa hivi kumekuwa na wimbi la washiriki wengi JF ambao wamekuwa wakivamia kwa kasi kwa tabia za ambazo ni hatarishi kwa hadhi ya JF. Kama vile uandishi ambao ni maarufu kutumika kwa njia ya text message, vi thread visivo vya msingi (member anafungua thread kwa kimstari kimoja bila maelezo kama kakurupuka tu) n.k. Mmejipanga vipi kuepusha huu uvamizi/mabadiliko ambayo yanaweza shusha hadhi ya JF?
Kungekuwa na mfano ningeshukuru kwakuwa tungeutumia kutoa ufafanuzi; hata hivyo, niseme uandishi wa ki-SMS ni wa vijana wetu wengi walio vyuoni na walio katika sekondari. Wengine ndio kwanza wamehitimu vyuoni, hili halitokei kwenye majukwaa yote; ni baadhi ya majukwaa kama Jukwaa la Elimu, MMU, ChitChat nadhani na kwenye Jokes. Ni nadra kukuta wanafanya hivyo kwenye siasa, timu ya wasaidizi wetu inajitahidi kufanya uhariri ili maandishi hayo yasomeke na kuweza kuwasaidia wale wasioelewa kilichoandikwa.
Nikuhakikishieni, hili ni suala la msimu tu na litapita tu. Kwa ambao wameitumia JF muda mrefu wanaelewa namaanisha nini kwa kusema hivi.
'Rating' ya hoja ili ionekane si ya msingi inategemeana na anayethaminisha hoja. Hata hivyo, JF ni mkusanyiko wa
JAMII; ni lazima tukumbane na watu wa namna hii, kuwafukuza si kuwatendea haki, kuwafungia si kuwatendea haki pia; ni kuwarekebisha taratibu nao ni wazi watajifunza. Ni wengi wamebadilika, wahariri wetu hujitahidi kuwafahamisha wanaokosea kwa mitindo hii na wengi wanaonekana kubadilika.
Hata hivyo, tumeweka viunganishi vya kuwashtua wahariri wetu ili kama kuna hoja haijakaa sawa watuarifu ili ifanyiwe kazi haraka. Dawa si kuwafukuza wahusika, ni kuwaelekeza kistaarabu, wakikosa ustaarabu basi hawastahili kuwa sehemu yetu, tunawaweka kando kwa kuwafungia! Tunajaribu kujenga Taifa lenye critical thinkers, huwezi tarajia kupata critics bila kuwa na wanaokosea. Naamini kwenye kuwajenga wasio na uwezo wa kujenga hoja katika kujenga jamii yenye kuchambua hoja na matatizo yanayowakabili.
Kitufe cha REPORT ABUSE kikitumika kikamilifu, basi hili litarahisishwa sana.
B]. Kukua kwa JF kutakuwa kumesababisha challenges nyingi upande wa wanachama wachache wa kitambo; kwa mfano naomba ninukuu "JF used to be more of 'WIKILEAKS' kind of, and over the years, I have observed JF undergoing complete 'metamorphosis' into some form of a SOCIAL MEDIA". Unakubaliana na hizi tuhuma baridi dhidi ya JF?
Naam, kukua hakukwepeki; na tunapokua tunakumbana na mengi njiani.
- Kwamba JF 'used to be' lakini bila kusema nani alikuwa anasababisha iwe hivyo 'WikiLeaks' tunazunguka mbuyu. Ni nani alikuwa anaweka hizo 'nyaraka nyeti'? Ameondoka JF? Yupo? Hao niliowataja hapo juu wanaweza kufafanua wana uzoefu gani. The "key guy" is still around!
Nini kilipelekea kuacha kufanya hivi (kusitisha kwa muda)?
- Wengi waliomba tusiendelee kumwaga mambo ya UFISADI, ilifikia wakati watu wakaanza kuichukia nchi yao, hili si lengo letu! Ikumbukwe kuwa mengi yaliyokuwa yakiwekwa JF yaliwekwa na aidha sisi au mtu wetu wa karibu. Ilikuja EPA, Ikaja CIS, Ikaja MEREMETA, Ikaja Deep Green, Ikaja RICHMOND/DOWANS, zikafuatana nyingi kweli; watu wakakosa mwelekeo, wakaanza kuona kama nchi haifai hata kuishi! Nakumbuka mwaka 2008 ilitolewa tip juu ya fedha zilizofichwa Uswiss, ni wachache walioelewa; wengi walishakata tamaa, walishachoka kusoma habari za UFISADI au wizi wa aina yoyote. Limekuja kuibuka 2012, linaonekana ni jipya. Watu hawakujiuliza, tuna majina ya watu hao? Tuna details gani? Walitaka kujua tuhuma za mwanzo zinafanyiwaje kazi au ndio tunaendelea kupiga kelele lakini hakuna anayejali.
JF isilaumiwe kwa hili, kila mmoja achukulie kuwa kulinda rasilimali za nchi ni jukumu letu sote.
- Hatujasitisha moja kwa moja, kuna mengi yameibuliwa JF tangu hiyo 2008/2009. Naelewa, wengi hawajajua watayaona vipi, siku takribani 90 zijazo yataonekana kirahisi na ndilo hili tunalifanyia kazi kuhakikisha JF inakuwa rahisi kutumiwa na wengi na ikiwezekana na kila mtumiaji.
- Watanzania wengi ni waoga, nahisi wengine kupitiliza; hata jinsi ya kuelezea inakuwa vigumu. Kuna nyaraka kadhaa zilikuwa zikiwekwa JF, wao wanaogopa hata kuzipakua (download). Inaweza kuchekesha lakini ndiyo hali halisi.
- Habari za 'UFISADI' kwa sasa ni kama zimezoeleka masikioni mwa watanzania, si habari tena! Wengi wamekata tamaa, hata ukiweka ni wachache sana wanaozisoma! Woga umeenda mbali, hata kusoma thread ambayo ina 'sensitive' data mtu anasoma akiwa aidha amejificha au akiwa na wasiwasi mwingi.
Watakuita 'Jembe' lakini ikitokea ukapata matatizo kila mtu atadai 'nilijua tu' au 'anaonewa' lakini hawatachukua hatua kivitendo kuhakikisha unatoka matatizoni! Ndivyo tulivyo.
C]. Ni kwa kiasi gani msemo wa mahala penye uhuru wa kuongea (where you dare express openly) inazingatiwa katika Jamii Forums?
Ni vigumu kujibu hili, lakini anayelalamika huenda hajasoma Sheria za JF. Zipo kila sehemu na ziko wazi kabisa.
Napendekeza mtu asome hii thread -
JamiiForums' Community Engagement Guidelines imesheheni mengi yanayojibu maswali juu ya hili na juu ya mengine ambayo huwa naona watu wanauliza hapa JF.
D]. Kuna madai toka kwa members baadhi kuwa kuna habari nyeti zinaletwa hapa jamvini lakini ndani ya muda mfupi zinafutwa bila maelezo ya kutosha; inayowatia mashaka baadhi ya hao members; unasemaje kuhusu hili?
Kama nilivyojibu hapo juu; wengi hawajasoma hiyo link niliyotoa. Ufafanuzi juu ya hili umetolewa hapa:
Topic gani hufungwa au kufutwa kabisa JF?