Intelligence heredity: Je, uwezo wa akili hurithiwa?

Intelligence heredity: Je, uwezo wa akili hurithiwa?

Aisee . yaani ndani ya miezi 12 tu anakuwa sawa na mtu mwenye umri wa miaka 50... sasa mkuu hizi nchi zilizoendelea sizitakuwa na wanausalama wengi sana ambao ni human cloning " kwa mantik hiyo neno hasara ya rasilimali watu pindi itakapo tokea maafa kwao itakuwa ni msamiati tu

mkuu watu walishaaanza kitambo haya mambo..wakiona wew ni mtu muhimu kwao ni kutengeneza clone yako ambayo wataisubject mahala ambapo pataifaaa ili ikafanye kazi zingine mbadla bila kupoteza maarifa ya recipient( original ) yake..

Tumebaki tu sisi huku kuhangaika na kusoma eti ukawe usalama wa taifa ...ha ha ha utasubiri sana labda kuwa barozi wa nyumba kumi huku kwetu ndo usalama wa taifa.. 😕 😕
 

Attachments

  • Screenshot_20181109-135509~2.jpg
    Screenshot_20181109-135509~2.jpg
    89 KB · Views: 36
  • Screenshot_20181109-135452~2.jpg
    Screenshot_20181109-135452~2.jpg
    87.2 KB · Views: 36
Ohppsss .. kichwa chote kizito "

nimekuelewa vyema mkuu " salute
hiyo ni Bio frofile ya Jim acosta...nguli wa Mwanahabari white house mbishi ,kichwa wa kuchambua habari za white house ,mpiga maswali mazito maraisi wanaoingia Ikulu huwa wanamwogopa huyu jamaa..
Ila sasa ukisoma profile yake utashindwa kutrace familia yake..
 

Attachments

  • Screenshot_20181109-135157~2.jpg
    Screenshot_20181109-135157~2.jpg
    116.7 KB · Views: 36
  • Screenshot_20181109-135157~2.jpg
    Screenshot_20181109-135157~2.jpg
    116.7 KB · Views: 35
hiyo ni Bio frofile ya Jim acosta...nguli wa Mwanahabari white house mbishi ,kichwa wa kuchambua habari za white house ,mpiga maswali mazito maraisi wanaoingia Ikulu huwa wanamwogopa huyu jamaa..
Ila sasa ukisoma profile yake utashindwa kutrace familia yake..
Aisee Kazi kweli kweli ... lmfao
 
mkuu watu walishaaanza kitambo haya mambo..wakiona wew ni mtu muhimu kwao ni kutengeneza clone yako ambayo wataisubject mahala ambapo pataifaaa ili ikafanye kazi zingine mbadla bila kupoteza maarifa ya recipient( original ) yake..

Tumebaki tu sisi huku kuhangaika na kusoma eti ukawe usalama wa taifa ...ha ha ha utasubiri sana labda kuwa barozi wa nyumba kumi huku kwetu ndo usalama wa taifa.. 😕 😕
hahaa " inafikirisha sana .. hiyo Tech imekuja kuleta kizaa zaa kikubwa sana duniani "... hili ni zaidi ya balaa
 
Habari za weekend wana JF, kuna swali nimekua nikijiuliza muda mrefu sana na kuna mada iliwekwa humu JF ambapo wachangiaji wengi kina Wick na Malcom Lumumba waliijadili hii issue ila kwa kugusia tu maana haikuwa kiini cha mada.

Ukweli mchungu: Pasipo anguko la Malaika (Sons of Gods/Watchers/Anunnakis/Aliens), Mwanadamu angeendelea kubaki kilaza. - JamiiForums

Humo ndani kuliibuka debate kama akili za binadamu ni hereditary/genetic au ni mazingira. Baada ya kusoma tafiti /makala kadhaa nikaona nilete mada humu ili tuweze kujadili suala hili kwa upana zaidi na niweze kupata conclusive answer kwa mjadala ule. Na source yangu kubwa ni study hii ya huyu neurosurgeon niliyeambatanisha pdf yake hapo chini.
View attachment 919915

UTANGULIZI
Akili kwa kifupi tu tunaweza kusema ni uwezo wa kufikiri au kuchanganua masuala mbalimbali yanayotuzunguka na kwa mingi wanasayansi wamejaribu kupima hiyo "akili" kati ya mtu na mtu ili kuweza kufahamu sababu halisi za kuwepo utofauti huo yaani mtu kuwa na akili ''ndogo'' au ''kubwa'' kuliko mwenzake.

Mnamo mwaka 1905 serikali ya ufaransa ilitaka kuanzisha mfumo wa "elimu kwa wote" hivyo ikataka kugundua watoto wenye ''akili ndogo'' ili wapewe elimu maalum kuwawezesha kusoma kwa spidi yao kuliko kuwabakisha nyumbani tu au kuitwa "wehu". Mtihani huu uliitwa stanford-simon test ambapo ulikuwa unapima vitu vikuu vitano ambako na sisi ningependa tutumie tunapoendelea na mjadala huu sababu hizi factors ndio zimeweka msingi wa IQ tests na mbinu karibu zote duniani za kupima akili ya mtu.

1.Maarifa (knowledge) ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kuelewa mambo yanayomzunguka mfano mtoto aliulizwa kushiba au kuchoka ndio nini?

2. uchanganuzi wa hesabu (Quantitative reasoning) ; Hapa mtoto anaulizwa masuala ya hesabu ili kupima uwezo wa akili yake mfano kujumlisha,kutoa,kugawanya n.k

3. Working memory yaani Kumbukumbu ya muda mfupi ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kutunza mambo aliyofundishwa au kuyashuhudia muda mfupi tu uliopita mfano kama unawaonyesha picha basi unawauliza picha ya kwanza kuwaonyesha ilikuwa ya nani.

4. Visual-spatial processing yaani utambuzi wa vitu kwa kuangalia mfano uhusiano baina ya picha na zaidi inayotumika ni puzzle ambapo mtoto alitakiwa kupanga vipande tofauti ili vitengeneze picha moja.
View attachment 919908
5.Ya mwisho ni uwezo wa kuchanganua (fluid reasoning) yaani uwezo wa kufikiri na kupata suluhisho kwa jambo ambalo halitegemei kitu ulichowahi fundishwa au kukutana nacho huko nyuma mfano kuunganisha dots za suala fulani fulani ili upate picha kamili mfano hapa chini ambapo mtoto ataulizwa umbo gani ndio sahihi kuwekwa kwenye alama ya kiulizo??
View attachment 919909
NADHARIA
Baada ya kujua baadhi ya vitu tunavyopima kwenye uwezo wa akili ya mtu.... Basi tuangalie nadharia mbalimbali zilizoletwa juu ya mjadala huu.

1. Akili hurithishwa /Heritability.
Kwenye nadharia hii baadhi ya wanasaikolojia wamejaribu kufanya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa akili ya mtu hurtishishwa kutoka kwa mzazi hivyo uwezo wa akili za wazazi ndio utaamua uwezo wa wanaye kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa tafiti nilioambatanisha hapo chini inaonyesha mapacha wakufanana wana wana akili (IQ) zinazofanana kuliko mapacha wasiofanana ikimaanisha jenetiki zina nafasi ya kucheza kwenye kuamua akili ya mtoto. Vilevile utafiti mwingine ukaonyesha ndugu waliokuzwa kwenye nyumba moja wana akili zinazofanana kuliko watoto wasio na undugu waliokuzwa eneo moja ikimaanisha genetics za kifamilia ndio huamua akili ya mtoto na sio makuzi/malezi n.k

Nadhari nyingine inayotumika humu ni wilson effect ambayo inasema mtu anapozidi kukua basi uwezo wa akili yake unakuwa umechangiwa na akili za kurithi kuliko sababu zingine zozote na alihitimisha kwa utafiti unaoonyesha 60% mpaka 80% ya akili ya mtu mzima huwa imerithiwa kutoka kwa kizazi chake na zilizobaki ndio sababu zingine kama elimu,makuzi,mazingira,uzoefu,afya n.k

2. Mazingira/makuzi
Nadharia ya pili inadai mtoto huzaliwa na uwezo wa akili wa kawaida ila mazingira au makuzi atayakayopata ndio yataamua akili yake hapa duniani. Tafiti mbalimbali zimefanyika mfano weinberg (1989) unaonyesha mapacha wanaofanana waliokuzwa mazingira tofauti kabisa uwezo wa akili zao haukufanana ikimaanisha uwezo wa akili huamuliwa na mazingira ambayo mtoto anakulia na sio kurithi akili za mzazi. Mfano mtoto ambaye baba na mama yake wana akili ila amekulia mazingira ya umaskini hivyo kula yake ni ya shida na hapati lishe bora hasa udogoni inaathiri size ya ubongo wake hasa ubongo wa mbele (frontal lobes) hivyo itasababisha uwezo wake wa akili kupungua sana. Ama mtoto mwenye uwezo mdogo wa akili akikulia mazingira ambayo wazazi wanamjengea uwezo wa kufikiri kama kumpa maarifa kadha wa kadha toka akiwa mdogo,kusoma vitabu,mitihani ya kimaisha ya kumfanya afikiri basi mtoto huyu akili yake (IQ) itapanuka muda unavyozidi kusogea.

View attachment 919916

Tabula rasa
Hii ni nadharia iliyoanzishwa na John locke (1690) inayodai mtoto akizaliwa huwa ni MWEUPE kichwani ila uwezo wake wa akili utaamuliwa na mazingira,uzoefu,maarifa atakayopata kwenye makuzi,mazingira au uzoefu anavyozidi kukua. Hivyo kwa kiujumla nadharia hii inasema haijalishi mtoto kazaliwa na akili gani ila makuzi yake ndio yataamuwa kama atakuwa na akili ''kubwa'' au ''ndogo''.

NB: tunapoongelea akili hatumaanishi za darasani na hatumaanishi jinsi mtu anavyozitumia bali tunamaanisha UWEZO wa juu zaidi ambao anaweza kutumia kufikiri hata kama bado hajaamua kuutumia ipasavyo. Kiufupi tunaangalia brain CAPACITY sio PERFORMANCE. Maana kuna wengine wana akili kubwa ila hawajawekewa mazingira ya kuzitumia kwa ukamilifu wake so tunapojadili tuwe nalo hili kichwani.

Naomba kuwasilisha
Cc
Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu

Hongera sana Bwana Athenian,kwa kuleta mada nzuri! Na pongezi kwa Wadau wote kwa kuonesha jinsi gani mlivyo makini na mambo maridadi kama haya ya Ufahamu juu ya HISA YA AKILI.(IQ).

Mambo yote ya msingi yameelezwa na wachangiaji wengine na mimi nitachangia kiduchu tu.
Jambo hili la Kuwa na HISA YA AKILI(IQ) kubwa au ndogo limekuwa mjadala wa muda mrefu kabla hata ya kristo!
Myunani Socrates yeye aliafiki kuwa binadamu huzaliwa na Uwezo Tofauti tofauti wa hisa ya akili na kwa kadri ya Uwezo huo alishauri kuwa watu hawa wapewe majukumu kulingana na kundi la hisa ya akili wanayoangukia!
Yeye akadai Kuna makundi yafuatayo ya hisa ya Akili:-

1.GOLDEN BOYS/GIRLS - (Highest IQ) Huwa na IQ kubwa sana hutegemewa kuwa Viongozi wa Wakuu waandamizi katika Nchi!
Kama Vile;Wakuu wa Vitengo nyeti vya Serikali( Fedha,Ulinzi,Afya na Elimu- Chief Treasurer,Wanasayansi wavumbuzi,Professors,Wachumi,Mabalozi,Wakurugenzi na nk)
2.SILVER BOYS/GIRLS - (Average IQ) Huwa na hisa ya kati ya Akili hawa hutegemewa kuwa Watendaji muhimu wa kazi za kawaida katika nchi - Kama vile Walimu,Wanasheria,Askari,Clerks na nk)
3.IRON BOYS/GIRLS - (Low IQ) Hawa huwa na hisa ya chini ya akili,hivyo hutegemewa kufanya kazi za nguvu zaidi kuliko kufanya kazi za akili,mfano shambani,wachimbaji migodini,Wasukuma mikokoteni,eti hawa jamaa hata tu kutandika kitanda huwa ni shida!
Hivyo ndivyo Socrates alichambua Hisa ya Akili.

Lakini nadharia nyingine ikaja baada ya majaribio ya Kisayansi - Walichukuliwa mapacha wa Mama na Baba mmoja wakawekwa kwenye mazingira yanayofanana wakapewa mahitaji sawa;lakini mwisho wa siku hawakuonesha hisa ya akili inayofanana! walitofautiana kwenye mambo mengi hiyo ikatoa shaka sana juu ya maelezo kuwa hisa ya akili inachangiwa na mazingira na lishe!
Ndipo ikaja nadharia ambayo wengi lazima tuikubali kwa sababu usipoikubali hii basi tena:- MULTIPLE INTELLIGENCE.- There are multiple intelligence not one general intelligence.
Hii inasema binadamu huzaliwa na Uwezo tofauti tofauti sana! na wote wanaweza uonesha Ufanikio mkubwa sana katika hisa mbali mbali za akili hapa!
Kama ifuatavyo:-
1.Lugha
2.Mantiki
3.Ujuzi vitu - udereva
4.Muziki
5.Sarakasi na michezo
6.Uwezo wa Kusema na kushawishi
7.Uwezo wa kujitambua na kujiongoza vema


Hivyo unakuta mtu ni Prof. lakini Hajui kabisa na utamuua ukimwambia kupiga kinanda ama sarakasi hata ajitahidi vipi hataweza au akiweza inakuwa underperformed/mediocre!
Mtaalam wa Saikolojia anaweza asiweze kabisa kusuluhisha mizozo ingawaje amejifunza saikolojia vema.
Mwalimu/msomi mzuri wa Physics akashindwa kabisa kuelekeza wengine wakaelewa somo lake akaishia kushika darasa zima.
Hivyo unapopima Intelligence Quotient zingatia sana kuwa hatupo tena katika mfumo wakupima one general intelligence(Intellect). Pima pia na uwezo mwingine mbali na ule wa darasani.

Nimewahi sikia pia, ila sina uhakika kwamba Mama ndiye mbeba akili ya watoto wako! Hivyo kabla ya kuoa fanya kautafiti kadogo hivi! angalia shemeji zako watarajiwa wa kike na wakiume wanafanya shughuli gani! Kabla yakuja laumu kuwa watoto wako wanashida!

Jambo lingine la Ajabu-Ni hisa ya Akili ya Walemavu wa Akili - Mental disabled individuals, hawa bwana wale "profound!" Huwa wanauwezo wa ajabu wa kubuni,kuchonga na mitambo! anaweza fanya jambo mpaka ukaogopa! Niliwahi shuhudia jamaa - katengeneza mashine ya kukoboa ya ukubwa wa box la kilo moja hivi.Anaweka mpunga unapita na kukobolewa lakini ukimtazama ni profound kabisa.
Hivyo hii inathibitisha mtu anaweza asiwe mzuri wa alama A+ za formal examinations,lakini akawa na uwezo mkubwa tu katika eneo lingine la maisha!.
Swali kwa wanajamii! Je Mfalme au Rais ( Viongozi wetu) lazima wawe katika kundi na 1 la IQ? au wazungukwe na kundi namba la IQ1?
Shukrani!
 
ha ha ha ha inawezekana kabsa kuzaa au kupata mtoto taahira katika mazingira yote haijalishi nyumbani kwenu kuna natural history ya mental disorders among familiy members au laaa...

Lakini kuna study nyingi zimeshafanyika kuhusu kuzaaa watoto wenye mental disability huku wazazi wao wakiwa wazima kabsaa bila hata kuwa na family history ya ugonjwa huo.

kwa mfano mama anapokuwa na stress za kufaaa mtu wakati akiwa mjamzito anakuwa anazuia baadhi ya vichocheo( hormones) kusafirishwa kwenda kwa mtoto hasa vichocheo vinavyohusika na brain formation vinapokuwa haba kwa mtoto ,hapo mtoto lazima azaliwe na mental disorder flani..

Mama akiwa na depression( msongo wa mawazo) akiwa mjamzito lazima apate effects kubwa sana mtoto wake..

lakini pia inawezekana kabisa professor mzima akapata watoto taahira kama msomi huyu atapata mental disconfiguration akiwa mzima( namanisha akiwekwa kwenye mazingira ambayo yatachange au ku alter mental status yake ) hapo percent ya kupata mtoto taahira ni 25% .


Kwa hiyo Intelligence inabaki ni multifactorial continnum hasa katika inheritance yake..

