Imetokea loliondo

Imetokea loliondo

Fununu zinaanza kuzagaa kuwa babu anawapotosha watu, je hii ni kweli? nionavyo mimi babu hahusiki kwa lolote hajamuita mtu Loliondo wala hajajitangaza isipokuwa vyombo vya habari ndio vimepotosha umma.Nawasilisha!!
 
Wakati kikao cha kutafuta njia bora ya kuwawezesha wananchi kupata tiba ya magonjwa sugu huko Loliondo kilichoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na viongozi wa mikoa sita wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdore Shirima na mwenzake wa Mara, Enos Mfuru kimeahirishwa juzi saa 3:35 usiku hadi kupata baraka za Mchungaji "Babu" Ambilikile Mwasapile;

Na wakati zinaripotiwa taarifa kuwa viongozi wanazua balaa na wananchi kwa 'kudandia foleni kwa mbele' hadi kusababisha wananchi kusukuma magari yao mtaroni na kuwajeruhi;

Na Liliondo wakiwa wanashuhudiwa makumi kwa mamia ya watu toka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi hadi baadhi ya Raia wa Ulaya wakimiminika kuelekea kijijini Samunge;

Waziri wa Afya ya Jamii wa Kenya Bi. Beth Mugo amesema, Mchungaji Mwasapile "anajifanya ndiye Yesu kabisa" il hali yeye "ni muganga" anastahili kukamatwa na kufungwa kwa kuwa anauhadaa umma.

Ili kufanikisha azma hiyo Waziri Mugo amesema watakapokutana Mawaziri wa Afya nchini Burundi wiki ijayo, atamwomba Waziri wa Afya wa Tanzania amkamate Mchungaji Mwasapile na kufunga "kliniki" yake.

Nikimnukuu katika habari cha NTV Kenya, Bi. Mugo anasema, "...na Mimi nitamwuliza, Minister wa Afya wa Tanzania, atusaidie na kufunga huyo mutu. Afunge hiyo clinic, afunge hiyo mahali watu wetu wanaenda kwa sababu hawapitii njia ile ya boda".

Ukitaka kumsikia Bi. Mugo, bofya hapa (video dk. 2:42 tu) umsikie. Mara zote mimi hufurahia maoni yanayoifuatia video au picha. Na katika video hii, yapo maoni mchanganyiko, bofya hapa kuyasoma.
Zaidi juu ya kikao cha baadhi ya viongozi wa Serikali kutafuta kurahisisha kumfikia Babu, bofya hapa
Kusoma zaidi kuhusu wananchi kukerwa na 'viongozi waingiliaji foleni' bofya hapa.


from: Waziri wa Afya wa Kenya asema "Babu" akamatwe! - Wavuti
 
Waziri wa Afya wa Kenya, Bi. Beth Mugo, amewakemea waganga wa kienyeji na wale wanaojigamba kwamba wanaponya kwa imani. Amesema kuwa serikali haitawaacha waipotoshe jamii kwamba wanaweza kuponya magonjwa yote. Aliyasema hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya Kifua Kikuu duniani. Aliendelea kusema kwamba waganga wa kienyeji wanahatarisha afya ya Wananchi wa Kenya. Alisema kitendo cha waganga hao wa kienyeji kudai kwamba wanaweza kuponya magonjwa sugu kama vile Ukimwi, kimesababisha magonjwa hayo kuenea zaidi kwa watu wengine. Aliendelea kusema kuwa huo ni uongo unaowafanya watu wachanganyikiwe.

Vile vile Bi Mugo amezitupilia mbali taarifa za vyombo vya habari kuwa mganga wa kienyeji anayejulikana kama babu huko Loliondo Tanzania, anaponya maradhi sugu, kwa kuwapa wagonjwa dawa inayotokana na mti wenye sumu. Bi. Beth Mugo ameiomba serikali ya Tanzania ikifunge kituo hicho cha Loliondo na kuwapiga marufuku watu wanaokwenda kwa babu huyo. Amedai kuwa watu wanaokwenda huko wakirudi wataeneza zaidi Kifua Kikuu na Ukimwi. "Tutakapokutana huko Burundi na Mawaziri wengine wa Afya wa nchi za Afrika Mashariki , nitamuomba Waziri wa Afya wa Tanzania, amtie gerezani babu huyo na kuipiga marufuku biashara yake ya uganga" alisema Bi. Mugo. Habari hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Kenya, KBC.

Habari hizo zinadhihirisha wazi kuwa "zimeichafua" sana akili ya Waziri huyo kama mtu aliyetupiwa madongo, ndio maana ameamua kujibu mapigo hadharani. Wakati huo huo Waziri wa Afya wa Tanzania naye pia amewakaripia vikali waganga wa kienyeji waache kudai kwamba wanaweza kuponya magonjwa sugu kama Kifua Kikuu. Hata hivyo, haijaeleweka wazi iwapo karipio hilo linamhusu pia babu wa Loliondo.

Babu wa Loliondo pamoja na kujiita mchungaji anaingia pia katika kundi la waganga wa kienyeji maana misingi ya tiba yake haitofautiani na ile ya waganga wengine wa kienyeji.

Kwa heshima na taadhima tunaiomba serikali yetu impige marufuku wazi wazi babu huyo ili kudumisha amani na utulivu uliopo kati ya Tanzania na Kenya. Babu asitusababishie chuki, uhasama na mgawanyiko kati yetu na Wakenya. Ni kweli, baadhi ya viongozi wa serikali yetu nao pia wamepata kikombe, kwa sababu hiyo wanaweza kuona aibu kumpiga marufuku babu. Tunaomba wasione aibu, maana wao pia sio malaika, ni wanadamu wanaoweza kukosea kama wengine. Kwa sababu hiyo wasilifumbie macho tamko hilo la Waziri wa Afya wa Kenya. Waziri huyo wa Kenya "ametema cheche" zinazoweza kutuongezea matatizo makubwa tuliyo nayo ya kiuchumi na kijamii. Wahenga walisema dalili ya mvua ni mawingu, na kinga ni bora kuliko tiba. Wakenya tunawategemea kwa mengi, wasije wakatufungia mpaka tukakosa bidhaa zao. Maduka mengi hapa TZ yamejaa bidhaa za Kenya – kuanzia mafuta, sabuni, vinywaji, nguo mpaka pipi. Inaonekana viwanda vyetu vinashindwa kuzalisha bidhaa bora.

Makampuni ya uchapaji, ya TZ, yaliyopo jirani na Kenya yanategemea sana kupata karatasi na vifaa vya uchapaji kutoka Kenya maana huko vinapatikana kwa bei nafuu. Sio hilo tu kuna Watanzania wengi waliopeleka watoto wao Kenya ili wajue vizuri Kiingereza maana shule nyingi za TZ hazina walimu wazuri wa lugha hiyo muhimu kwa mawasiliano kimataifa.

Dawa nzuri za kutibu hata mafua na kikohozi, ukiingia katika maduka ya madawa, utaona zimeandikwa Made in Kenya! Hata wanaotaka kuagiza magari kutoka Japan, wanaona nafuu magari yao yapitie bandari ya Mombasa, Kenya, maana bandari yetu ina ukiritimba mwingi na inachelewesha sana utoaji wa bidhaa.

Tembelea maduka ya vifaa vya ujenzi mjini Arusha, utashangaa kuona vifaa vizuri vya ujenzi, kama vile ceiling board, vimetoka Kenya. Siwapigii debe Wakenya, ila ukweli ndio huo tunawategemea kwa mengi ndio maana hata suala la Jumuia ya Afrika Mashariki bado linasua sua maana tunaogopa Wakenya watazidi kuushusha chini uchumi wetu.

We babu wa Loliondo, usiwafanye Wakenya watuchukie bure kwa sababu yako. Tukakosa hata Panadol(made in Kenya) ya kutibu maumivu ya kichwa. Usisahau Obama asili yake ni Kenya. Na Obama akiamua kuingilia suala lako, na kutuletea manowari na "mizaili" zake, kama alivyofanya kwa Kadafi, dawa zako haziwezi kumzuia. Kama hukupata mshahara mzuri kabla hujastaafu uchungaji, usitake kuwapora Watanzania walalahoi, pesa ndogo wanayoipata kwa shida, maana mishahara yao haitoshi hata kulipia nauli ya kuja huko Loliondo, mpaka wasafirishwe bure na Wabunge wa Chadema!
 
ivi mnaoenda huko wote ni wagonjwa? au wengine mnadai mnaenda kusafisha mwili? sijamsema m2 hapa ni mawazo tu wakuu
 
:juggle:Kwa kweli natamani kwenda huko Loliondo ili nami ninywe hiyo dawa 'takatifu'. Nadhani hao ambao hawaponi hawana imani au walikiuka utaratibu wa kunywa.
 
kosa lako labda kwa sababu huumwi laiti ungekuawa unaumwa ungeamini tu, au umvivu wakufanya utafiti..........usiwe mtu wakusikiliza sanaaaahebu jitose mwenye ukaone THE LOLIONDO WONDER......Matibabu yapo kiimani zaidi
====Kwataarifa yako ule mti anaotumia babu kama dawa ni moja ya miti yenye sumu kali sana duniani...according to german doctors Reseach...ile dawa ya babu ilipopelekwa maabara iligundulika it takes five to ten ten min mtu kuaga dunia pindi anywapo...sasa jiulize kwa nn wanasavaive

Kwa sasa nina mashaka na hiyo sumu inayopigiwa debe saana kwenye huo mti. Reason? Mbona records zinaonyesha kwamba wenyeji wa eneo hilo walikuwa wanatumia mti huo huo kuwapatia tiba wazazi? Something is dodge somewhere.
 
Waziri wa Afya wa Kenya, Bi. Beth Mugo, amewakemea waganga wa kienyeji na wale wanaojigamba kwamba wanaponya kwa imani. Amesema kuwa serikali haitawaacha waipotoshe jamii kwamba wanaweza kuponya magonjwa yote.Aliyasema hayo katika sherehe za kuadhimisha siku ya Kifua Kikuu duniani. Aliendelea kusema kwamba waganga wa kienyeji wanahatarisha afya ya Wananchi. Alisema kitendo cha waganga hao wa kienyeji kudai kwamba wanaweza kuponya magonjwa sugu kama vile Ukimwi, kimesababisha magonjwa hayo kuenea zaidi kwa watu wengine. Aliendelea kusema kuwa huo ni uongo unaowafanya watu wachanganyikiwe.

Vile vile Bi Mugo amezitupilia mbali taarifa za vyombo vya habari kuwa mganga wa kienyeji anayejulikana kama babu huko Loliondo Tanzania, anaponya maradhi sugu, kwa kuwapa wagonjwa dawa inayotokana na mti wenye sumu. Bi. Beth Mugo ameiomba serikali ya Tanzania ikifunge kituo hicho cha Loliondo na kuwapiga marufuku watu wanaokwenda kwa babu huyo. Amedai kuwa watu wanaokwenda huko wakirudi wataeneza zaidi Kifua Kikuu na Ukimwi. Tutakapokutana huko Burundi na Mawaziri wengine wa Afya wa nchi za Afrika Mashariki , nitamuomba Waziri wa Afya wa Tanzania, amtie gerezani babu huyo na kuipiga marufuku biashara yake ya uganga alisema Bi. Mugo. Habari hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Kenya, KBC.

Wakati huo huo Waziri wa Afya wa Tanzania naye pia amewakaripia vikali waganga wa kienyeji waache kudai kwamba wanaweza kuponya magonjwa sugu kama Kifua Kikuu. Hata hivyo, haijaeleweka wazi iwapo karipio hilo linamhusu pia babu wa Loliondo.

Babu wa Loliondo pamoja na kujiita mchungaji anaingia pia katika kundi la waganga wa kienyeji maana misingi ya tiba yake haitofautiani na ile ya waganga wengine wa kienyeji.

Kwa heshima na taadhima tunaiomba serikali yetu impige marufuku wazi wazi babu huyo ili kudumisha amani na utulivu uliopo kati ya Tanzania na Kenya. Babu asitusababishie chuki, uhasama na mgawanyiko kati yetu na Wakenya. Ni kweli, baadhi ya viongozi wa serikali yetu nao pia wamepata kikombe, kwa sababu hiyo wanaweza kuona aibu kumpiga marufuku babu. Tunaomba wasione aibu, maana wao pia sio malaika, ni wanadamu wanaoweza kukosea kama wengine. Kwa sababu hiyo wasilifumbie macho tamko hilo la Waziri wa Afya wa Kenya. Waziri huyo wa Kenya ametema cheche zinazoweza kutuongezea matatizo makubwa tuliyo nayo ya kiuchumi na kijamii. Wahenga walisema dalili ya mvua ni mawingu, na kinga ni bora kuliko tiba. Wakenya tunawategemea kwa mengi, wasije wakatufungia mpaka tukakosa bidhaa zao. Maduka mengi hapa TZ yamejaa bidhaa za Kenya  kuanzia mafuta, sabuni, vinywaji, nguo mpaka pipi. Inaonekana viwanda vyetu vinashindwa kuzalisha bidhaa bora.

Makampuni ya uchapaji, ya TZ, yaliyopo jirani na Kenya yanategemea sana kupata karatasi na vifaa vya uchapaji kutoka Kenya maana huko vinapatikana kwa bei nafuu. Sio hilo tu kuna Watanzania wengi waliopeleka watoto wao Kenya ili wajue vizuri Kiingereza maana shule nyingi za TZ hazina walimu wazuri wa lugha hiyo muhimu kwa mawasiliano kimataifa.

Dawa nzuri za kutibu hata mafua na kikohozi, ukiingia katika maduka ya madawa, utaona zimeandikwa Made in Kenya! Hata wanaotaka kuagiza magari kutoka Japan, wanaona nafuu magari yao yapitie bandari ya Mombasa, Kenya, maana bandari yetu ina ukiritimba mwingi na inachelewesha sana utoaji wa bidhaa.

Tembelea maduka ya vifaa vya ujenzi mjini Arusha, utashangaa kuona vifaa vizuri vya ujenzi, kama vile ceiling board, vimetoka Kenya. Siwapigii debe Wakenya, ila ukweli ndio huo tunawategemea kwa mengi ndio maana hata suala la Jumuia ya Afrika Mashariki bado linasua sua maana tunaogopa Wakenya watazidi kuushusha chini uchumi wetu.

We babu wa Loliondo, usiwafanye Wakenya watuchukie bure kwa sababu yako. Tukakosa hata Panadol(made in Kenya) ya kutibu maumivu ya kichwa. Usisahau Obama asili yake ni Kenya. Na Obama akiamua kuingilia suala lako, na kutuletea manowari na mizaili zake, kama alivyofanya kwa Kadafi, dawa zako haziwezi kumzuia. Kama hukupata mshahara mzuri kabla hujastaafu uchungaji, usitake kuwapora Watanzania walalahoi, pesa ndogo wanayoipata kwa shida, maana mishahara yao haitoshi hata kulipia nauli ya kuja huko Loliondo, mpaka wasafirishwe bure na Wabunge wa Chadema!
...confused! Tutakosana na Waziri au Wakenya? (ambao wapo kibao Loliondo wakinufaika na Babu) Makala ndeeeefu saaaana, duh!?
W
 
Hivi ni wapi babu amesema yeye ni jesus, huyu waziri ni kituko ndio waheshimiwa wasiojua kazi zao babu hajawalazimisha kenyans kwenda huko kwa nini wao kenyans wasifunge mpaka kuzuia raia wao?
 
...confused! Tutakosana na Waziri au Wakenya? (ambao wapo kibao Loliondo wakinufaika na Babu) Makala ndeeeefu saaaana, duh!?
W

Chachu kidogo huchachua donge zima. Waziri ana wajomba, ana mashangazi, ana mawifi. Ukikosana naye umekosana na wote hao maana lazima watamuunga mkono.
 
Nimependa satirical message yako kwa WAKENYA!
Nani aliwaita TZ na kuwalazimisha kunywa dawa ya Babu? Kama Babu anawaharibia soko la dawa zao zilizokuwa zinapita njia za panya basi wajipange tena upya.
 
Hivi ni wapi babu amesema yeye ni jesus, huyu waziri ni kituko ndio waheshimiwa wasiojua kazi zao babu hajawalazimisha kenyans kwenda huko kwa nini wao kenyans wasifunge mpaka kuzuia raia wao?

Hee, hujaisoma vizuri hiyo post? Unataka wafunge mpaka halafu watoto wetu wakose Blue Band kwa mkate na KIWI(Made in Kenya) ya kung'arisha viatu vyetu angalau mara moja kwa mwezi!
 
Mwanzo thread yako nilitaka kuielewa. Huku mbele ulipoanza kuchanganya ma international relations ,international marketing(ambayo nayo haujaielewa vizuri),national security sijui Obama mkenya ndio haujaeleweka na umeharibu kabisa. Wewe na huyo waziri wa Kenya mkapate kikombe ili akili zitulie. Mbona wakenya ndio wamejaa pale Loliondo. Tuwaache ili tupate 'balance of trade' na hizo panadol zao unazosema wanatuuzia.
 
Back
Top Bottom