Mkuu, umeongea point sana, ila kuna mahali umepiga msituni kidogo. Unaposema kuwa asilimia 60 ya bajeti imekwenda kwenye mishahara na Posho, na kiasi kilichosalia kikaenda kwenye maendeleo siyo kweli. Kwa heasabu nyepesi kabisa, unachotaka kuwaambia watanzania ni kwamba Bajeti ya Tanzania= Posho+ Mishahara+ Maendeleo. Kama hiyo ndiyo tafsiri yako ya Bajeti, utakuwa umepotoka. Tafsisi sahihi ni hii:
bajeti ya Tanzania= Mishahara+Posho+ Matumizi ya kawaida ( mafuta, vitabu, madawa, ukarabati nk)+ maendeleo. Kwa tafsiri halisi ya serikali( kwa mujibu wa vitabu vya bajeti) bajeti yetu = Personal Emoluments ( Mshahara na mafao)+ Other charges ( ghrama za uendeshaji) + developement Expenditure( Maendeleo). Kwa miaka mingi sasa, bajeti ya maendeleo imekuwa ni kama asilmia 20 tu ya bajeti nzima.
Kwenye tafsiri yako, utakuwa umesahau fedha za uendeshaji ( other charges ) ambazo ni karibia asilimia 40 ya pesa pesa zote za matumizi ya kwaida yaani ( recurrent Expenditure)
Viginevyo, point zako ni za msingi sana.
Sawa sawa mkuu. Ebu tusaidiane kuchambua hili:
Mkullo June 2011
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, katika mwaka 2011/12 Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi
bilioni 13,525.9 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 8,600.3 kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha shilingi bilioni 3,270.3 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Serikali, taasisi na wakala za Serikali na shilingi bilioni 1,910.4 kwa ajili ya Mfuko Mkuu wa Serikali.
Aidha, jumla ya shilingi bilioni 4,925.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo shilingi bilioni 1,871.5 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 3,054.1 ni fedha za nje.
Mapato:
A: Mapato ya Ndani 6,775,952
(i) Mapato ya Kodi (TRA) 6,228,836
(ii) Mapato Yasiyo ya Kodi 547,116
B: Mapato ya Halmashauri 350,496
C: Mikopo na Misaada ya Nje 3,923,551
D: Mikopo ya Ndani 1,204,262
E: Mikopo ya Masharti ya Kibiashara 1,271,634
JUMLA YA MAPATO YOTE 13,525,895
F: Matumizi ya Kawaida 8,600,287
(i) Mfuko Mkuu wa Serikali 1,910,376
(ii) Mishahara 3,270,292
(iii)Matumizi Mengineyo 3,419,619
Wizara 2,727,472
Mikoa 49,981
Halmashauri 642,166
G: Matumizi ya Maendeleo 4,924,608
(i) Fedha za Ndani 1,871,471
(ii)Fedha za Nje 3,054,137
JUMLA YA MATUMIZI YOTE 13,525,895
---
Ukisoma katika ufunguzi utaona kuna takwimu zimefinywa finywa, hazielezwi zimeenda wapi na mantiki yake ni matumizi ya kawaida in the form of posho, mishahara, repairs za majengo haya na yale, dhfa za kitaifa n.k - kwa ufupi i still hold kwamba 60% of the budget goes to other things than maendeleo ya Mtanzania. Thats the bottomo line.