JamiiTalks Interview with Maxence Melo: The story of JamiiForums - history and operations of the platform

Status
Not open for further replies.

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
Pamoja na kusma 'sikuelewa' lakini nilijitahidi kujibu kwa nilivyoelewa. Ni kwa kuwa tayari suala la uboreshaji wa UI ya JF nilikwisha kuligusia hapo awali.

Kuna swala zima la JF Premium membership, hili suala limezungumziwa kwa kina sana na Mike McKee katika nyuzi mahsusi ya maelezo yalioambatanishwa na maswali na majibu ya Members na wahusika wenyewe (ambao ni utawala). Kwa hapa tunaomba tu ugusie machache:-
Naam,
A]. Siku zote hio JF Premium Membership ilikuwa member kutoa kiwango alichonacho tena akisha panda ngazi hio anabaki papo hapo bila kujali malipo upya. Ni kitu gani kimefanya hii ibadilike kwa viwango pangwa?
Wanachama hawahawa ndio walipendekeza 'Premium Membership' iwe na kikomo ili JF ipate namna ya kujiendesha. Halikuwa pendekezo la mtu mmoja, ni wengi waliafiki hili hivyo nasi kutokana na kuona umuhimu wa kulifanikisha hili tukaanzisha utaratibu huu.

Kiwango cha chini kwa mwaka (siku 365) ni TZS 20,000/- kiasi ambacho naamini mtumiaji wa JF kama kweli anaona umuhimu wa JF kuendelea kuwa hewani hakimshindi.

Tukiwa 'serious' na kudhamiria kuiboresha JF na ikatuhudumia tunavyotaka basi walau wanachama 25,000 kati ya wanachama takribani 90,000 wakachangia 20,000 maana yake JF itapata walau TZS 500,000,000/- kwa mwaka; fedha ambayo ikipatikana ni wazi JF itaboresha mengi, itaanzisha gazeti na zaidi mengi ya mapendekezo yatafanyiwa kazi.

B]. Hadi sasa toka mtambulishe viwango vipya kumekuwa na mafanikio ya kufikia malengo/matakwa yenu ya lengo lenyewe la kuanzisha huo utaratibu mpya?
Ni mapema sana kupata kusema kama mafanikio yapo makubwa, lakini yapo. Ndio maana mnawaona wenye hizo badges za Premium Membership.

Inasikitisha, watanzania ni wepesi kusema lakini kutenda ni wagumu sana. Ukiiangalia TZS 20,000 ukaigawa kwa miezi 12 unaweza kuona ni kiasi gani mtu anakuwa katusaidia katika kuhakikisha tunamhudumia vema zaidi (TZS 1,667/- au US$1 kwa mwezi); sidhani kiasi hiki kinatushinda, ila ndio hali halisi, tunaongea na kutaka makubwa lakini hatupo tayari kuwa sehemu ya mabadiliko tunatoyataka.

C]. Kuna member mmoja ameuliza sana kama kuna mna mpango wa kuanzisha utaratibu wa JF Premium Membership tokana na wingi wa post za mshiriki; una nini la kusema kuhusu hili?
Ni wazo zuri, manake huyu hawezi kupata $1 kwa mwezi?

Ingekuwa hivyo, wadau kama Nyani Ngabu, Rutashubanyuma n.k wangepewa huzo badges bure kwakuwa wana mabandiko mengi, lakini sidhani kama kiuhalisia yeyote anayetumia JF hawezi kupata $1 (ya ziada kuichangia JF) kwa mwezi.

Ndugu zangu, tunahitaji kuwezeshwa ili tuwahudumie vema. Nakosa hata lugha ya kutumia ili watu wanielewe, nawashukuru wote ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatuchangia kwa hali na mali ili tuweze kutoa huduma hii. Kwa niaba ya wenzangu, tunashukuru sana.
D]. Na kwa faida ya wengi kuna member anaomba kujua wale wenye vibandiko vya JF Bronze, Gold ama Platinum (chini ya JF Premium Membership) huwa wana hisa JF?
Premium Members hawana hisa, ni wanachama waliojitolea kuhakikisha wanaichangia JF ili iendelee kuwepo hewani. Mfano ni watu kama Pasco, Ritz, Edwin Mtei, ndetichia, Elli, Nyunyu, Kashaijabutege, Zogwale, Mwalimu, Kimbunga n.k na wengine ni wanafunzi. Wanapata/watapata nini baadae kama ziada, nisingependa kuliongelea kwa sasa (natumaini hutohoji kwanini, lol)
 
Last edited:

AshaDii

Platinum Member
Joined
Apr 16, 2011
Messages
16,232
Points
1,500

AshaDii

Platinum Member
Joined Apr 16, 2011
16,232 1,500
Premium Members hawana hisa, ni wanachama waliojitolea kuhakikisha wanaichangia JF ili iendelee kuwepo hewani. Mfano ni watu kama Pasco, Ritz, Edwin Mtei, ndetichia, Elli, Nyunyu, Kashaijabutege, Zogwale, Mwalimu, Kimbunga n.k na wengine ni wanafunzi. Wanapata/watapata nini baadae kama ziada, nisingependa kuliongelea kwa sasa (natumaini hutohoji kwanini, lol)
Bora tu ungezitaja ili ituvutie hata sie ambao tumevuliwa baada ya cheo chetu kuisha muda wake lol. Asante kwa majibu, swali linalofuata:-

Swali # 14

Imewahi gusiwa na baadhi ya members kwa wakati mbali mbali kuwa wangependa Jamii Forums ije iandae gathering kwa ajili ya members watakaopenda kukutana kwa pamoja hata bila kutoa ID zao wazitumiazo hapa JF. Unalipokea vipi hili? Imewahi tokea mkusanyiko kama huo?
 

Maxence Melo

JF Founder
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,918
Points
2,000

Maxence Melo

JF Founder
Joined Feb 10, 2006
2,918 2,000
Bora tu ungezitaja ili ituvutie hata sie ambao tumevuliwa baada ya cheo chetu kuisha muda wake lol.
Waliowahi kuchangia ni wazi bado wataona umuhimu wa kuendelea kutuwezesha, hata hivyo safari hii tumepanga kuwanufaisha japo kidogo, sintoandika kivipi.
Imewahi gusiwa na baadhi ya members kwa wakati mbali mbali kuwa wangependa Jamii Forums ije iandae gathering kwa ajili ya members watakaopenda kukutana kwa pamoja hata bila kutoa ID zao wazitumiazo hapa JF. Unalipokea vipi hili? Imewahi tokea mkusanyiko kama huo?
Kuna mikusanyiko kadhaa imefanyika Dar na Arusha. Bado nasisitiza kuwa endapo wadau wanaamua kukutana, mtu anapoamua kui-disclose ID yake ya JF ni juu yake lakini ningeshauri watu kujiepusha kutaja IDs zao wala kujadili masuala ya siasa (labda pale inapolazimu).

Hatujawa na mpango (kama JF) wa kuitisha mkutano lakini endapo wadau watatuhitaji kuwasaidia katika kuhakikisha hili linafanikiwa tutatoa ushirikiano. Wanaotaka kujua namna ya kufanikisha hili nashauri wawasiliane na PakaJimmy na Preta kwani wana uzoefu wa shughuli kama hizi.
 

Umasikini wa fikra

Senior Member
Joined
Aug 17, 2017
Messages
103
Points
225

Umasikini wa fikra

Senior Member
Joined Aug 17, 2017
103 225
amani ya Mungu iwe juu yenu wakuu kama kichwa cha habari kinavyosomeka hapo juu kua nahitaji kumfahamu mtu aliyeianzisha jamii forum.. jamii forum imenifunza mengi sana mengine yanayo andikwa humu yanananiacha mdomo wazi binafsi nimepata kufaham mengi na shukrani zungu za dhati kabisa ziwaendee wale wote ambao uwoga wameusaliti na kuamua kuandika ukweli bila kumuogopa yoyote kwa hili Mungu awabariki sana. images%2B%2828%29.jpg
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,382,194
Members 526,298
Posts 33,821,776
Top