DOKEZO 'NIULIZE MIMI' ni chanzo cha rushwa Hospitali ya Mnazi - (Dar), mamlaka chukueni hatua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
photo_2023-12-11_12-57-55.jpg

Kutokana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kupokea idadi kubwa ya wagonjwa, iliamua kuanzisha kitengo maalumu (dawati) la 'NIULIZE MIMI' kama ambavyo baadhi ya hospitali nyingine zinafanya.

Kitengo hicho lengo la kuanzishwa kwake ni sehemu ya kurahisha huduma kwa wagonjwa kufahamu kwa urahisi maeneo stahiki ambapo utakiwa kwenda kupatiwa huduma mbalimbali.

Pia kitengo hicho utazamiwa kuwa kinalenga kuwasaidia wazee na watu wengine wasiojua kusoma na kuandika au watu wenye ulemavu wanapofika katika hospitali hiyo kupata kwa urahisi matibabu au huduma nyingine za kiutawala.

Kitengo hicho pia ukusudia kurahisisha huduma na kutoa utaratibu ambao unaweza kuepusha changamoto mbalimbali mfano mrundikano usio wa lazima pia ulenga kuwaelekeza wagonjwa taratibu mbalimbali za kuzingatiwa kupata huduma.

Lakini katika hali ya kushangaza licha ya umuhimu wa kitengo hicho, kwa siku hivi karibuni limeonekana kuwa 'Dawati la Rushwa', ambapo kwa sasa wapo baadhi ya watu wenye uwezo wa kiuchumi kutoa rushwa wakifika pale wanaongea na 'NIULIZE MIMI', anawasiliana na Daktari husika wanapelekwa moja kwa moja na kupatiwa huduma huku wahitaji wengine wakiwa wameketi kwenye benchi muda mrefu hata wengine wanaweza kufika jioni bila kuona Daktari husika jambo ambalo ni kero.

Hali hiyo kwa sasa inaonekana kuzoeleka ambapo wapo baadhi ya 'niulize mimi' wanakwambia toa chochote kama unataka kupatiwa huduma ya haraka na ukifanya hivyo uchelewi kupata huduma, lakini tofauti na hivyo unasugua benchi mpaka kinaeleweka, cha kushangaza unaweza kukuta Wazee au watu wenye ulemavu wanasugua benchi jambo ambalo ni kinyume.

Inavyoonekana kuna mkakati wa wazi wa rushwa baina ya Wahudumu hususani Madaktari na 'NIULIZE MIMI' ambapo wameamua kutumia dawati hilo kujiingizia pesa kwa utaratibu usio rasmi licha ya mabango ya 'Usitoe wala kupokea Rushwa' kuwepo kwenye eneo la hospitali.

Mwenendo huu umepekea baadhi ya wagonjwa kukosa huduma kwa wakati na kuwepo kwa malalamiko mengi kuhusu upendeleo wa huduma bila kufuata taratibu ambapo kwa sasa umeanza kujengeka utamaduni wa wagonjwa wengine kuanza kutumia utaratibu huo mithili ya utaratibu rasimi, ambapo wakifika hospitali wanatoa fedha (rushwa) kupitia 'NIULIZE MIMI' kisha wanapewa idhini ya kupatiwa huduma kwa haraka na kuondoka.

Tunaomba Serikali yetu kuliona suala hili na kuchukua hatua za haraka kuokoa maisha ya raia wake ambao wapo hatarini kutokana na utaratibu huo.

TAKUKURU wachukue hatua za kuchunguza wahudumu wa hospitali hiyo hasa kitengo hicho na wasiishie kuweka mabango ya kukataza vitendo vya rushwa badala yake wajikite zaidi kufuatilia kwa kina kwenye maeneo ambayo wanaona yanaweza kuwa na viashiria vya rushwa.

Kutokana na hali niliyobaini eneo hilo nashauri Serikali kwa kuona umuhimu wa kitengo hicho, Hospital kupitia mamlaka husika ziendeshe kwa ubia vitengo vya aina hiyo na wadau wa sekta binafsi hususani wadau wa huduma kwa wateja kupitia wahudumu wenye ujuzi na wanaotambua miiko ya kazi yao ili ikitokea changamoto mfano za Rushwa iwe rahisi kuchukuliwa hatua kwa wahusika na itachochea uwajibikaji zaidi.

Utaratibu huo unaweza kupunguza changamoto ya Rushwa kwa sababu kampuni za aina hiyo zitakuwa na ushindani wa kutoa huduma bora na zimekuwa na desturi ya wahudumu kubadilishana vituo vya kazi mara kwa mara jambo ambalo linaweza kuwa na tija, lakini kwa mazingira ya sasa vitengo hivyo hususani kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja inaonesha wazi wahudumu hawana uweledi na kazi zao na uenda hawaelewi miiko ya kazi yao ndio maana.
 
Changamoto kubwa sana. Mimi huwa sipendi watu wanaoleta rushwa kwenye mambo ya Afya,
 
Hili binafsi nakuunga mkono nilienda pale kwa ajili ya kupeleka barua yangu ya medical form kwa ajili ya ajira ,aiseeh! ilikuwa mikiki sana yani nikawa navutwa na huyu mara yule ili nitoe hela kwa jili ya kusaini form yangu nilivyosema nakiasi fulani,kila mtu akaanza kuniona adui ,mara kpange foleni kule ,kama huna hela yaani ni hatari
 
Back
Top Bottom