Ilikuwa ni lazima Masogange afe?

Ilikuwa ni lazima Masogange afe?

R. Kelly ktk wimbo wake uitwao be careful kuna maneno anasema;
"Be careful in what you say to me bcoz it might turn around on you, be careful in what you do to me bcoz somebody might dob it to you"

Mi nakushauri kuwa makini na hilo ulilolisema juu ya mwenzio kwa sababu linaweza likasemwa pia wewe utakapokufa. Si vyema kuweka mzaha kama huu wakati mwenzio kafa. Sikatai upo utani lakini sio kama huu wako.


Unadai ulitaka umuwahi wa moto moto, kumbuka kuna watu watataka wamuwahi dada, mwanao, shangazio au mama yako akiwa wa "motomoto" siku atakapokufa. Najua ntakukera kwa maneno yangu haya ila nimetaka nikuzindue maana umejitoa ufahamu
Mizaha ya Humu usiichukuli siriasi ...wewe huuu ni mtando unaweza ukawa unachati na Babako na wote mpo hapo ukumbinibkwenu na msifahamiane.

Usipende kukasirikia vitu vya humu...wengine Majini na Roboti zinaandika

Tu.

Kafanye usafi pale Dukani kwako leo Jmos
 
Narudi naenda kuoga....yajayo yanafurahisha sana
 
JamiiForums naomba msiunganishe uzi huu na zile nyingine nyingi zilizoripoti kifo cha Agnes Masogange... Maudhui yake ni tofauti kabisa

Kuna kitu kinaendelea lakini bado hakijawa wazi sana... Ngoja mshtuko wa habari za kifo utulie... Kuna mengi yatajitokeza......
Wiki iliyopita kuna binti aliuawa gesti Chalinze... ALINYONGWA.... Lakini muda mchache kabla ya mauaji kufanyika alipigiwa simu na ndugu yake wakati wauaji wakiwa tayari chumbani kwake... Akiwasiliana kilugha na huyo ndugu yake alimwambia kuna wanawake wanne wamemvamia chumbani lakini watatu anawafahamu
Baada ya hapo simu zake hazikupatikana tena! Maiti yake iligundulika siku ya pili... Katika kufuatilia undani wake ikaonekana alikuwa kwenye mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya... Na kulikuwa na tatizo kati yake na hao wauaji wake... Hii ilitokana na mawasiliano yaliyofumwa kwenye simu yake
Mchana wa siku aliyouliwa kulikuwa na majibizano kwa njia ya maandishi
Yeye aliandika kuwa kwakuwa wao wamemwaga mboga basi yeye atatoboa sufuria kabisa... Naye akajibiwa kuwa.. Hatasubiri afanye hivyo... Watamfuata huko huko juu.....

Baada ya mazishi kaka yake mmoja akapigiwa simu kupewa pole na kuambiwa kila kilichotokea pale msibani mpaka kuzika... (Kwahiyo wauaji walikuwepo msibani) kisha akaambiwa kuwa MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI
Baada ya kama siku tatu za mauti yake binti mwingine akakutwa kauliwa kwa kuchomwa visu mwili mzima (alikuja Kutambuliwa kama mmojawapo aliyeshiriki mauaji ya kwanza), na mwingine naye akaponea chupuchupu akiwa keshakula visu vya kutosha na sasa hajulikani alipo
Scenario nzima inaonesha ni mauaji ya visasi kati ya makundi mawili na kuna kitu kikubwa kinafichwa!!!!
Ni vigumu kwasasa kulink kifo cha Agnes na hayo mauaji mengine lakini tayari kuna watu wameshaanza kutuhumiwa. ..
Agnes Masogange amekuja kuwa maarufu zaidi baada ya kuja kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya... Tuhuma dhidi ya madawa ya kulevya zilipelekea akamatwe na kufunguliwa kesi... Ni juzi tu hapa mwezi uliopita alikutwa na hatia na kuhukumiwa kulipa faini au kifungo... Alinusurika kifungo kwa kulipa faini iliyolalamikiwa na wengi
Mabush lawyer wengi walisema kuwa kesi kama ile kama huna watu wazito nyuma yako unaondoka na maji...

Kwanini kifo chake kimeacha mashaka!?
Mitandao ya hizi biashara haramu., haipatani kabisa na kitu kinaitwa polisi... Kwa baadhi ya nchi watuhumiwa hufuatwa na kuuliwa huko huko jela au mahabusu
Masogange akiwa tayari kwenye spotlight ya polisi... Nini ingekuwa future yake!? Kumbuka ni vigumu tena kumtumia kwenye hiyo biashara.. Tayari ana file.. Hivyo keshakuwa ndege mweupe!
Lakini je anafahamu mangapi!? Je hawezi kuropoka?!?
Je ni nani aliyekuwa tayari kugharamia maisha yake ya anasa wakati sasa hawezi tena kuzalisha!?
Risk ni zipi akiachwa hai?
Risk ni zipi akinyamazishwa!!?
Je baada ya kesi kwisha alikuwa na madai kwa washirika wake kibiashara!?
Kifo hupangwa na Mungu kwa wale waamini.. Lakini nyuma yake kuna sababu za kifo... Naamini siku moja ukweli utajulikana
RIP ⚰ Agnes!

Hakika, magenge ya wauza madawa ya kulevya ni hatari sana na yana mitandao mipana mno. Wakihisi wewe ni hatari kwa biashara yao kuua ndio njia rahisi ya kumnyamazisha mbaya wao.
 
Mashaka ya watu ni hospitali aliyofia, pale kwa mama ngoma ni pa kawaida sana tukubali/tukatae (uzuri wa jengo sio usasa wa matibabu) nimetibiwa mara nyingi mno pale.

Magonjwa yanayosadikiwa kumuondoa ni ya kawaida sana tena yenye matibabu pale National Hospital/Agha kan na kwingineko,

Kama pale waliona dalili mbaya kwa mgonjwa kwanini wasimpe rufaa?? haiingii akilini mtu anakufa gafla bila kuonesha dalili za kuzidiwa

Mwisho wa siku maiti ndiyo inapewa rufaa
Bila kuonyesha dalili? Mama si wamekwambia mpaka ugonjwa aliokuwa anaumwa,

Kwa mama ngoma ni pa kawaida sana kivipi hujui kama wanaotibu huko unapopakubali hawatofautiani na hao wa kwa mama ngoma?

Una uhakika gani kama angetibiwa huko unapopasema angepona?
 
El chapo Jr bado yupo jela.
Huyu jamaa ndo anajua kuzicheza.
Huyu ndo kazaliwa kwa biashara hizi sio hawa wengne wanafuata mikumbo tu.

Ukitaka ufanye biashara hizi kuwa mafia na ujipange kimkakati na ujue mambo yakiharibika ufanye nini ukwepane na hawa jamaa na usiwepo kwenye Target yao endapo mambo yamekuharbikia.
Ndo maana unakuta wengne mambo yakiharbka wanasepa fasta mjini wanaenda kuanza maisha yao mapya mikoa mingne tena vijijini tanzania kubwa sanaaaa hii....

Kama mimi kuna sehemu Tanzania hii hii nikikupeleka sehemu unaweza hisi haupo tanzania kumbe upo tanzania na unaanza maisha yako mapya na unabadr kila kitu ili kupoteza Target zao.

Ukiingia huko unaingia kwenye UMAFIA UMAFIANI
 
Sku yake ilikua imefka
Kila mtu amepangiwa
Kifo atakachokufa

Ilivyoandikwa haikwepek
Yatasemekana mengi Ila
Sku yake ilishafka

Rest in peace Agnes
Punzika kwa aman
 
Back
Top Bottom