JamiiTalks Interview with Maxence Melo: The story of JamiiForums - history and operations of the platform

Status
Not open for further replies.

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Mkuu hio post yako naishukuru kwa majibu yako. Niwe wazi kuwa nitaisoma kesho na kujibu pindi pale ambapo tutaendeleza mjadala huu na kumalizia kipengele cha pili cha swali # 7.

Naomba ruhusa niweze pumzika mjadala ufungwe hadi hapo kesho tena tutapopata muda unaowiana kama ilivokuwa leo. Natanguliza shukrani kwa majibu na ushiriki wako katika mahojiano haya. Naomba nikutakie mapumziko mema.

Pamoja Saana.
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Maxence Melo kwa mara nyingine tena naomba nikukaribishe tuendelee na mahojiano. Nikianzia pale ambapo tuliishia jana, naomba niseme yafuatayo:

Kwanini CHADEMA & CCM tu?
Hapa maoni yako yalihitajika zaidi kwa kutumia CHADEMA & CCM sababu swali lilihitaji zaidi ujibu kwa kutumia hivi vyama viwili ambavo ndio vina matumaini ya kuweza chuana vema na kutoa Ki/viongozi wengine uchaguzi mkuu ujao (2015). Kwa mtazamo wangu binafsi tunapoongelea Vyama vya siasa nchini akili yangu moja kwa moja hugotea katika hivo vyama viwili.

Naomba nishukuru pia kwa hicho 'kiunganisho' cha majadiliano ya kipengele cha dini. Nikiri kuwa sikutegemea kuwa kuna watu mwaka 2007 waliona mbali kwa kuona kuwa kuna suala zima la 'Udini' ambalo linakuwa katika nchi yetu ambayo ni maarufu kwa Amani.

Kinachofuata ni kipengele cha pili cha swali la 7.

Swali # 7 (kundi B)

D]. Kumekuwa na kukuwa kwa habari za ziwa Nyasa inayotokana na madai ya Malawi kupitia rais wake Bi. Joyce Banda kuwa ziwa lote ni la Malawi na hali Tanzania tunatambua kuwa ni letu pia. Ni nini msimamo wako juu ya hili? Unaridhika na hatua ambazo zimechukuliwa na Serkali yetu kupitia wawakilishi ambao ni viongozi wetu?

E]. Swali la kizushi, Naomba utaje moja ya kitu ambacho unaona ni sifa kuu katika personality ya Mheshimiwa Rais JK na Mheshimiwa DK. Slaa.
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
D]. Kumekuwa na kukuwa kwa habari za ziwa Nyasa inayotokana na madai ya Malawi kupitia rais wake Bi. Joyce Banda kuwa ziwa lote ni la Malawi na hali Tanzania tunatambua kuwa ni letu pia. Ni nini msimamo wako juu ya hili? Unaridhika na hatua ambazo zimechukuliwa na Serkali yetu kupitia wawakilishi ambao ni viongozi wetu?
Suala la mgogoro wa Ziwa Nyasa (wao wanaliita Ziwa Malawi) bado liko katika mjadala; ni mapema sana kuliongelea kwa mapana.

Nirudie, tangu mapema kabisa hapa JF kulikuwa na hoja iliyokuwa inaashiria kuwa suala hili japo halijaibuliwa huenda likaibuliwa; ukisoma hii thread ya Oktoba 2007 (takribani miaka 5 iliyopita) utabaini kuwa wengi walishaonyesha wasiwasi wa kuweza kutokea mgogoro uliopo sasa, juhudi za kidiplomasia zingechukuliwa mapema na siasa zikawekwa kando basi huenda huu mgogoro usingekuwepo:

Ref: Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

Nayaheshimu sana maamuzi ya Tanzania na Malawi kukaa kutatua mgogoro huu, nashauri tuwape muda lakini tukisisitiza kuwa wawakilishi wetu watambue jukumu la kila mtanzania kuilinda mipaka yetu.
E]. Swali la kizushi, Naomba utaje moja ya kitu ambacho unaona ni sifa kuu katika personality ya Mheshimiwa Rais JK na Mheshimiwa DK. Slaa.
Nimepewa mipaka ya kutaja kimoja kwa kila mmoja:

Kikwete - Mtu wa watu (inategemeana na mtu anaitafsiri vipi)

Slaa - Jasiri, mwenye uthubutu.
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Asante sana Maxence kwa jibu lako. Swali linalofuata;

Swali # 8

Jamii Forums kwa upana wake, ni moja ya media ya jamii inayokuwa kwa kasi ikiwa inaongezeka watumiaji kila siku ipitayo. Kwa kuzingatia hili unatatua vipi yafuatayo:-

A]. Kuna mikakati yoyote ya kuweza weka kuwezesha uendeshaji wa Jamii Forum hasa upande wa kifedha? Na tunapoogelea upande wa uendeshaji unaoegemea kifedha - ni vitu gani hasa ambavo huhitaji matumizi ya pesa upande wa Jamii Forums ili kuiendesha? Je una msaada wowote katika kuweza kufund uendeshaji wa Jamii forum hata toka Serkalini? Wahisani? Wakubwa ama shareholders (kama wapo)? Na pia mna mikakati ya Biashara yoyote ya JF iwe kwa kipindi kirefu ama kifupi?

B]. Baada ya kufanikiwa katika internet, kuwa na wafuasi katika majukwaa na vionjo tofuati, je, JF ina mpango gani wa kuendelea katika eneo la Audio (mathalani FM station, au Internet radio) au kushirikiana na wadau wengine waliotanuka na kupata access za visual za vitu kama 'streamline' za michezo na habari japo kwa muda mfupi kwa kuanzia.

C]. Kwa mtazamo wako ni nini kinafanya Jamii Forums kuzidi kupanuka na kukuwa? Unadhani ni nini siri ya mafanikio iwe ni forum ambayo inakubalika saa kuliko Forums zingine nchini?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
A]. Kuna mikakati yoyote ya kuweza weka kuwezesha uendeshaji wa Jamii Forum hasa upande wa kifedha? Na tunapoogelea upande wa uendeshaji unaoegemea kifedha - ni vitu gani hasa ambavo huhitaji matumizi ya pesa upande wa Jamii Forums ili kuiendesha? Je una msaada wowote katika kuweza kufund uendeshaji wa Jamii forum hata toka Serkalini? Wahisani? Wakubwa ama shareholders (kama wapo)? Na pia mna mikakati ya Biashara yoyote ya JF iwe kwa kipindi kirefu ama kifupi?
- JF ina mikakati ya muda mfupi na ya muda mrefu.

Muda Mfupi:
- Tunaandaa mkakati wa kuwa na hoja ya siku, ya wiki kulingana na hoja zinazokuwa zimeonekana kugusa jamii (si lazima siasa tu)
- Tuna mpango mkakati wa kuwa na mielekezo kwa wahariri wetu (mods) ikiwa ni pamoja na kuwapa majukumu kulingana na tunavyoona utendaji wao. Hata hivyo, tuna mkakati wa kuongeza wahariri wa kulipwa ambao watakaa JF muda wote.
- Tuna mkakati wa kujenga heshima ya jina la JamiiForums (as a brand) na hivyo tunaandaa 'Publicity/PR plan' kuhakikisha hili linafanikiwa.
- Tunaadaa mchanganuo wa kibiashara wa kuifanya JF isitegemee michango ya wanachama na misaada ya wahisani tu.
- JF itaboreshwa mwonekano [User Interface (UI)] hivi karibuni ili kuweza kuendana na mabadiliko ya teknolojia, maombi/mapendekezo ya vitu vingi vya kuhakikisha JF inakuwa rahisi kutumiwa na ushiriki wa wengi unaongezeka vitazingatiwa.

Mikakati ya muda mrefu:

  • Tunaandaa mikakati ya kushirikiana na vyombo vya habari vya nyumbani katika kuhakikisha JF inajipanua na ujumbe unasambaa ili kuifikia jamii isiyotumia mtandao wa intaneti.
  • Tuna mkakati wa kushirikiana na makampuni ya simu ili kuwa na namna ya kuwafikia wengi kwa njia ya SMS (walau SMS 3 kwa siku); tayari mkakati huu umefikia 75% kukamilika
  • Kuna watu wanafanya tafiti kupitia JF, tunaandaa database ambayo itawarahisishia kazi hii
  • Tuna mkakati wa kuanzisha midahalo au kushirikiana na wadau wengine katika kuandaa midahalo ambayo italeta tija katika Jamii yetu.
  • Kuanzisha kituo cha Redio kwa Tanzania
  • Tumekwishaanza, lakini tunaendelea kuandaa mkakati wa kushirikiana na vyombo vya habari vya kimataifa kama Al-Jazeera, BBC, CRI n,k (tayari tumekwisha kukaa na niliowataja)
JF ipo ilipo kutokana na uwezeshwaji toka kwa Wanachama wake (Premium Members), kutokana na jitihada zetu binafsi, kutokana na matangazo na hasa kutokana na ufadhili wa Mfuko wa Udhamini wa vyombo vya Habari (Tanzania Media Fund, TMF).

Ni wazi mikakati niliyoianisha hapo juu ikikamilika; JF itaweza kuingiza kipato na huenda tukapunguza kutegemea michango ya wanachama na wahisani.
B]. Baada ya kufanikiwa katika internet, kuwa na wafuasi katika majukwaa na vionjo tofuati, je, JF ina mpango gani wa kuendelea katika eneo la Audio (mathalani FM station, au Internet radio) au kushirikiana na wadau wengine waliotanuka na kupata access za visual za vitu kama 'streamline' za michezo na habari japo kwa muda mfupi kwa kuanzia.
Tumewahi kuwa na internet Radio (Jambo Radio); hatukuifuta, ipo kuiendesha kunahitaji raslimali watu na fedha; bado tunaweza kulifanikisha tena hili tukijipanga.

Mwaka 2006 tulijaribu kufuatilia kusajili redio kwa Tanzania (tulifuata taratibu zote), bado kulikuwa na ugumu wa kupata leseni, heunda baada ya kuingia mfumo wa digitali tutaweza kufanikisha mpango huu kama inavyoonekana kwenye mipango mkakati hapo juu.
C]. Kwa mtazamo wako ni nini kinafanya Jamii Forums kuzidi kupanuka na kukuwa? Unadhani ni nini siri ya mafanikio iwe ni forum ambayo inakubalika saa kuliko Forums zingine nchini?
Hili wanaweza zaidi kuliongelea wanachama. Ila, niseme ni persistence imetufikisha hapa. Kushikilia katika tunachokiamini na kutoyumbishwa na dhoruba zinazotupiga.

Kimsingi, kuwa na tovuti nzuri kwa mwonekano, na hata kwa utumiaji wake ni rahisi; kuwatunza wateja na kuhakikisha wanaridhika (japo si wote) ni kazi ngumu sana.
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Swali la nyongeza kwa jibu la swali # 8.

