Inakuwaje ni Mihimili mitatu wakati Rais ndiye huteua Majaji wote na ana uwezo wa kulivunja Bunge?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Kwa kawaida huwa tunasema tunayo mihimili mitatu inayojitegemea yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

Ni ukweli pia kuwa mkuu wa serikali ni Rais, mkuu wa bunge ni Spika na mkuu wa mahakama ni Jaji mkuu.

Ni ukweli pia kuwa Rais huteua Jaji mkuu na majaji wengine wote.

Kadhalika Rais anaweza kumteua mbunge yoyote kuingia serikalini au kulivunja Bunge bila kuhojiwa na yoyote.

Sasa, kujitegemea/ kutoingiliwa kwa bunge na mahakama kuko katika maeneo gani ilhali juu yake yuko Rais?

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mbali ya kuteua waandamizi mahakama ,Katibu wa mbunge ni mteule wa rais pia. Kwa ufupi Rais ni kama mfalme kwa mujibu wa katiba yetu.

Hapana sio mfalme, ni zaidi ya mfalme. Yaani ni mungu.
 
Hotuba Ya Mheshimiwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Aliyoitoa Mkoani Morogoro Alisema
Ndugu Zangu Kulala Katikati Ni Kuzuri, Maana Hapa Morogoro Ni Katikati Unapata ya Dar es Salaam Na Dodoma

Watani Zangu Ninyi Mmewaza Vinginevyo!!

Mhimili Ni Mmoja Upo Katikati Kama Ilivyo Morogoro
Huo Mhimili Unapata Vyote Kwa Wakati Mmoja
 
Njoo huku

Kwa kawaida huwa tunasema tunayo mihimili mitatu inayojitegemea yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

Ni ukweli pia kuwa mkuu wa serikali ni Rais, mkuu wa bunge ni Spika na mkuu wa mahakama ni Jaji mkuu.

Ni ukweli pia kuwa Rais huteua Jaji mkuu na majaji wengine wote.

Kadhalika Rais anaweza kumteua mbunge yoyote kuingia serikalini au kulivunja Bun

Nawatakia Dominica yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom