Intelligence heredity: Je, uwezo wa akili hurithiwa?

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
19,039
28,690
Habari za weekend wana JF, kuna swali nimekua nikijiuliza muda mrefu sana na kuna mada iliwekwa humu JF ambapo wachangiaji wengi kina Wick na Malcom Lumumba waliijadili hii issue ila kwa kugusia tu maana haikuwa kiini cha mada.

Ukweli mchungu: Pasipo anguko la Malaika (Sons of Gods/Watchers/Anunnakis/Aliens), Mwanadamu angeendelea kubaki kilaza. - JamiiForums

Humo ndani kuliibuka debate kama akili za binadamu ni hereditary/genetic au ni mazingira. Baada ya kusoma tafiti /makala kadhaa nikaona nilete mada humu ili tuweze kujadili suala hili kwa upana zaidi na niweze kupata conclusive answer kwa mjadala ule. Na source yangu kubwa ni study hii ya huyu neurosurgeon niliyeambatanisha pdf yake hapo chini.
making-algebra-actually-mean-something.jpg


UTANGULIZI
Akili kwa kifupi tu tunaweza kusema ni uwezo wa kufikiri au kuchanganua masuala mbalimbali yanayotuzunguka na kwa mingi wanasayansi wamejaribu kupima hiyo "akili" kati ya mtu na mtu ili kuweza kufahamu sababu halisi za kuwepo utofauti huo yaani mtu kuwa na akili ''ndogo'' au ''kubwa'' kuliko mwenzake.

Mnamo mwaka 1905 serikali ya ufaransa ilitaka kuanzisha mfumo wa "elimu kwa wote" hivyo ikataka kugundua watoto wenye ''akili ndogo'' ili wapewe elimu maalum kuwawezesha kusoma kwa spidi yao kuliko kuwabakisha nyumbani tu au kuitwa "wehu". Mtihani huu uliitwa stanford-simon test ambapo ulikuwa unapima vitu vikuu vitano ambako na sisi ningependa tutumie tunapoendelea na mjadala huu sababu hizi factors ndio zimeweka msingi wa IQ tests na mbinu karibu zote duniani za kupima akili ya mtu.

1.Maarifa (knowledge) ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kuelewa mambo yanayomzunguka mfano mtoto aliulizwa kushiba au kuchoka ndio nini?

2. uchanganuzi wa hesabu (Quantitative reasoning) ; Hapa mtoto anaulizwa masuala ya hesabu ili kupima uwezo wa akili yake mfano kujumlisha,kutoa,kugawanya n.k

3. Working memory yaani Kumbukumbu ya muda mfupi ambapo hapa wanapima kama mtoto ana uwezo wa kutunza mambo aliyofundishwa au kuyashuhudia muda mfupi tu uliopita mfano kama unawaonyesha picha basi unawauliza picha ya kwanza kuwaonyesha ilikuwa ya nani.

4. Visual-spatial processing yaani utambuzi wa vitu kwa kuangalia mfano uhusiano baina ya picha na zaidi inayotumika ni puzzle ambapo mtoto alitakiwa kupanga vipande tofauti ili vitengeneze picha moja.
images (69).jpg

5.Ya mwisho ni uwezo wa kuchanganua (fluid reasoning) yaani uwezo wa kufikiri na kupata suluhisho kwa jambo ambalo halitegemei kitu ulichowahi fundishwa au kukutana nacho huko nyuma mfano kuunganisha dots za suala fulani fulani ili upate picha kamili mfano hapa chini ambapo mtoto ataulizwa umbo gani ndio sahihi kuwekwa kwenye alama ya kiulizo??
Screenshot_2018-11-03-09-07-24-1.png

NADHARIA
Baada ya kujua baadhi ya vitu tunavyopima kwenye uwezo wa akili ya mtu.... Basi tuangalie nadharia mbalimbali zilizoletwa juu ya mjadala huu.

1. Akili hurithishwa /Heritability.
Kwenye nadharia hii baadhi ya wanasaikolojia wamejaribu kufanya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa akili ya mtu hurtishishwa kutoka kwa mzazi hivyo uwezo wa akili za wazazi ndio utaamua uwezo wa wanaye kwa kiasi kikubwa. Kwa mujibu wa tafiti nilioambatanisha hapo chini inaonyesha mapacha wakufanana wana wana akili (IQ) zinazofanana kuliko mapacha wasiofanana ikimaanisha jenetiki zina nafasi ya kucheza kwenye kuamua akili ya mtoto. Vilevile utafiti mwingine ukaonyesha ndugu waliokuzwa kwenye nyumba moja wana akili zinazofanana kuliko watoto wasio na undugu waliokuzwa eneo moja ikimaanisha genetics za kifamilia ndio huamua akili ya mtoto na sio makuzi/malezi n.k

Nadhari nyingine inayotumika humu ni wilson effect ambayo inasema mtu anapozidi kukua basi uwezo wa akili yake unakuwa umechangiwa na akili za kurithi kuliko sababu zingine zozote na alihitimisha kwa utafiti unaoonyesha 60% mpaka 80% ya akili ya mtu mzima huwa imerithiwa kutoka kwa kizazi chake na zilizobaki ndio sababu zingine kama elimu,makuzi,mazingira,uzoefu,afya n.k

2. Mazingira/makuzi
Nadharia ya pili inadai mtoto huzaliwa na uwezo wa akili wa kawaida ila mazingira au makuzi atayakayopata ndio yataamua akili yake hapa duniani. Tafiti mbalimbali zimefanyika mfano weinberg (1989) unaonyesha mapacha wanaofanana waliokuzwa mazingira tofauti kabisa uwezo wa akili zao haukufanana ikimaanisha uwezo wa akili huamuliwa na mazingira ambayo mtoto anakulia na sio kurithi akili za mzazi. Mfano mtoto ambaye baba na mama yake wana akili ila amekulia mazingira ya umaskini hivyo kula yake ni ya shida na hapati lishe bora hasa udogoni inaathiri size ya ubongo wake hasa ubongo wa mbele (frontal lobes) hivyo itasababisha uwezo wake wa akili kupungua sana. Ama mtoto mwenye uwezo mdogo wa akili akikulia mazingira ambayo wazazi wanamjengea uwezo wa kufikiri kama kumpa maarifa kadha wa kadha toka akiwa mdogo,kusoma vitabu,mitihani ya kimaisha ya kumfanya afikiri basi mtoto huyu akili yake (IQ) itapanuka muda unavyozidi kusogea.

p05f7npk.jpg


Tabula rasa
Hii ni nadharia iliyoanzishwa na John locke (1690) inayodai mtoto akizaliwa huwa ni MWEUPE kichwani ila uwezo wake wa akili utaamuliwa na mazingira,uzoefu,maarifa atakayopata kwenye makuzi,mazingira au uzoefu anavyozidi kukua. Hivyo kwa kiujumla nadharia hii inasema haijalishi mtoto kazaliwa na akili gani ila makuzi yake ndio yataamuwa kama atakuwa na akili ''kubwa'' au ''ndogo''.

NB: tunapoongelea akili hatumaanishi za darasani na hatumaanishi jinsi mtu anavyozitumia bali tunamaanisha UWEZO wa juu zaidi ambao anaweza kutumia kufikiri hata kama bado hajaamua kuutumia ipasavyo. Kiufupi tunaangalia brain CAPACITY sio PERFORMANCE. Maana kuna wengine wana akili kubwa ila hawajawekewa mazingira ya kuzitumia kwa ukamilifu wake so tunapojadili tuwe nalo hili kichwani.

Naomba kuwasilisha
Cc
Mchawi Mkuu Malcom Lumumba Elungata Da'Vinci Mshana Jr Eiyer Kudo900 Vi rendra N J subi Bujibuji Kipanga boy Kiranga Che mittoga Ip man 3 mitale na midimu Mzee wa Torano Blaki Womani Grahnman za chembe jimmykb197 911sep11 afsa Francis3 mtu chake NJOLO Msolo Shubiri Pori Pendael24 Mr Miller Elli Khalifavinnie Kennedy Son of Gamba Kanungila Karim Mgambilwa ni mntu Mr FCB Mr Q geesten66 Jerry Ekky Mnabuduhe Chrisvern Dabby Jr kibuyu180 IGWE SALA NA KAZI
Wick Dukeson lifecoded Daimler monde arabe mtu watu
 

Attachments

  • JNSK-01-00023.pdf
    3.1 MB · Views: 78
Mada ipo vizuri,binafsi nafikili akili ya mtoto inajengwa (vyakula,malezi,changamoto za maisha) au kutengenezwa,japo kuwa kuna familia ambazo wote uwa na IQ kubwa bila kujali mazingira yao.
Mara nyingi tulipokuwa Tuna soma na jamii za watoto wa wafugaji au waishio kiasili,uwa wanakuwa na uelewa mkubwa mno.Pia watoto waliopata bahati ya kula vizuri,shule nzuri(sio hizi za kawaida),malezi mazuri(mtoto anapata kila kifaacho kielimu).Hawa watoto ukiwalinganisha na wale wanaosoma shule mbovu,wanakula chakula kilichopo na sio wanachotaka,utagundua kuwa ipo tofauti kubwa kimtazamo,kiufanisi wa akili,uwezo wa akili,na kimaisha Kwa ujumla.
 
Intelligence is inheritance factor, ila pia mtoto anatengenezwa tokea tumboni kwa mama kupata mlo kamili, omega 3 kwa wingi, madini chuma and the like apumzike na kupewa support ya kutosha kumuepusha na msongo wa mawazo.

Hata mtoto akizaliwa aendele kupewa nutrients kamili kupitia kunyonya mpaka akianza kula, samaki kwa wingi, madagaa dagaa, parachichi maji(just few to mention) mazingira pia yanachangia watu wanaomzunguka matendo yao usitegemee mtoto asubuhi mpaka jioni anasikia sabufa imefunguliwa rusha roho au heka heka matusi makali mambo meusi meusi tu hayaelewekihapo lazima kutakuwa na tatizo tofauti
 
Hapo familia yote kuwa na IQ kubwa ndo kurithi kwenyewe huko,
Mada ipo vizuri,binafsi nafikili akili ya mtoto inajengwa (vyakula,malezi,changamoto za maisha) au kutengenezwa,japo kuwa kuna familia ambazo wote uwa na IQ kubwa bila kujali mazingira yao.
Mara nyingi tulipokuwa Tuna soma na jamii za watoto wa wafugaji au waishio kiasili,uwa wanakuwa na uelewa mkubwa mno.Pia watoto waliopata bahati ya kula vizuri,shule nzuri(sio hizi za kawaida),malezi mazuri(mtoto anapata kila kifaacho kielimu).Hawa watoto ukiwalinganisha na wale wanaosoma shule mbovu,wanakula chakula kilichopo na sio wanachotaka,utagundua kuwa ipo tofauti kubwa kimtazamo,kiufanisi wa akili,uwezo wa akili,na kimaisha Kwa ujumla.

Umeshawahi kujiuliza kwa nini hizo jamii za wafugaji wanakuwa na akili sana?
 
Hili ni swala Complex kiaina,Kwanza kabisa tutofautishe Memory na IQ.. ila tuiweke katika mtazamo mwepesi kama huu, Akili ni swala Pana.. ila kwa kiasi kikubwa akili hurithiwa.. swala la vyakula hasa hasa linaplay ro, le ya kuimarisha Memory na si kuongeza Akili, Bahati mbaya wengi wetu wenye uwezo wa ku memorize bila kuelewa nao huonekana wana IQ kubwa, Kingine ni swala la mazingira.. Hii inaplay role ya kumchangamsha tu mtu, yaani kupata exposure ya haraka kwenye vitu mbali mbali na kupanua uelewa..!

Kwa Kumalizia Kama baba ndo ana IQ kubwa uwezekano mkubwa atarithisha watoto wa kike, kama ni mama basi watoto wa kiume.. Hii nimeshuhudia familia nyingi ikiwemo yangu!

Divine Khan
 
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya LISHE na AKILI mfano hapa TANZANIA wakazi wa maeneo yenye chakula cha kutosha chenye viini lishe vya kutosha wana uwezo mkubwa kwenye ubongo wao (IZINGATIWE HAPA KWAMBA KIPIMO CHA HUO UWEZO WA AKILI NI ELIMU YA DARASANI.

Mazingira pia na makuzi vinachangia pakubwa kujenga uwezo wa akili kufanya kazi, mathalani jamii za wafugaji watoto wao wana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo ila wamekoseshwa elimu ya darasani...lakini wanaweza kuyakabili mazingira yao.

Maeneo yenye misosi ya kutosha na elimu imetiliwa mkazo + malezi watoto wao wameelimika sana mfano Kilimanjaro,Kagera,Mwanza,Mbeya,Ukerewe na kwingineko....Rukwa kwa mfano chakula kipo lakini kwa mtazamo wangu umaskini na kukosekana hamasa jamii yake kubwa haijapata sana elimu.

Jamii za pwani kwa mfano unawaona kabisa wana akili ila wamekosa hamasa/malezi ya kuzijenga akili zao kupitia maarifa ya kitabuni...mchukulie mfano Mbwiga,zembwela wangesoma sana wale ungekuwa moto mkali zaidi...

Ukifuatilia watoto walioonyesha maajabu angali wadogo kabisa walilelewa kwa dhati kabisa kuwa na uwezo mkubwa at a tender age.

Kwa hiyo mimi nadhani malezi,lishe,na kwa uchache vinasaba huamua uwezo wa akili kuwa wa kiwango gani...kama kwa wale super geneous kama kina Einstein na wengine.

Hivyo mi nadhani malezi yana nafasi kubwa sana kujenga uwezo wa akili wa mtu sasa tatizo kujenga akili ya vijana wetu tumeachia malimwengu kwa sababu tuko eti bize
 
Akili inarithiwa ila sio kwa uzao wako wote, kwa mfano unakuta mzazi mwenye akili kubwa anazaa watoto watatu wenye akili halafu dogo mmoja anakuwa mwenye uwezo mdogo kiakili.
Hii naichukulia kama magonjwa ya kurithi ambapo unakuta mzazi mwenye pumu au kifafa anazaa mtoto mmoja mwenye pumu au kifafa halafu madogo watatu wanakuwa salama.
Niko tayari kukosolewa na kuelimishwa zaidi
 
Sio watoto wote wanao rith akili kutoka kwa wazazi kuna baadhi yao akili yao inakuwa kulingana na mazingira ya mtoto na malez ya mtoto
Baba anaweza kuwa anaakili sana ila malez ya mtoto yakawa kama ya amber ruty au wema sepenga mwisho wa siku mtoto akili inadumaa haikui
Ila unaweza kuta mtoto ana akili ila baba na mama akili za kawaida hapa malez ya mtoto kama yalikuwa vizur mazingira yake yapo vizuri lishe iko vizur
 
Dogo umenikimbia kule!!....Nitakusaka popote ulipo!!

Nimekuwa dogo tena kwako ? Huwa sikimbiagi hoja bro,kuna mambo yalinizonga muda ule,ila na kuna lingine sikutaka kulihudhurisha pale kwani nilichelea kuzua mada nyingine kwayo isingekuwa na tija kwa muda ule.

Nipo .....!
 
Nimekuwa dogo tena kwako ? Huwa sikimbiagi hoja bro,kuna mambo yalinizonga muda ule,ila na kuna lingine sikutaka kulihudhurisha pale kwani nilichelea kuzua mada nyingine kwayo isingekuwa na tija kwa muda ule.

Nipo .....!
Mimi nina 50yrs siyo sahihi kukuita wewe ni dogo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom