Imetokea loliondo

Imetokea loliondo

Et usipotoa ushuhuda huponi, sasa utatoaje ushuhuda bila kupona? Sion mantik hapa
 
babu alitoa onyo kusikia habari za eti fulan kaja kupata kikombe..haina tija
Leo hii nimepata taarifa kuwa yule Professor wa ujanja ujanja, Sheikh Yahya Hussein ameonekana leo Loliondo kwa Babu kwenda kupata dozi,
 
Kule Loliondo Babu aliamua kutibu kutokana na matatizo mbalimbali.

Basi kukawepo foleni ya watu wa kisukari, ya athma, ya presha, ya kansa mbalimbali na ya wenye HIV.

Hii ilikuwa ni katika kuboresha huduma tu!

Basi ile foleni ya wenye HIV haikuwa na watu. Babu akasimama akasema ""kwa kuwa hii foleni ya wenye HIV hakuna watu basi inabidi dawa yake tuimwage!""

Weeee watu wakang'aka.... aaaaaaaaaaaaaagh wapi sisi tutainywa hata hiyo hivyo hivyo tu.
 
Unajua walijibuje..aaaha babu usimwage tumejichanganya tu!!!
 
ok..sio Loriondo..ni Loliondo wasonjo wakikusikia unapaita Loriondo...watakutoa mbiooo
 
Mzee Wa Loliondo
Inasemekana Mzee kaoteshwa dawa ya kutibu “magonjwa yote ”. Wapo watu wanaoamini kuwa ni kweli inaponya na wapo wale wanao tarajia iponye magonjwa yanayowasibu vile vile wapo wengine matarajio yao ni kupona magonjwa wanayofikiria.
Kupatikana kwa dawa hii tunaweza kuangalia katika mitazamo mitatu.
1) Magonjwa yote
2) Watibiwa ( Watu )
3) Gharama ( Tsh 500.00 tu )
Mogonjwa yote.
Kama ni kweli inaweza kutibu magonjwa yote basi hii dawa ni mwisho wa utafiti wa matibabu. Hapa kuna maswali mengi sana ya kujiuliza,
1) Nini maana ya magonjwa yote?, ni mangapi?, kuna sehemu ipo orodha ya hayo magonjwa?, ili kila anayehisi au kusikia na hata kuona kwamba anaumwa atarajie kupona. Vipi ugonjwa kama wa kusahau ( kupoteza kumbukumbu ), kuona karibu, n.k, dawa inatibu?.
2) Babu anayo haja ya kujua mgonjwa wake anaumwa nini?, nadhani hiyo dawa ni ya aina moja tu, kwa hiyo kubwa kawake ni wewe kuwa mbele yake na hiyo Tsh 500.00 ( kazi ni kukusanya pesa tu ).
3) Hii dawa ni lazima mgonjwa utoke popote pale ulipo na uende Loliondo ( wakazi wanaozunguka eneo la Loliondo na Arusha kwa ujumla ulaji huo = utalii.
Watibiwa ( Watu )
Ugonjwa wowote unaweza kumpata mtu yoyote awe Mtoto au Mtu Mzima , awe amesoma au awe hajasoma, lakini dawa hii imewafanya watu hawa wote kuwa kitu kimoja , ( hi ni Brainwashing, the attempt to change the thoughts and beliefs of another person against their will ) . Hapa usishangae kuambiwa kwamba karibu wabongo wote ni wagonjwa , lazima babu atasema hii
Gharama ( Tsh 500.00 na 1000.00 kwa wageni )
Babu amewafanya wabongo wanaoishi chini ya Dollar moja kwa siku kuiona Sh.500 kama bure, hapa kweli babu kafanikiwa sana kibiashara.
Jaribu kufikiria watu 2500 wanapata kibombe kwa Babu cha Sh. 500 tu,
Kwa siku anapata Sh. 1,25,000.00
Kwa week Sh. 8,750,000.00
Kwa mwezi Sh. 271,250,000 .00

SIJUI.
Watu wote pale Loliondo wanapata wapi huduma nyingine kama za malazi, za usafi , choo n.k.
Wahusika ( Serikali ) lazima wanafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha matatizo ya kulipuka magonjwa mengine , vile vile wahusika ni lazima wanahakikisha watu wanapata dawa sahihi.
Kipato anachopata babu kitakuwa shared na wakazi jirani baada ya Kamishna wa mapato kutoa kodi yake.
Wabongo baada ya kupata kikombe tutarajie kuchapa kazi kwa bidii ( kuongeza uzalishaji ) kwani watakuwa wamepona, hii dawa inaweza kusaidia sana kukuza uchumi.
Idadi ya Hospitali na Wauguzi zilizopo, ikiwa wahusika ( Serikali ) watabadilisha matumizi ya majengo ya hizo Hospitali baada ya wagomgwa wote kuwa mamepona au wapo kwa Babu. Wauguzi (Waganga) wote watapoteza ajira zao.

IMANI.
Kama huna imani kupata kikombe kwa Babu huwezi kupona. Baadhi ya watu wapo wanaanza kuuliza watapata wapi dawa ya kupata imani kwanza ili wakienda kwa babu waweze kupata kikombe na kupona ?
 
Mzee Wa Loliondo
Inasemekana Mzee kaoteshwa dawa ya kutibu "magonjwa yote ".

Babu hadai kutibu magonjwa yote; bali anadai 'dawa' yake kutibu kansa aina yeyote, kisukari, UKIMWI/VVU, pumu, na kifafa. Hii 'yote' sijui umeitoa wapi?
 
Babu hadai kutibu magonjwa yote; bali anadai 'dawa' yake kutibu kansa aina yeyote, kisukari, UKIMWI/VVU, pumu, na kifafa. Hii 'yote' sijui umeitoa wapi?

hii list imebandikwa wapi?umesahau B.P
 
:embarassed2: hii imani ya babu have to be tested with carbon 14.
 
Back
Top Bottom