Lakini haimanishi kuwa mtoto akiwa taahira tayari anakuwa na uwezo mdogo wa akili hapana..
kuna watu ni vichaaa lakini wana intelligence kubwa,inategemea na eneo gani kwenye ubongo( mind) limekuwa disfigured na enveronmental factors...

Intelligence ipo vice versa na mental disability...tena inasemekana kwamba kadri mtu anavyozidi kuwa na IQ kubwa ndipo anazidi kuwa na symptoms ( Dalili) za ukichaaa kuliko mtu anayejiheshimu zaidi!!

Fuatilia maisha ya akina Tesla,Isaac newton,Galileo Gallilei na Albert Einsten na wengine kibao ,yani maisha yao yalikuwa ni kujitengetenga na jamii na unakuta sometimes mambo ambayo jamaaa imekubaliana tusiyafanye wao ndo walikuwa wanayafanya na ndo mana walikuwa wanaonekana kituko simply because their sense of cognition ipo katika dimension kubwa sana kuanzia 6D huko kuliko Ng'ng'ona wengine wenye 2D recognition view..

Ndo mana unaweza uka asses intelligence spectrum range ya mtoto wako akiwa mdogo kabsaa...

Key factor ya kwanza ni mtoto kujitenga na wenzie..yani unakuta anapenda kucheza peke yake..ukiona hivyo jua mtoto wako ni bonge la genius wa kutupa usimwachanize mazingira yakamharibu..kaa naye makini sana.

Keys factor nyingine kudetermine mtoto wako ni intelligence ni utundu wa kutupa huku akiwa lonely muda mwingi hawa tunawaweka kwenye Autistic spectrum disorders japo study nyingi zinasema watoto watundu wanakuwa na IQ ndogo kwa sababu wanakosa concentration ya kusikiliza lakini 25% ya watoto ambao ni Autistic ( wana Autism) wana IQ kubwa sana...

Kwa hiyo intelligence bado inaonekana kuwa ni multifactorial continnum kabsaa...japo gene ndo zinabaki kuwa wahusika wakuu sana wa kuleta intelligence ya mtu..
Shukran mkuu, umeongelea factor mbali mbali zinaweza kuleta hayo matatizo ya vichocheo vya kulisha ubongo kukosekana na kuleta hizo mental disability. Na vipi haya ma chromosomal disorder, kama mutation na mengine kwenye hii inteligency issue. Sijui ni gene gani zina husika kutengeneza bongo zetu, lakini hii brain ina tokana na gene pairing during meiosis kama sikosei, na sayansi ya embriology haisemi ni nini au genes zipi zinaunda ubongo au sijui ndio akili, wao husema tu viungo mbali mbali hutengenezwa during differentiation ya mesenchymal sterm cells, humo ndimo hutokea deletions, invertion, translocation na mengine hadi tuna pata hayo ma disabilities mbalimbali.
Sasa swali langu, hivyo vichocheo sijui ni hormones au nini vinaweza kuponyesha chromosomal disorder kama vitazalishwa kwa wingi kuulisha ubongo ambao tayari una configuration defects/disconfigured au niseme ubongo ambao hau kukamilika una miss kitu, au kuna kitu zaidi ndani yake?! Could be mutational factors, Na je ubongo ulio kamilika kimuundo, lakini haukupata hivi vichocheo kabisa unaweza kufunction sawa?! Maana naanza kuchanganyikiwa ikiwa normal brain ndiyo akili au akili ni hivi vichocheo?! Sijui utanielewa maana hata mimi napotea sasa.
 
Fuatilia namna ya kuajili wataalamu wa intelligensia nchi zilizoendelea utakuta bioprofile data zao zinachekesha kama sio kuchanganya...

Utakuta baba yake kaandikwa kuwa ni mzawa wa Israel na mamake ni mzawa wa Australia ili iwe ngumu kumtrace zaidi..

ndo mana inakuwa ngumu sana kujua originality ya Intelligence officers...

fuatilia utakuja kunambia...

nasikia hata ikulu maalumu zimeanza kuwa na Artificial Intelligence officers..

Kwa mfano ikulu ya marekani inamshitukia sana mwanahabari wa CNN Abilio James "Jim" Acosta ambaye juzi kama sio jana kapigwa marufuku kuingia white house huku kwa kuwa na kibuli cha kubishana na jiwe( Trump) 😀 akiwa na nature ya kuwa clone...jamaa inasemekana ni clone na kapandikizwa pale white huse kuwa reporter wa CNN lakini inasemekana jamaa ni replica clone wa mtu ..

Na ukifuatilia uraia wake jamaa unashangaza mara baba yake sijui ni nani na mamake taifa gani ...

Aise wenzetu wapo level zingine kabsa sasa hivi...

Juzi juzi tu nchi ya tunisia imepewa Ma Intelligence officers kutoka Israel lakini inasemekana ni ma clone kabssa na lengo lao ni kuchota taarifa muhimu...
Hii hatari had Tanzania tuje tufike hii level ya wenzetu tutakuwa hatuwezi tena ku fikiria tena aisee.
Huyo mwandishi wa CNN mubishi Trump Ana allergy naye aisee.

Nchi yetu inahtaji kuwekeza mno kwenye science
 
anakuwa ni replica Intelligence...ila ananyimwa kumbukumbu ...ne needs memory booster kumrejeshea ya nyuma but after that anakuwa sawa...

Mammbo mazito chief...
Nadhani hii ya cloning kafanyiwa pia Kanye West maana kichwa chake siku hizi pia ma star wa kubwa ni ma cloning ka kina Oprah nilisoma hizi habari za cloning zikanichaganya Ila ufafanuzi wako umenifunua akili
 
Mimi kutokana na kusom soma kwa mambo ya akili huwa changiwa na mabo makuu mawil ambayo
Kurithi
Kurithi huchukua nafasi kubwa sana ya akili ya binadamu na

Mazingr
Mazingr yananafis kiac ila c kubwa sana kama kurithi

Uhusiano upo kwa 60% kurithi na 40% mazingr
 
Duh umeeleza sana katika molecular level/proffesional explanation...sasa sijui wataelewa wangapi
Hahaha hii JF unauliza wataelewa wangapi?! Kwa taarifa yako humu kila mtu genius, JF bana ukieleza issue shallow utapondwa sana, mi nakubali lifecoded anavyoeleza, hizi ID fake za JF nyuma yake kuna watu wa kila aina, na interest tofauti. Unaweza mdharau mtu kumbe lecturer wa cell biology huko havard. Uwe unasoma tu na kupita, ni kweli wapo tusioelewa lakini kwa like alizopata lifecoded ina maana wameelewa hao.
 
lakini pia kuna ukakasi sana juu ya kutumia Surrogate mother kwenye human cloning ambapo tunaona kuwa watu wanatak kutoa specie au clone yenye uelewa ule ule na mhusika ila wanampandikizia mother ( surrogate) na anakuja kedeliver product ile ile desired....

sasa hapa najiuliza tena mchango wa mama unakosekana....ha ha ha hatari snaa...
Hahaha hili swala la sorrogate mothers linaweza kulisha swali langu la taahira aliyebakwa na kuzaa mtoto mzima, sijui huyu mama ana mchango gani ikuwa embryology ikiishatokea kinachofuata ni mesenchymal cell differentiation mpaka kuzaliwa?! Vipi watoto wa chupa yaani IVF baby wanapata wapi vichocheo hivi kutengeneza brain zao ikiwa zaidi ya 6 weeks w ako nje mama?!
 
Me naona analogy ya akili, ni sawa na kusema sigara zina sababisha kansa. Hatuwezi kusema sigara zinasababisha kansa moja kwa moja kuna watu wamevuta miaka nenda rudi na wapo poa, lakini sasa kuna wengine kweli chanzo cha kansa yao ni sigara!!! Kwa hyo hakuna jibu kamili

Akili siamini kama ni ya kurithi, mazingira unaweza ukapewa mazuri tu na bado ukawa lofa, na unaweza ukawa na mazingira mabaya tu na uwezo wako wa akili ukawa vizuri. Kwa hiyo siamini kama mazingira ni chanzo, na akili si za kurithi!!! Watu wanaweza pewa mazingira sawa ila mmoja akawa na akili kuliko mwenzake. Nina amini tuna akili sawa ila tunatofautiana u "sharp' wa akili. Kwa hyo hakuna jibu kamili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom