In Edward Lowassa, I trust...

Mkuu! Ngoja atoe tamko lake Bungeni kuhusu Richmond kama nilivyosikia kwenye vyombo vya habari then from there nitapanda mtumbwi wako,......

Kwenye hili la Richmond, mmesahau kuwa alimfuata Rais alipogundua kosa na kutaka mkataba usitishwe na kufutwa na ni Rais aliyekataa ushauri wa Lowassa kwa kisingizio eti tutapelekwa mahakama ya dunia ya biashara bila hata kuwasiliana na Wanasheria kujua tukivunja mkataba tungepata hasara gani?
 
Of course. But, seriously,the guy was making everyone busy. He was not sleeping.

Companero,

Unakumbuka wale wakuu wa mikoa au wilaya ambao walianza kutoa utumbo akawapiga stop mbele ya hadhara na kwaambia waache kubabaisha?

Pitia safu za viongozi wote Tanzania utakuwa baada ya Nyerere na Sokoine, next aliyekuwa na ubavu wa kupiga ngwala blah blah za Watendaji ni Lowassa
 
Of course. But, seriously,the guy was making everyone busy. He was not sleeping.

Oooh well kama mnamtaka huyo sawa. Hilo ni shauri lenu. Mnaanza kunikumbusha 2005. Nilipinga uteuzi wa Kikwete na nilijikuta niko peke yangu. Na hapa naona itakuwa deja vu all over again..
 
Yaani Tanzania nzima hakuna mtu mchapakazi hadi Jambazi Fisadi Edward Lowassa aonekane ndie anaefaa, huyu mtu hafai kabisa kwenye uongozi na sehemu pekee anayostahili kuwepo hivi sasa ni jela.
 
Sure, he was busy thinking of making another Richmond....mvua ya kutengeneza,.....be President 2015 etc etc

So was Mkapa with Kiwira, Kikwete with Barrick and Richmond and so will be Membe with National ID and Mbowe with Billicanas!

Lets not forget Lipumba with Utajirisho and Mrema with Seven days!
 
Yaani Tanzania nzima hakuna mtu mchapakazi hadi Jambazi Fisadi Edward Lowassa aonekane ndie anaefaa, huyu mtu hafai kabisa kwenye uongozi na sehemu pekee anayostahili kuwepo hivi sasa ni jela.

Where is the proof kuwa Kaiba au Kahujumu?
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!
Unasahau makusudi sifa zake nyingine
-anahusika na RICHMOND
-aliwahi kupora kiwanja cha kanisa Mbezi Beach
-sakata la utajiri wake usioelezeka
-suala la jengo la UVCCM nalo je?

Nivyema kama unampenda ukanywe naye chai!!
 
Rev.mi niko pamoja nawe..he was good and alikuwa anajua kuchapa kazi.Yaani ni afadhali ya Lowassa kuliko Pinda anayefanya maigizo kila siku mara msivae suti mara magari haya ya kifahari...kizunguzungu tupu..Lowassa was a man of action and result oriented...
 
Where is the proof kuwa Kaiba au Kahujumu?
Naomba pia proof kuwa hajaiba au kuhujumu uchumi pale Tanzania. Inabidi atuonyeshe utajiri wake na kwa familia yake umetokea wapi na kwa kipato gani? Atuonyeshe vyanzo vyake vyote vya mapato vilivyomfanya awe tajiri na kuweza kuwekeza hisa katika makampuni mbalimbali huku akimiliki biashara na majumba mbalimbali kutoka Dar mpaka Arusha.
 
Companero,

Unakumbuka wale wakuu wa mikoa au wilaya ambao walianza kutoa utumbo akawapiga stop mbele ya hadhara na kwaambia waache kubabaisha?

Pitia safu za viongozi wote Tanzania utakuwa baada ya Nyerere na Sokoine, next aliyekuwa na ubavu wa kupiga ngwala blah blah za Watendaji ni Lowassa

Pia alivunja mkataba wa DARCITY WATER bila kuogopa eti wawekezaji watafungua kesi !!. Sasa hivi kuna mikataba kibao inaendeshwa kinyume na mikataba inavyotaka, lakini hakuna jasiri anayesimama kufuta mikataba hiyo, kisa JK anaogopa kesi, EL siyo muoga hivyo, love him or hate him, the guy got balls !! which is what this country needs, strong leadership.
 
Bravo Rev.
Mtu huyu ni muhimu sana hasa kipindi hiki cha Swine Flu, ukizingatia uongozi uliopo umeshindwa hata kuzuia vyombo vya usafiri kutoka manyara kwenda mikoa mbali mbali ndani ya Tanzania? Mkoa wenyewe unachukua blood sample zitumwe dar ndio wahudumie wagonjwa? siku 3 - 5 baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa?
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Jamaa ana uwezo mkubwa wa crissis management.
Eg. Alivyo weza kupeleka sekondari kidato cha kwanza wanafunzi wengi mwaka 2006?
 
Naomba pia proof kuwa hajaiba au kuhujumu uchumi pale Tanzania. Inabidi atuonyeshe utajiri wake na kwa familia yake umetokea wapi na kwa kipato gani? Atuonyeshe vyanzo vyake vyote vya mapato vilivyomfanya awe tajiri na kuweza kuwekeza hisa katika makampuni mbalimbali huku akimiliki biashara na majumba mbalimbali kutoka Dar mpaka Arusha.

GQ,

Burden of proof iko wako maana wewe ndiye unadai eti yeye ni Jambazi, Fisadi ana majumba mengi na mali nyingi. Tuletee basi hivyo vyeti vya umiliki vya mali unazodai ni za Lowassa ndipo defense counsel wawasilishe majibu :)
 
Unasahau makusudi sifa zake nyingine
-anahusika na RICHMOND
-aliwahi kupora kiwanja cha kanisa Mbezi Beach
-sakata la utajiri wake usioelezeka
-suala la jengo la UVCCM nalo je?

Nivyema kama unampenda ukanywe naye chai!!

RICHMOND report does not implicate him directly!this is my understanding na kama anahusika why serikali haimfikishi mahakamani?the problem is not him ni weekness ya serikali yenu ya kuungaunga hii

Kama alipora kiwanja cha kanisa Mbezi ,mbona mkapa na sumaye kapora mahekta ya ardhi kibaigwa hamsemi.

Utajiri wake wewe ndo huuelewi na huuelewi kwa kuwa wewe ni masikini so utaendelea kutoelewa kwa kuwa wewe si miongoni mwa matajiri

Suala la jengo la vijana CCM akongelee huko CCM sio hapa ndo maana wenyewe waliona hana kosa na mpaka leo ujenzi unaendelea..na aliyeleta kidomodomo juu ya jengo hilo Nnape kilichompata umekiona.

mengine ni chuki binafsi na umasikini ndo unawasumbua walio wengi...
 
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!

Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.

Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.

Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!

Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!

Rev. unamtaka Lowassa katika nafasi gani?
 
Swali kwenu, je yeye Lowassa ni fanisi au si fanisi?

Je ni mchapa kazi au mbangaizaji?

Je ni mfuatiliaji au ni selule?

Je ni mfanya maamuzi bila kuogopa sura au mtu au ni mwoga akiogopa political fall out?

Kama ni tamaa za mali, au ufisadi, ni Mtanzania gani ambey si mwenye tamaa ya mali au fisadi?

Mhhh!! aisee TIME never lies...
 
Kweli Tanzania ndio maana bado Masikini ikiwa hadi baadhi ya members wa Home Of Great Thinkers wanashindwa kung'amua ni nani asiefaa kwenye uongozi Tanzania, hivi mnategemea mtu wa kijijini ambaye si msomi na wala hana muda wa kufuatilia maadili ya viongozi mbalimbali achague mtu anaefaa. Kweli nchi yetu imeishiwa. Ukweli ni kwamba Edward Lowassa ni mmoja wa Jambazi na Fisadi Mkuu Nchini Tanzania. Hafai kwenye Uongozi si uraiani pekee bali hata huko jela hafai kupewa hata Unyapara.
 
Back
Top Bottom