Illuminati and Freemasons

Illuminati and Freemasons

Unganisha kwenye ule uzi wa sehemu ya kwanza kwani kulikuwa na haja ya kuanzisha uzi mwingine
 
SKULLS AND BONES - 1

Hili ni kundi lenye nguvu kushinda FREEMASON

Leo tuwa kodolee Macho kidogo Wazee wa mafuvu na Mifupa,
Lilianzishwa mwaka 1832 na watu wawili William Huntington Russell na Alphonso Taft hawa jamaa walikua na kawaida ya kuiba mavufu ya watu maarufu na mashujaa na kuyaifadhi. -

Nikupe kisa kimoja 10/2/2017 ndugu mmoja ( Haryln Geronimo (Kitukuu cha shujaa Geronimo) mwenye miaka 61) katika jamii hii alifungua mashtaka akiwashtaki Skull and bones jamii ya siri ambayo ilianzia Katika chuo kikuu cha YALE huko marekani kuwa iruhusika na kuiba mabaki ya Shujaa Geronimo ambaye alikuwa ni shujaa kutoka Jamii ya APACHE (Red Indians).
-

Miaka kadhaa imekuwa ikipigiwa kelele jamii hii ya Fuvu na Mifupa kuwa imeshikilia mabaki ya Geronimo ikiyatumia kwa shughuli zake za kiimani.
Anasema “naamini kabisa toka moyoni mwangu kuwa roho ya Geronimo haikuachiliwa"
-

Wakongwe Kama Prescott S. Bush ambaye ni baba wa aliyekuwa Rais George W. Bush na Babu wa George W Bush huyu na wenzie wengine wanachama wa Skull and Bones walichimba mabaki ya Geronimo toka kaburini mwaka 1918 wakaiba fuvu la Huyu Shujaa, Na Mifupa miwili na mavazi yake kivita kutoka katika Kaburi lake huko Fort Sill.
-

Jamii hii ikachukua mabaki haya na kuyaweka Makao yao Makuu ambayo yalikuwa yameanzishwa toka mwaka 1832.
Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yaki zungumzwa kuhusiana na kundi au jamii hii. -

Ni kundi ambalo nchi za huku kwetu hali fahamiki na watu wengi lakini kwa huko kwa wenzetu ni Kundi kubwa na la kutisha sana.
Ni Kundi lenye viongozi wakubwa sana duniani na watu maarufu likihusishwa na kundi la mafia kwa miaka hiyo.
Pia Wana Patikana Katika Vyuo Vikuu Mbali Mbali Duniani na siku hizi hata Vyuo vya kawaida. -

Vyuo vikuu Kuna elimu inaitwa THE SECRET DOCTRINE OF HYPOTHESIS IN SCIENCE, RELIGION AND PHILOSOPHY ukikutana na mtu haamini uwepo wa mwenyezi Mungu mara baada ya kutoka chuo basi jua SKULLS AND BONES Wamesha fanya yao. -

Sahau kuhusu Freemasons hili ndilo kundi lenye nguvu zaidi ndani ya Illuminati. -

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Interesting, ila uandishi huu itakuchukua muda mrefu kufikisha ulichodhamiria.

Labda iwe ni moja ya malengo yako kuufanya uzi uwe mrefu na wachangiaji njiani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri uwe unafanya proof reading na pia uwe unafuatilia hizi historia kwa umakini na ukaribu wa hali ya juu ili utuletee content isiyo na error ambazo zinaweza kuepukika mfano ,nanukuu.

"Hata haijulikani kilitokea nini! labla kwasababu ya kukosa nguvu ya ushawishi na kuungwa mkono, Baadae wakaanza kuvishawishi vikundi ambavyo kwa wakati huo vilionekana vina ushawishi kama vile Order of Assassins, Skull and Bones, Masons (Waashi/Wajenzi kabla hata hawajawa wajenzi huru {Freemasons}),"

mwisho wa kunukuu.
Umebainisha kuwa skull and bones ni moja ya chama kilichokuwa na ushawishi kipindi illuminati imeanzishwa bila kugundua kuwa adam weishaup alifariki November 18, 1830 na skull and bones imeanzishwa mwaka 1832 so ni miaka miwili baada ya weishaup kufariki .
 
g
ILLUMINATI - 1
Illuminati ilianzishwa rasmi tarehe 1 mwezi wa 5 mwaka 1776 na Adam Weishaupt huko Ingolstadt, Germany huku lengo kuu likiwa "Into the bright" wakati kinaanzishwa walikua na malengo mengi mazuri, ikiwemo kupinga imani za jadi, kupinga matumizi ya nguvu za giza, kupinga unjanyasaji na kupinga na dora kubwa kubwa.

Hata haijulikani kilitokea nini! labla kwasababu ya kukosa nguvu ya ushawishi na kuungwa mkono, Baadae wakaanza kuvishawishi vikundi ambavyo kwa wakati huo vilionekana vina ushawishi kama vile Order of Assassins, Skull and Bones, Masons (Waashi/Wajenzi kabla hata hawajawa wajenzi huru {Freemasons}),

Hivi vyama ni kizungumkuti kuvielewa na kuvifuatilia kwa undani wengi tunaishia kusoma makala za kwenye magazeti na kujiona tuna vifahamu. Neno Freemasons sio ngeni masikio kwa watu na wengi wetu tuna wasikia zaidi Freemasons (Hatuwafahu kama tunavyo jiaminisha) kwa maneno mengine Freemasons ni maarufu kuliko hata Illuminati.

Kimsingi hawa Wote ni wamoja lakini wana tofautiana katika utendaji kwa mfano Freemasons hawa wana husika na mambo ya Imani hawa tunao kwenye Dini zetu, kwenye makanisa yetu na kwenye misikiti yetu wamesha piga kambi toka muda mrefu sana,

Hapa sina maana ya Dini fulani au kanisa au Msikiti fulani ni wa Freemasons, Lakini hawa wanakua na kikundi chao cha siri kinafanya kazi kwa siri kwenye imani fulani (Makanisa & Misikiti) wanacho kifanya hawa ni kufuata taratibu zote husika lakini Kuna vitu Wana anza kupandikiza kwenye imani husika na kuchunguza taratibu zote za Imani husika.

Freemasons wamekuwa maarufu zaidi kuliko vikundi vingine kutokana na wao kufanya kazi inayo husisha Imani na walikua maarufu kabla hata ya kuwa chini ya Illuminati, Pamoja na kwamba Freemasons ni kikundi ndani ya Illuminati nao kama Freemasons wanaongoza kuwa na vikundi vingi vya siri labla ndio sababu nyingine ya inayo wafanya kuwa maarufu.

Kuna Sect hatari ndani ya Freemasons inaitwa Propaganda Due (P2) maarufu sana kama "Trust Control" habari za Freemasons zote unazosoma kwenye machapisho mbali mbali asili yake ni wao ukisha sikia "Wadhibiti Ukweli" bila shaka usha fahamu nini kinaendelea.

ITAENDELEA

Sent using Jamii Forums mobile app
gusa hapa
Vatican inamiliki dunia - JamiiForums
 
Zote hizo ni tools za Jesuits
Wao hufanya mambo kisha mikono ya Jesuit inabaki kuwa msafi
 
Future Lawyer unawaokota sana wazembe wa kuutafuta ukweli. Hakuna sehemu yeyote Freemasons ikawa tawi la Illuminati, bali wanachama wengi wa mwanzo wa Illuminati walikuwa wanachama wa Freemasons. Historia hii iko wazi kabisa kwenye Wikipedia.
 
Hizi informations huwa zinapatikana wap?

I'm just curious tu,Future Lawyer.
 
Back
Top Bottom