Hapa tunazungumzia nadharia tu au mgombea halisia 2010? Kama ni halisia basi ni JK na hana mpinzani. Kama ni nadharia tu basi tungoje 2011 baada tu ya JK kuingia 2nd term. Hapo na mimi nitakuja na jina langu, most likely from the opposition. Nadhani mnajua ni nani...Sitaki kumtaja sasa wasije waka Mkolimba mapema.
TK,
How do we build opposition? By exploring and exploiting the current environment.
!
- Jamani sometimes hizi theory ni incredible, yaani ku-build up political opposition Tanzania ni lazima kumtumia kiongozi ambaye rather than facing Wananchi bungeni on his charges za wizi yeye akaamua kukimbia mwenyewe bila kufukuzwa, wala kukubali responsibility ya wizi wake, sasa leo eti the right political thinking ni kumtumia kiongozi huyo huyo mwizi as a tool of exploring and exploiting the current political environment as the opposing figure kwa a legitimate sitting government, and no other way arround kwamba afikishwe kwenye mkondo wa sheria kujibu mashitaka yake as away of cleaning our political system na uozo?
- I mean this kind of thinking inakatisha tamaa sana, ni wa-Tanzania wangapi wanaoweza ku-figure out kwamba the intention ya hii thread ni just an-exploitation of the current political environment na sio exactly meaning what it says? Wakuu huu uwanja JF ni mkubwa sana think before you write anything hapa, we are JF the best in the political analysis business ya our nation na hasa on what direction tunahitaji kwenda kiuongozi, sasa tunahitaji kuwa makini sana na ushauri wetu kwa taifa.
- Sasa kushauri kwamba Lowassa ni the best ever yaani kama Mwalimu, sijui kama ni the right thinking, hasa kwa vijana wetu, na kudai eti ushahidi wa ufisadi wake uko wapi ni an insult kwetu wananchi wa Tanzania hasa the JFs, ambao tumewahi kulala macho kusaidia ripoti ya tume ya Mwakyembe, on Richimonduli ambayo ndiyo iliyoishia kumfanya Lowassa akimbie uongozi bila kufukuzwa.
Respect.
Field Marshall Es!
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!
Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.
Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.
Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!
Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!
Kaka unaweza kuwa huko sahihi na mawazo ya kweli japo umeyaweka kwenye jamvi la watoto wa Mwakyembe na Mengi...........leo nawashangaa watu wanaoshindwa kuwaza na wala kujiuliza kwa nini mpaka sasa mitambo ya umeme haijaletwa nchini na bado watu hawajui ni kwa nini tuko gizani mpaka sasa.
Rais ameamua tuwashe mitambo ya IPTL kwa gharama ya shilingi billioni 23 kwa mwezi kwa kuwa tuna roho mbaya na chuki dhidi ya mitambio ya dowans na ukijumlisha hofu ya kikwete kwa mwkymb,tunaacha kusave hela zetu kwa kuwasha mitambo ya dowans yenye sifa zifuatazo to compare with iptl
1.tungelipa bilioni 3 kwa mwezi kwa dowans na tutalipa bil 23 kwa mwezi kwa iptl.
2.tunatumia fedha za kigeni kununua mafuta lita elfu 5 kwa siku kwa iptl na tunatumia gas ya asili kwa mitambo ya dowans
3.dowans ni rafiki wa mazingira wakati iptl inachafua mazingira.
4.mitambo yote miwili ina kashfa ya ufisadi na ina kesi mahakamani na inazalisha megawati 100
Fisadi mtoto,
Waswahili wanasema Ukikosa ziwa la mama hata la Punda linafaa.. sasa wewe unapokuja pima sababu kwa nini isiwe la nguruwe au mbwa ambaye anapatikana na rahisi kumfuga kuliko Punda unaleta habari nyingine..
Dowans ni Noo! Noo! hili sakata lake linahusiana na Kiongozi wa juu huyu Lowassa anayesifika ambaye tunataka afikishwe yeye mahakamani achana na habari ya Dowans kuwa mahakamani pia.. Hawa wameweka hivyo tu buy time tu na sababu..
IPTL nayo ina matatizo yake lakini ndo tambara la kiraka kuziba pachu la takoni..Binafsi naelewa kwa nini IPTL inasisitizwa kuingia mkataba hatuna sababu nyingine fedha zimeshaliwa kwa mtindo wa EPA..Ni vurugu tupu hatuna la maana zaidi ya kukubali matokeo..
Kwa maneno ya Jk mwenyewe anasema, hii ni mitihani ya Mungu yaani mnajaribishwa imani zenu!
Yes, I have said it. Ili tuendelee, tunamhitaji Edward Ngoyayi Lowassa!
Ni mchapakazi, mfuatiliaji na mkali asiye na masikhara na walioko chini yake si kuwa wanamheshimu tuu, wanaogopa kushukiwa na zali kutokana na ukali na ufuatiliaji wake.
Kila kazi aliyopewa, kaifanya kwa bidii na kwa ufanisi. Kuna tofauti kubwa sana za kiutendaji kati yake na wenzake walioshika nafasi za uongozi ambazo alizishikilia.
Naamini kwa dhati kuwa ili Tanzania iweze kuamka na kurudi katika mstari ulionyooka wa kujituma, kufanya kazi kwa bidii na maarifa bora na la zaidi kwa nidhamu ili tuendelee vyema na safari yetu ya kujijenga kiuchumi na kijamii ili kuleta maendeleo ya kweli, basi hakuna mwingine zaidi ya Lowassa!
Kama unaye wa kwako, tupe jina na umnadi, wangu miye ni Lowassa!
Fisadi mtoto,
Waswahili wanasema Ukikosa ziwa la mama hata la Punda linafaa.. sasa wewe unapokuja pima sababu kwa nini isiwe la nguruwe au mbwa ambaye anapatikana na rahisi kumfuga kuliko Punda unaleta habari nyingine..
Dowans ni Noo! Noo! hili sakata lake linahusiana na Kiongozi wa juu huyu Lowassa anayesifika ambaye tunataka afikishwe yeye mahakamani achana na habari ya Dowans kuwa mahakamani pia.. Hawa wameweka hivyo tu buy time tu na sababu..
IPTL nayo ina matatizo yake lakini ndo tambara la kiraka kuziba pachu la takoni..Binafsi naelewa kwa nini IPTL inasisitizwa kuingia mkataba hatuna sababu nyingine fedha zimeshaliwa kwa mtindo wa EPA..Ni vurugu tupu hatuna la maana zaidi ya kukubali matokeo..
Kwa maneno ya Jk mwenyewe anasema, hii ni mitihani ya Mungu yaani mnajaribishwa imani zenu!
Mchungaji Kishoka,
Nimesoma hii mistari uliyotiririsha hapa na kuirudia tena na tena. Halafu nikatafakari mambo unayoyaandika hapa siku zote, na hat uliyopata kuyaandika kuhusu huyuhuyu mmasai/mmeru nikakusikitikia sana na zaidi nikaisikitikia nchi yangu Tanganyika.
Naamini sasa kwamba ulipojiita kishoka hukufanya hivyo kwa bahati mbaya, yaani nimewakumbuka vishoka wanaotuunganishia umeme huku mitaani, nikasema kwakuwa jina umejipa mwenyewe sasa umeamua kujidhihirisha sura yako halisi.
Pamoja na yote unayosema, mafisadi mtawatumikia nyie msiokuwa na uzalendo halisi na nchi yenu. Hata ukimpaka mafuta na vikorombwezo vyoote madukani, fisadi lowasa hasafishiki!!!!
Mwita wa Maranya,
Je uliponisoma ulinielewa vizuri? Kama umeshanisoma miaka mingi ya kutosha na kuelewa weledi au siha ya Mchungaji, kimekushinda nini kunielewa na kufikia timilisho kuwa nami ni sawa na vishoka wa Tanesco au Dawasco?
Unajua nakumbuka Kitila Mkumbo aliposema kuwa kina Mwakyembe hawakufuata haki na kanuni kumsulubu Lowassa, watu tulifumbia macho ukweli wa kufuata haki na kanuni na kusema Kitila kapewa chochote na hatukusimamia haki.
Wakati Mwakyembe alipotukanana na Rostam kuhumu umeme wa nguvu za upepo, watu wakadai ah, hakuna kosa kwa Mwakyembe kuwa na kampuni ya umeme alimradi kitendo chake ambaco dhahiri ilikuwa ni kukiukwa miiko na kanuni tukakifanya ni sahihi kwa kuwa yeye ni "mkombozi".
Sasa leo "mkombozi na mpiganaji" akivunja miiko na kukiuka kanuni tunadai Ruksa, lakini tusiyempenda akifanya hilo hilo tunalia apelekwe kwa Pilato asulubbiwe, je haki iko wapi? je lini tunaweza kujenga jamii na Taifa lenye kufuata kanuni, lenye utu na lenye kusimamia haki?
Nimesema tena kwa kujikosoa kuwa hata pamoja na hasira zangu na maudhiko yangu hata chuku dhidi ya Lowassa nilizozisema kwenye Deconstructing Lowassa, bado kuna vitu ambavyo Lowassa alivvyokuwa akifanya kiutendaji kama uchapa kazi, ufuatiliaji na ile uwezo wa kuwa na nguvu za kidola na kufanya watu wachacharike bado anao na ni haiba yake.
Ndio maana nikasema, kuna haja ya kuwa na sacrifice na compromise kutoka kwetu, maana kati kundi na chama alichoko Lowassa, hakuna mwenye nguvu au uwezo wa kuongoza kiutendaji na hata hili la vita vya Ufisadi ni gumu kwao.
Lakini tabia yetu hapa JF ni kutaka tubainishiwe kila kitu, ndio maana umesikia watu wakilialia "aah Mchungaji mbona unatuchanganya, tukueleweje, sasa tufuate lipi unlosema" nami nimewajibu kwa kusema kuwa wao ni watu wazima wenye uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi bila kumtegemea Mchungaji.
Nimewaambia watmie busara zao wanapopewa Kuku na Yai wapigie kura kimoja wapo, lakini wengi humu ndani, wanadai eti wanatakak kujua ni kipi kilitangulia, Kuku au Yai! Ndio maana mko njia panda hamuelewi ninachokisema!
Mchungaji maandiko yako ninayasoma na kuyaelewa sana. Nikizungumzia hapo nilipoweka nyekundu, nataka nikuthibitishie kuwa ni BIG NO. kuna watu wenye uwezo mkubwa kuliko lowasa, tatizo ni kwamba hawajapata nafasi, hawajapewa nafasi. Hebu tuthibitishie pasipo shaka kwamba Tanzania hii imekosa kabisa mtu wa kusimamia kiamilifu maendeleo ya wananchi. Yaani bila lowasa mambo hayaendi? kwani sokoine alitokea wapi?nani alikuwa anamfahamu kabla hajawa waziri wa ulinzi na baadae waziri mkuu? wacha masihara kabisa mchungaji. Nataka nikuhakikishie wewe pamoja na wenzako mnaompigia debe lowasa kwamba, ni afadhali Nape Nnauye apewe huo uPM kuliko fisadi lowasa. Na hii nchi hata siku moja haitajuta wala kusikitika kwa lowasa kutorudi serikalini, zaidi sana itaendelea kusikitika kwa udhalimu alioufanya. Kaulizwa swali dogo tu na mtoto wa kidato cha kwanza pale mwanza kashindwa kujibu halafu unakuja hapa kumtetea hadi povu linakutoka, hapana aisee kwa hili hapana bana.