In Edward Lowassa, I trust...

 

- Bob hebu soma vizuri sana haya maneno kuhusu Lowassa, na aliyeyaandika ambaye sasa anadai Lowassa anafaa na sio mwizi maana hakuna ushaidi JF sometimes labda kuna spirits zinaiba Code zetu I mean no way tukawa tunageuka geuka rangi namna hii! phew!

- siku moja Lowassa ni Yuda, next day ni a hero na hakuna ushahidi tunachekesha sana sometimes!

Respect.

FMEs!
 

- Kama kushauri kwamba Lowassa ni kiongozi bora ndio kuwa the best political strategist katika Tanzania ya leo, basi mkuu keep it siuhitaji, uongozi wa Lowassa hauwezi kua kwa faida yangu labda yako wewe, simuhitaji kuniongoza mahali popote pale kwa sababu ni kiongozi mwizi na ushahidi upo tena wa wazi sana ndio maana akakimbia uongozi bila kufukuzwa, kuandika andika kila mahali JF haina maana kwamba ndio unakuwa the best strategist hasa na hizi context za ubora wa Lowassa, ni mufilisi tupu.

- Siasa ni mchezo mchafu haina maana kuongozwa na viongozi wezi, huku ukishangilia kwamba eti siasa ni mchezo mchafu, watu wenye akili nyingi wanapoongelea uchafu wa siasa, hawana maana kwamba fisadi kama Lowassa kurudishwa kwenye uongozi, hilo ni tatizo la utawala usioheshimu sheria kama wa kwetu, wanaposema siasa ni mchezo mchafu wana maana kama vile Mama Clinton alivyopambana na Obama kwenye uchaguzi na leo ni waziri wake, hawaongelei viongozi wezi kama Lowassa, ambaye hata Mwalimu alimsema wazi kwamba ni mwizi, leo wewe etu unashauri arudishwe tena kwenye uongozi, na kwamba eti ni kwa sababu siasa ni mchezo mchafu na kwamba wewe ni the best strategist hapa JF kwa kuwa na mawazo haya, it is absurd!

- Lowassa belongs to jail sio kwenye uongozi, inasikitisha sana kuwa hata na this kind of thinking kwa kisingizio cha siasa mchezo mchafu, kwa sababu it does not apply na hizi theory zako not even close.

Respect.

FMEs!
 
The only Edward I trust is Edward Moringe Sokoine
 
Ninachojua ni kwamba nikiletewa Lowassa na kikwete nichague na hakuna choice nyingine walai nampa Lowassa kuliko huyu ndugu yetu
 
Mbona me sikuhizi nashindwa kuelewa? Habari za kumpongeza EL zinashamiri kila kona na kila siku mambo haya yanazidi...JAMANI HUYU JAMAA..........SANA HATUFAI KWA KWELI...he should be charged to the crt of law
 
FMES,

Naomba usome tena nilichoandika. Tea soma vizuri sana na tumia zile hekima na busara zako za Ki-Sauti ya Umeme!

Kama bado hujanielewa, nipigie simu nikueleweshe!
 

Reverand unasema ili tuendelee tunamuhitaji Lowassa,at the same time unakiri kwamba ufisadi ni kikwazo cha maendeleo,kwa maana kwamba umemsafisha Lowassa maana maneno "I trust in" ni mazito. Pengine una insight zaidi,kama unakubaliana kuwa ufisadi ni kikwazo cha maendeleo then kumchagua kiongozi fisadi mchapa kazi ni sawa na ile wanaita maktaimu....Narudia mkuu inawezekana una insight nzuri zaidi kuhusiana na kashfa za Richmond nk. Binafsi ikigundulika kuwa Lowassa hakuwa na makosa ya ufisadi kwenye kashfa hizo basi nitakuunga mkono.
 

Mushi,

Umeshawahi jiuliza kwa nini Lowassa hajafikishwa mahakamani kwa uzembe wa Richmond au kupewa karipio na Kamati Kuu au NEC ya CCM?
 
FMES,
Mkuu wangu la Udini wala sidhani utapenda kwenda huko kwa sababu wanijua vizuri sana na nakufahamu vizuri sana. Kati yetu mimi na wewe huwezi kamwe kuniita mimi mdini wakati unafahamu fika wewe ni Mlokole na mimi napiga mai kama jana. Dini ni ELIMU tu kwangu ambayo inaniongoza mimi ktk maisha yangu..Naitumia Dini kama navyotumia masomo mengine ktk kuendesha maisha yangu na sii kuabudu maandishi kama mnavyofanya kina nyie.. Najua jina unaloitumia unapokuwa huko kwenye mijadala ya dini... mkuu sidhani kama unataka kwenda huko ambako nilikwisha mwambia usinivae kabisa ktk maswala hayo ya dini..

