Intelligence heredity: Je, uwezo wa akili hurithiwa?

Habari za weekend wana JF, kuna swali nimekua nikijiuliza muda mrefu sana na kuna mada iliwekwa humu JF ambapo wachangiaji wengi kina Wick na Malcom Lumumba waliijadili hii issue ila kwa kugusia tu maana haikuwa kiini cha mada.

Ukweli mchungu: Pasipo anguko la Malaika (Sons of Gods/Watchers/Anunnakis/Aliens), Mwanadamu angeendelea kubaki kilaza. - JamiiForums

Humo ndani kuliibuka debate kama akili za binadamu ni hereditary/genetic au ni mazingira. Baada ya kusoma tafiti /makala kadhaa nikaona nilete mada humu ili tuweze kujadili suala hili kwa upana zaidi na niweze kupata conclusive answer kwa mjadala ule. Na source yangu kubwa ni study hii ya huyu neurosurgeon niliyeambatanisha pdf yake hapo chini.
View attachment 919915

UTANGULIZI
Akili kwa kifupi tu tunaweza kusema ni uwezo wa kufikiri au kuchanganua masuala mbalimbali yanayotuzunguka na kwa mingi wanasayansi wamejaribu kupima hiyo "akili" kati ya mtu na mtu ili kuweza kufahamu sababu halisi za kuwepo utofauti huo yaani mtu kuwa na akili ''ndogo'' au ''kubwa'' kuliko mwenzake.

Mnamo mwaka 1905 serikali ya ufaransa ilitaka kuanzisha mfumo wa "elimu kwa wote" hivyo ikataka kugundua watoto wenye ''akili ndogo'' ili wapewe elimu maalum kuwawezesha kusoma kwa spidi yao kuliko kuwabakisha nyumbani tu au kuitwa "wehu". Mtihani huu uliitwa stanford-simon test ambapo ulikuwa unapima vitu vikuu vitano ambako na sisi ningependa tutumie tunapoendelea na mjadala huu sababu hizi factors ndio zimeweka msingi wa IQ tests na mbinu karibu zote duniani za kupima akili ya mtu.

1.Maarifa (knowledge) ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kuelewa mambo yanayomzunguka mfano mtoto aliulizwa kushiba au kuchoka ndio nini?

2. uchanganuzi wa hesabu (Quantitative reasoning) ; Hapa mtoto anaulizwa masuala ya hesabu ili kupima uwezo wa akili yake mfano kujumlisha,kutoa,kugawanya n.k

3. Working memory yaani Kumbukumbu ya muda mfupi ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kutunza mambo aliyofundishwa au kuyashuhudia muda mfupi tu uliopita mfano kama unawaonyesha picha basi unawauliza picha ya kwanza kuwaonyesha ilikuwa ya nani.

4. Visual-spatial processing yaani utambuzi wa vitu kwa kuangalia mfano uhusiano baina ya picha na zaidi inayotumika ni puzzle ambapo mtoto alitakiwa kupanga vipande tofauti ili vitengeneze picha moja.
View attachment 919908
5.Ya mwisho ni uwezo wa kuchanganua (fluid reasoning) yaani uwezo wa kufikiri na kupata suluhisho kwa jambo ambalo halitegemei kitu ulichowahi fundishwa au kukutana nacho huko nyuma mfano kuunganisha dots za suala fulani fulani ili upate picha kamili mfano hapa chini ambapo mtoto ataulizwa umbo gani ndio sahihi kuwekwa kwenye alama ya kiulizo??
View attachment 919909
NADHARIA
Baada ya kujua baadhi ya vitu tunavyopima kwenye uwezo wa akili ya mtu.... Basi tuangalie nadharia mbalimbali zilizoletwa juu ya mjadala huu.

1. Akili hurithishwa /Heritability.
Kwenye nadharia hii baadhi ya wanasaikolojia wamejaribu kufanya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa akili ya mtu hurtishishwa kutoka kwa mzazi hivyo uwezo wa akili za wazazi ndio utaamua uwezo wa wanaye kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa tafiti nilioambatanisha hapo chini inaonyesha mapacha wakufanana wana wana akili (IQ) zinazofanana kuliko mapacha wasiofanana ikimaanisha jenetiki zina nafasi ya kucheza kwenye kuamua akili ya mtoto. Vilevile utafiti mwingine ukaonyesha ndugu waliokuzwa kwenye nyumba moja wana akili zinazofanana kuliko watoto wasio na undugu waliokuzwa eneo moja ikimaanisha genetics za kifamilia ndio huamua akili ya mtoto na sio makuzi/malezi n.k

Nadhari nyingine inayotumika humu ni wilson effect ambayo inasema mtu anapozidi kukua basi uwezo wa akili yake unakuwa umechangiwa na akili za kurithi kuliko sababu zingine zozote na alihitimisha kwa utafiti unaoonyesha 60% mpaka 80% ya akili ya mtu mzima huwa imerithiwa kutoka kwa kizazi chake na zilizobaki ndio sababu zingine kama elimu,makuzi,mazingira,uzoefu,afya n.k

2. Mazingira/makuzi
Nadharia ya pili inadai mtoto huzaliwa na uwezo wa akili wa kawaida ila mazingira au makuzi atayakayopata ndio yataamua akili yake hapa duniani. Tafiti mbalimbali zimefanyika mfano weinberg (1989) unaonyesha mapacha wanaofanana waliokuzwa mazingira tofauti kabisa uwezo wa akili zao haukufanana ikimaanisha uwezo wa akili huamuliwa na mazingira ambayo mtoto anakulia na sio kurithi akili za mzazi. Mfano mtoto ambaye baba na mama yake wana akili ila amekulia mazingira ya umaskini hivyo kula yake ni ya shida na hapati lishe bora hasa udogoni inaathiri size ya ubongo wake hasa ubongo wa mbele (frontal lobes) hivyo itasababisha uwezo wake wa akili kupungua sana. Ama mtoto mwenye uwezo mdogo wa akili akikulia mazingira ambayo wazazi wanamjengea uwezo wa kufikiri kama kumpa maarifa kadha wa kadha toka akiwa mdogo,kusoma vitabu,mitihani ya kimaisha ya kumfanya afikiri basi mtoto huyu akili yake (IQ) itapanuka muda unavyozidi kusogea.

View attachment 919916

Tabula rasa
Hii ni nadharia iliyoanzishwa na John locke (1690) inayodai mtoto akizaliwa huwa ni MWEUPE kichwani ila uwezo wake wa akili utaamuliwa na mazingira,uzoefu,maarifa atakayopata kwenye makuzi,mazingira au uzoefu anavyozidi kukua. Hivyo kwa kiujumla nadharia hii inasema haijalishi mtoto kazaliwa na akili gani ila makuzi yake ndio yataamuwa kama atakuwa na akili ''kubwa'' au ''ndogo''.

NB: tunapoongelea akili hatumaanishi za darasani na hatumaanishi jinsi mtu anavyozitumia bali tunamaanisha UWEZO wa juu zaidi ambao anaweza kutumia kufikiri hata kama bado hajaamua kuutumia ipasavyo. Kiufupi tunaangalia brain CAPACITY sio PERFORMANCE. Maana kuna wengine wana akili kubwa ila hawajawekewa mazingira ya kuzitumia kwa ukamilifu wake so tunapojadili tuwe nalo hili kichwani.

Naomba kuwasilisha
Cc
Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu
Ahsante mkuu kuna mjambo mkubwa sana hapa nimejifunza natanguliza shukran kwa madini haya narudi kuchangia hoja
 
Kimsingi Akili zinaweza kurithiwa na hutegemea mazingira pia nakumbuka nlisomaga somewhere kuwa watoto watakao zaliwa mbeleni lets say 2080 watakuwa wanvichwa vikubwa coz ubongo wao utakuwa mkubwa zaid ya hii tulionayo kwa manaa wazazi wa watoto husika watakuwa wanatumia nguvu ya akili nyingi kung'amua yale yanayowazunguka kwa kipindi hicho hata ukiangalia kiuhalisia kizazi chetu ndo kinaishia baba zetu wengi hawakusoma i mean darasa hata moja na wakaishi lakini after 20 years unafikiri ni wazaz wangapi wa watoto watakao zaliwa wakati huo watakuwa hawajasoma na kuwa na uwezo mdogo kimaarifa?hivo naamini katika akili hurithiwa kutoka kizazi na kizazi lakini kwa kupewa nafasi ya kizazi kujijua
 
Swala la akili linategemea vitu mbalimbali(multifactorial factors) ambavyo kwa pamoja vina play part ku-determine level ya akili

Kitu kinacho kuwa determined na multifactorial factors huwa ni very complex kukielezea

Level ya akili haiwezi kuwa attributed to a single factor
 
Daaaah...umenitag mkuu...!! aya bana ..

But hongera kwa maada fikilishi...

lakini nataka nichangia mada hii katika analysis ambayo inaweza isiwe imebase na jinsi wengine wanavyoweza kuchangia kwa facts za lishe bora pamoja na genetic influence kutoka kwa wazazi hasa mama...

Mpaka sasa bado jopo la madakatri hasa Neural scietists pamoja na psychiatrists ambao kazi yao kubwa ni kucheza na cognitive brain function ambayo inahusisha eneo moja pekee la ubongo lijulikanalo kama Prefrontal cotex ....

Wanasema kuwa Cognitive function ya ubongo( sehemu inayohusika na uelewa katika ubongo wa mwanadamu) ipo under neural circuit guided na Neural transmitter nyingi sana including Dopamine,Noradrenaline,Adrenaline yenyewe,serotonin,melatonin,GABA, pamoja na zinginr kibaoa ambayo utendaji kazi wake upo Antagost au agonizing zaid kutegemea na hitaji la ubongo au akili katika kutenda...

Kuna neurol transmitter hapo zinahusika na mambo ya firing au kuruhusu transimssion ya impulse kwa speed kubwa sana na zingine zinahusika na kudhibiti high neural firing rate hence zinazuia impulse rate changes katika specific part ya ubongo ...

Ukisoma mambo ya Dopaminergic pathways hapa unaweza ukaelewa ninachoongelea...

Twende kwenye mada yenyew what guides intelligence to a singular person ..??

Kuna kitu kinaitwa CPH4 ( 6-carboxytetrahydropterin synthase) hii ni enzymes ambayo mara nyingi inahusika na conversion snyingi sana ambazo huwa zinagive out Queuosine, ambayo ni component muhimu sana katika kuincrease neural firing ratio ya chemical maalumu ambazo zinahusika na prefrontal cotex capacity inayohusika na mambo ya cognitive function ya brain hasa maeneo ya limbic system ,amygdala na mengine ambayo yanahusika na memory pamoja na Intelligence brain centre...

Ili mtu tuseme kuwa ana akili nyingi sana au ana Intelligence kubwa ni lazima eneo flani la ubongo lazima liwe busy sana anapokuwa anafikilia au kufanya mazungumzo juu ya swali aliloulizwa...

Madaktari kutoka Armstadam ,Netherland walifanya jaribio moja kwa kutumia Electroencephalogram (EEG) kupima brain hyperactivity wakati mtu anapokuwa kwenye maswali magumu yanayomfanya mtu afikilie sana ila wakaja kugundua kuwa ni eneo moja tu la prefrontal cotex ndo lilionekana kuwa busy snaa wakati wa kufikilia...pia eneo hili ndilo linalohusika na mambo ya kuactivate brain function hasa mtu akiwa bado mdogo sana,,,consider about Mutism spectrum disorders kwa watoto wadogo ambao ni moj wapo ya mental disorder amabyo inawapata watoto wanapozaliwa na mara nyingi huathiri cognitive behavioral pattern ya mtoto husika.

Hivyo iliwafanya waanze kuchunguza zaidi why eneo lile ..Ila cha kushangaza walikuja kugundua kuwa eneo hilo ndo lilikuww na high neural firing rate za neural transimtter ambazo zinahusika zaidi na mambo ya cognitive function...siyo kila neural transmitter( vichocheo katika ubongo) inahusika na cognitive function...

Unaweza ukawa na high level ya dopamine( katika manic episodes) lakini ukawa na low cognitive function na mwingine akawa na high dopamine neural firing rate lakini akawa na cognitive function kubwa snaa zaidi kuliko mwingine despite wote wapo manic episode au Bipolar conditioned state...

Ukitaka kuelewa zaidi hapa nenda magaereza ya wafungwa ambao ni wagonjwa ndo utaelewa ninachozungumza hapa kuwa kuna vichaaa utakuta uwezo wake upo juu sana yani kawa geniuz mpaka karun mental disability ila ana high IQ score na mwingine ni mgonjwa wa vile vile bipolar lakini ni mbumbumbu wa kutupa though wote wana high level za dopamine...

Kwa hiyo dopamine sio kigezo sana za kujudge intelligence ...we need something else...

Sas kuna hiyo chemical substance ambayo inaitwa CPH4 ambayo mara nyingi watu wa Neural molecular science hawataki kuweka wazi na wanasema kazi yake bado haijagundukika lakini sio kweli kazi yake inafahamika na ndio chemical wanayoitumia hasa kupima ya Intelligence ya mwanadamu kuanzia akiwa tumboni kwa mama( Embryology) mpaka anapofikisha miaka 25 ...

Inasemekana kuwa japo ni kweli kuwa mama mjamzito akiwa na umri wa mimba ndani ya week 6 ndipo hormone hiyo au chemical hiyo huzalishwa kwa lengo la kwenda kuhimiza utengenezaji wa capacity ya kutosha ya neural circuit receptors kwa ajili ya high firing rate ya imuplse katika specific cognitive brain centre...

Ifahamike kuwa ubongo wa mwanadamu hutengenezwa mtoto akiwa na umri wa week 4 tumboni kwa mama yake kwa hiyo ubongo ukianza kutengenezwa tayari mwili wa mama unasense kuwa tayari ubongo wa mtoto umeanza kutengenezwa na tayari mwili wa mama unaamliwa kuanza kutoa hizo chemicali aina ya CPH4 ambazo zinaenda moja kwa moja kwa mtoto kwa ajili ya kuenhece cerebral formation hasa cognitive area ambalo kazi yake kubwa ni kujenga neural firing receptor za kutosha ili ubongo uwe na high receptors za hizo neural transmitter kwa ajili ya kuprocess information za kutosha katika eneo husika kwenye ubongo kila unapogundua kuwa hilo wazo linatakiwa lifanyiwe kazi katika eneo flani la ubongo basi taarifa muhimu inapelekwa kule kwa speed kubwa sana ambao ni millsecond ndani ya millsecond na tayari cognitive centre inainterprete kuwa hicho kitu jawabu lake ni hili...

The difference in Intelligence between us ni kwa sababu tunazidiana neural firing rate ya taarifa kufika eneo husika kwa muda mfupi sana na kufanyiwa interpretation yake..

Mtu ambaye ni Genius ana high neural firing rate kuliko mtu wa kawaida...manake nini...??

Kuna kitu kinaitwa processor,hiki ndo kifaaa kinachospeed up rate ya taarifa kusafili kwa haraka zaidi kwenye electronic component yoyote..ndo mana hata ubora wa komputer ni processor pamoja na RAM....manake nini kama Laptop au computer yako ina processor ndogo lets say 1.7 GHZ manake utakuwa kila ukiclick file lifunguke linachukua sekunde 4 ndo linafunguka lakini mwenye processor ya 2.7 GHZ akiclik inafunguka ndani ya fraction of second...processor ndo kila kitu ...

Same applied kwenye ubongo wa mwanadamu kinachomfanya mtu aww na upeo mkubwa wa kufikri na kupata jawabu lililo sahihi ni uwezo wa taarifa kufika eneo husika kwa haraka zaidi kisha kufanyiwa interpretation iliyosahihi ndani ya muda ule ule na taarifa zake kupelekwa kwenye cognitive centre kwa ajili ya kumfahamisha mwanadamu kuwa anachowaza au kuhisi ni hiki hapa ...

So kila mwanadamu ana ubongo ule ule the difference is the CPH4 level ambayo inahusika na kutengeneza more brain circuit kwa ajili ya impulse transduction na hapo ndipo hata anatomy(umbo katika physical morphology) ya ubongo huwa ina ratio tofauti za Gyrus na sulcus ambazo ndo zinazoupa ubongo folding morphology kuincrease surface area ya neural firing rate ...

So the level of CPH4 Itaendelea kuwa maintained mpaka pale ubongo utakapokuwa umekamilika...kwa hiyo kama productiom ya hormone hizo ikiwa ndogo basi hata uwezo wa akili wa mtoto unakuwa hafifu ..ndo mana tunasema mama ndo mtu pekeee anayechangia Intelligence ya mtoto na sio baba( hapa katika percent ratio mama anakuwa na nafasi kubwa)..

So kama ukitaka kumaintain high brain au cerebral capacity ya mtoto inabidi mama aproduce high level ya CPH4 during pregnacy kulikoa wakati akiwa ananyonyesha japo huwa ipo kwa kiwango kidogo snaa kwenye colostrum( maziwa ya mwazo kabsa ambayo mtoto hatakiwi kukosa)..

Lakina kuna study zilifanyika miaka ya nyuma na kugundua kuwa mwanadamu wa sasa ( tulio wengi) tunatumia only 10% ya cerebral capacity kisha 90% ya ubongo wetu haufanyi kazi na ikasemekana kuwa laiti binadamu angelitambua hilo kuwa yeye ni infirnity and Immortal basi angeweza kuraise energy na anaweza kuexpand cerebral capacity mpsaka hata 40% kisha anaweza akadevelop some features kama Telekinepathy, psychopathy abilities ambapo anaweza akafungua mambo mazito yaliyo nyuma ya ulimwengu huu na kisha kumfanya aanze kuiview universe katika 8 dimension state....kadri anavyoascend kwenye 100% ndipo uwezo wake unabdilika kwa kasi kubwa sana na anaweza akawa na nguvu ambazo ni uncontrolled =====pengine ndo mana serikali hazitaki kufundisha elimu ya kuraise CPH4 hasa kwa binadamu wa kawaida kwa sababu madhara yake ni makubwa sana.

Nchi za wenzetu wameweza atleast kujua namna ya kummonitor mama mjamzito hasa kuepuka stress wakati wa ujauzito kwani stress ni factor moja kubwa sana inayozuia production ya CPH4 na kumfanya mtoto anakuwa tumboni katika low level ya cerebral capacity formation hence anakuja kuwa na low IQ japo vyakula na lishe bora zinaweza kuboost lakini kwa kiwango kidogo sana....

