Imetokea loliondo

Imetokea loliondo

Ok.

Let's wait and see..

Shukrani kwa taarifa Superman.
 
Asupile Mwasapile al-maarufu BABU wa Loliondo kwa sasa ameleta hali na mwelekeo tofauti kabisa kwa nchi yetu Tanzania. Babu huyu ambaye ni retired Pastor wa kanisa la Kilutheri Tanzania amejizolea sifa na heshima kubwa sana baada ya madai yake kuwa Mungu alimwotesha ndoto ya dawa itakayotibu magonjwa sugu ukiwemo ukimwi!

Huyu Babu tayari amekuwa aking'ara kwenye medani ya vyombo vya habari kuliko hata viongozi waandamizi wa Srikali ya JK akiwemo Kiwete mwenyewe.

Habari za kuaminika ni kuwa vigogo karibu wote wa CCM na SERIKALI akiwemo KIWETE wameshakwenda kunywa KIKOMBE cha BABU chenye dawa inayoitwa MUGARIGA.

Kitu iinachoshangaza ni kuwa BABU ametokea kuogopewa na Serikali ya KIWETE kama vile yeye ndiye Rais. Babu kwa sasa ndiye anayeiendesha Serikali ya CCM. Yeye ndiye anayeipangia Serikali ifanye nini,lini na wapi.

Habari ya kuchekesha kama siyo kusikitisha ni pale jana Serikali ikiongozwa na William Lukuvi ilipotaka kutoa TAMKO kuhusu Tiba ya BABU na hali halisi iliyoko pale Samunge.

Jambo la kushangaza ni kwamba Lukuvi na jopo lake walioenda kuchunguza na kutathmini hali halisi ya kile kinachoendelea huko Samunge ilishindwa kutoa Tamko baada ya kupigwa STOP na BABU kwa masharti kwamba haiwezi kutoa tamko kabla ya yeye kutoa tamko lake! Serikali kweli ikasitisha kutoa tamko kwa AMRI YA BABU!

Tafsiri yake ni nini? Hii imethinbitisha kuwa serikali ya CCM kwa sasa haina serikali. Maana yake HAINA WATU/VIONGOZI MAKINI WENYE KUCHUJA MAMBO KWA KINA NA KUTOA MATAMKO AU MAAMUZI MAGUMU KUHUSU MSTAKABALI WA NCHI HII.

Ndiyo maana kwa sasa Serikali inahangaika na CDM kama vile ndiyo mchawi wake aliyesababisha KUCHUKIWA KWA CCM NCHI NZIMA! Ndiyo maana CCM kwa sasa imesahau MAMBO YA MSINGI YA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI yakiwemo ya TATIZO LA UMEME,KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA(Mafuta ya mitambo na ya kula,Chakula,Sukari,Nauli n.k.)!Badala yake inahangaika na BABU WA LILIONDO KANA KWAMBA YEYE NDIYE ATALETA DAWA YA MATATIZO HAYA YA WATANZANIA. Hii ni aibu kubwa kwa serikali ya CCM.

Kikwete na Baraza lake la Mawaziri wameshindwa kazi. Mimi naamini kuwa huyu Babu hakuinuliwa na Mungu kwa ajili ya kutoa DAWA tu ya kutibu magonjwa sugu ya Wa-TZ baali atakuwa ameinuliwa vilevile KWA AJILI YA KUWAONYESHA WA-TZ kuwa MUDA WA KUIONDOA SERIKALI YA CCM MADARAKANI UMEWADIA!!

Yes, Peoples Power from Semunge,Loliondo.com.

Nawasilisha.
 
Maggid anakataa kuwa babu kaoteshwa na Mungu kwa kuwa Biblia inasema "Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Ninyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake Yohana 5:37" Maggid anathibitisha kuwa Biblia inasema kuwa sisi pamoja na "babu" hatujapata kamwe kusikia sauti ya Mungu wala kuuona uso wake!Nadhani babu ana zaidi ya majini Maimuna Tafakari!

umekariri vibaya hiyo bible.
 
Ukimuona mtu na akili zake anaenda kwa babu kutafuta uzima, ujue kahangaika sana muda mrefu sasa hanabudi kuenda kujaribu ili apate uponyaji ambao kautafuta bilamafanikio kwa muda mrefu. Mtu kama maggid na wapambe wake, hawajapatwa na matatizo km ya hiv, kifua kikuu, saratani, na kisukari wakaonja adha yake.pemgine km wangeshapata wangetushuhudia kuwa wao japokuwa wanaumwa hawawezi kwenda ila wanasubiri kuendelea na mateso yao hadi wafe.... Pengine hapo wanganza nishawishi nami kwa hoja zao... Lakini kupayuka tu huku wengine wakipata taaaaaaabu kiafya haiingii akilini mwangu!!!
Imeandikwa. Siku za mwisho watatoka watu na kusema tazama bwana yuko huku. Na wengine watakwambia tazama kumbe yuko kule. Usiende! Bali palipo na mzoga ndipo wakutanikapo tai! Tafakari ujumbe huu kabla ya kumlaum maggid
Ad
 
Hizo dawa za ukimwi kutoka USA mmezikumbatia ingawaje wengi tu wanakufa tena mnanunua kwa bei ya juu kuliko hiyo shillingi mia tano ... .... ..... ...... mwacheni Babu naye akombe mpunga jamani ... ... huyu Majidi hata Mafisadi amawatetea lakini kwenye ukweli lazima atapinga bado hajaumwa na kisukari huyu mwacheni akianza kuumwa na ile line yake ya mpunga kutoka kwa RA ikikatwa ndio mtajua Majidi ni nani? Kama mnakumbuka alikuja hapa JF kwa unyenyekevu sana chacha pata bana kono mbele.
 
Kwani hii dawa ina tofauti gani na ile dawa iliyotumika kwenye vita vya maji maji aliyoitoa Mganga Kinjikitile Ngwale, ambaye naye alidai kuwa kaoteshwa na Mungu aitwaye Hongo kupitia roho wake wenye umbo la nyoka Bokera, kuwa dawa yake ina uwezo wa kubadirisha risasi za Mjerumani kuwa maji, na hazita wazuru. Dawa iliyotokana na mchanganyiko wa mafuta ya yaliyo tokana na mbegu za Mbarika na Mtama... Na matokeo yake kila mtu anayajuwa.
 
Hujaugua wewe, mtu anaumwa abaki nyumbani kusubiri kifo si bora anaona akafie kwa babu? Anayeenda mwenyewe asimfanye babu alaumiwe. Hakuna anayesukumwa!
 
Nilishasema na ntarudia tena na tena:

Kama Ndugu yangu au Mie anaumwa Kansa au AIDS na ninafahamu kuwa HAKUNA DAWA na anasubiri Kifo tu, sintasita kumchukua au kujisafirisha mwenyewe kwa Babu kupata Kikombe.

Nikinywa Kikombe, SINA unakika wa Kupona. Nisipokunywa, nina UHAKIKA WA KUFA.

Sasa weee njoo na Mahubiri yako Kuhusu Babu, wala sikuelewi.

Wengi wanabwabwaja hapa kwa sababu ni WAZIMA. Wakiuguliwa, watakuwa wa kwanza kwenda kwa BABU.

Nikinywa Kikombe cha Babu, SINA unakika wa Kupona. Nisipokunywa, nina UHAKIKA WA KUFA. Be Blessed all.
 
Back
Top Bottom