Nimependa jibu ya swali lako hili la nane (8) ambalo kwa kiasi kikubwa limejitosheleza na imetowa picha hasa ya Mikakati ya Jamii Forums. Tokana na majibu ya mikakati ambayo tokana na muono wangu imenyumbulishwa vema, ni dhahiri kuwa mipango yenu inawezekana kabisa; Hata hivo kuna dalili ambazo naweza sema zipo 'salient' kuwa tatizo kubwa la kuwezesha yote haya yameegemea katika fedha ya kuweza kuendesha na kuwezesha kwa kupitia kuajiri wasaidizi/ wasimamizi, kukarabati /kuboresha, kujidhibiti na kujitangaza pia; Kwa muktadha huo kama hutajali naomba kujua haya:-
  • Kuna 'mpaka muda' wowote ule ambao mmepanga kuwa hio mikakati iwe tayari?
  • Mko tayari kupokea shareholders kuwezesha kulainisha uendeshaji kwa njia ya pesa?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
Kuna 'mpaka muda' wowote ule ambao mmepanga kuwa hio mikakati iwe tayari?
Ukiangalia nimesisitiza kwenye majibu yangu kuwa ndani ya siku 90; hizi hazimaanishi kujivua magamba, bali utekelezaji wa baadhi ya mipangomkakati niliyoainisha.
Mko tayari kupokea shareholders kuwezesha kulainisha uendeshaji kwa njia ya pesa?
JF haipokei wanahisa, lakini kampuni mama inaweza kupokea wanahisa ili kuweza kujipanua.

Ukiangalia, mpangomkakati wa kupanuka maziwa makuu haujawekwa kwenye mipango ya muda mfupi wala muda mrefu, ni kwakuwa utekelezaji wake unahitaji sana kuwezeshwa kifedha. Hata hivyo, haujafutika!
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Maxence Asante kwa majibu yako katika swali la 8 la nyongeza. Swali linalofuata:-

Swali # 9

Jamii Forums imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kusambaza kwa habari hapa nchini na Afrika Mashariki, acha maeneo mbalimbali ya Dunia. Tukitolea mfano wa habari ambazo zimekuwa zikitambuliwa zimetoka katika chombo hiki cha JF kama vile ilivowahi tangazwa na BBC kutumia JF kama chanzo. Na pia kutajwa mara kadhaa na viongozi wa ngazi za juu hadi kwenye Bunge letu tukufu la Tanzania; kwa msimu huu imetajwa sio chini ya mara 3.

A]. U/mmejipanga vipi kuhimili kukua kwa kasi kwa JF ili kuweza enda sambamba na mabadiliko hayo?

B]. U/mmejipanga vipi kuhimili matakwa ya baadhi ya viongozi kutaka Jamii Forum ifungwe kwa madai kuwa haifai na inaleta uchochezi?

C]. Nini kinachokuongoza kuweza kusimamia chombo hiki kwa haki bila upendeleo na unafikiri una misingi inayoweza kufanya team yako yote isimame pale unapoamini bila kuyumbisha lengo na msimamo wa JF?

D]. Kuna mpango gani wa kuvihusisha vyombo vingine vya habari hasa Radio na TV kwa vipindi vya mahojiano mahususi kama vile anavyofanya ndugu yangu Yahya Mohamed pale Star TV Mwanza?

E]. Last time jf ilikuwa offline sababu ya service ilichukua muda kurudi na baadhi ya data kupotea kama vile threads na matendo (actions) nyingine kupotea. je mnajiandaaje na changamoto hiyo siku za mbele kwa kuweza fanya marekebisho ya haraka nay a kutopoteza chochote kilichokuwa tayari kipo?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
JamiiForums imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kusambaza kwa habari hapa nchini na Afrika Mashariki, acha maeneo mbalimbali ya Dunia. Tukitolea mfano wa habari ambazo zimekuwa zikitambuliwa zimetoka katika chombo hiki cha JF kama vile ilivowahi tangazwa na BBC kutumia JF kama chanzo. Na pia kutajwa mara kadhaa na viongozi wa ngazi za juu hadi kwenye Bunge letu tukufu la Tanzania; kwa msimu huu imetajwa sio chini ya mara 3.
Naam,
A]. U/mmejipanga vipi kuhimili kukua kwa kasi kwa JF ili kuweza enda sambamba na mabadiliko hayo?
Kama nilivyofafanua awali; mipango mkakati ya muda mfupi na ya muda mrefu itaweza kutatua hili.
B]. U/mmejipanga vipi kuhimili matakwa ya baadhi ya viongozi kutaka JamiiForums ifungwe kwa madai kuwa haifai na inaleta uchochezi?
Wana haki ya kupendekeza vyovyote, ndiyo demokrasia.
Sidhani kuna uchochezi uliofanywa ndani ya JF, hapana. Ni wengine kuguswa na watumiaji wa JF na huenda wahariri wetu wakawa hawajaona kilichoandikwa na kikawakera wahusika. Kuongeza idadi ya wahariri, wahusika kuwasiliana nasi haraka pindi wanapoona kitu kisicho sahihi au kisicho cha kawaida kunaweza kupungua kwa malalamiko haya. Hatufurahishwi na watu kuchafuana ama kuchochea vurugu za namna yoyote.

Hata hivyo; kufungia tovuti si suluhisho la matatizo! Bahati ni kuwa waendeshaji wa JF wapo Tanzania, wakipewa ushirikiano mambo mengi yanaweza kukaa sawa. Kwanini wanaolalamika na kutaka ifungwe wasilalamike kuwa iwezeshwe iweze kuboresha utoaji wa huduma? Mara zote, hata kama una mazuri kiasi gani, baya moja humfumba macho mwanadamu.

