Inasikitisha sana: TTCL Yafilisika Rasmi

Inasikitisha sana: TTCL Yafilisika Rasmi

Nadhani lile wazo wabunge wa Upinzani MIKATABA yote ya Serikali au Taasisi za umma zijadiliwe Bunguni kwanza ndo litakuwa suluhisho kwa tatizo la Mikataba mibovu. TTCL ilitakiwa iwe kimbilio kwa watu wa chini.
 
Hawa mafisadi ccm mpaka watoke madarakani watakuwa wamemaliza rasilimali za nchi,shame on them
 
kumbe ttcl bado ipo? wanauza nini? manake sijaona hata tangazo kwenye tv wala gazeti si kuuza sim card, au product mpya wala hata kuajiri ama walau kutangaza msiba wa mfanyakazi!
 
Sasa Bharti Airtel anayemiliki 35% na Serikali anayemiliki 65% nani anatakiwa atoe mtaji? Au hiyo 35% ni hisa hewa ambazo hazijalipiwa?

HII nayo ni ESCROW nyingine na zipo nyingi. Hebu wanajamvi fuatilieni huyu Omari Issa na uhusiano wake huko Sudan, kuna jambo zito litagungulika. Huenda hata Escrow ina maelezo ya kuunga unga, lakini hili la TTCL ni wizi wa mchana kweupe na wenye akili walijua mapema kwamba hii ni kashfa inakuja.
 
Tanzania shamba la bibi asiyeona !!!
Mafisadi hawana huruma kwanini tunawaonea huruma???
 
TTCL ilikua na mali kibao majumba kama zile apartment za LAMADA wajanja wakajimilikisha kituo kipya cha simu2000 wajanja wakajimilikisha lile eneo nafkuri wafuatilie hasa nani aliingia mkataba huo m bovu na airtel mana kuna tetesi zilisikika hizo ela airtel wanazolipwa kama m bia na ttcl haziendi airtel zinaingia kwa wajanja.
 
Toka awamu ya Alli Hassan Mwiny iliamuliwa kuwa shirika la umma lisiloweza kujiendesha lenyewe halitopewa ruzuku.

Wizi, Uzembe, Uvivu, Uongo ndiyo unayapeekea mashirika yote ya umma kufa.

Ukiona lipo ujuwe hilo amma linajiendesha lenyewe au linapewa ruzuku kwa kuwa hakuna mbadala wa mashirika binafsi, mfano TANESCO, kama si kusaidiwa na Serikali lingeshakufilia mbali zamani sana.

Sishangai.
 
Huyu anayeutaka Uraisi ambaye kitabu chake kimetoka juzi, ameshindwa kuifufua hii kampuni ambayo iko direct chini ya wizara yake ni utendaji upi sasa aliofanikiwa mpaka tumkabidhi nchi, wakati TTCL Shirika la kizalendo kashindwa kulifufua linakufa chini yake. Only in Tanzania where mtu anashindwa kabisa kiutendaji halafu anataka tumpromote mpaka Urais. Mafisadi wamefanikisha azma yao ya kuua shirika la kizalendo lilokuwa na mtandao nchi nzima na branch Ofisi karibia kila mkoa na ilikuwa inaajiri watanzania wengi. Inasikitisha sana!!


Source:Habari Leo

Ukiona hivyo tayari washaliandaa kampuni nyingine mbadala ya kifisadi.
 
Issa, mtanzania ambaye alikuwa CEO wa airtel/celtel wakati wa kuweka mikataba hii mibovu ndiye amepewa kuongoza BRN sasa. Ikumbukwe pia kuna malalamiko kwamba airtel ilianzishwa kwa mtaji wa TTCL, na baada ya kuji establish, wakafanya ujanja wa kujitenga na TTCL. Wakavuna mpunga wee kisha wakauza kampuni ili kujiweka salama.

Ikumbukwe pia kulikuwa na malalamiko ya malipo ya kodi wakati wa kuhamisha umiliki wa kampuni hiyo ya airtel

Ndio ufisadi mwingine huu ambao jamii haiuoni
 
Ama kweli upele humuota mtu asiye na kucha na pia wahenga walinena kuwa penye miti hapana wajenzi...kweli leo makampuni ya mawasiliano yanavyopig ahela ya maana hivi halafu wao TTC wanomiliki mkongo wa taifawanafilisika na kufa kibudu?? Kuna haja ya serikali kufanya maamuzi magumu kwani mkiua TTCL basi nina hakika na shirika la posta linaenda kufa kifo cha mende muda si mrefu.
 
TTCL imehujumiwa sana na viongozi wa serikali kwa asilimia kubwa. Jamani nchi imeuzwa hii mnyonge anasurubiwa na manyang'au, Kunawatu yatupasa kuwaua ili nchi iweze kwenda mbele
 
Wazito hebu tusaidiane katika hili. Ati TTCL imefilisika kutokana na ndoa yake haramu na Celtel? Kabla ya kuingia kwa undani wanajamvi hebu tuuchunguze uhusiano wa Celtel na mtandao wa Osama Bin Laden hasa huko Sudan. Taarifa hizi zilifika Tanzania na wazito wanajua lakini kutokana na njaa ya pesa TTCL ikaingizwa kufanya biashara na Celtel ambayo wengi walijua haifiki mbali. Si wingi wa hela iliyohusika, bali mashaka ya usafi wa Celtel, kashfa hii inazidi ya Escrow.
 
Back
Top Bottom