Imetokea loliondo

Imetokea loliondo

Mijadala kama hii mimi naona haifai kabisa swala la kuumwa na kutibiwa ni swala binafsi kabisa ambalo lina mhusu mtu mmojammoja na familia yake........hivyo huwezi kumlazimisha mtu atoe ushuhuda wa kunywa kikombe cha babu na kupona au kuto pona. Wakati ana umwa na kuhangaika kwenye hospitali tofauti tofauti na kwenye maombi alikuhusisha iweje leo akuhusishe katika mahangaiko yake.........

Mwenye kuamini na aamini,mwenye kutibiwa na akatibiwe na asiye amini na asiamini na asiye taka kutibiwa asiende kunywa kikombe cha babu.Msijaribu kuleta maswala yenu ya udadisi kwenye maswala binafsi hakika hamuwezi kupata majawabu. Serikali kwa utafiti wao kupitia vituo vya afya wanaweza kutoa majibu haya kwa kuona watu wao walio kuwa wna enda clinic wanastatus tofauti na awali au wagonjwa wanapungua kama wanavyo pungua waumuni kwenye baadhi ya makanisa yakinananihii................
 
Mkuu wa wilaya ya Mbinga amekiri kwenda kupata kikombe cha babu na kumponyesha ugonjwa wa kisukari uliomsumbua kwa takriban miaka 20.

Source- TBC1 taarifa ya habari usiku huu
 
Nimeiona iyo Tbc(TELEVISHENI YA TAIFA). Mawaziri waliomtembelea kuona jinsi gani ya kuweza kutatua wimbi la watu na kuboresha miundo mbinu mwishoni walimwomba Babu awape kikombe wanywe.
 
1. Kisukari - 100% ACTIVE
2. Saratani - 100% ACTIVE
3. Vidonda vya Tumbo - 100% ACTIVE
4. Ukimwi - 99% ACTIVE

Superman au yeyote anayefahamu, wanaposema '100% au 99% active' maana yake nini hasa kitaalam?
 
Taarifa ya saa mbili usiku TBC 1 wameonesha picha za watu wakiwa wamekufa kwa babu Loliondo.

This is very serious, tuamke tuachane na imani potofu, nna amini Mungu ameanza kudhihirisha kuwa he is not involved in that business because otherwise angewaponya hata kabla hawajafika kwa babu.

Nashauri serikali iingilie kati because soon wananchi wataigeukia na kuilaumu na hata kuanzisha maandamano kwa kutowajali wananchi wake ambao wanakufa hovyo porini.
 
leo nimemuona waziri MAIGE,itv akiomba kikombe na pia watalii wapewe ratiba maalumu ya kupata kikombe cha babu!
 
Cha ajabu gari bado zinapakia pale chini ya mti pembeni ya Sheikh Abeid Stad, ila nimepita Meserani polisi wanazuia wote wanaoenda huko (wanakagua magari yote yaliyobeba watu wengi-wengi hivi na yote ya abiria) na kizuizi kingine kipo Makuyuni
 
Muda si Mrefu wakina KAKOBE, MUNGIRA NA GEorDavie watahabika ... maana wamepinga sana huyu Babu.
 
Mbona waziri MAIGE KAOMBA kibali kwa babu ili watalii wapewe ratiba maalumu ya kupata kikombe?naye kanywa leo
 
Wizara wametangaza au watatangaza lini tupate matokeo kamili.
 
Taarifa ya saa mbili usiku TBC 1 wameonesha picha za watu wakiwa wamekufa kwa babu Loliondo.

This is very serious, tuamke tuachane na imani potofu, nna amini Mungu ameanza kudhihirisha kuwa he is not involved in that business because otherwise angewaponya hata kabla hawajafika kwa babu.

Nashauri serikali iingilie kati because soon wananchi wataigeukia na kuilaumu na hata kuanzisha maandamano kwa kutowajali wananchi wake ambao wanakufa hovyo porini.

Hayo niliyopigia mstari yanaonesha jinsi gani ulivyo.
 
Mpaka sasa hivi hakuna daktari yeyote aliyethibitisha kwamba m(wa)gonjwa aliyemfahamu/aliyowafahamu (w)akiwa na ugonjwa wa muda mrefu kama kisukari, ukimwi n.k. ambaye/ambao alipata/walipata kikombe cha maji ya uzima toka kwa Babu (w)amepona kabisa na vipimo vyote vinaonyesha kwamba kisukari, ukimwi au gonjwa lolote lile limepotea kabisa, lakini pamoja na kutokuwa na uthibitisho wowote ule bado watu wanamiminika tu!
 
Toa ushauri hao wagonjwa wakatibiwe wapi?maana hospital imeshindikana sindano ya insulin asubuhi na jioni maisha yote si mateso hayo?
 
Viongozi wengi wa serikali wameenda huko na serikali ipo. Kwa nini tamko rasmi la serikali lisitolewe hata kwa jambo kama hili?? Nchi Hii inakwenda wapi?
Hata swala la babu linahitaji kikao cha baraza la mawaziri (ambalo mwenyekiti wake ni rais)?
 
Hayo niliyopigia mstari yanaonesha jinsi gani ulivyo.

unajua mlevi hata ukimuonesha sura katika bible inayokataza pome hawezi elewa, au teja umpe maneno ya kusaidia asitumie midawa ya kulevya hatokuelewa, sasa ndio wewe. Ivi unadhani mungu siangemwambia pia kuwa watu watakuwa wengi kwahiyo mazingira yalekebishwe?
 
Mpaka sasa hivi hakuna daktari yeyote aliyethibitisha kwamba m(wa)gonjwa aliyemfahamu/aliyowafahamu (w)akiwa na ugonjwa wa muda mrefu kama kisukari, ukimwi n.k. ambaye/ambao alipata/walipata kikombe cha maji ya uzima toka kwa Babu (w)amepona kabisa na vipimo vyote vinaonyesha kwamba kisukari, ukimwi au gonjwa lolote lile limepotea kabisa, lakini pamoja na kutokuwa na uthibitisho wowote ule bado watu wanamiminika tu!

Good, consider this, CCM wana miaka mingi madarakani, bila mafanikio yoyote, na bado wamo madarakani. Hii ndio TZ, i am not surprised.
 
Back
Top Bottom