Lakini pia kama wewe ni mdau wa kufuatilia mambo ya human cloning hasa kupitia project yake ya Maffin project and human cloning kupitia process za somatic-cell nuclear transfer au pluripotent stem cell induction basi hutumia normalizimg ratio ya CPH4 .Lakini pia kisha ukasoma hizo documentaries na scientific writtings zinazoelezea jinsi mradi huo wa siri wa kutengeneza exactly copy wa kiumbe unaemtaka bila kubadili chochote utagundua kuwa wanatumia technolojia under the help ya hizo chemicals hasa during blastula formation wanainduce the same ratio ya CPH4 kwenye morula ya yule clone kwa kufuatisha ratio alizonazo yule recipient wake...

Kabla ya kufanyiwa clone wake unapimwa kwanza cerebral capacity in relation ta CPH4 level kisha ndo anatengenezwa clone wako ambayo atakuja kuwa na Intelligence ile ile uliyokuwa nayo before ..

Forget about human cloning now make sio mada husika...ina nafasi yake..japo ipo siku nitaidondosha hapa rasmi...

kwa mara ya kwanza maabara ya The Thomas J. Watson Research Center. ambayo ilipata kashikashi kwa kuuza taarifa za kimolecular za CPH4 katika maabara kuu tatu ambazo ni ni Argonne National Laboratory,Oak Ridge National Laboratory pamoja na The Center for Integrated Nanotechnologies (CINT) kisha taarifa hizo kuuzwa wa badhi ya director mmoja ambapo kulipelekea kuelezea kazi ya chemical hiyo kwenye movie ya Lucy( 2010) japo usiri umeendelea kutawala zaidi juu ya uwezo au Intelligence ya mwanadamu...

kuna study nyingi zimefanyika kupima kiwango cha CPH4 kwa kina mama tofauti wakiwa wajawazito na kupima Intelligence outcome ya watoto wao na kukuta kuwa kulikuwa na utofauti mkubwa snaa depending na blood chemical level...

Nahitimisha kwa kusema kuwa Intelligence ya mwanadamu imekuwa ni swala gumu sana kulielewa kwani mambo mengi yanakuwa siri nzito sana....

wachache wanatuendesha watakavyo na huenda Nanotechnology ikaja kusolve hiyo paradoxy...

Asanteni...huo ndo mchango wangu kwa mwenye kung'amua machache unaweza fuatilia zaidi hasa kwa kusoma mambo ya Neural science in relatiom to neurotransmitter receptors that govern human Intelligence nadhani utajifunza mengi kuliko hata niliyoelezea .View attachment 920547View attachment 920549
Duh umeeleza sana katika molecular level/proffesional explanation...sasa sijui wataelewa wangapi
 
waniwie radhi...nilikosa maneno sahihi ya kiswahili....

lakini pengine unapoona neno geni kwako ndo mwanzo wa kulifuatilia na kujua mengi zaidi...

Its the source of real exposure ya kujua mengi...

Hata mimi mwanzoni kipindi nafuatia mambo nilikiwa nakutana na terminology za namna hiyo...

Any way kikubwa kujua maana ya neno...
 
Duh kwa haya maisha ya bongo mtu akae chini kuchimba mambo ya prefrontal cortex...aende kutafuta excitatory na inhibitory pathways za neural transmission...amalize hapo aende kucheck kemikali za mama mjamzito zinavyo influence neural circuits za developing fetus

Sidhani kama ni rahisi kiasi hicho
 
mkuu..siyo kwamba et tunaweza kuwa tunaishi nayo ...ni hivi tunaishi na hao viumbe sana mpaka mtaani kwako wapo ila wew unawaona kama binadamu wa kawaida but its not...

Human cloning ilipigwa marufuku kiaina siyo kuwa kufanyika kabisa...kilichopigwa marufuku ni utoaji wa taarifa kwenye jamii( sharing experimental results) ...

Baada ya hapo ndo ikaaanza kupigwa vizuri mpaka leo...

Genetic modified ambayo inatupa vyakula kama samaki,na kuku wa kizungu,ng'ombe pamoja na kondoo ni product ya cloning ...

Huko china,south korea na Singapore wamefikia sehemu wanazalisha samaki kwa kutumia cloned nuclei...

yani unanunua mbegu za samaki maabara kisha unaenda kumwaga kwenye bwawa lako kisha unatupia growth hormones bada ya mwezi mmoja unavuna samaki wako na hao samaki wana minofu tu hakuna mifupa mingi kama wa huku...ni nyama kwenda mbele...

Hiyo ni ndogo,kubwa zaidi ,maffin project ambayo inazalisha clone( human) wenye desired product unayotaka...

yani sasa hivi wanazalisha clone hata ambaye recipient alishakufa miaka ya 1980 huko...

Kuna siri pia ambayo inasemekana jamaa washatengeneza clone ya Albert Einstein pamoja na Nikola tesla ambazo zipo Massecheute Institute of Technology( hii inasemekena lakini) japo sijajua ukweli wake umekaaaja hapa...

Na wale jamaaa sasa hivi wanazalisha watu kisha kuwapandika watu wakiwemo politicians pamoaj na wataalamu kibao kwenye taasisi zetu huku bila sisi kujua ...

uzuri wa clone unaweza ukammodify kwa rangi au race unayoitaka ili kuepuka kushitukiwa kwenye interacting society..

Kuna baadhi ya nchi kama Angola,South Africa na Tunisia zimeingia mkataba na Maffin project kukopeshwa clones zinaziweka kuwasaidia hasa kwenye mambo ya utafiti na kuongoza watu kwa siri ...

Haya mambo ni mazito sana...yani mwisho wa siku utakuja kujuwa kuwa clones wamejaaa mtaani bila kuwajua...kuna baadhi ya documentaries zinavuja kuhusiana na watu maarufu kama kina Rick Ross ,Eminem ,P.Didy,Avril Lavigne,Katty Perry ,Taylor swift na wengine kibao kuhusisha clone zao kuwa ndo zinazoimba na kuratibu mambo yote huku baadhi yao kusemekana kuwa washakufa kitambo sana kwa kushindwa kusell their soul kwa mshirika wao mkubwa...wengine kutokana na umuhimu wao wanaamua kuwaua kisha wanatengeneza clone yao ambayo itakuwa ni mind controlled na wao ili iwe rahisi kuimba na kutoa maudhui yanayoendana na hizo jamiii za siri kuhusu namna wanavyotaka jamiii iishi ..

Juzi juzi tu tumeona skendo ya bwana mdogo Kodack black baada ya kukamatwa na kupelekwa gerezani lakini badae akatoleaa lakini inasemekana iliyotolewa ni clone yake na yeye wamemfungia huko chini wanakowatunza hao original recipient kwa kuwatengenezea mazingira ya kitajiri ambayo yana kila aina ya starehe kiasi kwamba kukumbuka huku duniani inakuwa ngumu snaa na hawawezi kurudi tena ...ndo inakuwa nitoleee...

..mambo mazito sana haya...usione kwanini underground cities zinajengwa ukafikiri watu wanaigiza ..hayo ni makao ya hao produced clone pamoja na recipient zao..

Kwa hiyo swala la Intelligence lipo another level of realm mkuu

so be careful with your leading system tusijekuwa tunaongozwa na clone zao make sio kwa scenario hizi...ha ha ha
After how long cloned human anaweza kumfikia(umri &body size) yule real human?
 
Swala la akili linategemea vitu mbalimbali(multifactorial factors) ambavyo kwa pamoja vina play part ku-determine level ya akili

Kitu kinacho kuwa determined na multifactorial factors huwa ni very complex kukielezea

Level ya akili haiwezi kuwa attributed to a single factor
Ni kweli mkuu hatuwezi peg kwa factor moja tu lakini kwa mtazamo wako kati ya factors tofauti tofauti ni ipi ambayo ndio dominant kwenye kuamua uwezo wa akili ya binadamu?
 
Hapa sasa ndo tunapofika ile point ya kuanza kusema hivi..."Baadhi ya tafiti inaonyesha kwamba akili ya mtu hurisishwa"..."Baadhi ya tafiti inaonyesha akili ya mtu hutegemea mazingira aliyopitia...n.k

So nadhani ni ngumu kusema kipi huwa exactly kina determine akili ya mtu..otherwise uwe unaamini kwamba tafiti fulani ni bora kuliko nyingine
 
Duh kwa haya maisha ya bongo mtu akae chini kuchimba mambo ya prefrontal cortex...aende kutafuta excitatory na inhibitory pathways za neural transmission...amalize hapo aende kucheck kemikali za mama mjamzito zinavyo influence neural circuits za developing fetus

Sidhani kama ni rahisi kiasi hicho
kama vile nimekunotes unabelong kwa Alien's empire.... 🙂 🙂 samahani lakini ....sio kwa kutupia mambo ya excitatory inhibition....ha ha ha just jokin...ila mkuu mpaka leo sijapata jibu kwanini intelligence haitafanana duniani baina ya watu waliopo ...

kama jinsi DNA zilivyo na utafauti na kila mtu basi intelligence nayo haitafanana kamwe....

We differ intelectually by minor fraction but won't be the same... 🙂

Basi nitaconclude kwa kusema kuwa Multifactorial consideration inatumika kuhakikisha gene arrangement kwenye DNA base seqeency inakuwa tofauti kwa kila kiumbe...na hizo hizo multifactorial components ndo zinahusika pia kuregard intelligence ya kila kiumbe husika...

Kuna nadharia pia za dopamine effects wakati mama anapokuwa mjamzito kuwa zinainfluence hormanal balance and distribution katika ukuaji wa mtoto..ila sijawahi kuielewa vizuri hiyo shule yeke...

Lakini pia inasemekana kuwa moody ya mama ndiyo inayogovern neural + hormonal balance katika ukuaji wa mtoto...nahisi kuna study moja ilifanyika ya different pregnant mothers subjected katika different moody swings na kujikuta wakitoa product tofauti tofauti despite ya kuwa subjected kwenye equilibrium food diet ....

wakaja wakaconclude kuwa moody affects more hormonal release kwa mtoto hasa akiwa tumboni kwa mama...

Ndo mana jamaaa wanasisitiza mama mjamzito kuwa away from negative deviation ya moody chart...

hapo unazungumziaje mzeee baba ..?? 😀 😀
 
Hapa sasa ndo tunapofika ile point ya kuanza kusema hivi..."Baadhi ya tafiti inaonyesha kwamba akili ya mtu hurisishwa"..."Baadhi ya tafiti inaonyesha akili ya mtu hutegemea mazingira aliyopitia...n.k

So nadhani ni ngumu kusema kipi huwa exactly kina determine akili ya mtu..otherwise uwe unaamini kwamba tafiti fulani ni bora kuliko nyingine
multifactorial based continuum...

Kuna several factors hapa zina apply ila kuna factor moja kuu itaendelea kuheshimika milele na milele despite uwepo wa enveronment ,diet pamoja na zingine lakini pia genetic nayo ina pary yake.

lakini mkuu unafahamu kuwa kuna mazingira ukiwa subjected ( hasa core of the universe where knowlege na inspiration landers) ukiwa subjected pale tayari intelligence yako inabadilika...??

did you know that ..?

mi nahis ...there is something tries to balance the universal intelligence kulingana na race husika ...

Lakini kama sijakosea ukisoma Intelligence trend inasema kuwa "" Intelligence is governed by gene bases arrangement kwenye DNA strand...

Manake nin....
kuna specific arrangement ndo zinagovern mtu atoke vipi....

make nakumbuka kuna kitabu kimoja kilikuwa kinaelezea maisha ya watu wenye uwezo mkubwa kiakili na nakumbuka point niliyodaka mule ni kwamba inasemekana kuwa eti kwa mfano arrangement yennye base sequence ya lets say CGA GCC GGA huwa inatoa IQ kuanzia 120- 170 yani watakao kuwa kwenye IQ hiyo basi arrangement zao kwenye baadhi ya maaeneo ya DNA kuna sequence hiyo...

Sasa ndo nikawa najiuliza manake huenda ni kweli gene bado zinabeba mambo mengi sana ambayo we need to know exactly ni GIGABYTE NGAPI GENE ZINABEBA MAKE KINACHOGUNDULIKA MULE NI KIDOGO SANA compared na efdects ambazo gene inazalisha kisha tunakimbia kusema kuna mchango wa njee...ndo mana inafikia mahala tunasema unknown causes and effects...

Genetically bado kuna mambo yanahitaji kufanyiwa kazi aise.....

