Internet ya uhakika na bei sawa na bure ni Adsl ya TTCL

Internet ya uhakika na bei sawa na bure ni Adsl ya TTCL

Ndio bei rahisi ila user wengi kwaiyo mbps nayo inapungua
Internet za waya mara nyingi hazina hii shida, adsl tabu yake tu ni Analog tu, ukiwasha router inasoma 3+ Mbps unatumia wee speed inashuka hadi 2mbps ama 1mbps inabidi restart router tena speed inarudi tena etc. Ila overall sio internet mbaya kwa 25,000.
 
View attachment 2332959
Usije ukadhani haya manguzo yenye nyaya zile nyembaba za ttcl zilizokuwa zinatumika zamani kwenye simu za mezani ni uchafu kwenye miji, nakujuza kwamba hizo nyaya ndizo zilikuwa zinasambaza internet miaka ile 2000 hadi 2010 enzi hizo ili upate internet inabidi uende internet cafe ambayo ilikuwa ni sehemu yenye computer zilizoungwa kwenye mtandao.. kwenye miaka ya kuanzia 2012 simu za kisasa zilianza kushika kasi tukaanza kutumia internet za minara ya simu, hali hii ilifafanya internet cafes nyingi zikafungwa, lakini licha ya haya yote bado huduma ya internet ya kwenye nyaya za zamani bado ipo mpaka leo ila ni watu wachache sana wanatumia tena kwa elf 25 tu.

Tunasikia sikia hizi kelele za internet ya fiber ambayo ni internet ya kisasa lakini ubaya ni kwamba hii fiber ipo kwenye majiji na mbaya zaidi hata kwenye hayo majiji ni yale maeneo center kati, wanasema kwa sasa wanafanya survey panapo majaliwa itasambaa mwezi wa 11 lakini ni nani asiezijua ahadi za serikali ?

Nadhani ni bora tujikite zaidi huku kwenye adsl ambayo tayari ipo kuliko kusubiri ahadi za fiber, kwa sasa uhakika ni kutumia adsl ambayo ipo tangu zamani, Uzuri wa Adsl ni kwamba imesambaa kila mikoa na wilaya nyingi.

Kama upo eneo lina nguzo za ttcl zenye zile nyaya nyembamba zilizokuwa zinatumika kwenye simu za mezani zamani basi hapo tayari una internet. Utachotakiwa kufanya ni kwenda ofisi ya ttcl, fanya jitihada ukutane na mafundi, pale mapokezi mara nyingi hawana uelewa wa mambo haya wanaweza kukwambia hio huduma haipo.

nenda na fundi wao nyumbani au ofisi unayaotaka kuwekewa, baada ya hapo utanunua kifaa cha kuchomeka ule waya kinachosambaza internet kwa elf 55, ni zoezi la muda mfupi tu, wakimaliza unalipia kifurushi cha elf 25..

Speed ni nzuri unaweza kucheki video HD 720P kwenye Youtube, netflix, n.k.

Kwa wale wazee wa kushusha muvi, series, games, mafaili

MB 1 ndani ya sekunde mbili
MB 30 ndani ya dakika
GB 1.8 ndani ya saa
Kwa siku unaweza kuchota hata gb 30


kama unahitaji spidi maradufu ya hapo inabifdi ulipie elf 50,
Hahahaaa hii router ya ADSL2 ndiyo ninayo hapa ndani siku hizi naitumia tu kama AP (Access Point) si ina ports za Ethernet, nmezima tu DHCP Server..
 
Back
Top Bottom