JamiiForums si siasa tu. Kuna majukwaa kama JF Doctor ambapo watumiaji wengi wamenufaika na kupata msaada kwa matatizo yao ya kiafya; kuna forum ya Great Thinkers (hawa ndio naweza kuwaita nguli wa JF) ambapo watumiaji wa forum hii hawajadili propaganda bali kujadili 'issues'. Kuna Forum ya Sheria ambapo wadau wengi hupata kujadili mambo mengi yanayohusiana na sheria, na nyingine nyingi!

C]. Nini kinachokuongoza kuweza kusimamia chombo hiki kwa haki bila upendeleo na unafikiri una misingi inayoweza kufanya team yako yote isimame pale unapoamini bila kuyumbisha lengo na msimamo wa JF?
Tuna mwongozo wa utendaji kwa wahariri, mwongozo huu unasomwa na wahariri wetu wote. Hata hivyo, kuna namna ambayo mhariri yeyote anaangaliwa kila kitendo anachofanya. Iwe ni kumfungia mtu, kuhamisha hoja au kuifuta hoja. Tunafanya hivyo ili kuweza kuhakikisha kila kitu kinaenda tunavyotarajia.
D]. Kuna mpango gani wa kuvihusisha vyombo vingine vya habari hasa Radio na TV kwa vipindi vya mahojiano mahususi kama vile anavyofanya ndugu yangu Yahya Mohamed pale Star TV Mwanza?
Kwanza niwapongeze vyombo vya Habari kama Star TV na Magic FM walioamua kuwapa ushirikiano wana JF kuhakikisha hoja zao zinaenda nje ya mtandao. Huu ni mwanzo mzuri, ndugu Yahya Mohamed wa Star Tv ni mwandishi wa kwanza Tanzania kuitumia JF kuweza kukusanya maoni na kuyafikisha nje ya mtandao akifuatiwa na dada Fina Mango (kupitia Magic FM kila Jumamosi); kwa hili kwa niaba ya JF, niwapongeze na kuwatia moyo kuwa tutahakikisha tunaboresha kadiri siku zinavyokwenda.

Hata hivyo, kama nilivyoeleza hapo awali; tayari tuna mkakati wa kuongeza vyombo vya nyumbani tutakavyokuwa na ushirikiano nao; tumekwisha kuongea na ITV na huenda tukafanikisha karibuni.

Zaidi, tumeongea na vyombo vya nje kama Aljazeera, BBC, Redio Ujerumani na CRI kuhakikisha tunawafikia wasikilizaji/wasomaji wao pia. Mikakati ya ushirikiano inaendelea.

E]. Last time jf ilikuwa offline sababu ya service ilichukua muda kurudi na baadhi ya data kupotea kama vile threads na matendo (actions) nyingine kupotea. je mnajiandaaje na changamoto hiyo siku za mbele kwa kuweza fanya marekebisho ya haraka nay a kutopoteza chochote kilichokuwa tayari kipo?
Kwanza:
- Kabla ya kufanya maboresho (miundombinu) tulitoa taarifa; tuliahidi ingechukua siku 2 na kwamba tungejitahidi kufanikisha hili.
- Nini kilifanyika? JF ilikuwa inahama kutoka server moja kwenda nyingine na huku ikiongezwa server ya ziada kwa ajili ya kutunza data endapo kutatokea tatizo lolote. Tulijitahidi lakini kosa lililotokea likawa ni kuruhusu watu kuendelea kuitumia JF wakati tunahamisha data, hapa ikatokea kukuta kuwa kilichokuwa kinawekwa kwenye server ya zamani hakikuhamia kwenye server mpya, tukarudia zoezi, ikafikia siku 3 lakini pia bado tulikuwa hatujashtukia kuwa bado watu walikuwa wanaandika na havichukuliwi; tukaamua kuzima kabisa server ili tufanye kazi ikiwa offline.

Pili:
Tuliomba radhi, tulitambua makosa yetu ambayo kimsingi lengo la kazi lilikuwa ni kuboresha lakini katikati tukakumbana na changamoto; kwetu lilikuwa ni funzo kubwa na tunalitilia maanani ili lisitokee wakati mwingine. Miundombinu tuliyo nayo kwa sasa inaweza kuihudumia jamii yetu kwa miaka mingine walau 4 bila kuathirika; hivyo kwa sasa kinachotakiwa ni kuhakikisha tunaitunza vema kwa manufaa ya watumiaji wa JF.
*ADDED* LALAMIKENI kuhusu JF kutoweka hewani kwa muda mrefu na posts nyingi na watu waliojisajili kati ya May 13 - May 15 kupotea!

Tunastahili lawama katika hili lakini tunaomba sana radhi kwakuwa kilichotokea hakikutarajiwa. Kimsingi lengo la kufungua ili watu waweze kuendelea na mijadala ni kutaka kutowaudhi wateja wetu. Tumejifunza kutokana na kosa hili na tunawahakikishia halitajirudia.

NINI KILITOKEA?
Tuliona JF kuendelea kuwa katika server moja japo ilikuwa kubwa ilikuwa ni risk kubwa kwetu, tukaamua kupanua wigo wa JF kuweza kupatikana kwa urahisi na kuhakikisha inakuwa salama zaidi; katika mchakato huo, kitendo cha kuhamisha data toka kwenye server moja kwenda nyingine kilishaanza tangu tarehe 12 (kama tulivyowatangazia) na tukajikuta kumbe vyote vilivyoongezeka siku hiyo havikuweza kuingia kwenye database vikawa vimeachwa!