Isije ndo ile program ya kuscan abnormal genes kwwnye miili yetu kisha kureplace with desired gene kwa matokeo mazuri ya kiumbe wa baadae ( Kama Physics of the future by MICHIO KOKU inavyoelezea ila kupunguza kama sio kutokomeza magonjwa kama Kansa,hypertensuon na stroke kwa miaka ya badae ..))

nawaza tu kama inaweza ikawa ni genetic basing analysis
 
kama vile nimekunotes unabelong kwa Alien's empire.... 🙂🙂 samahani lakini ....sio kwa kutupia mambo ya excitatory inhibition....ha ha ha just jokin...ila mkuu mpaka leo sijapata jibu kwanini intelligence haitafanana duniani baina ya watu waliopo ...

kama jinsi DNA zilivyo na utafauti na kila mtu basi intelligence nayo haitafanana kamwe....

We differ intelectually by minor fraction but won't be the same... 🙂

Basi nitaconclude kwa kusema kuwa Multifactorial consideration inatumika kuhakikisha gene arrangement kwenye DNA base seqeency inakuwa tofauti kwa kila kiumbe...na hizo hizo multifactorial components ndo zinahusika pia kuregard intelligence ya kila kiumbe husika...

Kuna nadharia pia za dopamine effects wakati mama anapokuwa mjamzito kuwa zinainfluence hormanal balance and distribution katika ukuaji wa mtoto..ila sijawahi kuielewa vizuri hiyo shule yeke...

Lakini pia inasemekana kuwa moody ya mama ndiyo inayogovern neural + hormonal balance katika ukuaji wa mtoto...nahisi kuna study moja ilifanyika ya different pregnant mothers subjected katika different moody swings na kujikuta wakitoa product tofauti tofauti despite ya kuwa subjected kwenye equilibrium food diet ....

wakaja wakaconclude kuwa moody affects more hormonal release kwa mtoto hasa akiwa tumboni kwa mama...

Ndo mana jamaaa wanasisitiza mama mjamzito kuwa away from negative deviation ya moody chart...

hapo unazungumziaje mzeee baba ..?? 😀😀
Duh sina la kusema mzee baba...

Ila huwa mimi nikionaga wameandika statement kama hii..."The exact mechanism is unknown or is unclear" kitu kama hicho huwa nakosa morali nacho kabisa kwa kuwa utakutana na a lot of studies (kuanzia huko mwaka 1690's mpaka saiv)...na kila moja ya study unakuta inakuja na findings tofauti tena za kupasua kichwa chako...otherwise labda uwe interested enough na hicho kitu bila kujali kina any useful outcomes kwako mwenyewe
 
multifactorial based continuum...

Kuna several factors hapa zina apply ila kuna factor moja kuu itaendelea kuheshimika milele na milele despite uwepo wa enveronment ,diet pamoja na zingine lakini pia genetic nayo ina pary yake.

lakini mkuu unafahamu kuwa kuna mazingira ukiwa subjected ( hasa core of the universe where knowlege na inspiration landers) ukiwa subjected pale tayari intelligence yako inabadilika...??

did you know that ..?

mi nahis ...there is something tries to balance the universal intelligence kulingana na race husika ...

Lakini kama sijakosea ukisoma Intelligence trend inasema kuwa "" Intelligence is governed by gene bases arrangement kwenye DNA strand...

Manake nin....
kuna specific arrangement ndo zinagovern mtu atoke vipi....

make nakumbuka kuna kitabu kimoja kilikuwa kinaelezea maisha ya watu wenye uwezo mkubwa kiakili na nakumbuka point niliyodaka mule ni kwamba inasemekana kuwa eti kwa mfano arrangement yennye base sequence ya lets say CGA GCC GGA huwa inatoa IQ kuanzia 120- 170 yani watakao kuwa kwenye IQ hiyo basi arrangement zao kwenye baadhi ya maaeneo ya DNA kuna sequence hiyo...

Sasa ndo nikawa najiuliza manake huenda ni kweli gene bado zinabeba mambo mengi sana ambayo we need to know exactly ni GIGABYTE NGAPI GENE ZINABEBA MAKE KINACHOGUNDULIKA MULE NI KIDOGO SANA compared na efdects ambazo gene inazalisha kisha tunakimbia kusema kuna mchango wa njee...ndo mana inafikia mahala tunasema unknown causes and effects...

Genetically bado kuna mambo yanahitaji kufanyiwa kazi aise.....

Isije ndo ile program ya kuscan abnormal genes kwwnye miili yetu kisha kureplace with desired gene kwa matokeo mazuri ya kiumbe wa baadae ( Kama Physics of the future by MICHIO KOKU inavyoelezea ila kupunguza kama sio kutokomeza magonjwa kama Kansa,hypertensuon na stroke kwa miaka ya badae ..))

nawaza tu kama inaweza ikawa ni genetic basing analysis
DNA is our blueprint(thus,even neural circuits formation zinakuwa coded na gene zako)...so probably kwa asilimia kubwa ni vizuri kuamini kwamba katika hizi multifactorial factor,the most predominant factor ni DNA
 
Apo nimepata kitu. Kikubwa sana
Daaaah...umenitag mkuu...!! aya bana ..

But hongera kwa maada fikilishi...

lakini nataka nichangia mada hii katika analysis ambayo inaweza isiwe imebase na jinsi wengine wanavyoweza kuchangia kwa facts za lishe bora pamoja na genetic influence kutoka kwa wazazi hasa mama...

Mpaka sasa bado jopo la madakatri hasa Neural scietists pamoja na psychiatrists ambao kazi yao kubwa ni kucheza na cognitive brain function ambayo inahusisha eneo moja pekee la ubongo lijulikanalo kama Prefrontal cotex ....

Wanasema kuwa Cognitive function ya ubongo( sehemu inayohusika na uelewa katika ubongo wa mwanadamu) ipo under neural circuit guided na Neural transmitter nyingi sana including Dopamine,Noradrenaline,Adrenaline yenyewe,serotonin,melatonin,GABA, pamoja na zinginr kibaoa ambayo utendaji kazi wake upo Antagost au agonizing zaid kutegemea na hitaji la ubongo au akili katika kutenda...

Kuna neurol transmitter hapo zinahusika na mambo ya firing au kuruhusu transimssion ya impulse kwa speed kubwa sana na zingine zinahusika na kudhibiti high neural firing rate hence zinazuia impulse rate changes katika specific part ya ubongo ...

Ukisoma mambo ya Dopaminergic pathways hapa unaweza ukaelewa ninachoongelea...

Twende kwenye mada yenyew what guides intelligence to a singular person ..??

Kuna kitu kinaitwa CPH4 ( 6-carboxytetrahydropterin synthase) hii ni enzymes ambayo mara nyingi inahusika na conversion snyingi sana ambazo huwa zinagive out Queuosine, ambayo ni component muhimu sana katika kuincrease neural firing ratio ya chemical maalumu ambazo zinahusika na prefrontal cotex capacity inayohusika na mambo ya cognitive function ya brain hasa maeneo ya limbic system ,amygdala na mengine ambayo yanahusika na memory pamoja na Intelligence brain centre...

Ili mtu tuseme kuwa ana akili nyingi sana au ana Intelligence kubwa ni lazima eneo flani la ubongo lazima liwe busy sana anapokuwa anafikilia au kufanya mazungumzo juu ya swali aliloulizwa...

Madaktari kutoka Armstadam ,Netherland walifanya jaribio moja kwa kutumia Electroencephalogram (EEG) kupima brain hyperactivity wakati mtu anapokuwa kwenye maswali magumu yanayomfanya mtu afikilie sana ila wakaja kugundua kuwa ni eneo moja tu la prefrontal cotex ndo lilionekana kuwa busy snaa wakati wa kufikilia...pia eneo hili ndilo linalohusika na mambo ya kuactivate brain function hasa mtu akiwa bado mdogo sana,,,consider about Mutism spectrum disorders kwa watoto wadogo ambao ni moj wapo ya mental disorder amabyo inawapata watoto wanapozaliwa na mara nyingi huathiri cognitive behavioral pattern ya mtoto husika.

Hivyo iliwafanya waanze kuchunguza zaidi why eneo lile ..Ila cha kushangaza walikuja kugundua kuwa eneo hilo ndo lilikuww na high neural firing rate za neural transimtter ambazo zinahusika zaidi na mambo ya cognitive function...siyo kila neural transmitter( vichocheo katika ubongo) inahusika na cognitive function...

Unaweza ukawa na high level ya dopamine( katika manic episodes) lakini ukawa na low cognitive function na mwingine akawa na high dopamine neural firing rate lakini akawa na cognitive function kubwa snaa zaidi kuliko mwingine despite wote wapo manic episode au Bipolar conditioned state...

Ukitaka kuelewa zaidi hapa nenda magaereza ya wafungwa ambao ni wagonjwa ndo utaelewa ninachozungumza hapa kuwa kuna vichaaa utakuta uwezo wake upo juu sana yani kawa geniuz mpaka karun mental disability ila ana high IQ score na mwingine ni mgonjwa wa vile vile bipolar lakini ni mbumbumbu wa kutupa though wote wana high level za dopamine...

Kwa hiyo dopamine sio kigezo sana za kujudge intelligence ...we need something else...

Sas kuna hiyo chemical substance ambayo inaitwa CPH4 ambayo mara nyingi watu wa Neural molecular science hawataki kuweka wazi na wanasema kazi yake bado haijagundukika lakini sio kweli kazi yake inafahamika na ndio chemical wanayoitumia hasa kupima ya Intelligence ya mwanadamu kuanzia akiwa tumboni kwa mama( Embryology) mpaka anapofikisha miaka 25 ...

Inasemekana kuwa japo ni kweli kuwa mama mjamzito akiwa na umri wa mimba ndani ya week 6 ndipo hormone hiyo au chemical hiyo huzalishwa kwa lengo la kwenda kuhimiza utengenezaji wa capacity ya kutosha ya neural circuit receptors kwa ajili ya high firing rate ya imuplse katika specific cognitive brain centre...

Ifahamike kuwa ubongo wa mwanadamu hutengenezwa mtoto akiwa na umri wa week 4 tumboni kwa mama yake kwa hiyo ubongo ukianza kutengenezwa tayari mwili wa mama unasense kuwa tayari ubongo wa mtoto umeanza kutengenezwa na tayari mwili wa mama unaamliwa kuanza kutoa hizo chemicali aina ya CPH4 ambazo zinaenda moja kwa moja kwa mtoto kwa ajili ya kuenhece cerebral formation hasa cognitive area ambalo kazi yake kubwa ni kujenga neural firing receptor za kutosha ili ubongo uwe na high receptors za hizo neural transmitter kwa ajili ya kuprocess information za kutosha katika eneo husika kwenye ubongo kila unapogundua kuwa hilo wazo linatakiwa lifanyiwe kazi katika eneo flani la ubongo basi taarifa muhimu inapelekwa kule kwa speed kubwa sana ambao ni millsecond ndani ya millsecond na tayari cognitive centre inainterprete kuwa hicho kitu jawabu lake ni hili...

The difference in Intelligence between us ni kwa sababu tunazidiana neural firing rate ya taarifa kufika eneo husika kwa muda mfupi sana na kufanyiwa interpretation yake..

Mtu ambaye ni Genius ana high neural firing rate kuliko mtu wa kawaida...manake nini...??

Kuna kitu kinaitwa processor,hiki ndo kifaaa kinachospeed up rate ya taarifa kusafili kwa haraka zaidi kwenye electronic component yoyote..ndo mana hata ubora wa komputer ni processor pamoja na RAM....manake nini kama Laptop au computer yako ina processor ndogo lets say 1.7 GHZ manake utakuwa kila ukiclick file lifunguke linachukua sekunde 4 ndo linafunguka lakini mwenye processor ya 2.7 GHZ akiclik inafunguka ndani ya fraction of second...processor ndo kila kitu ...

Same applied kwenye ubongo wa mwanadamu kinachomfanya mtu aww na upeo mkubwa wa kufikri na kupata jawabu lililo sahihi ni uwezo wa taarifa kufika eneo husika kwa haraka zaidi kisha kufanyiwa interpretation iliyosahihi ndani ya muda ule ule na taarifa zake kupelekwa kwenye cognitive centre kwa ajili ya kumfahamisha mwanadamu kuwa anachowaza au kuhisi ni hiki hapa ...

