Ujue kwa ufupi: Mkataba wa Songas na TANESCO unaotarajiwa kufika tamati Julai 2024

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,576
17,718
1. Songas kampuni binafsi iliyoingia mkataba wa kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO mwaka 2004 kwa kutumia mitambo ya gesi. Songas iko Ubungo mataa kama unaatokea Mwenge kwenda Riverside ama Buguruni.

2. Songas ilianzishwa kwa mtaji wa Dola milioni 306, yaani 75% ( Serikali ya Tanzania kupitia mkopo) na 25% mtaji. Kwa maana serikali ya Tanzania ilichangia 75% ya mtaji ama Dola 234M kuanzisha kampuni ya Songas na Globeleq kampuni inayomilikiwa na Uingireza na Norway kuchangia 25% sawa na Dola 72M kwenye uanzishwaji wa Songas.

3. Serikali ya Tanzania ilichukua mkopo wa Dolar 234m ili kuchangia kuanzia kampuni ya Songas kutoka Benki ya Dunia (Dola183m) na Benki ya Umoja wa Ulaya (Dola 51m).

4. Serikali ya Tanzania inaimiliki hisa 40% ya kampuni ya songas pamoja na kwamba ndio ilichangia sehemu kubwa ya kuanzisha Songas. 75/25 lakini sasa inamiliki 40% tu.

5. Pamoja na serikali ya Tanzania kuchangia 75% ya kuanzishwa kwa Songas, bado mitambo inabaki kua mali ya Songas baada ya mkataba kuisha mwaka 2024.

6. Mkataba wa Songas ulipaswa uwe ni build, operate and transfer lakini uko build, own and operate.

7. Tanzania tayari imelipa mkopo wote wa dola 234 lakini Songas bado sio mali yake. Hii ni kama Pride Tanzania. Serikali ilitoa mtaji 100% kuanzisha Pride Tanzania lakini baadae ikaja kuonekana Pride Tanzania ni mali ya Iddi Simba😂.

8. Pamoja na kwamba serikali ya Tanzania ilichukua mkopo kutoka WB na EIB lakini riba ilikua kubwa kuliko hata mikopo ya kibiashara ama Commercial loans.

9. Mkataba wa Songas ulikua wa miaka 20 ambao unaisha muda wake July 2024.

Je serikali itaongeza mkataba wa Songas, je isipoongeza na imelipa mkopo wote na bado mitambo sio yake itakuaje?

Soma pia:

1) Songas: Tuko tayari mkataba kupitiwa upya

2) TANESCO yashitukia mkataba wa Songas

3) Serikali yaagiza TANESCO na Songas waanze kugawana mapato kwa usaw

4) Mkataba wa Songas na TANESCO bora uvunjwe, hauna maslahi kwa Taifa!
 
Hivi ndivyo CCM wanavyoibia Watanganyika mali zao..

Unaweza kufikiri kama hawana akili vile wanapoingia mikataba hii..

Lakini ukweli ni kuwa wana akili zao timamu kabisa ila ni akili corrupt za kishetani mwanzo mwisho..

Lakini utashangaa Chawa na Wadudu wanashangilia na kupiga mayowe tu kama mazuzu kwa sababu baba na babu zao ni mazuzu..!!
 
unafikiri kwa nini akina tundu lisu &co. wanamshambulia raisi samia sasa hivi ? timing is everything.
hapo ujue wameshaona dalili za samia kutokokuongeza mkataba na songas yao na siajabu kuwapa waarabu au irani, hakuna mtu corrupt na evil nchi hii kama tundu lisu…
Lete Ushahidi
 
unafikiri kwa nini akina tundu lisu &co. wanamshambulia raisi samia sasa hivi ? timing is everything.
hapo ujue wameshaona dalili za samia kutokokuongeza mkataba na songas yao na siajabu kuwapa waarabu au irani, hakuna mtu corrupt na evil nchi hii kama tundu lisu…
Bora ukose vyote lakini sio akili.
 
Watetezi wa wezi ufipa tunasubiri maoni yao walimtetea lowasa na dowans wakamtetea singh na rugemalira sasa nawaona wakiwa upande songas!
 
Hapo Wahuni Wanajipatia Kampuni Kama Mzilankende Alipookota Vichwa Vya Treni Bandari
Ambavyo Havina Mwenyewe Wala TRC Pia Hawana Habari


Ama Yale Makontena Ya Jersey
Umenikumbusha na yale magari zaidi ya Mia yaliyoagizwa kwa anwani ya ikulu.. JPM aliishia kuyagawa polisi.

Hawa watu wakiwa nje ya system wanakua na ngozi ya kondoo wakishaingia tu ndo unajua kumbee ni mbwa mwitu wakali
 
Back
Top Bottom