TREE OF LIFE FOUNDATION
Member
- Aug 15, 2022
- 19
- 46
Kampuni ya matangazo ya Imaging Africa usiku wa jumamosi tarehe 24.06.2023 walifanya uharibifu mkubwa wa kimazingira kwa kukata miti iliyooteshwa pembezoni mwa barabara.
Imaging Africa imefyeka miti hiyo ambayo hawakushiriki kuiotesha wala kuitunza.
Wamefyeka miti ili ubao wao wa matangazo ya biashara uonekane. Ubao huu wameufunga mwaka huu, lakini miti hii ina miaka isiyopungua mitatu.
TREE OF LIFE FOUNDATION tunakemea vikali kitendo hiki, na tunawaonya Imaging Africa waache mara moja vitendo vya ukataji miti kwani ni ukatili dhidi ya mazingira yetu.