Pili, unayoandika hapo juu kuhusu CCM haihusu kabisa.. CCM sio chama changu ati kwa sababu kinaniongoza kwa miaka 45.. Hizi fikra ni finyu mkuu wangu, na ndio maana huwezi kuelewa na haswa mimi.
Labda niweke lugha safi na nyepesi kwako.. Kutawaliwa na CCM ni sawa na kutawaliwa na mkoloni sasa nambie unapotawaliwa na mkoloni basi nawe unabadilika kuwa mkoloni kwa sababu tu ya hesabu ya miaka ulotawaliwa!.. Utaweza vipi kuwa mwana mapinduzi au Mpiganaji ikiwa wewe mwenyewe umeshakubali kutawaliwa..Hayo ni mawazo ya kina Raila na Morgan ambao wapo tayari kusalimu amri kuungana na shetani. Sii mimi na ndio maana siwezi kuitetea CCM hata siku moja wala kutenganisha matendoi ya viongozi wake na chama...Injini ya gario lenu CCM ni viongozi wake haiwezekani injini ya gari kuwa mbovu ukasema gari zima isipokuwa injini ndio mbaya.. Hiyo ni lugha muflisi..Binafsi CCM ni watu, CCM ni Uongozi wake kama ulivyokuwa Ukoloni..
 
FMES,

Watu tuliacha kuwa wanachama na wafuasi wa CCM vlipokuja vyama vingi miaka 18 iliyopita. Aliyebakia king'ang'anizi kuwa CCM ndio jibu ni wewe peke yako!

Sasa kwa hili la CCM si wewe uliyedai miezi miwili iliyopita kuwa wapiganaji 11 hawana ubavu kushindana na mafisadi 5000 ndani ya CCM au nawe ulikuwa umeingiwa pepo na mtu kukuibia password yako ulipotoa kauli hiyo?

Then acheni majority y CCM ishike hatamu na Lowassa si ndio kiongozi wao, la sivyo tunadanganyana kuwa CCM itafanikiwa kuondoa Ufisadi!

Labda nikuulize, ni nani vile alimtetea na kusababisha kurudishwa Lowassa kwenye uongozi baada ya lile kata funua la Nyerere 1995?

 

jaji
kulikoni tena??
tatizo la tz ni tatizo la kitanzania ,tatizo kubwa mime nilionalo ni kujaribu kutumia ccm kama steping stone ya ku escape utanzania wetu.

ccm has nothing to do na ujinga wetu,but ujinga wetu has something to do with ccm.

Kikwete hoyeeeeee, ccm hoyeeeeeee
 
Mchungaji,hatimaye nimekuelewa sasa! Tatizo lugha uliotumia imekuwa ngumu kueleweka na wengi waliochangia tangu mwanz😵mbi langu,siku nyingine tumia lugha nyepesi kidogo,vinginevyo utafanya watu wazimie bure lol!
 
Mushi,

Umeshawahi jiuliza kwa nini Lowassa hajafikishwa mahakamani kwa uzembe wa Richmond au kupewa karipio na Kamati Kuu au NEC ya CCM?

Mkuu umesema three quaters ya CCM wanamsikiliza Lowassa ama wana imani naye,na kwamba ni mtu mwenye kufanya kazi kwa bidii,asiyetaka mchezo,hata hivyo alishindwa kusimamia ukweli,na bila kuwa mkweli sifa nyinginezo hazina uzito kwani trust haitakuwepo. Ikasemekana alijiuluzulu ili kukinusuru chama,kama ni kweli utendaji wake haukuwa na mashaka sidhani kama angejiuzulu given sifa zote hizi anazomwagiwa....Kwamba ni kiongozi jasiri,sasa kujiuzulu na kushindwa kusimamia ukweli ni sawa na usaliti kwa wananchi amabao ndio anaowatumikia.Anaposema anakinusuru chama in leu of National interests and security,then sifa nyingine zote zinakuwa hazina maana kwasababu impact ya ufisadi ni kubwa mno,umetembelea bongo umekumbushwa reality,na ndio maisha ya kawaida,kama EL atashindwa kuwa mfano basi hata awe mkali kiasi gani na ufuatiliaji wa aina gani kama wananchi hawatakuwa na imani naye maendeleo yatabakia kuwa hadithi.

Najuwa EL hajafikishwa mahakamani,lakini bado nina haki ya kujuwa what went down,yani ukweli wote kabla sijachukuwa uamuzi wa kusema i trust in him....Sitaki kuingia mtegoni na kucheza kwenye tope....Walichunguzana wenyewe na wote wanajuwa ukweli ila wanatoa habari nusu nusu kila mtu akitoa zile zitakazoonyesha kuwa yeye ndio mkweli na huku wakitumia sababu mbali mbali za wao kutozitoa habari zote,sitoingia mtegoni na kufanya maamuzi kutokana na kauli za kisiasa....Siyo kweli kwamba kwasababu hakufikishwa mahakamani basi hakuhusika,maybe kisiasa...Lakini kwakuwa hakujiuzulu bure,then tunataka tujue ukweli....Hawezi tu kujiuzulu aseme ni kwa kukinusuru chama then na sisi tu conclude kuwa ni mkweli na safi. Pia sikubali kuwa solution ni kuwapa mafisadi nchi....Ni sawa na kumpa shetani mamlaka yote kwasababu malaika wa bwana wameshindwa kazi yao na hivyo kutegemea kuwa shetani atazifanya kazi za malaika hao wa bwana,kwa niaba yao...Mkuu binafsi naamini kuwa maendeleo na ufisadi ni kama mwanga na giza,haviwezi ku coexist,lazima kimoja kitake over,pia kumbuka ufisadi kwa nchi zinazoendelea na zilizoendelea una impact za tofauti na hivyo kutegemea kuwa mafisadi wataleta maendeleo ni ndot ya mchana unless uni convince otherwise.
 
- CCM itaendelea kututawala mpaka siku moja tutakapoamuka usingizini na kuanza ku-think right, otherwise tutaendelea kurushiana maneno yasiyo na faida which is good for CCM anyways,

- Mchungaji siku moja unasema Lowassa ni yuda, halafu siku nyingine unasema In Lowassa you trust, na maneno mengi ambayo hayana faida yoyote kwa masilahi ya taifa zaidi tu ya kujenga chuki katika jamii, taifa letu lina matatizo ambayo wote tumeshindwa kuyatafutia majibu ni tatizo letu wote wananchi wa Tanzania, hakuna alie juu au bora kuliko au mwenye akili kuliko, wote tumekwama, ndio maana ninawaheshimu sana wapiganaji maana angalau wanafanya kwa vitendo.

- Bob, kama unataka kujadili hoja ya IN Edward I Trust, ninakukaribisha anytime, hayo mengine sina time maana hayana faida yoyote kwa taifa.

Kwa kumaliza ni either Lowassa ni Yuda Iskariote, au ni the best ever chagua moja mkuu!, na muwe mnafikiri kabla ya kuandika kwamba tutakaosoma ni wananchi wenye akili ya kutosha sana.

Respect na Later!, I mean nitarudi niktakapopata nafasi tena.

FMEs!
 
 
Haya ndio maneno mkuu wangu wanijua vizuri kuliko watu wote humu JF... Kesho likinitokea baya ni wewe utakaye peleka habari kwa ndugu na kjamaa zangu haya maswala ya dini sijui yametokea wapi..

Kifupi ni wewe ulotaka kunihukumu mimi kwa sababu sijala Nguruwe..Kwa mtazamo wako watu wote wasiokula nguruwe ni waislaam hivyo yeyote anayebisha usafi wa nguruwe ni lazima awe Muislaam..Na kwa bahati mbaya kweli I'm a muslim lakini haiondoi hoja ya usafi wa nguruwe hata kama ningekuwa Mkristu...
A man must be big enough to admit mistakes, smart enough to profit from them, and strong enough to coreect them..That's me!.

Ya Lowassa mkuu wangu nakubaliana nawe pale unapomkwaa Rev. kwa kumnadi Lowassa..hilo tupo pamoja lakini kumtenganisha Lowassa na CCM wakati ni kiongozi ndani ya chama ati kwa sababu tu kajiuzuru uongozi wa nchi..Hapo mkuu wangu sipo, U miss the point, kwani ktk mtazamo huo mwenye kustahiri sifa anatakiwa kuwa Lowassa. he was a leader strong enough kuachia ngazi, sifa ambayo hakuna waziri mkuu aliyewahi kuifanya.
 
Haya ndio maneno mkuu wangu wanijua vizuri kuliko watu wote humu JF... Kesho likinitokea baya ni wewe utakaye peleka habari kwa ndugu na kjamaa zangu haya maswala ya dini sijui yametokea wapi..

Kifupi ni wewe ulotaka kunihukumu mimi kwa sababu sijala Nguruwe..Kwa mtazamo wako watu wote wasiokula nguruwe ni waislaam hivyo yeyote anayebisha usafi wa nguruwe ni lazima awe Muislaam..Na kwa bahati mbaya kweli I'm a muslim lakini haiondoi hoja ya usafi wa nguruwe hata kama ningekuwa Mkristu...
A man must be big enough to admit mistakes, smart enough to profit from them, and strong enough to coreect them..That's me!.

Ya Lowassa mkuu wangu nakubaliana nawe pale unapomkwaa Rev. kwa kumnadi Lowassa..hilo tupo pamoja lakini kumtenganisha Lowassa na CCM wakati ni kiongozi ndani ya chama ati kwa sababu tu kajiuzuru uongozi wa nchi..Hapo mkuu wangu sipo, U miss the point, kwani ktk mtazamo huo mwenye kustahili sifa hapa anatakiwa kuwa Lowassa, he was a leader strong enough kuachia ngazi, sifa ambayo hakuna waziri mkuu aliyewahi kuifanya. Kuondoka kwa Lowaasa ktk madaraka kimsingi kunaharibu jina la chama kizima ikiwa chama hakitachukua hatua yoyote dhidi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…