Inasikitisha sana: TTCL Yafilisika Rasmi

Inasikitisha sana: TTCL Yafilisika Rasmi

kuna tetesi zilikuwepo miaka ile celtel inaingia nchini kuwa kuna mkono wa mwinyi na salim ahmed salim!

Juzi kuna mtu alinambia kuwa yule mzee hasiye na wizara maalumu pale ikulu ndio ana hisa za kutosha ktk airtel
 
Huyu anayeutaka Uraisi ambaye kitabu chake kimetoka juzi, ameshindwa kuifufua hii kampuni ambayo iko direct chini ya wizara yake ni utendaji upi sasa aliofanikiwa mpaka tumkabidhi nchi, wakati TTCL Shirika la kizalendo kashindwa kulifufua linakufa chini yake. Only in Tanzania where mtu anashindwa kabisa kiutendaji halafu anataka tumpromote mpaka Urais. Mafisadi wamefanikisha azma yao ya kuua shirika la kizalendo lilokuwa na mtandao nchi nzima na branch Ofisi karibia kila mkoa na ilikuwa inaajiri watanzania wengi. Inasikitisha sana!!

Source:Habari Leo

Huu ndio utawala wa Ma-CCM, na ufilisi wa kila kilichokuwa cha Umma..wanakuza tu matumbo yao, kuwekeza ktk wizi na kutetea kuwa wanalinda 'amani na utulivu'!!...Tunawaambia CCM kuwa siku zinakaribia mwisho, na kila aliyekula hata chembe ya rasilimali ya umma, amefilisi mashirika, ameshiriki kuhujumu urithi wa taifa...ataona cha mtema kuni! Watakuwa wanapishana gerezani na ikibidi wafanyiwe ambayo hayajawahi kutokea hapa tz ili kukomesha manyang'au haya...! Kila kona ni wizi tu, kila kukicha ni taarifa za kuifilisi nchi...! na mnaomba kuendelea kuchaguliwa tena Oct?? Mtasaga meno walaah...labda hakutakucha siku hiyo...inauma sana, nikiona li-CCM popote natamani kutapika!
 
Ama kweli upele humuota mtu asiye na kucha na pia wahenga walinena kuwa penye miti hapana wajenzi...kweli leo makampuni ya mawasiliano yanavyopig ahela ya maana hivi halafu wao TTC wanomiliki mkongo wa taifawanafilisika na kufa kibudu?? Kuna haja ya serikali kufanya maamuzi magumu kwani mkiua TTCL basi nina hakika na shirika la posta linaenda kufa kifo cha mende muda si mrefu.

Hiyo haipo mbali na si ajabu utasikia anapewa mchina kuliendesha hilo shirika.
 
Toka awamu ya Alli Hassan Mwiny iliamuliwa kuwa shirika la umma lisiloweza kujiendesha lenyewe halitopewa ruzuku.

Wizi, Uzembe, Uvivu, Uongo ndiyo unayapeekea mashirika yote ya umma kufa.

Ukiona lipo ujuwe hilo amma linajiendesha lenyewe au linapewa ruzuku kwa kuwa hakuna mbadala wa mashirika binafsi, mfano TANESCO, kama si kusaidiwa na Serikali lingeshakufilia mbali zamani sana.

Sishangai.

Nani wasimamizi wa sera zilizoshindwa ni Chadema? Au Wadudu wa kijani na njano(nyinyiemu)
 
Kwa hiyo hili ni shirika la tatu linakufa chini ya mikono ya Kikwete.

Air Tanzania

Railway

TTCL

Tena mashirika ya ukweli kwa uchumi, usalama, na reputation ya nchi. Ingelikuwa ni viwanda vya ngozi, mabusati, n.k. wala isingekuwa issue sana. Air Tanzania; the national flag carrier! Railway(TRC & Tazara); the largest and cheapest cargo carrier! TTCL the national communication backbone! Hata bandari kadhaa zimekufa ikiwemo ya Tanga na Mtwara na za maziwani sidhani kama zina-operate.

Ukuifika maeneo ya Korogwe, Mombo, kuelekea Moshi/Arusha ukiona nyasi zilivyoota juu ya reli na sehemu nyingine imefukiwa na udongo au mataruma kuibwa kama chuma chakavu unaweza kulia machozi. Inauma!

Viwanda vingine uti wa mgongo japo vilikufa enzi za Mkapa ni General Tyre, Kilimanjaro Machine Tools, n.k. Hata TANESCO ilikuwa chupu chupu enzi za NetGroup Solutions.
 
Rostam, Chenge deal zote huwakosi
. .. na mgombea urais wanaye tena 2015 wanatuletea...kwanini hatuamki?
 
Huyu anayeutaka Uraisi ambaye kitabu chake kimetoka juzi, ameshindwa kuifufua hii kampuni ambayo iko direct chini ya wizara yake ni utendaji upi sasa aliofanikiwa mpaka tumkabidhi nchi, wakati TTCL Shirika la kizalendo kashindwa kulifufua linakufa chini yake. Only in Tanzania where mtu anashindwa kabisa kiutendaji halafu anataka tumpromote mpaka Urais. Mafisadi wamefanikisha azma yao ya kuua shirika la kizalendo lilokuwa na mtandao nchi nzima na branch Ofisi karibia kila mkoa na ilikuwa inaajiri watanzania wengi. Inasikitisha sana!!

Source:Habari Leo
kama watu wana kaa tu bila ubunifu waondoke
 
MKuu huo ndio ukweli,
1. wlaitumia leseni ya TTCL.
2. walitumia Miundo mbinu(Minara ya TTCL) kufunga redio na mitambo ya mwanzo, japo kwa sasa baaadhi ya sehemu wamejitoa.
3. Kumbuka makao makuu yao ilikuwa pale Airtel kijitonyama kabla Rostam ajala shavu na kuwajengea pale Ambaosdor kwenye hotel ya wazazi CCM.
Hawakuwekeza chochote, lakini Tanzania inaongea nao kuwalipa waondoke. Waliochonga madili haya ni watu tunaowaheshimu sana kwenye jamii, Tutaamka lini?
 
Kwa hiyo hili ni shirika la tatu linakufa chini ya mikono ya Kikwete.

Air Tanzania

Railway

TTCL

Mbona mashirika yote yamekufa mengi sana toka enzi ya Nyerere, Mwinyim, Mkapa na Kikwete? na Mwinyi ndiyo kabisa aliamuwa shirika lolote lisiloweza kuijinedesha lenyewe halitopewa ruzuku tena na Serikali, matokeo si unayajuwa au mpaka tuchambuwe?

Haya yaliyobaki mpaka hii leo yamejitahidi sana.

Huo uongozi wa TTCL ni mbovu kabisa si shirika la kufa lile kwa miuondombinu waliokuwa nayo, tazama attakaelinunuwa utaona linavyoshamiri.

Lakini ndiyo mashirika uya umma yalivyo kama halina ruzuku hayawezi kujiendesha, watu wanaiba tu mtindo mmoja.
 
Nani aliingia mkataba na hao bhat airtell? Sijarlewa vizuri ila hii mikataba mingine hii. Kuna watu wananufaika kabla hawajaingia

Kwa kuwa tarehe 21 Februari, 2001, TTCL ilisaini mkataba na Kampuni ya SMI/Detecon, ambayo ilinunua asilimia 35 ya hisa kwa Dola za Marekani 120 milioni (Sh bilioni 198).Hata hivyo, kiasi kilicholipwa ni Dola 65 milioni tu (Sh bilioni 107.3) kwa ahadi kwamba kiasi kilichosalia, kingelipwa baada ya hesabu za TTCL kukaguliwa. Baadaye MSI/Detecon ambao ulikuwa ushirika wa Kampuni ya Mobile Systems International ya Uholanzi na Detecon ya Ujerumani, ilitumia leseni ya biashara ya simu za mkononi iliyokuwa mali ya TTCL, kuanzisha Celtel Tanzania. Sasa naomba kujua, kwa nini hao ambao wamewahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi miaka ya 2001 hadi inafilisika 2015 wasiwajibishwe? Inawezekana kuna wakubwa walishaondoka na hisa za TTCL wamesepa nazo huko Celltel, Zain hadi Airtel Bhat!!!
 
TTCL aliiua Dr. Kilimbe na Mkapa, kitendo cha TTCL kuanzisha program ya kuwa na TTCL mobile wajanja wakaipora na kujiuzia kwa hela zake wenyewe akiwezi kuacha lawama kwa viongozi hawa hasa kwa Mr.Safi baada ya kudinafsisha kila kitu, Niliwahi kushuhudia Mgogoro uliokuwepo wa kiuongozi wakishutumiana jinsi walivyouza hisa kwa kampuni ya Mass Telecommunication , hii ndicho kilikuwa kifo cha TTCL na kuzaliwa kwa CELTEL, nakumbuka Enzi za Mh. Adolf mapunda TTCL ilikuwa kampuni bora ya serikali hadi kuizidi TANESCO. Mbaya zaidi TTCL waliingizwa mkenge na kampuni ya HUAWEI kufunga mitambo wa CDMA ambayo kwa Tanzania ni ngumu kufuatana na soko, kumbuka kampuni zote zilizotumia njia hii zimefilisika kuna BENSON ON LINE, ZANTEL CDMA, SASATEL zote ziko hoi.
 
Nani wasimamizi wa sera zilizoshindwa ni Chadema? Au Wadudu wa kijani na njano(nyinyiemu)

Haya mashirika yote yalikuwa chini ya sera iliyokufa ya kuendeshwa na serikali, serikali ilijitowa zamani katika kufanya biashara na kutoa ruzuku kwa mashirika yasiyoweza kujiendesha, toka enzi ya Mwinyi aliamuliwa hivyo, ndiyo maana ukaona mashirika na viwanda kibao vilivyokuwa vya umma vikabifsishwa, serikali inafanya pale tu ambapo hamna mbadala kwa sasa kama vile Tanesco na kwingineko pachache.

Kama waliopewa shirika kama TTCL wameshindwa kuliendesha na ndio wasomi wetu hao unategemea serikali iliweke hai kwa kuwapa ruzuku? na yapo mashirika kibao mbadala binafsi ya mawasiliano? Mawee, hayo yalipitwa na wakati.

Wewe kama mliapa kodi utakubali leo hii fedha zako zinapelekwa kila mwaka kutoa ruzuku ya shirika lisiloweza kujiendesha? fikiri!
 
Prof. Mwandosya na Maua Daftari ndio walikuwa mawaziri wa mawasiliano kipindi kile cha ttcl kuibiwa na celtel. Swala hili liliwahi kuibuka lakini lilizimwa na huyo mgombea urais (mwandosya). Zito wafuate hao wana taarifa zote za kuiuza ttcl kwa celtel bila pesa. Usiwaogope. Ipelekeni bungeni kama hoja binafsi ili serikali iwaamshe kina maua daftari waseme kilichotokea na kinachoendelea ttcl.
 
hiyo kampuni lazima ifilisike kwa sababu asilimia 90 ya wafanya kazi wa ufundi ni dini moja. Chunguza saa za ibada hasa saa 7 ukienda kwa nje lazima ukute kuna gari ya mafundi wa ttcl
 
Mbona mashirika yote yamekufa mengi sana toka enzi ya Nyerere, Mwinyim, Mkapa na Kikwete? na Mwinyi ndiyo kabisa aliamuwa shirika lolote lisiloweza kuijinedesha lenyewe halitopewa ruzuku tena na Serikali, matokeo si unayajuwa au mpaka tuchambuwe?

Haya yaliyobaki mpaka hii leo yamejitahidi sana.

Huo uongozi wa TTCL ni mbovu kabisa si shirika la kufa lile kwa miuondombinu waliokuwa nayo, tazama attakaelinunuwa utaona linavyoshamiri.

Lakini ndiyo mashirika uya umma yalivyo kama halina ruzuku hayawezi kujiendesha, watu wanaiba tu mtindo mmoja.

Kwa hiyo Mnauza TTCL? are you guys sane?
 
Huyu anayeutaka Uraisi ambaye kitabu chake kimetoka juzi, ameshindwa kuifufua hii kampuni ambayo iko direct chini ya wizara yake ni utendaji upi sasa aliofanikiwa mpaka tumkabidhi nchi, wakati TTCL Shirika la kizalendo kashindwa kulifufua linakufa chini yake. Only in Tanzania where mtu anashindwa kabisa kiutendaji halafu anataka tumpromote mpaka Urais. Mafisadi wamefanikisha azma yao ya kuua shirika la kizalendo lilokuwa na mtandao nchi nzima na branch Ofisi karibia kila mkoa na ilikuwa inaajiri watanzania wengi. Inasikitisha sana!!

Source:Habari Leo

Mtunzi wa kitabu yupo busy na padre wake kukipigia debe kitabu chake haya ya TTCL atakuambia kuna kikomo cha kushauri. Je kama katika wizara kuna madudu haya akipewa nchi si atauza kila kitu huyu????
 
Toka awamu ya Alli Hassan Mwiny iliamuliwa kuwa shirika la umma lisiloweza kujiendesha lenyewe halitopewa ruzuku.

Wizi, Uzembe, Uvivu, Uongo ndiyo unayapeekea mashirika yote ya umma kufa.

Ukiona lipo ujuwe hilo amma linajiendesha lenyewe au linapewa ruzuku kwa kuwa hakuna mbadala wa mashirika binafsi, mfano TANESCO, kama si kusaidiwa na Serikali lingeshakufilia mbali zamani sana.

Sishangai.

Umesema kweli hizi sifa za wizi,Uongo,uvivu na uzembe zote Jakaya anazo, zote.
Wizi-EPA,ESCROW,SUAKALI,Kura etc
Uongo-Ahadi za uongo kwenye Kampeni na nyingine nyingi bungeni na kwenye majukwaa ya siasa na hotuba za TBC
Uvivu na Uzembe-safari zisozoisha na zisizo na tija.
 
Back
Top Bottom