Taarifa rasmi kutoka Ikulu na sekta husika leo kuanzia saa moja asubuhi ya tarehe 27/03/2011 imesitisha watu wote kwenda Loliondo kwa Mchungaji mstaafu ndugu Ambilikile Mwasapile kwenda kupata tiba hadi hapo tarehe 2/04/2011 kutokana na miundombinu kuwa mibovu hadi kupelekea wananchi kushindwa kufika eneo husika na wananchi wengine kukwama na hadi kuishia kukaa porini kutokana na miondombinu ya kufika kwa mchungaji huyo kuwa ni kitendawili kutokana na mvua za masika zinazoanza kunyesha katika kanda ya kaskazini. Serikali imefikia uamuzi huo baada ya kupata malalamiko na isitoshe baadhi ya watu kushindwa kufika au kurejea kutoka kule Samunge Loliondo kutokana na hali hiyo, serikali imetamka kua haitaweza kustahimili kuona wananchi wanakwama katikati ya pori nene kutokana na kukwama japokua wananchi wanahitaji huduma hiyo ya mchungaji Mwasapile. Kwahiyo serikali imewaomba wananchi kua na subira hadi hapo tamko rasmi litakapotolewa hiyo tarehe 2 ya mwezi wa nne. Lakini serikali pia imesema kua wale walioko kule Loliondo wabakie wakisubiri huduma lakini hakuna magari au Helikopta kwenda huko.