Tumejitahidi sana kuvi-recover lakini ikaonyesha kuwa inaweza kutuchukua muda mrefu sana na kuathiri kuweza kuirejesha JF hewani, tukatambua kuwa kwakuwa wanachama wetu ni waungwana watatuelewa kuwa lengo japo lilikuwa jema lakini athari iliyojitokeza imekuwa nje ya uwezo wetu na hivyo tunawaomba radhi NYOTE.
Niwaombe wadau wachangie JF iweze kujiendesha bila utegemezi, kutuchangia kwa kuwa Premium Members ni kutusaidia kuweza kuwahudumia kirahisi bila vikinza kama hivi. Kuwa tunafanya kila kitu wenyewe ndiko kunapelekea kukumbana na vigingi kama hivi, tungekuwa tuko safi kifedha ni wazi tungewapa kazi hii wataalamu wengine wakasaidia kuhakikisha inafanyika ndani ya muda mfupi sana.

Wenye dhamira ya kuchangia wanaweza kusoma hii thread: JamiiForums Premium Member Subscription
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Kwa mara nyingine nishukuru kwa majibu yako yakinifu.

Kwa wale wote wanaofuatilia huu mjadala kwa ukaribu naomba watambue kuwa wanaposoma majibu ya maswali ya # 9, kuna kipengele Maxence ameongeza katika mtindo wa kunukuliwa (I.e. quoted post) yakiwa yamebeba ujumbe toka kwa Invisible.


Mkuu nikiri kuwa nikiwa ni mbegu ambayo imechipukia MMU (Mahusiano, Mapenzi & Urafiki) nime ‘mind' sana kutotaja hilo jukwaa letu pendwa kama moja ya majukwaa kwenye hio mifano ulioanisha hasa ukizingatia pia ni moja ya majukwaa ambayo pia hutumika na washiriki wengi. Swali lifuatalo:-

Swali # 10

Kuna hili suala zima la kutumia Jina halisi la mshiriki maarufu kwa "Verification" hapa JF.

A]. Unadhani ni kwa nini wengine wana verify na wengine hapana?

B]. Kuna faida gani ya kuverify?

C]. Unawashauri nini wale walio verify na wale ambao bado?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
Mkuu nikiri kuwa nikiwa ni mbegu ambayo imechipukia MMU (Mahusiano, Mapenzi & Urafiki) nime ‘mind' sana kutotaja hilo jukwaa letu pendwa kama moja ya majukwaa kwenye hio mifano ulioanisha hasa ukizingatia pia ni moja ya majukwaa ambayo pia hutumika na washiriki wengi.
Kumradhi, ni mojawapo ya majuwaa maarufu hapa JF na nimechukua jukumu la kuanza kulipitia mwenyewe. Kwa kuanzia kuna threads ambazo ni sticky pamoja na JF Doctor ambapo nimejitahidi kuhakikisha zile ambazo zinaonekana kurudiwa mara nyingi ziwe sticky ili watu waweze kupata ufumbuzi wa matatizo yao kama ilivyokwishaelezwa na wataalamu.

Kuna hili suala zima la kutumia Jina halisi la mshiriki maarufu kwa "Verification" hapa JF.

A]. Unadhani ni kwa nini wengine wana verify na wengine hapana?

B]. Kuna faida gani ya kuverify?
Ni vema mtu akapitia mjadala huu, JF: Majina bandia na uhuru wa maoni ili aweze kuelewa kwanini wengi si rahisi kutumia majina yao.

Hata hivyo, tujaribu kuangalia kwa mapana suala hili; hivi unachokiangalia JF ni jina la mwenye hoja ama hoja ya mleta hoja?

Wale wanao-verify wanafanya jambo jema sana na hata wale wanaoamua kubaki 'undercover' bado wanafanya vema ili mradi hawavunji sheria za JF katika uwasilishaji wao wa hoja.

Faida ya kuwa na verified account haswa kwa 'public figure' ni kuwafanya wananchi waelewe wanapokuwa wanajibizana nawe wakuulize yepi au wakushauri yepi. Hata kama si 'public figure' bado kuwa na account ambayo unaisajili hapa JF na ukawasiliana nasi tukaithibitisha kuwa wewe ndiye mwenye jina hilo basi inaepusha mtu kujisajili na jina lako na asili-verify na alitumie visivyo.

Faida ya kutumia 'pen name' ni kuwa mtu hata kama anabishana na boss wake au anabishana na askofu wake au rais wake hajui kuwa ndiye huyo anayembishia au anayemtaka aje na uthibitisho wa hoja yake. Hii inawapa uhuru wote, mwuliza swali na mwulizwaji lakini wote wakiwa wanazingatia sheria za JF.

C]. Unawashauri nini wale walio verify na wale ambao bado?
Mpaka sasa ninapoandika tuna 'Great Thinkers' 127 na 'Verified Users' 75 tunahitaji wengi kuwa kwenye makundi haya; katika kundi la members wote hawa takribani 90,000 hawa ni wachache sana. Wanaohitaji kuwa verified wakiwasiliana nasi kwa barua pepe support@jamiiforums.com au kutuma Private Message tutashirikiana nao kufanya verification na hata wanaotaka kushiriki kwenye jukwaa la Great Thinkers.
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Naomba kusisitiza kuna wadau wanafuatilia huu mjadala, baadhi wanatuma maswali kwa njia ya Private Messaging. Wengi wao wakiamini wamenyimwa ushiriki wa huu mjadala kitu ambacho sio kweli. Naomba niwasisitize kuwa wasome bandiko la kwanza kabisa la huu mjadala watakuta Link ya kutoa hoja/maswali na ya ziada yanayohusiana na hii.

Nikumbushe pia imefanywa hivi ili kuweza kukusanya yale yote ambayo tunataka kupata toka kwa mhojiwa ambae ni Maxence Melo. Tukisha maliza maswali ya moja kwa moja ndipo kila mshiriki mwenye access na hili Jukwaa ataweza kubandika bandiko lake kwenye hii thread. Kwa sasa (kwa mara nyingine tena) naomba tumia kiunganishi ichi kupata mjadala wa kubandikia. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/309781-jf-focus-side-comments-exclusive-interview-with-jamiiforums-founder-maxence-melo-4.html#post4477831
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
hahaha! Mkuu imebidi nicheke niliposoma kiunganishi bandiko cha mjadala mwingine! Ni kama vile kila kitu kimejadiliwa hapa JF! Asante kwa majibu yako, kwa kusonga mbele na mjadala swali lifuatalo:-

Swali # 11

Tumeona utambulisho na uwepo wa Forum za Kenya.

A]. Ni nini kilifanya Jamii Forums ihusishe na kutenga forum za Kenya katika JF?

B]. JF imeamua ipanuke kwenda kikanda? kwa maneno mengine ina mpango wa kuongeza nchi zengine za Afrika Mashariki?

C]. Je hamuoni kuwa kupanuka kwake inaweza haribu uhalisia na utambulisho wa kua JF ni ya Kitanzania?

D]. Tokana na uchaguzi wa Kenya unaokuja karibuni haitakuwa hatari kwa habari za KiTanzania kupunzwa na kupelekea za Kenya kupewa uzito kuliko?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
Tumeona utambulisho na uwepo wa Forum za Kenya.

A]. Ni nini kilifanya Jamii Forums ihusishe na kutenga forum za Kenya katika JF?
B]. JF imeamua ipanuke kwenda kikanda? kwa maneno mengine ina mpango wa kuongeza nchi zengine za Afrika Mashariki?

C]. Je hamuoni kuwa kupanuka kwake inaweza haribu uhalisia na utambulisho wa kua JF ni ya Kitanzania?[/QUOTE]
Nadhani niliyokazia wino (bold) yakiondoka nitaelewa vema zaidi.

JF ilikuwa na mkakati wa kupanuka kwa nchi za maziwa makuu, mkakati huu unahitaji raslimali watu na raslimali fedha. JamiiForums ipo mbioni kupata mshirika katika kufanikisha azma hii; tayari tuna mkakati wa kuwafikia Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo, Uganda na Rwanda, Kenya tumeanza na tumeanza nao katika tovuti mama ya JamiiForums.

Ieleweke kuwa JF haijaanzishwa kuhudumia watanzania tu, ipo kuhudumia Jamii nzima ya watumia kiswahili na kiingereza hasa wa maziwa makuu.

Kuna wakenya ambao tayari tupo nao ndani ya JF, tuna moderator mkenya Ab-Titchaz, tuna wanachama kama Alai, Smatta, Kabaridi n.k; hawa tumekaa nao, tunaweza kutofautiana kwenye hoja mbalimbali lakini bado dhamira ni moja, kushirikiana katika mijadala endelevu.

Tuna wahariri (moderators) wengine wawili tunawaandaa ili waweze kuwahudumia majukwaa ya Kenya. Tusiwe wabinafsi, kama tuna kitu ambacho tunaweza kukitumia kwa pamoja kwa manufaa ya eneo zima la Maziwa Makuu, basi kama watanzania kwa ukarimu tujitahidi kuwapa ushirikiano.

Tunachofikiria, ni kuepuka gharama za kuwa na tovuti zaidi ya moja ambapo tutalazimika kuwa tunahama tovuti kufuatilia mijadala inavyoendelea na kuhakikisha servers zinakaa imara.

D]. Tokana na uchaguzi wa Kenya unaokuja karibuni haitakuwa hatari kwa habari za KiTanzania kupunzwa na kupelekea za Kenya kupewa uzito kuliko?
Nimeshangaa, hivi watanzania wanawaogopa wakenya? Hatujiamini?

Ni kweli, watumiaji wa mtandao wa Kenya ni wengi sana; tena wakija JamiiForums kwa wingi; ni wazi majukwaa ya Kenya (kama yakiwa na uhariri mzuri) yatayapita yale yanayowagusa watanzania zaidi kwa kuwa na idadi kubwa ya washiriki na watembeleaji, lakini hili haliwezi kumaanisha habari za Tanzania kupuuzwa.
 
Last edited:

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Kwa mara nyingine tena mjadala unaendelea. Swali linalofuata:-

Swali # 12

Maxence kuna habari huwa zinasikika kuwa umewahi wekwa chini ya ulinzi na Police/Usalama kwa tuhuma zilizohusiana na Jamii Forums; ambayo pia ilisababisha kufungwa kwa JF kwa siku ama wiki kadhaa (sina hakika).

A]. Ni nini hasa kilisababisha kukamatwa kwako?

B]. Unadhani ni kwa nini uliachiwa huru na ukaruhusiwa kufungua upya tena JF kuwa hewani? Kuna madhara yoyote ambayo yalichukua mda mrefu kutatua tokana na kufungwa kwa JF kwa hizo siku?

C]. Unadhani kua uwezekano wa hilo kutokea tena? Ikitokea kwa bahati mbaya (God Forbid) JF imefugwa na kupigwa ganzi ama mauti na nguvu ama mkono wa Serkali kuna mbadala wake wowote? Kwa maneno halisi kuna "contingency Plan"?

D]. Tumeona wanaharakati hapa nchini wakikubwa na matatizo hasa pale ambapo wanapinga maslahi ya wakubwa hapa nchini; Huogopi kuwa na wewe linaweza kukuta? Ama mwenzetu haupo nchini?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
Maxence kuna habari huwa zinasikika kuwa umewahi wekwa chini ya ulinzi na Police/Usalama kwa tuhuma zilizohusiana na Jamii Forums; ambayo pia ilisababisha kufungwa kwa JF kwa siku ama wiki kadhaa (sina hakika).
Ndiyo, tulikamatwa wawili na ilikuwa ni mnamo Februari 18, 2008.

A]. Ni nini hasa kilisababisha kukamatwa kwako?
Taarifa zisizo sahihi ndizo zilipelekea vyombo vya dola kutumika dhidi yetu. Walichokuwa wanaelezwa ni kuwa JF (enzi hizo JamboForums) inachochea chuki dhidi ya serikali na hivyo tulikuwa tumetwishwa "Makosa ya jinai". Nakumbuka niliambiwa mimi ni gaidi.

Aidha, baada ya kuhojiwa tulikuja kubaini kuwa walikuwa wakidhani sisi ndio tuliokuwa tukiandika kinachoonekana ndani ya JF na hivyo kuamini tulikuwa na mkakati dhidi ya serikali. Ikumbukwe, ni wiki takribani mbili baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo (Edward Lowassa) kujiuzulu na data nyingi zilihisiwa kutolewa JF. Ni vema wengine wakasoma nini kilitokea hapa - Tanzania detains popular Web site editors - Committee to Protect Journalists

Aidha, kuna wanaodhani serikali iliifunga JF; hapana. Tuliifunga JF sisi wenyewe kwakuwa hatukutaka iwe hewani wakati tupo kwenye kuhojiwa kwa siku 7 na hivyo uangalizi ungekuwa dhaifu na ni wazi mashambulizi yangetumwa huenda yangeweza kuathiri kila kitu. Baadae tuliingia mkwaruzano wa jina 'JamboForums' kulikopelekea tubadilishe jina haraka kwenda JamiiForums wakati tukiendelea kulumbana kuhusu umiliki wa jina JamboForums (haki miliki).

B]. Unadhani ni kwanini uliachiwa huru na ukaruhusiwa kufungua upya tena JF kuwa hewani? Kuna madhara yoyote ambayo yalichukua mda mrefu kutatua tokana na kufungwa kwa JF kwa hizo siku?
Siwezi kuwasahau Tundu Lissu (kama mwanasheria wa kujitolea kwetu), Mzee Mwanakijiji, Zitto Kabwe ambao walijitolea kupiga kelele pindi tulipokamatwa. Aidha, vyombo vya habari vya BBC na VOA kupitia watangazaji wake walitupa ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha tunatendewa haki.

C]. Unadhani kua uwezekano wa hilo kutokea tena? Ikitokea kwa bahati mbaya (God Forbid) JF imefugwa na kupigwa ganzi ama mauti na nguvu ama mkono wa Serkali kuna mbadala wake wowote? Kwa maneno halisi kuna "contingency Plan"?
Kwa sasa hata tukikamatwa, kuna 'backup plans' nyingi; kiufundi na kiuhariri.

Kimsingi, linapotokea tatizo, japo linaweza kukuumiza kama binadamu lakini linakuwa ni fundisho kwako kujiandaa endapo jingine la namna hiyo au inayoshabihiana litatokea tena.

D]. Tumeona wanaharakati hapa nchini wakikumbwa na matatizo hasa pale ambapo wanapinga maslahi ya wakubwa hapa nchini; Huogopi kuwa na wewe linaweza kukuta? Ama mwenzetu haupo nchini?
Woga!

Woga, kukata tamaa n.k si jambo jema. What if we all gave up?

Nipo nchini, sijakimbia na sitarajii kukimbia kirahisi. Watanzania wakiacha woga, basi mengi yatawezekana. Nashauri watu wasome hii topic japo ni ya zamani kidogo (Disemba 1, 2008) na aliianzisha Mag3: Woga Umetudumaza Kifikra Watanzania!
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Maxence Hongereni na Poleni kwa masaibu yote yaliyowakuta kwa kipindi hicho. Nimependa swali # 12, majibu yamekuwa kama yametoa historia fupi ya Jamii Forums... Naomba nikiri pia naona hili jina la "Jamii Forums" ni zuri zaidi (labda sababu nimelizoea lol) kuliko hilo la Jambo Forums; sababu zangu zikiwa nikisikia 'Jambo' naihusisha zaidi na Kiswahili cha Kenya kuliko chetu.

Swali # 13

Tekinologia inaenda ikikuwa, ikibadilika na kusonga mbele. Hii inafanya kuwe na matumizi ya inteneti tokana na uwezo ama mapenzi ya mtumiaji. Kuna wenye Computers (iwe mpakato ama ya mezani); kuna Ipads (na tablets za aina mbali mbali), simu za kawaida na za hali ya juu na vengine vingi vinavoendelea kuvumbuliwa. Utumiaji wa hivi vifaa vimetofautiana katika ubora na pia katika kuweza kuipata na kuitumia Jamii Forums vilivo. Kwa msingi huu:-

A]. Ni namna gani mnawezesha washiriki kuweza kutumia JF kwa urahisi na mvuto (User friendly) kwa wote bila kuzingatia ubora ama ukubwa wa chombo anatumia?

B]. Katika mabandiko mbali mbali hapa karibuni kumekuwa na ujumbe katika baadhi ya mabandiko kama vile "Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums"; nini hasa maana yake? Au ni simu zinagaiwa JF kwa baadhi ya member (Lol).

C]. Kuna kitu kimekuwa kikitajwa na kutolewa ufafanuzi kuhusu Apps, naomba utoe maelezo juu ya hili. Mna maana gani kusema hivo? Ina maana na umuhimu gani? Na tafadhali toa maelezo ambayo yataweza kuwa faida hata kama sijagusia kuuliza.

D]. Mnalionaje suala la kutengeneza JF Developers API? Hii inaaminika itaongeza kasi ya ukuwaji wa JF ukifananisha na twitter na facebook kuna applications nyingi sana kuanzia computer simu hadi tablet. Pia mmefikiria kuwa kuna wale ambbao pengine wangependa ku iclude JF kwenye media zao mfano blogs n.k ?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
Tekinologia inaenda ikikuwa, ikibadilika na kusonga mbele. Hii inafanya kuwe na matumizi ya inteneti tokana na uwezo ama mapenzi ya mtumiaji. Kuna wenye Computers (iwe mpakato ama ya mezani); kuna Ipads (na tablets za aina mbali mbali), simu za kawaida na za hali ya juu na vengine vingi vinavoendelea kuvumbuliwa. Utumiaji wa hivi vifaa vimetofautiana katika ubora na pia katika kuweza kuipata na kuitumia Jamii Forums vilivo. Kwa msingi huu:-

A]. Ni namna gani mnawezesha washiriki kuweza kutumia JF kwa urahisi na mvuto (User friendly) kwa wote bila kuzingatia ubora ama ukubwa wa chombo anatumia?
Shukrani, lakini nadhani hapa kuna kitu sijaelewa.

Hata hivyo, kama nilivyosema awali kuwa tumekwisha anza mkakati wa kuboresha mwonekano na utumiaji rahisi (nalenga kumaanisha User Interface [UI] na functuonality) hivyo tutazingatia kuboresha kwa kila watumiaji wa vifaa vinavyotumia intaneti.

B]. Katika mabandiko mbali mbali hapa karibuni kumekuwa na ujumbe katika baadhi ya mabandiko kama vile "Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums"; nini hasa maana yake? Au ni simu zinagaiwa JF kwa baadhi ya member (Lol).
Hii ni 'default signature' kwenye app za JF, mtu anaweza kuiruhusu au kuizuia. JF haigawi simu (lol)

C]. Kuna kitu kimekuwa kikitajwa na kutolewa ufafanuzi kuhusu Apps, naomba utoe maelezo juu ya hili. Mna maana gani kusema hivo? Ina maana na umuhimu gani? Na tafadhali toa maelezo ambayo yataweza kuwa faida hata kama sijagusia kuuliza.
Nadhani swali hili kulijibu inahitaji mtu awe anatumia smartphone ili ninachojibu akijaribu.

Kuna 'features' nyingine zinawezekana kwenye smartphones na tablets lakini si kwenye kompyuta au simu ya kawaida (japo inapata intaneti.

Kwa wapsite (mobile version ya JF) simu hata ya kichina inaipata kirahisi lakini endapo tutataka anayetumia simu hiyohiyo apate 'touch site' au 'PC version' ni wazi itamchukua muda kufunguka.

Wapsite ni tovuti rafiki kwa simu za mikononi na inakuwa rahisi kufunguka japo vitu vingi vinakuwa vimeondolewa kurahisisha upatikanaji wake. Hata hivyo, tunaiboresha pia!

D]. Mnalionaje suala la kutengeneza JF Developers API? Hii inaaminika itaongeza kasi ya ukuwaji wa JF ukifananisha na twitter na facebook kuna applications nyingi sana kuanzia computer simu hadi tablet. Pia mmefikiria kuwa kuna wale ambbao pengine wangependa ku iclude JF kwenye media zao mfano blogs n.k ?
Wazo zuri, mwenye kuleta wazo hili tungepata mawasiliano naye ingekuwa vema tukaweza kuangalia tunalifanikishaje hili. Ukweli ni suala muhimu lakini linahitaji raslimali (watu na fedha) nyingi pia.
 

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Maxence Asante kwa majibu yako ambayo naamini kila mmoja ataelewa tokana na exposure aliyo nayo ya chombo (iwe simu, tablet ama computer kabisa) anachotumia. Hata hivo hapo mwanzo umegusa kuwa kuna kitu unadhani hujaelewa, naomba kama kwa njia yoyote ile imeathiri jibu lako utowe ufafanuzi ni kitu gani kimekuwa na utata.

Mkuu Ochutz, swali lako liliwekwa kwenye swali # 13 kipengele [D], ambacho kama hujaelewa, Maxence Melo katoa ruhusa ya kumtafuta kwa ufafanuzi zaidi kuhusu hilo. Naomba tusonge swali lifuatalo:-

Swali # 14

Kuna swala zima la JF Premium membership, hili suala limezungumziwa kwa kina sana na Mike McKee katika nyuzi mahsusi ya maelezo yalioambatanishwa na maswali na majibu ya Members na wahusika wenyewe (ambao ni utawala). Kwa hapa tunaomba tu ugusie machache:-

A]. Siku zote hio JF Premium Membership ilikuwa member kutoa kiwango alichonacho tena akisha panda ngazi hio anabaki papo hapo bila kujali malipo upya. Ni kitu gani kimefanya hii ibadilike kwa viwango pangwa?

B]. Hadi sasa toka mtambulishe viwango vipya kumekuwa na mafanikio ya kufikia malengo/matakwa yenu ya lengo lenyewe la kuanzisha huo utaratibu mpya?

C]. Kuna member mmoja ameuliza sana kama kuna mna mpango wa kuanzisha utaratibu wa JF Premium Membership tokana na wingi wa post za mshiriki; una nini la kusema kuhusu hili?

D]. Na kwa faida ya wengi kuna member anaomba kujua wale wenye vibandiko vya JF Bronce, Gold ama Platinum (chini ya JF Premium Membership) huwa wana hisa JF?
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,382,197
Members 526,298
Posts 33,821,854
Top