ILO imeandaa Jukwaa kwa Wadau Kujadili uboreshaji wa Changamoto na Uhamaji wa Kutafuta Fursa katika Nchi za Afrika Mashariki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
FnOARH1WYAAQCJe.jpg
Mkutano huu wa siku mbili unafanyika Zanzibar kwa muda wa siku mbili, Januari 24 na 25, 2023 ambapo lengo kuu ni majadiliano ya Wadau mbalimbali kuhusu mazingira ambayo wanakutana nayo wanaotafuta ajira kutoka sehemu moja kwenda kwingine, hasa wakilengwa zaidi vijana.

Wanaoratibu mjadala huu ni Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) kupitia program ya Better Regional Migration Management (BRMM).

Baadhi ya Wadau wanaoshiriki ni Mawaziri, Wakurugenzi Wakuu, Wakuu wa taasisi na vyama vya masuala ya kazi, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wafanyakazi na wawakilishi kutoka katika Nchi zote za Afrika Mashariki.

Jukwaa hili litatumika katika kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya ajira kwa Nchi Wanachama na wengine ambao sio Wanachama, ili kuwe na mazingira mazuri tofauti na ilivyo sasa.

Suala la uhamaji umekuwa na changamoto nyingi na kkubwa ambacho kinasababisha kuwe na uhamaji ni suala la kiuchumi, wengi wao wanafanya hivyo kutafuta maslahi bora na wengine wanahama kutokana na sababu za kijamii ikiwemo familia pamoja na sababu za kisiasa au kiusalama.

Wawakilishi waliopo katika mjadala huu Wanatoka katika Nchi za Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, South Sudan, Uganda na Tanzania

Ali.JPG

MGENI RASMI ANAFUNGUA MJADALA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Jamal Kassim Ali anafungua mjadala kwa kusema “Kuhamahama kwa wafanyakazi si jambo dogo, kumekuwa na changamoto kadhaa za sera zinazosababisha watu wengi kuhamahama kutafuta ajira.

“Asilimia kubwa maeneo mengi yanayokabiliwa na changamoto hiyo wengi wanafanya hivyo kutokana na malipo duni na kukosa uhakika wa ajira.

“Nafasi kama hii iliyotengenezwa na ILO inaonesha jinsi ambavyo wameshiriki katika kutengeneza mazingira bora ya kazi sehemu tofautitofauti.

“Ipo wazi kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kulinda haki za wafanyakazi wanaohama, kuna umuhimuwa wa kuwa na sera za uwazi ili kusaidia kutengeneza mazingira mazuri pamoja na ushirikiano wa taasisi kwa ajili ya kusaidia kuboresha mazingira.

“Ninaamini ndani ya siku mbili hizi tutajifunza vitu vingi na kutengeneza njia nzuri ya kuwa na mazingira mazuri ya watafutaji wa ajira wanaohama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.”

FnOARHvXEAA0_-O.jpg
Hamis Mwinyi, Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar
Anasema “Nawashukuru ILO kwa nafasi hii, nimejulishwa kuwa hii ni mara ya kwanza ya forum hii inafanyika kwa lengo la kushea elimu kuhusu kuhamahama kwa Wafanyakazi.

“Zanzibar pia kuna changamoto hiyo, hasa imekuwa ikisababishwa na upungufu wa ulinzi kazini na utawala mbovu kwenye taasisi. Kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha mazingira ya Wafanyakazi na utawala kwa faida ya taifa.

WAZIRI, JAMAL KASSIM ALI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Jamal Kassim Ali: Nchi zetu zina changamoto kwa vijana kuhama kutoka kwenye mataifa hayo kwa lengo la kutafuta kazi, kama nilivyosema hapa Wadau watabadilishana uzoefu na kuangalia jinsi gani tunaweza kuwa na kitu au vitu kwa ajili ya kufanyia kazi kupunguza changamoto hiyo.

Wapo wanaohama wakiwa hawana taarifa sahihi za huko wanapokwenda na mwisho wake wanajikuta katika matatizo.

Moja ya mambo ambayo tunashauri ni kuwa na sera bora ambazo zitawasaidia wanaotafuta kazi nje ya nchi zao, kuwaelewesha wa kile wanachokitaka kwa kuwa fursa zipo lakini hawana uelewa.

Pia tunatakiwa kuwa na udhibiti mzuri wa taasisi zetu katika kujiendesha ili wasije wakaondoka na kuishia kupata matatizo.

Pamoja na hivyo ni muhimu kuwa na sera na sheria zinazowiana katika Nchi wanachama wa Afrika Mashariki ili ziwe zinazungumza katika masuala ya uhamiaji.

ILO.JPG


Alexio Musindo, Mkurugenzi wa ILO Afrika
Kuna zaidi ya milioni wanateseka na kupitia mambo mengi ambayo ni kinyume cha ubinadamu kutokana na kupitia njia ambazo si halali za kuhama kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Tumewashirikisha wadau wengi muhimu wakiwemo Serikali kwa lengo la kupata majibu nan jia sahihi.

Lengo ni kushawishi na si kulazimisha nini kinafanyike, pia kwa wale ambao hawana wawakilishi katika mjadala huu ikumbukwe kuwa tunafanya kazi na ubalozi wa nchi mbalimbali.

Mfano mwaka 2022 tuliwakusanya wawakilishi wote wa ubalozi wa Afrika Mashariki na kujadiliana jinsi gani mamlaka za Uarabuni zinaweza kufanya nao kazi kuwasaidia raia wanaokwenda kufanya kazi kwenye mataifa hayo.

Mbali na hapo, pia tunafanya na Umoja wa Ulaya kuangalia jinsi ambavyo tunaweza kutoa msaada kusaidia wahamiaji wanaotafuta fursa pindi wanapokuwa na changamoto na namna ya kutengeneza njia za kufanya mazingira yawe mazuri.

Muhimu pia ni kutoa taarifa sahihi ili wale wanaohama kutoka upande mmoja kwenda kwingine wawe na uhakika wa taarifa sahihi, hapo inamaanisha tunazungumzia mawasiliano, nayo ni muhimu.

DKT. IRENE ISAKA, Mkurugenzi wa Sekta za Jamii wa East Africa Community
Masuala ya Uhamiaji ni jambo muhimu kwa kuwa kuna itifaki zinazoelekeza, ndio maana tunaweka sera na kanuni ili kwa wale wanaohama kutoka upande mmoja kwenda kwa Nchi wanachama wawe na mazingira mazuri ya kazi.

Wafanyakazi lazima wapate huduma sawa na wengine pindi wanapohama, ndio maana tunatengeneza mazingira ya wao waweze kupata huduma za Hifadhi ya Jamii ili unapoondoka kwenda kwingine uweze kutambulike huko unakokwenda.

Uwepo wa sheria na vipaumbele tofauti kwa kila nchi kunachangia ugumu wa mazingira ya kazi, tunaendelea na ushawishi kwa Nchi wanachama ili waweze kulinganisha ili vipaumbele viendane na mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Kamati.JPG

JOSEPH NGANGA
Mkurugenzi wa Huduma za Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Inayohusika na Masuala ya Kazi Ajira na Wenye Ulemavu


Mjadala huu ni mzuri kwa kuwa umoja unaweza kutufikisha mbali tofauti kila mmoja akifanya peke yake.

Tanzania Bara na Zanzibar tunatakiwa kuchangamka kuangalia maeneo ambayo tutanufaika ndani na nje ya Ukanda wa Afrika Mashariki.

Kuhusu wahamiaji wengi kuitumia Tanzania kama njia ipo kwa wingi na pia wapo Watanzania ambao nao wanatoka kwetu kwenda kwingine.

Inawezekana hao wanaopita kwetu kwao wanataratibu ngumu hivyo tukishauriana tunaweza kutengeneza ushirikiano mzuri na kupunguza changamoto kama hico za kuwa na wahamiaji wanaoingia nchini katika njia ambazo si sahihi.

Serikali iongoze kuziona fursa za kazi katika mataifa mengine na kuweka utaratibu mzuri na utaratibu mzuri ni makubaliano kuwawezesha raia wawe wanakwenda kwa utaratibu mzuri, ili hata kama ikitokea tatizo inakuwa rahisi kuripoti na hiyo itasaidia kulinda haki za kibinaadamu katika mataifa mengine.
 
Back
Top Bottom