So kila mwanadamu ana ubongo ule ule the difference is the CPH4 level ambayo inahusika na kutengeneza more brain circuit kwa ajili ya impulse transduction na hapo ndipo hata anatomy(umbo katika physical morphology) ya ubongo huwa ina ratio tofauti za Gyrus na sulcus ambazo ndo zinazoupa ubongo folding morphology kuincrease surface area ya neural firing rate ...

So the level of CPH4 Itaendelea kuwa maintained mpaka pale ubongo utakapokuwa umekamilika...kwa hiyo kama productiom ya hormone hizo ikiwa ndogo basi hata uwezo wa akili wa mtoto unakuwa hafifu ..ndo mana tunasema mama ndo mtu pekeee anayechangia Intelligence ya mtoto na sio baba( hapa katika percent ratio mama anakuwa na nafasi kubwa)..

So kama ukitaka kumaintain high brain au cerebral capacity ya mtoto inabidi mama aproduce high level ya CPH4 during pregnacy kulikoa wakati akiwa ananyonyesha japo huwa ipo kwa kiwango kidogo snaa kwenye colostrum( maziwa ya mwazo kabsa ambayo mtoto hatakiwi kukosa)..

Lakina kuna study zilifanyika miaka ya nyuma na kugundua kuwa mwanadamu wa sasa ( tulio wengi) tunatumia only 10% ya cerebral capacity kisha 90% ya ubongo wetu haufanyi kazi na ikasemekana kuwa laiti binadamu angelitambua hilo kuwa yeye ni infirnity and Immortal basi angeweza kuraise energy na anaweza kuexpand cerebral capacity mpsaka hata 40% kisha anaweza akadevelop some features kama Telekinepathy, psychopathy abilities ambapo anaweza akafungua mambo mazito yaliyo nyuma ya ulimwengu huu na kisha kumfanya aanze kuiview universe katika 8 dimension state....kadri anavyoascend kwenye 100% ndipo uwezo wake unabdilika kwa kasi kubwa sana na anaweza akawa na nguvu ambazo ni uncontrolled =====pengine ndo mana serikali hazitaki kufundisha elimu ya kuraise CPH4 hasa kwa binadamu wa kawaida kwa sababu madhara yake ni makubwa sana.

Nchi za wenzetu wameweza atleast kujua namna ya kummonitor mama mjamzito hasa kuepuka stress wakati wa ujauzito kwani stress ni factor moja kubwa sana inayozuia production ya CPH4 na kumfanya mtoto anakuwa tumboni katika low level ya cerebral capacity formation hence anakuja kuwa na low IQ japo vyakula na lishe bora zinaweza kuboost lakini kwa kiwango kidogo sana....

Lakini pia kama wewe ni mdau wa kufuatilia mambo ya human cloning hasa kupitia project yake ya Maffin project and human cloning kupitia process za somatic-cell nuclear transfer au pluripotent stem cell induction basi hutumia normalizimg ratio ya CPH4 .Lakini pia kisha ukasoma hizo documentaries na scientific writtings zinazoelezea jinsi mradi huo wa siri wa kutengeneza exactly copy wa kiumbe unaemtaka bila kubadili chochote utagundua kuwa wanatumia technolojia under the help ya hizo chemicals hasa during blastula formation wanainduce the same ratio ya CPH4 kwenye morula ya yule clone kwa kufuatisha ratio alizonazo yule recipient wake...

Kabla ya kufanyiwa clone wake unapimwa kwanza cerebral capacity in relation ta CPH4 level kisha ndo anatengenezwa clone wako ambayo atakuja kuwa na Intelligence ile ile uliyokuwa nayo before ..

Forget about human cloning now make sio mada husika...ina nafasi yake..japo ipo siku nitaidondosha hapa rasmi...

kwa mara ya kwanza maabara ya The Thomas J. Watson Research Center. ambayo ilipata kashikashi kwa kuuza taarifa za kimolecular za CPH4 katika maabara kuu tatu ambazo ni ni Argonne National Laboratory,Oak Ridge National Laboratory pamoja na The Center for Integrated Nanotechnologies (CINT) kisha taarifa hizo kuuzwa wa badhi ya director mmoja ambapo kulipelekea kuelezea kazi ya chemical hiyo kwenye movie ya Lucy( 2010) japo usiri umeendelea kutawala zaidi juu ya uwezo au Intelligence ya mwanadamu...

kuna study nyingi zimefanyika kupima kiwango cha CPH4 kwa kina mama tofauti wakiwa wajawazito na kupima Intelligence outcome ya watoto wao na kukuta kuwa kulikuwa na utofauti mkubwa snaa depending na blood chemical level...

Nahitimisha kwa kusema kuwa Intelligence ya mwanadamu imekuwa ni swala gumu sana kulielewa kwani mambo mengi yanakuwa siri nzito sana....

wachache wanatuendesha watakavyo na huenda Nanotechnology ikaja kusolve hiyo paradoxy...

Asanteni...huo ndo mchango wangu kwa mwenye kung'amua machache unaweza fuatilia zaidi hasa kwa kusoma mambo ya Neural science in relatiom to neurotransmitter receptors that govern human Intelligence nadhani utajifunza mengi kuliko hata niliyoelezea .View attachment 920547View attachment 920549
 
asante sana mleta mada na wachangiaji wote kwa ujumla. tunapata kujua kwa vyovyote uwezo mdogo au mkubwa wa akili hauusiki na kurithi kama sura rangi sauti nk. bali mazingira ndio huchangia jinsi gani uwezo wa akili ya mtu uwe,ni mekusoma kwa namna ya pekee lifecoded nikiri kukuelewa kwa kiasi kikubwa. mazingira yetu ya ukuajutoka kutungwa mimba yamekua sababu kuu ya kudumaa kwa aikli na kushinwa kuitumia akili tulio jaliwa na Mungu kwa kiasi kingi .
ni masikitiko kwamba hata asilimia kumi ya akili tulio nayo hatujafikia katika matumizi hiao 90 % zinapotea bure!!!!
nashukuru uwepo wa teknologia tunapata mwanga nini kinatupasa kufanya ili kufikia kiwango stahiki cha matumizi ya aikili. naamni tusingekua tunateswa na magonjwa njaa umaskini na pengine hata wana siasa. tuendelee kujifunza na kushirikishana huwenda siku moja ikawa tofauti.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom