Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,554
Sababu ya kufanya karabati na maboresho haya ni kuimarisha miundombinu ya umeme inayozunguka njia hiyo.
Umuhimu wa kazi hi ni kumarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya meme kwenye maeneo yanayopata meme kutoka kwenye vituo vya kupoza Umeme vya Dege na Kurasini na hivyo kuwezesha ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Kutokana na kazi hi baadhi ya maeneo yatakosa huduma ya umeme kwa tarehe na muda tajwa kama ifuatavyo, baadhi ya maeneo ya Bandarini, Mbagala, Kurasini, Dege, Kibada, Mjimwema, Kisarawe II, Pemba mnazi, Avic town, Tuangoma na Geza ulole.
Tutaendelea kuwataarifu maendeleo ya kazi hiyo mpaka itakapokamilika.
Shirika linawashukuru Wateja wake kwa uvumilivu katika kipindi chote ambacho huduma ya Umeme itakosekana.