Yanga yafungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
IMG_8344.jpeg

Klabu ya Young Africans iliyo Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Birigimana alifungua kesi FIFA kuhusiana na malipo ya ada ya usajili (sign on fee).

Klabu hivo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

Iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu.

===

Pia soma

Yanga yafutiwa adhabu ya kutosajili baada ya kumlipa Bigirimana
 
I
Hii habari itaenda viral yani itauza sana itafanya Yanga ijulikane World wide

Kutokana na profile ya mchezaji husika aliwahi kuwa mchezaji tegemeo pale Ulaya kwenye Club kubwa ya New Castle.
Iende tu
 
Klabu ya Young Africans iliyo Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana.

Vamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Birigimana alifungua kesi FIFA kuhusiana na malipo ya ada ya usajili (sign on fee). Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

Iwapo klabu inataka kuvunja mkataba a mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu.​
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom