Inadaiwa FIFA imeifungia Yanga kusajili madirisha matatu kutokana na deni la Kocha Luc Aymael

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Kocha.JPG
Kwa mujibu wa @FARPostZA, FIFA imeifungia klabu ya Yanga kusajili wachezaji kwa madirisha matatu (3) mfululizo baada ya kushindwa kumlipa fidia ya kuvunja mkataba aliyewahi kuwa Kocha wao Luc Aymael.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji ambaye pia amewahi kuzifundisha Free State Stars na Polokwane City za Afrika Kusini, Oktoba 2022 alishinda kesi ya kuvunjiwa mkataba na Yanga bila kufuata utaratibu.

Klabu ya Yanga ilipewa maelekezo ya kumlipa Kocha huyo jumla ya dola za Marekani 152,000 kufuatia kumfuta kazi pasipo kufuata taratibu miaka miwili iliyopita.

Baadae klabu ya Yanga ilipanga kulipa kiasi hicho kwa awamu tano (5) ambapo awamu ya kwanza alipaswa kuwa Oktoba 2022.

Kwa mujibu wa FARPost, Yanga ililipa deni hilo kwa awamu mbili, Oktoba na Novemba 2022.

Kwa maana hiyo, Yanga bado wanadaiwa na Eymael dola za Marekani 99,000 pamoja na ada ya adhabu ambayo ni dola za Marekani 5,000.
 
Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeifungia Klabu ya Yanga Kutosajili kwa Madirisha matatu yajayo kwa Kosa la Kutomlipa aliyekuwa Kocha Mkuu wao Luc Eymael Raia wa Ubelgiji.

Chanzo Taarifa: Shaffih Dauda

Na hivi Aziz K hivi sasa ni tia maji tia maji, huku Dumbia nae akiwa haeleweki kwa Kupigwa Miba na Nondo Namba hapati na Morisson nae amechagua Kushinda Juliana Pub Mbezi Beach badala ya Kucheza Mpira halafu Wachezaji wengi wakiwa Wameshanoki / Wameshachoka kuna Watu kwa Rungu hili la FIFA wanaweza kuweka Rekodi ya Kufungwa sana na Kufanya vibaya mno kwa Msimu ujao.

Na nawakumbusha tu kuwa huyu Kocha Luc Eymael anayewadai Yanga SC Pesa zake ndiyo yule yule aliyewatukana / aliyewaita wana Yanga SC wote kuwa ni Mbwa, Nyani na Some.

Kudadadeki imeisha hiyo Mkome!!!!
 
Na iwe hivyo

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom