Mkuu naomba nipingane na wewe! Toka binadamu wa kwanza kuletwa duniani(Adamu) Mungu ni yule yule! Tofauti za kiimani zilizopo sasa ulimwenguni zimetokana na wale wapokeaji wa ujumbe wa Mungu! Wapo walioamua kuchakachua ujumbe huo wa Mungu kwa personal interests, otherwise tungekua wote katika itikadi na imani moja.
Vilevile wapo wakristo ambao wanampinga Babu! Mmojawapo alisikika akisema toka asikie habari za Babu hakuwahi kumsikia Babu akitaja neno YESU. Babu huwa anamtaja Mungu! Hii imemfanya mama huyu mlokole awe na mashaka na amesema katu hatuthubutu kwenda Liliondo!
Kwa waislamu kuna maajabu mengi yameshaelezwa kuja kutokea wakati ambao inaaminika ni siku za mwisho kabisa wa Dunia. Case ya Babu wa Liliondo inashabihiana kwa karibu na baadhi ya cases zilizotabiriwa. Kwa muumin mzuri wa kiislamu, hii ni miongoni mwa mitihani ya Dunia, subra na kuzidisha ibada ndio njia pekee itakayokuvusha salama katika Dunia hii.