Lolote linaweza kuwa....Sijapingana na ripoti yoyote wala sijatoa conclusion yoyote.... Hii mada ina pande mbili. Upande wa kwanza ni mauaji ya moja kwa moja ya Chalinze... Hakuna hata mmoja aliyejishughulisha kuuliza nimejuaje mambo ya kipelelezi na ya ndani kwa kiasi kile..... Hakuna!!!
Upande wa pili ni Agnes Masogange ⚰RIP! post yangu kwake imejaa hojaji na maswali kwenye heading na hitimisho... Hebu tuitendee haki slogan ya GTs
Habari wana jamii, nimesikitishwa sana na kifo cha Video quen maarufu Agnes Gelard almaarufu Masogange, Pia nimesikitishwa hasa na watanzania tulivyo kuwa hatuna utu yaaninkuna watu wanmpost Agnes mitandaoni huku wakitoa na maneno ya kashfa ambayo hayafai kumtole Maiti kingine ambacho nashindwa kuelewa na nimesikitishwa zaidi ni jinsi picha ambazo watanzania wanatumia kumpost humo mitandaoni marehemu Masogange yaani ni picha chafu ambazo hazina maadili kwa umma nnacho kishangaa ni jee Masogange hana picha nzuri za staha ambazo watu wanaweza kuzitumia kuposti mitandaoni kushow apreciation? au ndio muendelezo wa kumzihaki marehemu?.
Kitu kingine ni hili swala la watu wanaohoji na kuhusisha kifo cha masogange na kikundi cha watu furani, yaani watu wanaamini Masogange hajafa bure yaani kuna watu wanahusika katika kifo chake, yaani kwa maana hiyo watu wanapuuza taharifa zilizotolewa hospitali kuwa marehemu alilazwa kwa siku nne kwa maradhi ya Pumu pamoja na upungufu wa damu,Nadhani wengi tunajuwa pumu likikubana unakuwa katika hali gani. Mimi mwenyewe nimeshawahi kuumwa Pumu mara kadhaa katika umri wangu kwa hiyo na declare interest Pumu ni ugonjwa hatari sana pale linapokuamulia kukushika haswa maana linahusiana moja kwa moja na mfumo wa upumuaji,Pia tunajuwa madhara ya upungufu wa damu lakini pia tujuwe kuwa Masogange hakupelekwa hospitali bali hospitali alikwenda yeye mwenyewe baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa pumu.
Naumia sana nnapo waona watu niliyokuwa nawaheshimu kama Mshana Jr naye ni miongoni mwa watu wanaohusisha kifo cha masogange na kikundi cha watu furani kupitia post zake tofauti zilizopo humu jukwaani.
Nnacho kiona hawa watu wote wanaokihusisha kifo cha masogange na kufanyiwa njama na watu flani naona ni upungufu wa akili pamoja na ukosefu wa kazi za kufanya kutokana na fikira zao finyu.
Masogange kafa kama Mwenyezi Mungu alivyotuambia katika Qur'an "Qullinafsi Dhaaikatul Mauti" Kila nafsi yenye uhai au yenye roho itaonja umauti. Kikubwa niwahusiye nafsi zenu wana jukwaa pamoja na kuihusia nafsi yangu jamani tumcheni Mola wetu haya maisha ya duniani ni mafupi mno huyo Masogange kafa nadhani hata miaka 35 hajafikisha leo yeye Masogange kesho ni mimi au wewe unaesoma uzi huu, jee umejiandaaje na siku yako ya kufa jee umejiandaaje na safari yako ya mwisho ya kurudi kwa Mola wako. Tuacheni kuchukulia matatizo ya watu wengine na kuyahusisha na masuala ya kisiasa. Kuna watu walinishangaza zaidi eti wanahitaji Postmoterm ya kifo cha Masogange wakati wanajuwa fika kama marehemu alikuwa anaumwa Pumu, jee wangapi hawajuwi kama pumu linauwa? nadhani wote tunajuwa kuwa Pumu linauwa na ndilo lililosababisha kifa cha mpendwa wetu Masogange.
Mwisho nitowe ushauri kwa wadada wote watakao soma uzi huu, tuangalie sana picha tunazozipost kwenye mitandao yetu ya kijamii zinaweza kuja kukuharibia sifa zako hapo baadaye maana picha zako zinaishi wewe mwenyewe hauishi muda mrefu. Agnes Masogange awe funzo kwenu maana R.I.P zote anazopewa ukianga photo attachment moyo razima uume hii nikutokana ndio picha nyingi alizokuwa nazo labda kwenye akaunti zake za social media. Lakini hata kama mtu alikuwa na matendo mabaya kwa wewe hnavyohisi sio vizuri kutoa aibu zake hadharani maana kwa sisi waislamu Mtume Muhammadi S.A.W anasema msithubutu kutoa aibu za maiti zenu hilo sio jambo jema kabisa.
Mwisho kabisa nasikitika Marehemu Masogange kaondoka hali yakuwa ndoto zangu hazijakamilika hata kidogo. Hakuna anayebisha Marehemu alikuwa ni mrembo haswa na mimi ni miongoni mwa wanaume wachache sana tuliyofanikiwa kuuona uzuri wa Masogange na nilikuwa nipo kwenye process za kutaka kwenda kwao na kupeleka barua ya uchumba. sio siri nimesikitika sana basi japo hata ningepata japo hata salamu yake tu kabla hajafa ili atleast ndoto yangu ifikie japo hata robo.
All in all Mungu ailaze roho ya marehemu Agness mahali pema peponi na Mwenyezi Mungu ampe kauli thabiti marehemu.
Asante sana nashukuru mkuu na hongera wewe mwenzangu uliyefika chuo kikuu naona uwezo wako wa kuchambua mambo ni mkubwa sana naomba na mimi unifundisheKwa assessment yangu ya haraka haraka... Form four ulifeli au hujafika. Uwezo wako wa kunyambua mambo ni mdogo mno.
sababu ya kifo cha Agnes kimeshasemwa ni Pumu au wewe unapingana na report ya madaktari mkuu?Kuna kitu kinaendelea lakini bado hakijawa wazi sana... Ngoja mshtuko wa habari za kifo utulie... Kuna mengi yatajitokeza......
Wiki iliyopita kuna binti aliuawa gesti Chalinze... ALINYONGWA.... Lakini muda mchache kabla ya mauaji kufanyika alipigiwa simu na ndugu yake wakati wauaji wakiwa tayari chumbani kwake... Akiwasiliana kilugha na huyo ndugu yake alimwambia kuna wanawake wanne wamemvamia chumbani lakini watatu anawafahamu
Baada ya hapo simu zake hazikupatikana tena! Maiti yake iligundulika siku ya pili... Katika kufuatilia undani wake ikaonekana alikuwa kwenye mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya... Na kulikuwa na tatizo kati yake na hao wauaji wake... Hii ilitokana na mawasiliano yaliyofumwa kwenye simu yake
Mchana wa siku aliyouliwa kulikuwa na majibizano kwa njia ya maandishi
Yeye aliandika kuwa kwakuwa wao wamemwaga mboga basi yeye atatoboa sufuria kabisa... Naye akajibiwa kuwa.. Hatasubiri afanye hivyo... Watamfuata huko huko juu.....
Baada ya mazishi kaka yake mmoja akapigiwa simu kupewa pole na kuambiwa kila kilichotokea pale msibani mpaka kuzika... (Kwahiyo wauaji walikuwepo msibani) kisha akaambiwa kuwa MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI
Baada ya kama siku tatu za mauti yake binti mwingine akakutwa kauliwa kwa kuchomwa visu mwili mzima (alikuja Kutambuliwa kama mmojawapo aliyeshiriki mauaji ya kwanza), na mwingine naye akaponea chupuchupu akiwa keshakula visu vya kutosha na sasa hajulikani alipo
Scenario nzima inaonesha ni mauaji ya visasi kati ya makundi mawili na kuna kitu kikubwa kinafichwa!!!!
Ni vigumu kwasasa kulink kifo cha Agnes na hayo mauaji mengine lakini tayari kuna watu wameshaanza kutuhumiwa. ..
Agnes Masogange amekuja kuwa maarufu zaidi baada ya kuja kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya... Tuhuma dhidi ya madawa ya kulevya zilipelekea akamatwe na kufunguliwa kesi... Ni juzi tu hapa mwezi uliopita alikutwa na hatia na kuhukumiwa kulipa faini au kifungo... Alinusurika kifungo kwa kulipa faini iliyolalamikiwa na wengi
Mabush lawyer wengi walisema kuwa kesi kama ile kama huna watu wazito nyuma yako unaondoka na maji...
Kwanini kifo chake kimeacha mashaka!?
Mitandao ya hizi biashara haramu., haipatani kabisa na kitu kinaitwa polisi... Kwa baadhi ya nchi watuhumiwa hufuatwa na kuuliwa huko huko jela au mahabusu
Masogange akiwa tayari kwenye spotlight ya polisi... Nini ingekuwa future yake!? Kumbuka ni vigumu tena kumtumia kwenye hiyo biashara.. Tayari ana file.. Hivyo keshakuwa ndege mweupe!
Lakini je anafahamu mangapi!? Je hawezi kuropoka?!?
Je ni nani aliyekuwa tayari kugharamia maisha yake ya anasa wakati sasa hawezi tena kuzalisha!?
Risk ni zipi akiachwa hai?
Risk ni zipi akinyamazishwa!!?
Je baada ya kesi kwisha alikuwa na madai kwa washirika wake kibiashara!?
Kifo hupangwa na Mungu kwa wale waamini.. Lakini nyuma yake kuna sababu za kifo... Naamini siku moja ukweli utajulikana
RIP [emoji1019] Agnes!
nadhani unaweza kuwa miongoni mwa wanawake wenye uelewa mkubwa wa kudadavua mambo hongera sana mkuuHaya basi,Kufa ni lazima.
Its the most certain thing a human being can be sure of.Alafu alilazwa siku nyingi.Amefariki kwa Typhoid.Just a natural death.Sidhani kama alikuwa na madhara tena kwenye biashara ile.Alidrop akaanza kujisogeza karibu na ibada.She was targeted alipokamatwa south.So hakuwa mtu sahihi tena kumpa kazi.
mnawasingizia tu hao drug dealers maana sio kwamba wao ndio wamempa hiyo pumu, na hospitali hakupelekwa na mtu kaenda mwenyewe na kalazwa 4 dayz sasa hapo wao wanaingiaje? au unataka kusema huyo daktari naye ni drug dealer mwenzao so kaamua kumuondoa kwa kumpiga sindano ya sumu?You're the next!!!! Drug dealers sio watu
Kama hujaelewa maada ungekaa kimya tuMjomba!Nasemaje waacheni watu wafe kwa amani.Maandamano yasiwe chanzo cha kusimamisha any natural creation.Death is natural.
Hata tukijamba sasa itakuwa tunataka kuwatoa kwenye reli.
Wewe huwezi kunizuia mimi kutoa mawazo yangu pamoja na ujinga wangu.Kama hujaelewa maada ungekaa kimya tu
mkuu huyu binti alikuwa anaishi maeneo ya makongo juu kwa hiyo hospitali ta haraka kwake ilikuwa ni mama ngoma hakufanya vibaya kwenda pale kifo chake kilisha pangwa na Mungu lazima afe kwa Pumu na ndio ikawa hivyo hata angeenda ocean road angekufa tuMshana katoa fact and fiction zake na hakuconclude. Wewe msomaji utajaza. Jiulize huyu binti alikosa pesa za kwenda Kairuki, Agha Khan, Muhimbili kuongezewa damu hata angepigia simu watu kumi si wangekwenda kumpeleka na angekosa damu fasta? Pneumonia inatibika especially kwa kijana kama yule siyo mtoto wa miaka mitatu au mzee wa miaka 90.
well said mkuuKila nafsi itaonja umauti, iwe mimi, Wewe, na mwingine huu ni ukweli mchungu ambao binadamu wengi hawapendi kuusikia. Ndio maana siku zote panapotokea umauti watu hawakosi sababu .
Siku yako ikifika hata mtu akitua kidole cha macho unaondokaa. Tufanye yoteee ila Iko siku tutakua ni Mauti Kama Agnes na wengineo waliotangulia.
Kifo ni moja ya ibada Kwa tuliopo Hai tupate kujifunza na kukubali kwamba kifo kipo hakikwepeki na ndipo watu Kwa kipindi hiki neno Mungu litatamalaki midomoni mwa watu. Hujui Kwa kupitia kifo cha Agness Wangapi watazaliwa upya kiroho .
Tufanyeee yote ila tukumbuke kuna kufaa hata Ukiwa MA Pesa kiasi gani, hate Ukiwa na nguvu kiasi gani utaondoka. Na Kama siku yako haijafika Hutokufa abadani.
alikua hasafiri kutokana na ile kesi iliyokuwa ina mkabili maana mahakama ilimzuwia kusafili bila idhini ya mahakamaMi machoshangaa Agy alipoaa kama uji wa mgonjwa muda mrefu kweli na akawa hasafiri tenaa
mkuu msamehe bure huyoWewe huwezi kunizuia mimi kutoa mawazo yangu pamoja na ujinga wangu.
Jf sio ya baba yako.Siwezi kukaa kimya.
Anatafuta mchumbaKwani dada wa taifa anasemaje???
mkuu mpaka unalazwa maana yake umezidiwa au mimi ndio sijuwi? halafu kwenye inshu ya kufa mtu anaweza kufa hata akiwa usingizini tu akiwa haumwi wala nini. unataka kunambia kifo cha Masogange hapo kwa Mama Ngoma yeye ndio mtu wa kwanza kufa hapo kwa magonjwa hayo ya kawaida?Mashaka ya watu ni hospitali aliyofia, pale kwa mama ngoma ni pa kawaida sana tukubali/tukatae (uzuri wa jengo sio usasa wa matibabu) nimetibiwa mara nyingi mno pale.
Magonjwa yanayosadikiwa kumuondoa ni ya kawaida sana tena yenye matibabu pale National Hospital/Agha kan na kwingineko,
Kama pale waliona dalili mbaya kwa mgonjwa kwanini wasimpe rufaa?? haiingii akilini mtu anakufa gafla bila kuonesha dalili za kuzidiwa
Mwisho wa siku maiti ndiyo inapewa rufaa
nimekuelewa sana mkuu lakini sidhani kama uliye mquote amekuelewaBila kuonyesha dalili? Mama si wamekwambia mpaka ugonjwa aliokuwa anaumwa,
Kwa mama ngoma ni pa kawaida sana kivipi hujui kama wanaotibu huko unapopakubali hawatofautiani na hao wa kwa mama ngoma?
Una uhakika gani kama angetibiwa huko unapopasema angepona?
asante mkuu kwa kunielewa