ndugu zangu,
kumekuwa na misimamo mingi na kinzani kuhusu uwezo wa dawa ya babu wa loliondo kutibu magonjwa sugu. Misimamo mingine ni ya kiimani kwamba kama ni huduma hiyo inatolewa kwa imani kwa nini babu atoze hela sh. 500? Wenye msimamo huu wanarejea biblia pale yesu kristo aliposema mmepewa bure toeni bure. Kwa hiyo, wenye msimamo huu wanasema hiyo kasoro ni dalili tosha kuwa huduma ya babu haijatoka kwa mungu. Lakini vilevile, wapo wanaoipinga huduma ya babu siyo kwa imani bali kwa mtazamo tofauti kwamba hiyo ni biashara kama zilivyo biashara zingine tu. Hao wanasema babu ametumia ujanja wa kuweka gharama ndogo sana ya tiba ambayo ni sh. 500 lakini ana uhakika na msururu wa wateja utakaojaa kuitaka tiba hiyo unatosha kumfanya yeye awe tajiri pengine kuliko wote katika nchi hii. Hao wanasema hesabu za babu zimejikita katika uwingi wa watu wanaosumbuliwa na magonjwa ambayo babu ameyatangaza kuwa anatibu.
Ni jambo lililo wazi kuwa hivi sasa nchi yetu na pengine dunia nzima afya limekuwa ni suala linaloisumbua sana jamii. Magonjwa ya ukimwi, kisukari, pumu, kansa, n.k. Yanasumbua na kupoteza maisha ya watu wengi. Hali hii pengine kwa nchi yetu ni mbaya zaidi kutokana na huduma za afya kuwa duni sana. Na ndiyo maana viongozi takriban wote na wananchi wa kawaida wenye uwezo wamekuwa wakienda nchi za nje kufuata tiba bora. Sasa katikati ya hali hii anapojitokeza mtu wa aina ya babu akatibu wagonjwa na wagonjwa hao wakashuhudia hadharani kwamba wamepona tena siyo mmoja wala wawili, ni wengi, unatarajia mwitikio utakuwaje?
Ndugu zangu tusidanganyane tena tuache porojo. Inawezekana tunafanya hivyo kwa sababu tuna afya njema. Hatujui kuumwa maana yake ni nini. Kwa mtu ambaye miaka yote amekuwa akiumwa tena kuumwa haswa na amekuwa akiombewa na kupata tiba kila hospitali kubwa hapa nchini bila mafanikio, anaposikia wagonjwa wenzie wamepona unatarajia nini? Kwa nini nae asiende kujaribu kama alivyojaribu kwenye hizo hospitali na hayo maombi? Kwa nini aendelee kutegemea tiba ambazo miaka na miaka zimeshindwa kumponya?
Kuna shemeji yangu ambaye amekuwa akisumbuliwa na ukimwi kwa miaka takriban saba. Mkewe alifariki kwa ugonjwa huo. Sasa ni wikiya tatu tangu apate kikombe cha babu amecheki afya yake hospitalini yupo negative. Hospitali ya kwanza ilikuwa ni agakhan dar es salaam, ya pili ilikuwa ni regency na ya tatu ni burhan. Sehemu zote ni negative. Pia, kuna watu wameshuhudia wamepona kisukari, pumu na vidonda vya tumbo. Acheni wagonjwa waende bwana. Wanaokufa ni kutokana na uchivu wa safari ya njia ndefu na mbovu. Muhimu ni kwa ndugu kuhakikisha kuwa mgonjwa aliyezidiwa anaenda kwa babu huku akiendela na tiba.