Tanzania, Rais ni zaidi ya mfalme!

lukubuzo Samsis

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
2,909
3,340
Tanzania, Rais ni zaidi ya mfalme, anateua kila kitu na kila mtu kwa kufuata au kutofuata matakwa ya katiba ya kifalme ambayo iliundwa kwa kuzingatia matakwa ya kulinda chama kimoja -CCM.

Kenya; Rais anateua majina kutoka katika majina yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo inaundwa na watu 11. Mwenyekiti ni Jaji Mkuu.

Brazili; Rais anapendekeza majina ya majaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho kwenda Bunge la senate. Lazima yapate idhini ya kura nyingi za wabunge

Poland; Majaji 15 wa Mahakama ya Katiba wanachaguliwa na Sejm (baraza la chini la Bunge) kwa kipindi cha miaka 9 ambayo haina nyongeza. ‘kutoka miongoni mwa watu wanaotofautishwa na ujuzi wao wa sheria’

France; Majaji tisa (9) wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Katiba, watatu (3) wanateuliwa na Rais wa Jamhuri, watatu (3) wanateuliwa na Rais wa Seneti, watatu wanateuliwa na Rais wa bunge.

Mongolia; theluthi moja ya majaji wa mahakama ya katiba wanateuliwa na Rais. Theluthi moja wanateuliwa na bunge na theluthi moja wanateuliwa na mahakama.

Bosnia and Herzegovina; Majaji wanne (4) wa mahakama ya katiba (Constitutional Court) wanateuliwa na bunge la wawakilishi wawili (2) na bunge Republika Srpska wawili (2).

Germany; Baraza la juu la bunge, ambalo linaundwa na wajumbe wa serikali za majimbo linateua nusu ya wajumbe wa mahakama ya katiba ya shirikisho.

Bolivia; Chaguzi za wananchi zitatumika kuchagua wajumbe wa mahakama kuu ya haki, lakini, kupunguza siasa, wagombea hawaruhusiwi kuwa wafuasi wa vyama vya siasa.

Netherlands; Majaji wa mahakama kuu huteuliwa na mfalme (kwa ushauri wa lazima wa serikali) kutoka katika orodha ya wateule watatu waliopendekezwa na baraza la chini la bunge.

El Salvador; Wajumbe 15 wa mahakama kuu wanachaguliwa kwa wingi wa ⅔ ya wabunge, ambayo inahakikisha kwamba hakuna chama kimoja cha siasa kinachoweza kudhibiti uteuzi.

Afrika Kusini; Majaji Mahakama ya Katiba wateuliwa na Rais kwa kushauriana na Jaji Mkuu na viongozi wa vyama vya siasa bungeni kutoka kwa orodha ya iliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama

Tanzania.

Tanzania; Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu na Majaji wengine wa Mahakama Kuu wasiopungua 15 watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na tume ya kuajiri ya mahakama.

Tanzania; Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani na Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani wasiopungua 2 watateuliwa na Rais na Jaji Mkuu atakuwa ndiye Kiongozi wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Idara ya Mahakama

Tanzania; Majaji wengineo wa Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais, baada ya kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu ambao wanaweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu

Tanzania; Ikitokea kiti cha Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufani kitakuwa wazi Rais baada ya kushauriana na Jaji Mkuu kama kawaida, kumteua Kaimu Jaji wa Mahakama ya Rufani

Tanzania; Tume ya kuajiri mahakimu na watumishi wengine wa mahakama pamoja na majukumu yake, Madaraka ya kuwathibitisha na kuwapandisha vyeo kazini watu hao yatakuwa mikononi kwa Rais

Tanzania; Wajumbe wa tume ya kuajiri ya Mahakama; Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Jaji wa mmoja wa mahakama ya rufani, Jaji kiongozi Mahakama Kuu, wajumbe wawili wanaoteuliwa na Rais. Tume yote wajumbe wameteuliwa na Rais.

MMM, Martin Maranja Masese

20230904_175902.jpg

View attachment 2739950
 
Back
Top Bottom