mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Ndio maana watu sasa wanaongelea zaidi Katiba mpya mkuu ambayo italeta mihimili mitatu na sio hii brabra tuliyonayo.
Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuisoma Katiba ya JMT (1977) kwa umakini.Kwa kawaida huwa tunasema tunayo mihimili mitatu inayojitegemea yaani Serikali, Bunge na Mahakama.
Ni ukweli pia kuwa mkuu wa serikali ni Rais, mkuu wa bunge ni Spika na mkuu wa mahakama ni Jaji mkuu.
Ni ukweli pia kuwa Rais huteua Jaji mkuu na majaji wengine wote.
Kadhalika Rais anaweza kumteua mbunge yoyote kuingia serikalini au kulivunja Bunge bila kuhojiwa na yoyote.
Sasa, kujitegemea/ kutoingiliwa kwa bunge na mahakama kuko katika maeneo gani ilhali juu yake yuko Rais?
Nawatakia Dominica yenye baraka.
Maendeleo hayana vyama!
Ibara ya 1 inatamka kwamba Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano
Ibara ya 33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Na
Ibara ya 33. -(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kwa Ibara hizo, kimsingi Rais ndiye kiongozi Mkuu wa Nchi mwenye mamlaka yote ya kuendesha nchi akisaidiwa na wafuatao kwa shughuli mbalimbali kama zilivyoainishwa kwenye Ibara ya 4.-(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma.
Vyombo hivyo Kikatiba ndivyo huunda Mihimili 3:
√ Serikali ikiongozwa na Waziri Mkuu ambaye huteuliwa na Rais - Ibara ya 51 ya Katiba ya JMT (1977);
√ Bunge likiongozwa na Spika ambaye huteuliwa na Wabunge - Ibara ya 84 ya Katiba ya JMT (1977); na
√ Idara ya Mahakama ikiongozwa na Jaji Mkuu ambaye huteuliwa na Rais - Ibara ya 118 ya Katiba ya JMT (1977).