IN PICTURES LIVE TOKA KARIMJEE - Buriani Dada Regia Mtema

Rejao bana.......Zanzibar ni ughaibuni siku hizi?

[h=3]MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU REGIA MTEMA KARIMJEE DSM LEO, KUZIKWA KESHO IFAKARA[/h]

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshma zake za mwisho kwa Marehemu Mhe. Regia Mtema katika viwanja vya Karimjee leo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.

Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.

Salaam Kutoka kwa Katibu mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Andrew Chenge pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Tundu Lissu, Vita Kawawa, pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na baadhi ya ndugu wa Marehemu.

Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mh. Jaji Fredrick Werema.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Sadick Meck, Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe wakimsubiri makamu wa Rais leo katika viwanja vya karimjee kuaga mwili wa Mbunge wa Chadema Viti Maalum Marehemu Regia Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari Jumamosi tarehe 14, 2012

Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu,Mh. Regia Mtema iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani wa OMR na Owen David wa BUNGE.

Posted by MUHIDIN MICHUZI at <a class="timestamp-link" href="http://michuzi-matukio.blogspot.com/2012/01/makamu-wa-rais-dkt-bilal-ashiriki-kuaga.html" rel="bookmark" title="permanent link" style="text-decoration: none; color: rgb(26, 34, 42); "><abbr class="published" title="2012-01-17T14:19:00+03:00" style="border-top-style: none; border-right-style: none; border-bottom-style: none; border-left-style: none; border-width: initial; border-color: initial; border-image: initial; ">Tuesday, January 17, 2012</abbr>
 
Hili li Rage halina bastola hapa kweli?

2.JPG
 
Hizi Picha quality yake mbovu sana! Tunaomba mwenye picha nzuri aziweke na areplace hizi zilizopo!!

sounds like shukrani ya punda ni mateke.
button ya dislike inahusu iwepo.
watu kibao wameenda huko lkn hawajaleta picha huyu aliyejitahidi kutuletea hizi sijui atajisikiaje kusikia maneno kama haya,
...............................................
R.I.P Regia,inauma sana kutuacha.
 
Ningekuwepo karibu ningehudhuria na tshirt yangu na bado nikaondoka bila mtu yeyote kujua mimi ni nani hapa JF au URAIANI. Sema tu hawakua tayari kuwakilisha kwa tshirt.

Labda tatizo ni upatikanaji wa t-shirts......MUDA.......haukutosha toka jana kwenye kutoa hoja ujumbe gani utumike,kuchapisha na kugawana
 
Wakuu mie nilisema je nitamuenzi vipi dada yetu mpendwa humu alietutoka kwa masikitiko makubwa? 1. Kuhudhuria kwenye kutoa heshima za mwisho 2. Kutumia kipaji changu cha matukio-picha kuchukua baadhi ya picha kwa manufaa ya ambao hawakupata fursa ya kuaga.

Kwa kweli najisikia faraja sana nimefanikiwa kwa hayo malengo mawili na angalau nimemuaga dada yetu mpendwa hivyo angalau simanzi na majonzi makubwa niliyonayo yamepungua kwa kiasi fulani.

PICHA nimepiga kwa kilonga longa changu cha mchina ambacho kimejitahidi kwa kweli kuwapa japo kwa muhtasari kilichotokea pale KARIMJEE....
 
Kaka umejitahidi sana....
 
sounds like shukrani ya punda ni mateke.
button ya dislike inahusu iwepo.
watu kibao wameenda huko lkn hawajaleta picha huyu aliyejitahidi kutuletea hizi sijui atajisikiaje kusikia maneno kama haya,
...............................................
R.I.P Regia,inauma sana kutuacha.

USijali wangu wala sijisikii vibaya hata punje kwa kweli nimefarijika sana moyoni kutimiza namna ya kumuenzi dada yetu mpendwa na mpiganaji REGIA (R.I.P)
 
Wakuu mie nilisema je nitamuenzi vipi dada yetu mpendwa humu alietutoka kwa masikitiko makubwa? 1. Kuhudhuria kwenye kutoa heshima za mwisho 2. Kutumia kipaji changu cha matukio-picha kuchukua baadhi ya picha kwa manufaa ya ambao hawakupata fursa ya kuaga.

Kwa kweli najisikia faraja sana nimefanikiwa kwa hayo malengo mawili na angalau nimemuaga dada yetu mpendwa hivyo angalau simanzi na majonzi makubwa niliyonayo yamepungua kwa kiasi fulani.

PICHA nimepiga kwa kilonga longa changu cha mchina ambacho kimejitahidi kwa kweli kuwapa japo kwa muhtasari kilichotokea pale KARIMJEE....

MUCH appreciated ET...kuna watu ni ngumu sana ku appreciate kidogo kizuri kinachofanywa na wengine!!! Learn to live with such kind of personalities!!!
 
Hao ni wale wenye tru IDs.......mimi na wewe hatuwezijionyesha hadharani....lakini tulikuwepo wengi tu

Mkuu Cama. inabidi ifike wakati watu tuache kuona kuwa member humu ni uhaini. Hatuvunji sheria ila tunasema kilicho kweli na hii ni kwa faida yetu sote na vizazi vijavyo tukiwaachia hawa bila kupiga kelele watakula mpaka vya vitukuu vyetu !
 
sounds like shukrani ya punda ni mateke.
button ya dislike inahusu iwepo.
watu kibao wameenda huko lkn hawajaleta picha huyu aliyejitahidi kutuletea hizi sijui atajisikiaje kusikia maneno kama haya,
...............................................
R.I.P Regia,inauma sana kutuacha.
Muhimu hapo haikuwa Quality ni ujumbe kwa wanaforum ambao hawakupata nafasi hiyo japo wapate picha ya tukio kiuhalisi...picha zinaexpress ukweli zaidi kuliko story
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom