Buriani mzee Kitwana Selemani Kondo (1930 - 2017) na Dk. Ramadhani Kitwana Dau

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,796
31,809
BURIANI MZEE KITWANA SELEMANI KONDO (1930 - 2017) NA DK. RAMADHANI KITWANA DAU

Mohamed Said May 30, 2017

xl_ChymWwJcjEkio_7YiN5nRj6j94M9tN_gQxviw-JA2Bo13GUAIlfFTPz164IcB1OVJ2I0xEM__HYhf5a60c9BToID-A3VyZEdYPqYsD2EjMrU1rTkwVQJlTKo12aZB1dJLBOyQqkFw91J7a1DR9h3SAkBQ5jj7DDx8cwRkuNpw0XZUp3r54BBIEYP5Phnw-uhhM7p4WQkNKXx_r_6WFUhJwkA99iY6q7etJPfPdcNAh4ErIFS3uXik5Ie8bOBxujVUESN3CICzIKsFNA7VKw034TM_OyfhZ3GDlfUb_idvi71KLadK-1RwSIPAeM8kedeB-Kj_QHBz8g38hIlhR_xp4Jf-tRsTFLIy-TG6WkqK1cnmHXW1MMxaJaaAXOpbg4yH8I0xkiE5Auz4Fx4AiE0D6gBjLunrBsWwwFt2NR9NCNB7NtIsMS41dfO1AehWULsJMV6nm9qRTYt5WaCzfOCcgvt4Suhx8VygWP6BeXq0UWZUCR6x7mF92NGd3F_vN4OumU0D0sFr9NkcRR3ak3MzXiQLjfAunskQlXn8ulyBOfHN2Yqv9z3jLOQGdYy8vVUy3oX97zfD9TmEY1_XV5XkNzKBr3sD3yVdZGAu5YiaaRXoug=w625-h629-no

Kitwana Selemani Kondo katika ujana

BURIANI MZEE KITWANA KONDO

Ramadhani K Dau

Siku ya Jumatano tarehe 24 Mei 2017 ni siku ambayo itakumbukwa na Watanzania wengi na haswa Waislamu kwa kuondokewa na mzee wetu Alhaj Kitwana Selemani Kondo maarufu “KK” au mzee wa mjini. Siku 4 kabla ya kifo chake, mwanawe wa kiume Bwana Adnan-Msakuzi alinitumia ujumbe kwenye WhatsApp akiniarifu kuwa Mzee KK amelazwa Hindu Mandal na hali ya afya yake inazidi kuzorota.

Siku ya pili yake nilimtumia ujumbe Adnan-Msakuzi kutaka kujua hali ya Mzee inaendeleaje. Majibu ya Adnan yaliniashiria kuwa mzee wetu amekaribia kufika mwisho wa safari yake hapa duniani. Aliniambia kuwa kwa sababu ya ukaribu wangu na Mzee KK hanabudi aniarifu ukweli ulivyo. Aliniarifu kuwa hali ya mzee ni mbaya sana na kwamba kinachosubiriwa na Rehma Zake Mwenyezi Mungu. Kwa kweli ujumbe ule ulinihuzunisha sana na sikuweza kuhimili uchungu ule peke yangu. Nikamwarifu Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo cha Waislamu Morogoro na Bwana Faraji Abdallah Tamim, mwalimu wa chuoni hapo.

Ilipofika siku ya Jumatano tarehe 24 Mei nikapata taarifa kupitia moja ya kundi sogozi (chat group) kuwa Mzee KK amefariki dunia. Pamoja ya kuwa hali hiyo ilikuwa tayari inatawala fikra zangu tokea siku niliyopata ujumbe kutoka kwa Adan lakini kifo hakizoeleki. Taarifa hiyo ilinikuta nikiwa najiandaa kwenda uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur kumsindikiza shemeji yangu. Wakati huo kwa saa za Malaysia ilikuwa kiasi cha saa 4 usiku. Nilipwelewa sana kwa sababu ya uhalisia kuwa sitowahi kumzika mzee wangu Mzee KK.

Haikuchukua dakika 10 baada ya taarifa hizo, Adnan kanipigia simu ambayo hatukuweza kuzungumza hata neno moja kutokana na vilio vyetu. Kila mmoja alikuwa analilia kwake. Ghafla akakata simu na kunitumia ujumbe mfupi uliosema “KK is dead. Allah is Great”. Mara tu baada ya kupata taarifa hiyo nilichanganyikiwa na kuona uchungu sana baada ya kuona kuwa sitoweza kumzika Mzee KK ambaye aliwahi kunitamkia mbele ya mkewe Bi Hanifa kuwa ikitokea atafariki kabla mimi basi angependa asaliwe Masjid Mtoro, azikwe makaburi ya Tambaza na mimi niwe mmoja kati ya watu watakaoingia kaburini.

Katika maishani mwangu, hii ni mara ya tano kuandika taazia yaani “obituary”. Buriani zilizotangulia ni za aliyekuwa mwalimu wangu Chuo Kikuu DSM na rafiki yangu wa karibu Profesa Ken Edwards mwenye asili ya Jamaika, aliyekuwa Afisa wa Uhusiano wa NSSF Alfred Ngotezi, rafiki yangu tokea utotoni Abubakar Mohamed Saleh Tambaza maarufu “Babu Chela” na Saidi Masimango aliyekuwa Mkurugenzi wa Teknohama NSSF. Kila niandikapo taazia huwa nafanya hivyo nikiwa na moyo mzito na huzuni sana. Kila niandikapo huwa naomba kuwa hiyo iwe ndio ya mwisho kwani kuandika taazia ni jambo zito sana haswa ikiwa inamuhusu mtu wa karibu yako kama nilivyo mimi kwa Mzee KK na hao waliotangulia kabla yake.

Kwa huzuni niliyokuwa nayo niliamua kutoandika taazia hii kwa sababu nisingeweza kufikia mwisho kwa kilio. Lakini mara tu baada ya habari za msiba kuenea nikaanza kupata salaam toka kwa watu mbali mbali akiwemo Prof Hamza Njozi, mdogo wangu Abdul Dau na Adnan-Msakuzi. Ujumbe kutoka kwa Adnan ndio ulizidisha majonzi yangu lakini pia ulinipa nguvu ya kuandika kwani kama alivyosema Adnan na nakuu “Dr please write a eulogy for KK. You knew him well, no one can talk of him better than you”.

Baada ya kutafakari nikaona kama sikuandika ntakuwa sikumtendea haki Mzee Kondo. Kwa kuwa nimekosa fursa ya kumtimizia wosia wake kuwa niwe miongoni mwa watu watakaoingia kaburini kumzika, nimeona nisikose vyote. Kwa kuzingatia kanuni ya fiqh kuwa kama jambo haliwezi kufanyika lote basi lisiachwe lote. Waswahili nao wana msemo wao “lisobudi hutendwa”. Hivyo basi nimeamua kuandika taazia hii kwa huzuni na unyonge mkubwa.

Mzee Kitwana Selemani Kondo alizaliwa Mtoni Kijichi, Dar es Salaam tarehe 1 Agosti 1930. Pale Mtoni Kijichi ukoo wake ni ulijulikana kwa jina la Mahembe. Wazazi wake wote wawili ni Wazaramo. Kiumeni kwake ni Mtoni Kijichi na kikeni kwake kijiji cha Gumba, Kisarawe. Alipata elimu ya msingi Mchikichini kisha akaenda Tabora Boys na baadae Chuo Kikuu cha Howard kilichopo Washington DC, Marekani. Pia Mzee Kondo alichukua masomo ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa darasa moja na marehemu Sheikh Mohamed Ali Al-Buhry.

Kwa upande wa kazi, Mzee Kondo alikuwa Polisi kwa muda mrefu hadi kufikia ngazi ya Inspekta na baadae akawa Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, marehemu Oscar Kambona. Wakati wa uhai wake Mzee KK ameongoza Taasisi kadhaa za Umma zikiwemo Shirika la Magari la Taifa yaani State Motors Corporation (Mkurugenzi Mkuu), Mwenyekiti wa Bodi za TANESCO, Mamlaka ya Bandari na Bodi ya Korosho. Wakati wa uhai wake, Mzee Kondo alijaaliwa kupata watoto 8. Kati ya hao wanaume 3 na wanawake 5.

Nimemfahamu Mzee tokea nikiwa mdogo kwa sababu ya kuzaliwa na kulelewa Mwembetogwa, jijini Dar es Salaam. Wakati wa utoto wangu sikuwa na ukaribu sana na Mzee Kondo kwa sababu ya tofauti ya umri. Ukaribu wangu kwake ulianza mwaka 1995 wakati alipoteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) ambapo mimi nilikuwa Mkurugenzi wa Masoko kwa miaka tisa. Nakumbuka siku moja mara tu baada ya kumaliza kikao cha Bodi niliamua kumsindikiza mpaka kwenye maegesho ya gari. Baada ya kufika kwenye gari yake, nikaona nichukue fursa hiyo nijitambulishe zaidi kwake kwani mpaka wakati huo alikuwa ananifahamu kama Mkurugenzi wa Masoko. Nikajitambulisha kuwa mimi nimezaliwa na nina asili ya Dar es Salaam.

Mara tu baada ya kumwambia hivyo haraka kabisa akaniuliza baba yangu nani. Ili kumtosheleza kiu chake sikutaka kumtambulisha baba yangu. Badala yake, na kwa makusudi kabisa nikamwambia mimi ni mtoto wa “John” Iddi. Mara tu nilivyojitambulisha akasema “wewe mwanangu, “John” Iddi alikuwa mkwe wangu”. Nilifanya makusudi kumtaja “John” Iddi ambaye ni baba yangu mkubwa. Jina lake halisi ni Thabit Iddi Dau. Jina la “John” aliitwa na mama yake baada ya kumzaa akiwa ana umri mkubwa sana.

ya kujifungua akasema mtoto huyu nimempata “Jioni” kwa maana ya kuwa amemzaa hali ya kuwa yeye ana umri mkubwa sana na alikwisha kata tamaa ya kupata mtoto. Pamoja ya kuwa jina lake halisi lilikuwa Thabit lakini tokea utotoni alijulikana kwa jina la “Jioni” ingawa kwa urahisi wa matamshi badala ya kusema “Jioni” likavuma jina la “John”. Marehemu Bwana Thabiti alijulikana sana kwa jina hilo la utani hadi kufa kwake.

Nimesema niliamua kujitambulisha kupitia baba yangu mkubwa kwa makusudi kwa sababu Mzee Kondo aliwahi kumuoa Bibi Kijakazi wa Mgoto ambaye alikuwa anafanyakazi Halmashauri ya Jiji (City Council). Kwa bahati mbaya hawakuwahi kupata mtoto. Katika ndoa yake nyingine, Bibi Kijakazi alijaaliwa mtoto wa kike ambaye jina lake ni Kurwa. Sasa huyu Bibi Kurwa ndiyo aliyekuwa mke wa kwanza wa marehemu Mzee “John” Iddi. Katika uhai wao walijaaliwa kupata watoto wawili. Iddi “John” na Mwatatu Thabit. Iddi alifariki mwaka 2001. Mwatatu yu hai ameolewa na Mohamed Mfaume maarufu “Difu” ambaye alikuwa golikipa wa Yanga, Cosmo na Timu ya Taifa. Mpaka sasa Mwatatu anaishi Kariakoo mtaa wa Swahili kwenye nyumba ya urithi wa mama yake.

Kinasaba, Mzee Kondo alikuwa anamwita Mzee “John” Iddi mkwe kwa sababu yeye (Mzee KK) alimuoa Bibi Kijakazi ambaye alikuwa mkwe wa Mzee “John” Iddi. Kwa upande mwingine, marehemu Mzee “John” Iddi (Thabit Iddi Dau) na marehemu baba yangu mzazi (Kitwana Ramadhani Dau) ni mtu na kaka yake. Wazungu wanasema ni first cousins, sisi Waswahili tunasema wamezaliwa nyumba kubwa na ndogo (kwa maana ya baba mkubwa na baba mdogo) au kwa lugha nyingine tunawaita watoto wa Simba kwa Simba. Kwa hiyo kinasaba, uhusiano wangu na Mzee Kondo ni kwa kupitia baba yangu mkubwa marehemu Mzee “John” Iddi Dau.

Tokea siku ile ambayo nilijitambulisha kwa Mzee Kondo, tukajenga ukaribu sana na alikuwa ananipenda sana. Ilikuwa haipiti wiki bila kwenda nyumbani kwake Hill Road Oyster Bay na baadae mtaa wa Mtitu Upanga kwenda kumwamkia na “kupata habari za mjini”. Ni kutokana na mazoea hayo ndipo Mzee KK akapata jina lingine la utani la “mzee wa mjini”. Na ni kweli, wakati wa uhai wake, kila utakapoenda nyumbani kwa Mzee KK hukosi kupata “habari za mjini” ingawa wakati mwingine zinakuwa ni habari au fikra zake yeye lakini ili kuzipa uzito atakwambia kuna habari mjini kuwa …(hapo anaeleza hiyo habari ilivyo). Moja katika hizo habari za mjini zilininufaisha sana na kuninusuru na janga kubwa sana ambalo lingenikuta. Leo hapa si mahala pake kuzungumzia habari hiyo. In Shaa Allah kuna siku ntaitafutia nafasi kuizungumza. Naendelea kumshukuru sana kwa hilo na mengine mengi ambayo amenifanyia mimi na watu wengine wengi.

Mzee KK atakumbukwa na kuliliwa na wengi kwani alikuwa mwepesi sana kusaidia watu wenye shida. Marehemu alikuwa mcheshi na mwenye kupenda maskhara sana. Alichanganyika na watu wa kila rika. Alikuwa mtu wa msaada sana kwa watu wa aina zote, wake kwa waume. Nyumbani kwake kulikuwa hawapungui wageni wa kila aina kuanzia wanasiasa, wana michezo, viongozi wa dini nk. Mmoja kati ya watu wengi waliosaidiwa na Mzee Kondo ni marehemu Profesa Idrisa Ali Mtulia. Wakati wa uhai wake, Profesa Mtulia alinisimulia namna ambavyo marehemu Mzee Kondo alivyomsaidia kwenda kusoma Uingereza. IIikuwa mwaka 1978 wakati Profesa Mtulia alipochaguliwa kwenda kusoma Clinical Fellowship kwa miaka miwili kwenye hospitali ya Hammersmith ambayo ni sehemu ya Chuo cha Imperial London, Uingereza. Gharama zote za masomo zilikuwa zilipwe na Serikali.

Kwa bahati mbaya siku chache kabla ya safari, jina la Profesa Mtulia halikuwemo kwenye orodha. Profesa akawa hana la kufanya. Akaamua kwenda kuomba msaada kwa Mzee Kitwana Kondo. Mzee Kondo akamhakikishia kuwa ataenda kusoma mwaka ule ule na wala asiwe na hofu. Mzee Kondo akazungumza na Karimjee na baada ya siku 4 tu Profesa Mtulia akapata udhamini kamili (full scholarship), ambao ulijumuisha tiketi ya ndege na fedha zote za matumizi akiwa Chuoni.

Udhamini huo ulitolewa na mama yake mzazi Karimjee. Kutokana na masomo hayo, Profesa Mtulia akatunukiwa kuwaMember of Royal College of Physicians (MRCP) na baada ya kudhihirisha umahiri wake akatunukiwa kuwa Fellow of Royal College of Physicians (FRCP). Profesa Mtulia alikuwa ni mmoja kati ya watu wengi waliosaidiwa na Mzee KK. Baada ya kurudi masomoni na baadaye kutunukiwa FRCP, Watanzania waliokuwa na hadhi hiyo walikuwa wachache sana; nadhani hawakufika 5. Mmoja kati ya hao alikuwa marehemu Dr. Aaron Chiduo; wengine nadhani ni Profesa William Makene na Profesa Shaba.

Kwa upande wa siasa Mzee Kondo ametoa mchango mkubwa sana kwa muda wote wa uhai wake nje na ndani ya Serikali, Bunge, TANU na CCM. Mzee KK alikuwa mzalendo ambaye aliitakia sana mema nchi yetu. Kwa wale wazee wa Dar es Salaam waliobaki watakumbuka sana mchango alioutoa tokea wakati wa Ukoloni na haswa baada ya Uhuru. Yapo mengi ya kihistoria aliyoyafanya kwa kuinusuru nchi yetu na kufika hapa ilipofika leo. Mambo mengine hapa si mahala pake.

Moja kati ya sifa zake nyingi ni ujasiri. Mzee KK hakuwa mwoga na alikuwa na ujasiri wa kusimamia jambo ambalo anaamini ni sahihi na lina manufaa kwa nchi yetu. Mifano iko mingi. Kwa leo itoshe tu kuwa alisimamia suala la upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro kwa kujenga hoja kwa Rais wa wakati huo Mhe Benjamin William Mkapa mpaka Mhe Rais akashawishika kuwa ni jambo jema kuanzishwa kwa chuo hicho kwenye majengo ya kilichokuwa Chuo cha Mafunzo cha TANESCO. Kama kuna mtu mmoja ambaye ametoa mchango wa kipekee uliopelekea upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) mtu huyo ni Mzee Kitwana Selemani Kondo.

Kwa kuenzi jitihada zake hizo, na kwa kuzingatia Mzee Kondo ni Mwenyekiti mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF), Taasisi ambayo ndiyo Mmiliki wa MUM, nashauri uongozi wa Chuo ubadili jina la kampasi ya Morogoro iitwe Muslim University of Morogoro, Kitwana Kondo Campus. Natoa rai hiyo kwa kujua kuwa Chuo kina mpango wa kujenga kampasi nyingine Lindi (Kitunda), Kilwa (Mpara), Morogoro (Sangasanga) na Dar es Salaam (Kigamboni). Kwa siku za usoni, Chuo kitakapoanza kutoa Shahada za Uzamivu (PhD), nashauri Mzee Kitwana Kondo atunukiwe PhD (Honoris Causa) posthumously.

Kwa kawaida, Shahada ya Uzamivu ya Heshima, yaani PhD (Honoris Causa), ndiyo shahada ya juu zaidi katika Chuo Kikuu chochote. Shahada hii hutolewa kwa watu ambao wanaoheshimika sana na ambao wametoa mchango mkubwa katika jamii kwenye nyanja mbalimbali. Mchango wa Mzee Kondo katika nchi yetu hauna mithali.

Aidha Mzee KK alikuwa mwepesi sana wa kuelewa vitu (sharp) na mtu wa mikakati sana. Hakuna alilofanya bila kufikiria nini kinachoweza kutokea usoni na ni namna gani anaweza kuikabili hiyo hali. Nimeyashuhudia hayo wakati akiongoza vikao vya Bodi ya Mamlaka ya Bandari na ushiriki wake katika vikao vya maandalizi ya kuazishwa kwa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Kwa wote ambao wamewahi kufanyakazi na Mzee Kondo, watakubaliana nami kuwa staha yake, weledi wake, busara zake na mchango wa katika taifa letu anastahili kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima, yaani PhD (Honoris Causa).

Wakati alipokuwa Meya wa Jiji, Mzee Kondo alithamini sana mchango wa watu mbalimbali walioshiriki katika harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika. Ili kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijao, Mzee Kondo aliwashawishi madiwani wenziwe kupitisha azimio la kubadili majina ya baadhi ya mitaa ya Dar es Salaam ili ipewe majina ya wazee wetu wa Dar es Salaam walioshiriki kwenye harakati hizo. Utaratibu uliotumika ni kuupa jina la mtaa kwa kila Mzee ambaye alieishi katika mtaa huo. Mifano ya mitaa iliyobadilishwa majina ni mtaa wa Kipata (Kleist Sykes), mtaa wa Tandamti (Mshume Kiyate), mtaa wa Aggrey (Makisi Mbwana), mtaa wa Somali (Omari Londo), mtaa wa Ndanda (John Rupia) na mtaa wa Mwananyamala (MwinyiJuma MwinyiKambi). Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi leo baadhi ya mitaa hiyo haijawekwa vibao vya majina mapya. Ili kuendeleza dhamira nzuri ya kuwaenzi wazee wetu waliotoa mchango mkubwa katika nchi yetu naishauri Manispaa ya Ilala ibadili jina la mtaa wa Mtitu ambapo alikuwa anaishi marehemu Mzee Kondo na kuitwa mtaa wa Kitwana Kondo.

Sambamba na ujasiri, Mzee KK alikuwa anaipenda sana dini yake na alikuwa mtetezi mkubwa wa Waislamu. Ilikuwa kila ukienda nyumbani kwake ukimtajia Aya kwenye Quran basi haraka huchukua kitabu chake kidogo (note book) na kuiandika ili akaifanyie kazi kwa vitendo au hata kwa kuzungumza kwa wengine. Miongoni mwa Aya ambazo Mzee KK alikuwa akizipenda sana ni Aya ya 10 na ya 11 kwenye Sura ya 61 (As-Saff), pia Aya ya 31 kwenye Sura ya 76 (Al-Insan au kwa jina lingine Dahr).

Kwa kumuenzi Mzee KK sitotoa tafsiri ya Aya hizo kwa makusudi ili msomaji upate ushawishi wa kwenda kuzisoma mwenyewe ili nawe upate fadhila za kuisoma Quran. Katika kuonesha mapenzi aliyonayo kwa dini yake, siku zote Mzee Kondo alikuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya Waislamu. Moja katika jitihada zake nyingi ni kupatikana kwa kiwanja ambacho kimejengwa Masjid Maamur, Upanga.

Mzee Kondo alijivunia sana Uswahili na Uzaramo wake. Watoto wake wengi aliwapa majina ya Kizaramo kama vile Mtogole, Azimala, Msakuzi nk. Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizokuwa nazo Serikalini, kamwe Mzee Kondo hakusahau marafiki zake ambao wengi wao walikuwa ni watu wa kipato cha chini sana. Baadhi yao ni marehemu Mzee Kibiriti, marehemu Mzee Sindano, marehemu Omar AbdulRahman maarufu “Ugundo”, Mzee Gulu, Captain Maliki, marehemu Ramadhani Mangilile, marehemu Ali Abbasi, na marehemu Mapepe. Wengine ni marehemu Hamisi George, marehemu Abbas Mzee, marehemu Saleh Mtumwa, marehemu Maalim Mbegu wote wa Egyptian Musical Club. Hao na wengine wengi wanaofanana na hao ndiyo waliokuwa wazungumzaji wa Mzee KK. Ilikuwa haipiti mwezi bila ya Mzee Kondo kwenda Kariakoo (na haswa klabu ya PAN) kwenda kupiga soga na watu wa mjini wenziwe.

Ukaribu wake na watu wa kawaida umefanya mpaka baadhi ya watu wafikirie kuwa Mzee Kondo hakusoma shule. Nakumbuka mwaka 1996 wakati Mzee Kondo akiwa Mwenyekiti wa Bandari nilikwenda Shirika la Bima ya Taifa (NIC) kufuatilia madai ya gari yangu MUSSO TZH 3336 ambayo ilipata ajali. Nilifika NIC na kuonana na Afisa mhusika wa madai. Katika mazungumzo yetu akabaini kuwa mimi ni Mkurugenzi wa Masoko wa THA. Alinipa pole sana kwa sababu kwa maneno yake mwenyewe, THA tumepata Mwenyekiti ambaye hajui kusoma. Alishangaa Mzee Kondo anawezaje kusoma makabrasha na kuongoza vikao vya Bodi ikiwa hata kuzungumza Kiingereza hawezi. Nikamjibu kuwa Mzee Kondo ni msomi kwani mwaka 1963 alihitimu shahada kwenye “Strategic Studies” kwenye Chuo Kikuu cha Howard Washington DC, Marekani. Aidha Mzee KK amepata mafunzo kwenye nchi kadhaa zikiwemo Ujerumani na Yugoslavia. Yule afisa hakuamini na tukawa na malumbano makali sana. Msingi wa hoja yake ni kuwa mzee KK anaandikwa vibaya sana kwenye gazeti (pamoja ya kuwa kwa sasa gazeti hilo limekufa lakini jina nalihifadhi) na picha inayojitokeza ni kuwa mzee huyu hakusoma kabisa.

Nimesema hapo awali kuwa Mzee Kondo alikuwa anajichanganya sana na watu wa aina na rika zote. Nina hakika si wengi wanaofahamu kuwa wakati wa uhai wake Mzee Kondo aliwahi kuwa Katibu wa klabu ya Yanga, Dar es Salaam miaka ya 1950s. Pia mwaka 1962 alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga. Wakati huo Mwenyekiti alikuwa Mzee Mohamed Sultan Mabosti, Katibu Mkuu ni Mzee Jabiri Katundu (alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Mzee Juma Vijiga) na Makamu wake Mzee Juma Shamte. Wote hao wameshatangulia isipokuwa Mzee Jabiri Katundu ambaye anaishi kwenye nyumba yake ile ile iliyopo Ilala mtaa wa Tabora. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Ampe Mzee Jabiri umri mrefu na wenye tija ili tuendelee kuvuna busara zake sio tu katika masuala ya mpira bali maisha kwa ujumla.

Kati ya mambo mengi sana ambayo nimejifunza kutoka kwa Mzee KK ni kuwa unapoitwa na mkubwa wako wa kazi iwe ofisini au nyumbani jiandae kwa kujua saa ya kuitwa na sio saa ya kuondoka. Katika hili alinisimulia kisa kimoja wakati akiwa Meya wa Dar es Salaam. Kuna Jumapili moja Mwalimu Nyerere aliwaita viongozi wa Mkoa (akiwemo Mzee KK) nyumbani kwake Msasani saa 4 asubuhi. Ujumbe huo uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa wakati huo. Walipofika Msasani wakakuta Mwalimu ameenda kanisani. Baada ya misa Mwalimu akaenda ofisini Ikulu. Ujumbe ulisubiri Msasani kwa muda mrefu. Ilipofika saa 7 mchana Mkuu wa Mkoa akatoa rai kuwa waondoke na kama kutakuwa na taarifa yoyote watafahamishana.

Mzee KK alirudi nyumbani kwake Hill Road Oyster Bay. Haikuchukua muda kapigiwa simu kuwa Mwalimu anamwita Msasani. Alipofika Msasani Mwalimu akataka kujua sababu zilizomfanya Mzee Kondo asiende nyumbani kwake saa 4 asubuhi kama alivyoagiza. Mzee Kondo akajitetea kuwa alikwenda saa 4 kama alivyoagiza na walisubiri hadi saa 7 ndipo kiongozi wa msafara wao Mkuu wa Mkoa akawaruhusu waondoke. Mwalimu akamwambia Mzee Kondo kuwa yeye aliwapa muda wa kufika Msasani saa 4 asubuhi lakini hakuwaambia muda wa kuondoka. Baada ya maneno hayo Mwalimu akamwambia kuwa ameshatengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa na kwamba yeye Mzee Kondo ana bahati kwani yeye ni diwani wa kuchaguliwa kwa hiyo hana namna ya kumfukuza kazi.

Mzee Kondo ameondoka na mambo mengi kifuani mwake. Alikuwa hazina kubwa sana kwa taifa. Mimi binafsi nimejaribu mara kadhaa kumwomba aandike historia yake lakini alikataa kabisa. Pamoja ya kuwa Mzee Kondo alinisikiliza na kukubali ushauri wangu kwenye mambo mengi, lakini hili la kuandika historia yake alikataa kabisa. Mara zote ninapokuwa namkumbusha kuhusu suala hili jibu lake lilikuwa “Bwana Dau, mie mzee, nataka nife huku nimenyooka”. Kwa bahati mbaya sana udhaifu huu wa kutoandika historia zao wanao viongozi wetu wengi. Wamebeba hazina kubwa na wakiondoka wanaondoka nazo bila kutuachia urithi huo adimu. Sisi wazee watarajiwa tusirudie makosa ya wazee wetu. Tujenge utamaduni wa kuandika ili watakaokuja baada ya sisi wanufaike na uzoefu wetu.

Yapo mengi sana ya kuandika kuhusu Mzee KK lakini nafasi hapa haitoshi. Kwa kumalizia, kwa wale wasiofahamu, Mzee KK alikuwa mpenda sana mashairi. Miongoni mwa mashairi yake aliyokuwa akiyapenda ni shairi la Muyaka bin Ghassany wa Mombasa. Alipoanza kuumwa kiasi miaka 3 iliyopita ilikuwa kila nikienda kumjulia hali huwa namsomea shairi la Muyaka. Pamoja na kutokuwa na fahamu lakini nikianza tu kumsomea shairi la Muyaka hufungua macho na kunitazama kisha akatokwa na machozi na baadae kufunga macho. Kwa kumuenzi Mzee Kitwana Kondo, nimeamua kulinukuu shairi ambalo wakati wa uhai wake, alikuwa analisoma ghibu:

Akutendeae Mema, Kushukuru ni lazima
Jaza ya mema ni mema, Maovu kutoyatia

Mbona umeghafilika? Kwa jambo lisilo shaka?
Shetani umemshika, Na kumuacha Nabia?

Unajifanya Mtesi, Kwa Mola wako Mkwasi
Unavitupa viasi, Sina la kukwambia

Silaha zote ni Zake, Wala na riziki Zake
Unakunywa maji Yake, Mbona umekosa haya?

Vita vyako fahamu, Havimdhuru Karimu
Ila wewe Bahaimu, Jijue Utaumia

Itunze yako fikara, Uwafikiri mabora
Wenye ngome na minara, Na panga za kuchinjia

Yatafakari mauti, Yeyote hayamuachi
Wala hayana wakati, Ghafla hukujilia

Yu wapi Firauni, Yu wapi Karuni
Na Shadadi maluuni, Wote wameangamia

Zao zilipokwisha, Ziraili kawafisha
Wameyawacha makasha, Na mambo haya na haya

Waimefika akhera, Madhalili mafukara
Uwapi wao bora, Wote umewakimbia

Kaburi zimewakaza, Hapana la kupumbaza
Kote kumefunga kiza, Adhabu kuwashukia

Adhabu hiyo ni kuu, Tena motoni kuwa juu
Majuto ni mjukuu, Tahadhari na dunia

Wapita na Siratini, Kuwangukia motoni
Kuteketea maini, Maisha kuteketea

Na yote ninayoyasema, Yatakufika lazima
Safari mbele na nyuma, Wengine hutangulia

KKdnBBYTMHRyxqu3UhZm-YHKuzK2zqnjuVm7rDvfvi2SaVwyBPjyEbMqoePiRVXclTzAue_uonCypXx7xCLF68KkyCF3lCJRqaA2z5xIO0nQvSgEkVMzj7OvxXAZ8QM3jUvHX5ra71zIBjNVbMBfgeGwZT_8QAIqn5DM9xZC3PTF4-hxxeRhydmDld8i0SqrvIP07LKF6lZeRL26M28Oa6UgFpGdzYL-7_oTIte3xUI9ZrAknERhLp26Toyj1FBjUOA6tTBej8aTL-BdyJ9O_KKcAFnBVtunuNEeB4JtfhlsYmOTC4uaNcaKr774ROaP76WQjXTUMcHc0g6thMVm2s3xOg5UjGz2zKggxQQkgRK1n7Sf1UC_TZr09sMabRoRXS1A3LVDXQEtWS4Ab3_orroOoMBIPlBJGExQD31us4fv-eC8VDMPU8TGXlniNe3G0PMStpO5FdtuI7CzPG66iOOWugJc1rpZE2PGJ4z2vL1z0fSfq_PkwG7rn4WXITIly5Cor5mm5cfDFrSmscOCwj8lUA3q0aoShzgbEIb237fa1ITIQ0fK7o52Ux7_jbH5jReL6bB1dRZZi-ST5yMTJescoMUtyTaPTgyWR5UrkX5Anbc30Q=s629-no

Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Dar es Salaam

Naam ni kweli kabisa safari ni mbele na nyuma wengine hutangulia. Mzee KK ametangulia. Kwa kuondokewa na Mzee Kitwana Selemani Kondo, Dar es Salaam imepwaya sana. Jiji limegubikwa na simanzi na ukiwa na hasa ukizingatia kuwa tokea mwaka huu uanze Dar es Salaam imeondokewa na Kamanda Dr. Mohamed Awadh (Chiko), Mzee Iddi Sungura, Mzee Issa Ausi (“Smart Boy”) na hivi karibuni Ali “Bob” wa Cosmopolitan. Maskini Dar es Salaam, imeondokewa na kubaki mkiwa.

Mwenyezi Mungu Amlipe mema na azipe uzito amali za Mzee Kitwana Kondo ziwe na mizani ya juu kuliko mapungufu yoyote ya kibinaadamu ambayo alikuwa nayo. In-ShaAllah Mwenyezi Mungu Amruzuku Pepo na In-ShaAllah Atukutanishe Peponi Firdaus, Ameen.

Taazia
 
Historia nzuri, Tafadhali mzee Mohamed Said Rekebisha kidogo kichwa cha habari maana hapo ulipo andika "na Dr.Dau inachanganya kana kwamba buriani ni kwa Kk na Dau.
 
BURIANI MZEE KITWANA SELEMANI KONDO (1930 - 2017) NA DK. RAMADHANI KITWANA DAU
Mohamed Said May 30, 2017 0

xl_ChymWwJcjEkio_7YiN5nRj6j94M9tN_gQxviw-JA2Bo13GUAIlfFTPz164IcB1OVJ2I0xEM__HYhf5a60c9BToID-A3VyZEdYPqYsD2EjMrU1rTkwVQJlTKo12aZB1dJLBOyQqkFw91J7a1DR9h3SAkBQ5jj7DDx8cwRkuNpw0XZUp3r54BBIEYP5Phnw-uhhM7p4WQkNKXx_r_6WFUhJwkA99iY6q7etJPfPdcNAh4ErIFS3uXik5Ie8bOBxujVUESN3CICzIKsFNA7VKw034TM_OyfhZ3GDlfUb_idvi71KLadK-1RwSIPAeM8kedeB-Kj_QHBz8g38hIlhR_xp4Jf-tRsTFLIy-TG6WkqK1cnmHXW1MMxaJaaAXOpbg4yH8I0xkiE5Auz4Fx4AiE0D6gBjLunrBsWwwFt2NR9NCNB7NtIsMS41dfO1AehWULsJMV6nm9qRTYt5WaCzfOCcgvt4Suhx8VygWP6BeXq0UWZUCR6x7mF92NGd3F_vN4OumU0D0sFr9NkcRR3ak3MzXiQLjfAunskQlXn8ulyBOfHN2Yqv9z3jLOQGdYy8vVUy3oX97zfD9TmEY1_XV5XkNzKBr3sD3yVdZGAu5YiaaRXoug=w625-h629-no

Kitwana Selemani Kondo katika ujana

BURIANI MZEE KITWANA KONDO

Ramadhani K Dau

Siku ya Jumatano tarehe 24 Mei 2017 ni siku ambayo itakumbukwa na Watanzania wengi na haswa Waislamu kwa kuondokewa na mzee wetu Alhaj Kitwana Selemani Kondo maarufu “KK” au mzee wa mjini. Siku 4 kabla ya kifo chake, mwanawe wa kiume Bwana Adnan-Msakuzi alinitumia ujumbe kwenye WhatsApp akiniarifu kuwa Mzee KK amelazwa Hindu Mandal na hali ya afya yake inazidi kuzorota. Siku ya pili yake nilimtumia ujumbe Adnan-Msakuzi kutaka kujua hali ya Mzee inaendeleaje. Majibu ya Adnan yaliniashiria kuwa mzee wetu amekaribia kufika mwisho wa safari yake hapa duniani. Aliniambia kuwa kwa sababu ya ukaribu wangu na Mzee KK hanabudi aniarifu ukweli ulivyo. Aliniarifu kuwa hali ya mzee ni mbaya sana na kwamba kinachosubiriwa na Rehma Zake Mwenyezi Mungu. Kwa kweli ujumbe ule ulinihuzunisha sana na sikuweza kuhimili uchungu ule peke yangu. Nikamwarifu Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo cha Waislamu Morogoro na Bwana Faraji Abdallah Tamim, mwalimu wa chuoni hapo.

Ilipofika siku ya Jumatano tarehe 24 Mei nikapata taarifa kupitia moja ya kundi sogozi (chat group) kuwa Mzee KK amefariki dunia. Pamoja ya kuwa hali hiyo ilikuwa tayari inatawala fikra zangu tokea siku niliyopata ujumbe kutoka kwa Adan lakini kifo hakizoeleki. Taarifa hiyo ilinikuta nikiwa najiandaa kwenda uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur kumsindikiza shemeji yangu. Wakati huo kwa saa za Malaysia ilikuwa kiasi cha saa 4 usiku. Nilipwelewa sana kwa sababu ya uhalisia kuwa sitowahi kumzika mzee wangu Mzee KK. Haikuchukua dakika 10 baada ya taarifa hizo, Adnan kanipigia simu ambayo hatukuweza kuzungumza hata neno moja kutokana na vilio vyetu. Kila mmoja alikuwa analilia kwake. Ghafla akakata simu na kunitumia ujumbe mfupi uliosema “KK is dead. Allah is Great”. Mara tu baada ya kupata taarifa hiyo nilichanganyikiwa na kuona uchungu sana baada ya kuona kuwa sitoweza kumzika Mzee KK ambaye aliwahi kunitamkia mbele ya mkewe Bi Hanifa kuwa ikitokea atafariki kabla mimi basi angependa asaliwe Masjid Mtoro, azikwe makaburi ya Tambaza na mimi niwe mmoja kati ya watu watakaoingia kaburini.

Katika maishani mwangu, hii ni mara ya tano kuandika taazia yaani “obituary”. Buriani zilizotangulia ni za aliyekuwa mwalimu wangu Chuo Kikuu DSM na rafiki yangu wa karibu Profesa Ken Edwards mwenye asili ya Jamaika, aliyekuwa Afisa wa Uhusiano wa NSSF Alfred Ngotezi, rafiki yangu tokea utotoni Abubakar Mohamed Saleh Tambaza maarufu “Babu Chela” na Saidi Masimango aliyekuwa Mkurugenzi wa Teknohama NSSF. Kila niandikapo taazia huwa nafanya hivyo nikiwa na moyo mzito na huzuni sana. Kila niandikapo huwa naomba kuwa hiyo iwe ndio ya mwisho kwani kuandika taazia ni jambo zito sana haswa ikiwa inamuhusu mtu wa karibu yako kama nilivyo mimi kwa Mzee KK na hao waliotangulia kabla yake.

Kwa huzuni niliyokuwa nayo niliamua kutoandika taazia hii kwa sababu nisingeweza kufikia mwisho kwa kilio. Lakini mara tu baada ya habari za msiba kuenea nikaanza kupata salaam toka kwa watu mbali mbali akiwemo Prof Hamza Njozi, mdogo wangu Abdul Dau na Adnan-Msakuzi. Ujumbe kutoka kwa Adnan ndio ulizidisha majonzi yangu lakini pia ulinipa nguvu ya kuandika kwani kama alivyosema Adnan na nakuu “Dr please write a eulogy for KK. You knew him well, no one can talk of him better than you”. Baada ya kutafakari nikaona kama sikuandika ntakuwa sikumtendea haki Mzee Kondo. Kwa kuwa nimekosa fursa ya kumtimizia wosia wake kuwa niwe miongoni mwa watu watakaoingia kaburini kumzika, nimeona nisikose vyote. Kwa kuzingatia kanuni ya fiqh kuwa kama jambo haliwezi kufanyika lote basi lisiachwe lote. Waswahili nao wana msemo wao “lisobudi hutendwa”. Hivyo basi nimeamua kuandika taazia hii kwa huzuni na unyonge mkubwa.

Mzee Kitwana Selemani Kondo alizaliwa Mtoni Kijichi, Dar es Salaam tarehe 1 Agosti 1930. Pale Mtoni Kijichi ukoo wake ni ulijulikana kwa jina la Mahembe. Wazazi wake wote wawili ni Wazaramo. Kiumeni kwake ni Mtoni Kijichi na kikeni kwake kijiji cha Gumba, Kisarawe. Alipata elimu ya msingi Mchikichini kisha akaenda Tabora Boys na baadae Chuo Kikuu cha Howard kilichopo Washington DC, Marekani. Pia Mzee Kondo alichukua masomo ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa darasa moja na marehemu Sheikh Mohamed Ali Al-Buhry.

Kwa upande wa kazi, Mzee Kondo alikuwa Polisi kwa muda mrefu hadi kufikia ngazi ya Inspekta na baadae akawa Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, marehemu Oscar Kambona. Wakati wa uhai wake Mzee KK ameongoza Taasisi kadhaa za Umma zikiwemo Shirika la Magari la Taifa yaani State Motors Corporation (Mkurugenzi Mkuu), Mwenyekiti wa Bodi za TANESCO, Mamlaka ya Bandari na Bodi ya Korosho. Wakati wa uhai wake, Mzee Kondo alijaaliwa kupata watoto 8. Kati ya hao wanaume 3 na wanawake 5.

Nimemfahamu Mzee tokea nikiwa mdogo kwa sababu ya kuzaliwa na kulelewa Mwembetogwa, jijini Dar es Salaam. Wakati wa utoto wangu sikuwa na ukaribu sana na Mzee Kondo kwa sababu ya tofauti ya umri. Ukaribu wangu kwake ulianza mwaka 1995 wakati alipoteuliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) ambapo mimi nilikuwa Mkurugenzi wa Masoko kwa miaka tisa. Nakumbuka siku moja mara tu baada ya kumaliza kikao cha Bodi niliamua kumsindikiza mpaka kwenye maegesho ya gari. Baada ya kufika kwenye gari yake, nikaona nichukue fursa hiyo nijitambulishe zaidi kwake kwani mpaka wakati huo alikuwa ananifahamu kama Mkurugenzi wa Masoko. Nikajitambulisha kuwa mimi nimezaliwa na nina asili ya Dar es Salaam.

Mara tu baada ya kumwambia hivyo haraka kabisa akaniuliza baba yangu nani. Ili kumtosheleza kiu chake sikutaka kumtambulisha baba yangu. Badala yake, na kwa makusudi kabisa nikamwambia mimi ni mtoto wa “John” Iddi. Mara tu nilivyojitambulisha akasema “wewe mwanangu, “John” Iddi alikuwa mkwe wangu”. Nilifanya makusudi kumtaja “John” Iddi ambaye ni baba yangu mkubwa. Jina lake halisi ni Thabit Iddi Dau. Jina la “John” aliitwa na mama yake baada ya kumzaa akiwa ana umri mkubwa sana. Baada ya kujifungua akasema mtoto huyu nimempata “Jioni” kwa maana ya kuwa amemzaa hali ya kuwa yeye ana umri mkubwa sana na alikwisha kata tamaa ya kupata mtoto. Pamoja ya kuwa jina lake halisi lilikuwa Thabit lakini tokea utotoni alijulikana kwa jina la “Jioni” ingawa kwa urahisi wa matamshi badala ya kusema “Jioni” likavuma jina la “John”. Marehemu Bwana Thabiti alijulikana sana kwa jina hilo la utani hadi kufa kwake.

Nimesema niliamua kujitambulisha kupitia baba yangu mkubwa kwa makusudi kwa sababu Mzee Kondo aliwahi kumuoa Bibi Kijakazi wa Mgoto ambaye alikuwa anafanyakazi Halmashauri ya Jiji (City Council). Kwa bahati mbaya hawakuwahi kupata mtoto. Katika ndoa yake nyingine, Bibi Kijakazi alijaaliwa mtoto wa kike ambaye jina lake ni Kurwa. Sasa huyu Bibi Kurwa ndiyo aliyekuwa mke wa kwanza wa marehemu Mzee “John” Iddi. Katika uhai wao walijaaliwa kupata watoto wawili. Iddi “John” na Mwatatu Thabit. Iddi alifariki mwaka 2001. Mwatatu yu hai ameolewa na Mohamed Mfaume maarufu “Difu” ambaye alikuwa golikipa wa Yanga, Cosmo na Timu ya Taifa. Mpaka sasa Mwatatu anaishi Kariakoo mtaa wa Swahili kwenye nyumba ya urithi wa mama yake.

Kinasaba, Mzee Kondo alikuwa anamwita Mzee “John” Iddi mkwe kwa sababu yeye (Mzee KK) alimuoa Bibi Kijakazi ambaye alikuwa mkwe wa Mzee “John” Iddi. Kwa upande mwingine, marehemu Mzee “John” Iddi (Thabit Iddi Dau) na marehemu baba yangu mzazi (Kitwana Ramadhani Dau) ni mtu na kaka yake. Wazungu wanasema ni first cousins, sisi Waswahili tunasema wamezaliwa nyumba kubwa na ndogo (kwa maana ya baba mkubwa na baba mdogo) au kwa lugha nyingine tunawaita watoto wa Simba kwa Simba. Kwa hiyo kinasaba, uhusiano wangu na Mzee Kondo ni kwa kupitia baba yangu mkubwa marehemu Mzee “John” Iddi Dau.
Tokea siku ile ambayo nilijitambulisha kwa Mzee Kondo, tukajenga ukaribu sana na alikuwa ananipenda sana. Ilikuwa haipiti wiki bila kwenda nyumbani kwake Hill Road Oyster Bay na baadae mtaa wa Mtitu Upanga kwenda kumwamkia na “kupata habari za mjini”. Ni kutokana na mazoea hayo ndipo Mzee KK akapata jina lingine la utani la “mzee wa mjini”. Na ni kweli, wakati wa uhai wake, kila utakapoenda nyumbani kwa Mzee KK hukosi kupata “habari za mjini” ingawa wakati mwingine zinakuwa ni habari au fikra zake yeye lakini ili kuzipa uzito atakwambia kuna habari mjini kuwa …(hapo anaeleza hiyo habari ilivyo). Moja katika hizo habari za mjini zilininufaisha sana na kuninusuru na janga kubwa sana ambalo lingenikuta. Leo hapa si mahala pake kuzungumzia habari hiyo. In Shaa Allah kuna siku ntaitafutia nafasi kuizungumza. Naendelea kumshukuru sana kwa hilo na mengine mengi ambayo amenifanyia mimi na watu wengine wengi.

Mzee KK atakumbukwa na kuliliwa na wengi kwani alikuwa mwepesi sana kusaidia watu wenye shida. Marehemu alikuwa mcheshi na mwenye kupenda maskhara sana. Alichanganyika na watu wa kila rika. Alikuwa mtu wa msaada sana kwa watu wa aina zote, wake kwa waume. Nyumbani kwake kulikuwa hawapungui wageni wa kila aina kuanzia wanasiasa, wana michezo, viongozi wa dini nk. Mmoja kati ya watu wengi waliosaidiwa na Mzee Kondo ni marehemu Profesa Idrisa Ali Mtulia. Wakati wa uhai wake, Profesa Mtulia alinisimulia namna ambavyo marehemu Mzee Kondo alivyomsaidia kwenda kusoma Uingereza. IIikuwa mwaka 1978 wakati Profesa Mtulia alipochaguliwa kwenda kusoma Clinical Fellowship kwa miaka miwili kwenye hospitali ya Hammersmith ambayo ni sehemu ya Chuo cha Imperial London, Uingereza. Gharama zote za masomo zilikuwa zilipwe na Serikali. Kwa bahati mbaya siku chache kabla ya safari, jina la Profesa Mtulia halikuwemo kwenye orodha. Profesa akawa hana la kufanya. Akaamua kwenda kuomba msaada kwa Mzee Kitwana Kondo. Mzee Kondo akamhakikishia kuwa ataenda kusoma mwaka ule ule na wala asiwe na hofu. Mzee Kondo akazungumza na Karimjee na baada ya siku 4 tu Profesa Mtulia akapata udhamini kamili (full scholarship), ambao ulijumuisha tiketi ya ndege na fedha zote za matumizi akiwa Chuoni. Udhamini huo ulitolewa na mama yake mzazi Karimjee. Kutokana na masomo hayo, Profesa Mtulia akatunukiwa kuwaMember of Royal College of Physicians (MRCP) na baada ya kudhihirisha umahiri wake akatunukiwa kuwa Fellow of Royal College of Physicians (FRCP). Profesa Mtulia alikuwa ni mmoja kati ya watu wengi waliosaidiwa na Mzee KK. Baada ya kurudi masomoni na baadaye kutunukiwa FRCP, Watanzania waliokuwa na hadhi hiyo walikuwa wachache sana; nadhani hawakufika 5. Mmoja kati ya hao alikuwa marehemu Dr. Aaron Chiduo; wengine nadhani ni Profesa William Makene na Profesa Shaba.
Kwa upande wa siasa Mzee Kondo ametoa mchango mkubwa sana kwa muda wote wa uhai wake nje na ndani ya Serikali, Bunge, TANU na CCM. Mzee KK alikuwa mzalendo ambaye aliitakia sana mema nchi yetu. Kwa wale wazee wa Dar es Salaam waliobaki watakumbuka sana mchango alioutoa tokea wakati wa Ukoloni na haswa baada ya Uhuru. Yapo mengi ya kihistoria aliyoyafanya kwa kuinusuru nchi yetu na kufika hapa ilipofika leo. Mambo mengine hapa si mahala pake.

Moja kati ya sifa zake nyingi ni ujasiri. Mzee KK hakuwa mwoga na alikuwa na ujasiri wa kusimamia jambo ambalo anaamini ni sahihi na lina manufaa kwa nchi yetu. Mifano iko mingi. Kwa leo itoshe tu kuwa alisimamia suala la upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro kwa kujenga hoja kwa Rais wa wakati huo Mhe Benjamin William Mkapa mpaka Mhe Rais akashawishika kuwa ni jambo jema kuanzishwa kwa chuo hicho kwenye majengo ya kilichokuwa Chuo cha Mafunzo cha TANESCO. Kama kuna mtu mmoja ambaye ametoa mchango wa kipekee uliopelekea upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) mtu huyo ni Mzee Kitwana Selemani Kondo. Kwa kuenzi jitihada zake hizo, na kwa kuzingatia Mzee Kondo ni Mwenyekiti mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF), Taasisi ambayo ndiyo Mmiliki wa MUM, nashauri uongozi wa Chuo ubadili jina la kampasi ya Morogoro iitwe Muslim University of Morogoro, Kitwana Kondo Campus. Natoa rai hiyo kwa kujua kuwa Chuo kina mpango wa kujenga kampasi nyingine Lindi (Kitunda), Kilwa (Mpara), Morogoro (Sangasanga) na Dar es Salaam (Kigamboni). Kwa siku za usoni, Chuo kitakapoanza kutoa Shahada za Uzamivu (PhD), nashauri Mzee Kitwana Kondo atunukiwe PhD (Honoris Causa) posthumously.

Kwa kawaida, Shahada ya Uzamivu ya Heshima, yaani PhD (Honoris Causa), ndiyo shahada ya juu zaidi katika Chuo Kikuu chochote. Shahada hii hutolewa kwa watu ambao wanaoheshimika sana na ambao wametoa mchango mkubwa katika jamii kwenye nyanja mbalimbali. Mchango wa Mzee Kondo katika nchi yetu hauna mithali. Aidha Mzee KK alikuwa mwepesi sana wa kuelewa vitu (sharp) na mtu wa mikakati sana. Hakuna alilofanya bila kufikiria nini kinachoweza kutokea usoni na ni namna gani anaweza kuikabili hiyo hali. Nimeyashuhudia hayo wakati akiongoza vikao vya Bodi ya Mamlaka ya Bandari na ushiriki wake katika vikao vya maandalizi ya kuazishwa kwa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Kwa wote ambao wamewahi kufanyakazi na Mzee Kondo, watakubaliana nami kuwa staha yake, weledi wake, busara zake na mchango wa katika taifa letu anastahili kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima, yaani PhD (Honoris Causa).
Wakati alipokuwa Meya wa Jiji, Mzee Kondo alithamini sana mchango wa watu mbalimbali walioshiriki katika harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika. Ili kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijao, Mzee Kondo aliwashawishi madiwani wenziwe kupitisha azimio la kubadili majina ya baadhi ya mitaa ya Dar es Salaam ili ipewe majina ya wazee wetu wa Dar es Salaam walioshiriki kwenye harakati hizo. Utaratibu uliotumika ni kuupa jina la mtaa kwa kila Mzee ambaye alieishi katika mtaa huo. Mifano ya mitaa iliyobadilishwa majina ni mtaa wa Kipata (Kleist Sykes), mtaa wa Tandamti (Mshume Kiyate), mtaa wa Aggrey (Makisi Mbwana), mtaa wa Somali (Omari Londo), mtaa wa Ndanda (John Rupia) na mtaa wa Mwananyamala (MwinyiJuma MwinyiKambi). Jambo la kusikitisha ni kuwa hadi leo baadhi ya mitaa hiyo haijawekwa vibao vya majina mapya. Ili kuendeleza dhamira nzuri ya kuwaenzi wazee wetu waliotoa mchango mkubwa katika nchi yetu naishauri Manispaa ya Ilala ibadili jina la mtaa wa Mtitu ambapo alikuwa anaishi marehemu Mzee Kondo na kuitwa mtaa wa Kitwana Kondo.

Sambamba na ujasiri, Mzee KK alikuwa anaipenda sana dini yake na alikuwa mtetezi mkubwa wa Waislamu. Ilikuwa kila ukienda nyumbani kwake ukimtajia Aya kwenye Quran basi haraka huchukua kitabu chake kidogo (note book) na kuiandika ili akaifanyie kazi kwa vitendo au hata kwa kuzungumza kwa wengine. Miongoni mwa Aya ambazo Mzee KK alikuwa akizipenda sana ni Aya ya 10 na ya 11 kwenye Sura ya 61 (As-Saff), pia Aya ya 31 kwenye Sura ya 76 (Al-Insan au kwa jina lingine Dahr). Kwa kumuenzi Mzee KK sitotoa tafsiri ya Aya hizo kwa makusudi ili msomaji upate ushawishi wa kwenda kuzisoma mwenyewe ili nawe upate fadhila za kuisoma Quran. Katika kuonesha mapenzi aliyonayo kwa dini yake, siku zote Mzee Kondo alikuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya Waislamu. Moja katika jitihada zake nyingi ni kupatikana kwa kiwanja ambacho kimejengwa Masjid Maamur, Upanga.

Mzee Kondo alijivunia sana Uswahili na Uzaramo wake. Watoto wake wengi aliwapa majina ya Kizaramo kama vile Mtogole, Azimala, Msakuzi nk. Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizokuwa nazo Serikalini, kamwe Mzee Kondo hakusahau marafiki zake ambao wengi wao walikuwa ni watu wa kipato cha chini sana. Baadhi yao ni marehemu Mzee Kibiriti, marehemu Mzee Sindano, marehemu Omar AbdulRahman maarufu “Ugundo”, Mzee Gulu, Captain Maliki, marehemu Ramadhani Mangilile, marehemu Ali Abbasi, na marehemu Mapepe. Wengine ni marehemu Hamisi George, marehemu Abbas Mzee, marehemu Saleh Mtumwa, marehemu Maalim Mbegu wote wa Egyptian Musical Club. Hao na wengine wengi wanaofanana na hao ndiyo waliokuwa wazungumzaji wa Mzee KK. Ilikuwa haipiti mwezi bila ya Mzee Kondo kwenda Kariakoo (na haswa klabu ya PAN) kwenda kupiga soga na watu wa mjini wenziwe.

Ukaribu wake na watu wa kawaida umefanya mpaka baadhi ya watu wafikirie kuwa Mzee Kondo hakusoma shule. Nakumbuka mwaka 1996 wakati Mzee Kondo akiwa Mwenyekiti wa Bandari nilikwenda Shirika la Bima ya Taifa (NIC) kufuatilia madai ya gari yangu MUSSO TZH 3336 ambayo ilipata ajali. Nilifika NIC na kuonana na Afisa mhusika wa madai. Katika mazungumzo yetu akabaini kuwa mimi ni Mkurugenzi wa Masoko wa THA. Alinipa pole sana kwa sababu kwa maneno yake mwenyewe, THA tumepata Mwenyekiti ambaye hajui kusoma. Alishangaa Mzee Kondo anawezaje kusoma makabrasha na kuongoza vikao vya Bodi ikiwa hata kuzungumza Kiingereza hawezi. Nikamjibu kuwa Mzee Kondo ni msomi kwani mwaka 1963 alihitimu shahada kwenye “Strategic Studies” kwenye Chuo Kikuu cha Howard Washington DC, Marekani. Aidha Mzee KK amepata mafunzo kwenye nchi kadhaa zikiwemo Ujerumani na Yugoslavia. Yule afisa hakuamini na tukawa na malumbano makali sana. Msingi wa hoja yake ni kuwa mzee KK anaandikwa vibaya sana kwenye gazeti (pamoja ya kuwa kwa sasa gazeti hilo limekufa lakini jina nalihifadhi) na picha inayojitokeza ni kuwa mzee huyu hakusoma kabisa.

Nimesema hapo awali kuwa Mzee Kondo alikuwa anajichanganya sana na watu wa aina na rika zote. Nina hakika si wengi wanaofahamu kuwa wakati wa uhai wake Mzee Kondo aliwahi kuwa Katibu wa klabu ya Yanga, Dar es Salaam miaka ya 1950s. Pia mwaka 1962 alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga. Wakati huo Mwenyekiti alikuwa Mzee Mohamed Sultan Mabosti, Katibu Mkuu ni Mzee Jabiri Katundu (alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Mzee Juma Vijiga) na Makamu wake Mzee Juma Shamte. Wote hao wameshatangulia isipokuwa Mzee Jabiri Katundu ambaye anaishi kwenye nyumba yake ile ile iliyopo Ilala mtaa wa Tabora. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Ampe Mzee Jabiri umri mrefu na wenye tija ili tuendelee kuvuna busara zake sio tu katika masuala ya mpira bali maisha kwa ujumla.

Kati ya mambo mengi sana ambayo nimejifunza kutoka kwa Mzee KK ni kuwa unapoitwa na mkubwa wako wa kazi iwe ofisini au nyumbani jiandae kwa kujua saa ya kuitwa na sio saa ya kuondoka. Katika hili alinisimulia kisa kimoja wakati akiwa Meya wa Dar es Salaam. Kuna Jumapili moja Mwalimu Nyerere aliwaita viongozi wa Mkoa (akiwemo Mzee KK) nyumbani kwake Msasani saa 4 asubuhi. Ujumbe huo uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa wakati huo. Walipofika Msasani wakakuta Mwalimu ameenda kanisani. Baada ya misa Mwalimu akaenda ofisini Ikulu. Ujumbe ulisubiri Msasani kwa muda mrefu. Ilipofika saa 7 mchana Mkuu wa Mkoa akatoa rai kuwa waondoke na kama kutakuwa na taarifa yoyote watafahamishana. Mzee KK alirudi nyumbani kwake Hill Road Oyster Bay. Haikuchukua muda kapigiwa simu kuwa Mwalimu anamwita Msasani. Alipofika Msasani Mwalimu akataka kujua sababu zilizomfanya Mzee Kondo asiende nyumbani kwake saa 4 asubuhi kama alivyoagiza. Mzee Kondo akajitetea kuwa alikwenda saa 4 kama alivyoagiza na walisubiri hadi saa 7 ndipo kiongozi wa msafara wao Mkuu wa Mkoa akawaruhusu waondoke. Mwalimu akamwambia Mzee Kondo kuwa yeye aliwapa muda wa kufika Msasani saa 4 asubuhi lakini hakuwaambia muda wa kuondoka. Baada ya maneno hayo Mwalimu akamwambia kuwa ameshatengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa na kwamba yeye Mzee Kondo ana bahati kwani yeye ni diwani wa kuchaguliwa kwa hiyo hana namna ya kumfukuza kazi.

Mzee Kondo ameondoka na mambo mengi kifuani mwake. Alikuwa hazina kubwa sana kwa taifa. Mimi binafsi nimejaribu mara kadhaa kumwomba aandike historia yake lakini alikataa kabisa. Pamoja ya kuwa Mzee Kondo alinisikiliza na kukubali ushauri wangu kwenye mambo mengi, lakini hili la kuandika historia yake alikataa kabisa. Mara zote ninapokuwa namkumbusha kuhusu suala hili jibu lake lilikuwa “Bwana Dau, mie mzee, nataka nife huku nimenyooka”. Kwa bahati mbaya sana udhaifu huu wa kutoandika historia zao wanao viongozi wetu wengi. Wamebeba hazina kubwa na wakiondoka wanaondoka nazo bila kutuachia urithi huo adimu. Sisi wazee watarajiwa tusirudie makosa ya wazee wetu. Tujenge utamaduni wa kuandika ili watakaokuja baada ya sisi wanufaike na uzoefu wetu.

Yapo mengi sana ya kuandika kuhusu Mzee KK lakini nafasi hapa haitoshi. Kwa kumalizia, kwa wale wasiofahamu, Mzee KK alikuwa mpenda sana mashairi. Miongoni mwa mashairi yake aliyokuwa akiyapenda ni shairi la Muyaka bin Ghassany wa Mombasa. Alipoanza kuumwa kiasi miaka 3 iliyopita ilikuwa kila nikienda kumjulia hali huwa namsomea shairi la Muyaka. Pamoja na kutokuwa na fahamu lakini nikianza tu kumsomea shairi la Muyaka hufungua macho na kunitazama kisha akatokwa na machozi na baadae kufunga macho. Kwa kumuenzi Mzee Kitwana Kondo, nimeamua kulinukuu shairi ambalo wakati wa uhai wake, alikuwa analisoma ghibu:

Akutendeae Mema, Kushukuru ni lazima
Jaza ya mema ni mema, Maovu kutoyatia

Mbona umeghafilika? Kwa jambo lisilo shaka?
Shetani umemshika, Na kumuacha Nabia?

Unajifanya Mtesi, Kwa Mola wako Mkwasi
Unavitupa viasi, Sina la kukwambia

Silaha zote ni Zake, Wala na riziki Zake
Unakunywa maji Yake, Mbona umekosa haya?

Vita vyako fahamu, Havimdhuru Karimu
Ila wewe Bahaimu, Jijue Utaumia

Itunze yako fikara, Uwafikiri mabora
Wenye ngome na minara, Na panga za kuchinjia

Yatafakari mauti, Yeyote hayamuachi
Wala hayana wakati, Ghafla hukujilia

Yu wapi Firauni, Yu wapi Karuni
Na Shadadi maluuni, Wote wameangamia

Zao zilipokwisha, Ziraili kawafisha
Wameyawacha makasha, Na mambo haya na haya

Waimefika akhera, Madhalili mafukara
Uwapi wao bora, Wote umewakimbia

Kaburi zimewakaza, Hapana la kupumbaza
Kote kumefunga kiza, Adhabu kuwashukia

Adhabu hiyo ni kuu, Tena motoni kuwa juu
Majuto ni mjukuu, Tahadhari na dunia

Wapita na Siratini, Kuwangukia motoni
Kuteketea maini, Maisha kuteketea

Na yote ninayoyasema, Yatakufika lazima
Safari mbele na nyuma, Wengine hutangulia

KKdnBBYTMHRyxqu3UhZm-YHKuzK2zqnjuVm7rDvfvi2SaVwyBPjyEbMqoePiRVXclTzAue_uonCypXx7xCLF68KkyCF3lCJRqaA2z5xIO0nQvSgEkVMzj7OvxXAZ8QM3jUvHX5ra71zIBjNVbMBfgeGwZT_8QAIqn5DM9xZC3PTF4-hxxeRhydmDld8i0SqrvIP07LKF6lZeRL26M28Oa6UgFpGdzYL-7_oTIte3xUI9ZrAknERhLp26Toyj1FBjUOA6tTBej8aTL-BdyJ9O_KKcAFnBVtunuNEeB4JtfhlsYmOTC4uaNcaKr774ROaP76WQjXTUMcHc0g6thMVm2s3xOg5UjGz2zKggxQQkgRK1n7Sf1UC_TZr09sMabRoRXS1A3LVDXQEtWS4Ab3_orroOoMBIPlBJGExQD31us4fv-eC8VDMPU8TGXlniNe3G0PMStpO5FdtuI7CzPG66iOOWugJc1rpZE2PGJ4z2vL1z0fSfq_PkwG7rn4WXITIly5Cor5mm5cfDFrSmscOCwj8lUA3q0aoShzgbEIb237fa1ITIQ0fK7o52Ux7_jbH5jReL6bB1dRZZi-ST5yMTJescoMUtyTaPTgyWR5UrkX5Anbc30Q=s629-no

Kitwana Kondo alipokuwa Meya wa Dar es Salaam

Naam ni kweli kabisa safari ni mbele na nyuma wengine hutangulia. Mzee KK ametangulia. Kwa kuondokewa na Mzee Kitwana Selemani Kondo, Dar es Salaam imepwaya sana. Jiji limegubikwa na simanzi na ukiwa na hasa ukizingatia kuwa tokea mwaka huu uanze Dar es Salaam imeondokewa na Kamanda Dr. Mohamed Awadh (Chiko), Mzee Iddi Sungura, Mzee Issa Ausi (“Smart Boy”) na hivi karibuni Ali “Bob” wa Cosmopolitan. Maskini Dar es Salaam, imeondokewa na kubaki mkiwa.

Mwenyezi Mungu Amlipe mema na azipe uzito amali za Mzee Kitwana Kondo ziwe na mizani ya juu kuliko mapungufu yoyote ya kibinaadamu ambayo alikuwa nayo. In-ShaAllah Mwenyezi Mungu Amruzuku Pepo na In-ShaAllah Atukutanishe Peponi Firdaus, Ameen.

Taazia
Mzee Said asante kwa hii tanzia nzuri ya mzee wetu KK. Pamoja na mapungufu yake alikuwa mtu muhimu katika historia ya nchi yetu.

Nina ombi moja kwako yupo mtu mmoja alikuwa akiitwa Bayume Mohamed Husen mwenyeji wa Dar es Salaam ambaye alilowea Ujerumani miaka ya 1920s na kukutana na mkasa wa kuangamizwa na askari wa Nazi katika moja ya kambi zao. Unaweza kutuletea historia yake kama umewahi kumsikia na kama yeye au wazazi wake walikuwa na interaction yoyote na wazee wa DSM wa enzi zake?

Bayume Mohamed Husen - Wikipedia
 
Historia nzuri, Tafadhali mzee Mohamed Said Rekebisha kidogo kichwa cha habari maana hapo ulipo andika "na Dr.Dau inachanganya kana kwamba buriani ni kwa Kk na Dau.
Madotto katika uandishi "na," ina maana imeandikwa na...
 
Mzee Said asante kwa hii tanzua nzuri ya mzee KK. Pamoja na mapungufu yake alikuwa mtu muhimu katika historia ya nchi yetu.

Nina ombi moja kwako yupo mtu mmoja alikuwa akiitwa Bayume Mohamed Husen mwenyeji wa Dar es Salaam ambaye alilowea Ujerumani miaka ya 1920s na kukutana na mkasa wa kuangamizwa na askari wa Nazi katika moja ya kambi zao. Unaweza kutuletea historia yake kama umewahi kumsikia na kama yeye au wazazi wake walikuwa na intaraction yoyote na wazee wa DSM wa enzi zake?

Bayume Mohamed Husen - Wikipedia
Kinyungu,
Hii ndiyo mara yangu ya kwanza kumsikia Bayume Mohamed Husen.

Sijapatapo hata kusikia jina hili la Bayume kwa watu wa Dar es Salaam
ingawa lipo Bayumi na ni familia maarufu Moshi na Arusha.
 
Kinyungu,
Hii ndiyo mara yangu ya kwanza kumsikia Bayume Mohamed Husen.

Sijapatapo hata kusikia jina hili la Bayume kwa watu wa Dar es Salaam
ingawa lipo Bayumi na ni familia maarufu Moshi na Arusha.
Shukran Mzee Said. Ngoja niendelee na kautafiki kangu kuhusu huyu Bwana maana historia yake kwa kweli inasisimua sana.
 
Ina lilah waina ilaihi rajiun.
Mzee wetu huyu alikuwa mmoja ya alama ya ustaarab wa watu wa pwani.
Nakumbuka aliandamwa sana sana na watu mbali mbali ikiwamo wa chama chake...alitukanwa na kupewa majina...lakini Mzee Kondo hakuwahi kujibu wala kununa siku zote alikua akionesha bashasha tu ya furaha....hakujibu na walomdharau kuwa ni mswahili hakusoma...akawaacha tu hivyo hivyo na ujinga wao.
Hii Tazia ya leo ndo inatujulisha kuwa ni msomi sawa sawa
Kuna kisa kimoja nili hadithiwa ingawa sina uthabit wake ni kuwa Mzee Kondo alikua constable wa police kabla uhuru...na kuna wakati Mwalimu alitiwa ndani ...ni Mzee Kondo ndie alo hakikisha Mwalimu yupo hali nzuri na kupata chakula huko rumande..
Labda Sheikh Mohamed Said atakuwa analijua hili..
 
Bopwe,
Hapana sina hakika na hicho kisa.

Ila nijuacho ni kuwa wakati Mwalimu Nyerere alipofika Dar es Salaam
1952 na kujiunga na kundi la kina Abdul Sykes katika siasa, Kitwana
Kondo
alikuwa Special Branch hivyo hakuwa tena katika uniform ya
Polisi.

Mtu mwingine aliyekuwa Special Branch na aliwataabisha sana viongozi
wa TAA kisha TANU kati ya 1950 hadi miaka michache kabla ya uhuru ni
Amiri Kweyamba.

Ali Sykes alinipa stori nyingi sana kati yake yeye na kachero huyu.
 
hii MUSSO naikumbuka nilikuwa naiona ikija kwa Mzee Masoud Mapande pale Temeke
 
Back
Top Bottom